Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 8, 2018

Mfumuko wa Bei Mwezi Septemba Wapanda

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Seotemba 2018 ambao umeongezeka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti,2018.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Ephraim Kwesigabo,amesema kuwa hii inamaanisha  kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018.

Aidha Bw.Kwesigabo amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kinacho ishia mwezi Septemba 2018 zikilinganishwa na mwezi septemba 2017.

Hata hivyo mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Septemba 2018 umeendelea kupungua hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 2.2 ilivyokuwa mwezi Agosti 2018.

Bw.Kwesigabo amesema kuwa baadhi ya bidhaa zisizo za chakula ambazo zilizochangia kuongezeaka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2018 ni pamoja na vileo na bidhaa za tumbaku kwa asilimia 1.9, nguo na viatu kwa asilimia 3.2, vifaa vya matengenezo na ukarabati wa nyumba kwa asilimia 5.2, mafuta ya taa kwa asilimia 18.7,Mkaa kwa asilimia 11.2,Gharama za kumuona Daktaria hospitali za binafsi kwa asilimia 5.5,Dizeli kwa asilimia 19.9 na Petroli kwa asilimia 15.8.

Aidha amesema kuwa hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba nchini Kenya umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.70 kutoka asilimia 4.04 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018.

Kwa upande wa Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )