Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 9, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 04

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

Mzee Klopp alizungumza kwa ukali kidogo.
“M…imi…nimehisi tu”
“Unahisi umekuwa malaika wewe?”
Mzee Ethan alizidi kufoka hadi sura ikaanza kuwa nyekundu jambo lililo nifanya nianze kupata woga.
“Na akifa mwanangu utanitambua”
“Likini bab…..”
“Koma mimi sio baba yako, mwanangu ni mmoja na anakimbizwa hospitalini sasa hivi unaniambia nini nikuelewe mjinga weweee”
Maneno ya mzee Klopp yakanikatisha tamaa kwa kweli ya kuendelea kuishi humu kwenye nyumba yake, kwa kweli kwa hapo awali nilihisi kwamba nitayafurahia maisha yangu ya hapa nchini Ujerumani, ila kile nilicho kifikiria sicho kinacho nitokea na nimekuwa ni tatizo toka niingie jana kwenye hili jumba.

ENDELEA
Mzee Klopp akatoka ndani humu na kuniacha nikiwa nimejawa na woga ulio ambatana na wasiwa mwingi sana.
“Utanata na huyu tumfanye nini?”
Sauti ya mwaume ambayo ninaihisi mimi mwenyewe ilizungumza na kunifanya nistuke kidogo.
“Ethan, unataka tumfanyaje na huyu mzee”
“Ngoja kwanza, unataka kuniambia kwamba wewe ndio msababishaji wa tatizo hili?”
“Ndio”
“Kwa nini sasa umesababisha”
“Kila ambaye anakujeruhi moyo wako, nilazima nihakikishe kwamba analipa kwa garama ya damu yake kumwagika”
“Ila umesikia nilichoa ambiwa hapa, kama dada wa watu akifa itanigarimu”
 
“Hawezi kufa”
“Kama hawezi kufa naomba unisaidie basi apone”
“Usijali, atapona”
“Sasa nitafanyaje?”
“Nenda sebleni, ukajumuike na bibi Jane, mutakwenda hospitali moja”
“Sawa”
Nikatoka ndani humu na kurudi sebleni, nikawakuta madaktari wakiwa wanampakiza bibi Jane Klopp kwenye machelea. Tukatoka ndani humu na wakamuingiza kwenye gari la wangonjwa na mimi nikaingia ndani ya gari hili na tukaondoka katika eneo hili.
‘Ehee nimekuja nipo na wewe, usizungumze kwa sauti, wewe niulize hata ndani ya nafsi yako ninaweza kukusikia na kukujibu’
Niliisikia sauti ya mwanaume huyu ikiendelea kuwa nami, jambo lililo nifanya nistuke kidogo ila manesi hawakuwea kugundua jambo lolote
 
‘Sasa kwa nini bibi Jane ameanguka’
‘Amestuka tu, ila atakuwa poa muda si mrefu’
‘Fanya azinduke sasa hivi bwana’
‘Ngoja tufike hospitalini’
‘Hapa huwezi ukamfanya akazinduka?’
‘Ninaweza, mshike mkono wake wa kulia’
Taratibu nikamshika bibi Jane Klopp mkono wake wa kulia, hazikupita hata sekunde tano bibi Jane Klopp akafumbua macho yake hadi manesi wakastuka kidogo.
“Ethan”
“Ndio mama”
Bibi Jane Klopp akawatazama manesi hawa.
“Mery yupo wapi?”
“Baba ametangulia hospitalini kumtazama”
“Amelazwa hospitali gani?”
Nikashindwa kulijibu swali hili kwa maana sifahamu ni hospitali gani.
‘Ni hospitali gani?’
‘Sio jukumu lako kumjibu subiri mutafika’
 
Baada ya muda tukafika hospitalini, bibi Jane Klopp akashuka huku akiwa kwenye kitanda hichi cha wagonjwa. Akapelekwa kwenye chumba cha mapumziko kwa muda huku nikijumuika naye. Baada ya muda kidogo akaja daktari aliye weza kutueleza juu ya eneo alipo Mery.
“Ethan hii ni hospitali yetu”
Bibi Jane Klopp alizugumza huku tukiwa tumeongozana na daktari huyu.
“Ahaa…hii ndio inayo simamiwa na dada Mery?”
“Ndio”
Tukafika nje ya mlango wa chumba cha upasuaji, tukamkuta mzee Klopp akiwa anazunguka zunguka tu. Akakumbatiana na mkewe, ila mimi hakushuhulika nami.
‘Usijali atakuwa salama’
Niliisikia sautu ya rafiki yangu huyu.
‘Una uhakika?’
‘Ndio’
Tukaendelea kusubiria zaidi ya masaa mawili. Mery akatolewa kwenye chumba cha upasuaji na kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ambacho kimeandikwa kwa lugha ya kijerumani intensivmedizin. 
 
“Ahaa wewe usiingie”
Mzee Klopp alizungumza huku akinizuia kuingia katika chumba hichi, jambo lililo mshangaza sana bi Jane Klopp. Sikutaka kuwa mbishi zaidi ya kukaa nje ya chumba hichi nikisubiria watoke katika chumba hicho. Baada ya muda kidogo wakatoka wakiwa wamejawa na sura za tabasamu kidogo.
“Anaendeleaje dada?”
“Yupo vizuri kiasi, madaktari wamesema kwamba watamlaza kwa siku chache kisha watamruhusu kurudi nyumbani?”
Bi Jane Klopp alinijibu kwa upole na unyenyekevu sana.
“Ameumia vibaya?”
“Hapana ni majeraha macheche, ila mguu wa kushoto ulivunjika mara mbili”
Mzee Klopp alinijibu kwa upole hadi mimi mwenyewe nikashangaa. 
 
    Siku zikazidi kusonga mbele huku hali ya Mery ikazidi kuimarika. Urafiki wangu na huyu rafiki yangu nisiye muona ambaye kwa haraka haraka ninaamini kwamba ni jini, zikazidi kusonga mbele. Siku ya kuanza masomo yangu rasmi kwenye shule ya msingi ya Berlin Metropolitan.
Nikaongozana na Bi Jane Klopp hadi kwenye shule hii na kutokana na umaarufu wa bibi huyu, waalimu waliweza kunifahamu kwa haraka sana.
“Ujitahidi mwanangu”
“Sawa bibi nitajitahidi”
“Kitu kingine hakikisha kwamba unakuwa na upendo na wezako, heshima na ukarimu kwa kia mtu. Pia jifunze kuwa na utamaduni wa kuwasaidia wezako pale anapo shindwa kwenye masomo”
“Sawa sawa mama”
“Nitakuwa ninakuja kukutembelea kila mwisho wa wiki ili kufahamu una endeleaje”
“Sawa mama”
 
Tukaagana na bi Jane Klopp, kisha nikabaki chini ya uangalizi wa mwalimu aliye weza kujitambulisha kwamba ni mwalimu wa michezo. Nikapelekwa bwenini, na kuingizwa kwenye chumba chenye viyanda viwili vya juu na chini.
“Kuna mwenzako mmoja amefika leo amachagua kitanda hichi, wewe utapenda kulala kitanda cha juu au chini?”
“Hichi hapa”
Nilichagua kitanda cha juu, kisha nikachagua kabati langu la kuhifadhia nguo na vitabu. Katika siku mbili hizi, waalimu na walezi wa wanafunzi walikuwa bize katika kuwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka maeneo mbali mbali ndani na nje ya nchi ya Ujerumani, katika wanafunzi wenye asili kutoka barani Afrika, hatuzidi kumi huku mimi ndio nikiwa Mtanzania pekee. Kitu nilicho weza kukigundua kwa haraka haraka kwa baadhi ya wanafunzi, ni wabaguzi wa rangi. Sisi wanafunzi weusi tunaonekana kama watu wa ajabu sana ambao hatuna thamani na uwezo wowote mbele yao.
 
‘Kwa nini wanatunyanyasa?’
Nimuuliza rafiki yangu huyu siku nikiwa nimekaa mwenyewe kwenye moja ya benchi la mapumziko, ambalo wanafunzi wengine wenye asili ya kizungu waliliacha kisa nimekaa mimi, kwa bahati mbaya sina rafiki zaidi ya yule ninaye lala naye chumba kimoja na yeye urafiki wetu ni usiku tu pale tunapo kuwa tumerudi kulala bwenini.
‘Unatakiwa kuhakikisha kwamba una wazidi kwa kila kitu’
‘Kwa kila kitu kivipi?’
‘Darasani hadi kwenye michezo’
‘Mmmm sasa masomo yenyewe ni magumu na wezangu wenyewe wana jibu maswali kuliko hata mimi’
‘Usijali huu ni mwanzo tu ila utafahamu kila kitu kinavyo kwenda’
 
Nikastuka baada ya kuguswa mgogoni, nikageuka nyuma nikakutana na kundi la watotoo wezangu kama sita hivi huku aliye nigusa ni kibonge na mrefu kwenda juu.
“Wewe mtu mweusi toka kwenye hili benchi”
Alizungumza kwa lugha ya Kijerumani huku akinitazama kwa sura inayo onyesha ana maanisha kwa kile anacho kizungumza.
“Hutusikii”
Kibonge alizungumza huku akinishika shati langu la shule, nikajaribu kukataa, ila kwa nguvu zake alizo nazo akanivuta kwa nguvu na kuniangusha chini. Wanafunzi wote katika hili eneo wakabaki wakishangaa tukio hili, machozi yakaanza kunilenga lenga, kwani Kibonge na wezake wote wananicheka huku wanafunzi wengine wasio na huruma nao wakinicheka.
 
“Watu weusi nyinyi ni masokwe tu”
Kibonge alizugumza huku akitoa ndizi kwenye mfuko wa suruali yake. Akaimenya kisha akanipiga na ganda la ndizi hiyo usoni mwangu, jambo lililo zidi kuongeza vicheko kwa watu wengi. Nikiwa katika hali ya simnzi na kujisikia vibaya, akasimama dada mmoja mdogo mdogo kama sisi mbele yangua, akanitazama kwa sura ya huruma kisha akanipa kitama cheupe kwa ajili ya kujifuta machozi. Kibonge akampokonya mtoto huyu wa kike kitambaa hichi kabla ya hata sijakipokea.
 
“Mrudishie kitambaa chake”
Mtoto huyu wa kike mwenye asili ya Kijerumani alizungumza kwa ukali kidogo na kuwafanya bonge na wezake kucheka cheka. Mtoto huyu wa kike akamzaba bonge kofi zito la shavuni na kuwafanya wezake kuguna. Bonge akanyanyuka kwa hasira kwenye kiti alicho kikalia, akataka kumpiga mtoto huyu, ila jamaa wawili walio valia suti nyeusi na miwani yeusi wakafika katika eneo hili na kumkinga mtoto huyu.
“Mrudishie kitambaa”
Jamaa mmoja alizungumza kwa ukali kidogo, taratibu bonge akarudisha kwa msichana huyu, kisha akanipatia mimia.
“Pole mwaya”
 
“Asante”
“Unaitwa nani?”
“Ethan Klopp”
“Ohoo ni jina zuri, baadae”
Msichana huyu baada ya kuzungumza hivyo akaondoka na walinzi wake hawa wawili jambo lililo nishangaza sana, kwa maana wanafunzi wote hatuna walinzi, inakuwaje yeye awe na walinzi. Kutokana sina sehemu yak ukaa, nikaamua kurudi zangu darasani ili kumalizia kipindi cha mwisho kabla ya kuruhusiwa kwenda kula kisha baada ya bapo tutaendelea na mambo mengine.
‘Mbona umeniacha nidhalilike kwa kina Bonge?’
Nilimuliza rafiki yangu kwa maana yeye ndio niliye mzoea kuzungumza naye mambo mengi sana’
‘Ulitaka nikufanye shujaa wa kupigana au?’
‘Ndio’
‘Umesahau uliyo ambiwa na mama yako juu ya kuishi na watu vizuri?’
 
Kabla sijamjibu, wanafunzi wengine wakaingia darasani, akiwemo bonge na kundi lake. Wakanitazama kwa muda huku wakionekana kuchukizwa nami. Mwalimu akaingia na kuanza kutufundisha somo la historia. Kwa mara ya kwanza na mimi leo nikaulizwa swali na mwalimu na nikalijibu kwa ufasaha. Wanafunzi wezangu wakaombwa na mwalimu wanipigie makofi, ila wakanipigia wachache na wengine wakaa kimya. Sikuona hatua yoyote ambayo mwalimu aliichukua kwa wale ambao hawajanipigia makofi, nikajua kwamba ubaguzi wa rangi haupo kwa wanafunzi wezangu tu kumbe hata kwa waalimu. 
 
Somu hili likaisha na tukatoka darasani na kuelekea kwenye holi kubwa la kupatia chakula. Kama kawaida, nikapanga foleni ya kwenda kuchukua chakula. Bonge na wezake wakafika na wakakaa mbele yangu kinguvu.
“Mumenikuta lakini”
Niliwaambia kwa lugha ya Kijerumani. Bonge akanigeukia, kitendo cha kunitazamana tu, nikajikuta nikiwa nipo kimya kutokana na kumuogopa. Nikasubiria bonge na wezake wachukua chakula kisha ikafwata zamu yangu ya kuchukua.
“Leo lazima utakoma”
Bonge alizungumza huku akinipiga kikumbo kidogo, bado nusu niagushe chakula changu ambacho ni wali na kuku. Nikaangaza angaza kwenye kila meza, nikaoga meza moja ikiwa ina jamaa mmoja mkubwa kidogo, taratibu nikaisogelea kisha nikaka kwenye kiti, jamaa huyu akanitazama kwa mcho makali, hadi nikatamani kuhamia katika meza nyingine.
“Dogo hujaona wa kukaa nao?”
 
“Ehee?”
“Hujaona wa kukaa nao?”
Taratibu nikanyanyuka na sahani yangu, nikaangaza maeneo mengine, nikaona meza moja wakinyanyuka kundi la wavulana wakubwa, nikafika katika meza hiyo waliyo ichafua kwa kumwaga mwaga chakula, kisha nikaa na kuanza kula.
‘Nachukia haya maisha ni bora niache shule tu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
‘Kwa nini?’
‘Nitaishije hivi kwa kunyanyaswa siku zote?’
‘Wata kuheshimu siku moja, piga moyo konde na pambana’
‘Nipambane vipi sasa, ikiwa kila mmoja ananichukia’
‘Si kwa yule aliye kupatia kitambaa chake’
‘Yule kwani ni nani?’
 
‘Ni mjukuu wa kwanza wa raisi wa hii nchi’
‘Kwa hiyo ni mjukuu wa raisi’
‘Ndio’
‘Sasa kwa nini amesoma shule hii?’
‘Hivi unahisi kwamba shule hii ni ndogo, hadi wewe kusoma hapa tambua kwamba una bahati kubwa sana, na acha kujidharau, chukulia haya maisha ambayo unaishi hapa ni ya kawaida, pambana katika masomo’
‘Mbona umekuwa ni mtu wa kunishauri tu, ila hunisaidi kwenye shida’
‘Ethan kumbuka kwamba mimi sio mtu’
‘Ni nani sasa, ikiwa tunazungumza na wewe unanisikia’
‘Muda na wakati ukifika basi utanifahamu, baade nina mambo ya kushuhulikia’
 
‘Wewe…..wewe…..’
Nilijitahidi kumuita ila hakuitika. Nikamaliza kula na nikaacha chombo changu hapa hapa juu ya meza kama utaratibu wa kawaida, kwani kuna wafanyakazia maalumu hushuhulika katika swala la kuosha vyombo, nikarudi bwenini, nikavua nguo zangu, nikajifunga taulo na kueleka katika bafu ambalo tunatumia wanafunzi wa darasa la kwanza kwenye bweni hili. Nikavua taulo langu na kulitundika kwenye msumari, nikajifunga taulo langu kisha taratibu nikaanza kuoga, nikiwa nimejipaka mapovu mwili mzima, akaingia bonge na kundi lake na wakaanza kunicheka huku wakizunguka jambo lililo sababisha nijawe na woga mwingi sana.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )