Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 5, 2018

RC Makonda Ammwagia Sifa Diamond....Amruhusu Kukata Mauno, Amshauri asioe kwanza

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam,  Paul Makonda amesema amempa ridhaa ya kutokuoa msanii Diamond na kumtaka aendelee kuwa ‘sukari ya mioyo ya watu’ sambamba na kuweka video za kukata mauno mtandaoni kutokana na alichokifanya kwa wakazi wa Tandale.

Makonda ambaye ni mlezi wa Kampuni ya WCB inayomilikiwa na Diamond amesema kwa kazi anayofanya huenda akioa mapema itamletea shida na kwamba anahitaji muda zaidi wa kufikiria kuwasaidia Watanzania wenzake.
 
 “Haya mambo mkiyajua vizuri bana kwanza ukiwa msanii halafu mashabiki wako wengi wakiwa wanawake ukioa wanaweza kukimbia, utafikiri ungewaoa wote,” Amesema

Makonda amewataka wasanii wote kuiga mfano wa Diamond wa kurudi na kusaidia jamii iliyowalea.

“Kwa alichokifanya Diamond hata nikiona video yake anakata mauno wala simfanyi, kitu Ila msanii hujafanya chochote halafu unasherehekea siku yako kwa kujirekodi video unakata mauno nakuweka ndani,” amesema.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )