Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, October 23, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 16

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

Ndani ya lisaa moja mameneja kumi na mbili pamoja na wanasheria wawili wakafika nyumbani humu, huku kila mmoja akishangazwa na wito wangu, kwani haukuwa ni wito wa kubembeleza zaidi ya kuwa wito wa kuamrisha.
“Kijana mdogo inakuwaje unatuita kwa kutuamrisha?”
Mzee mmojaa alizungumza kwa kufoka huku wakiwa wamekaa sebleni hapa.
“Mzee kabla sijamaliza kuzungumza nilicho waitia kuanzia hivi sasa huna kazi”
Maneno yangu yakawafanya watu wote kustuka sana, hata dada Mery mwenyewe akaonekana kustushwa kwani maamuzi yangu hakuna hata mmoja aliye yataarajia kwamba nitayatoa hivyo.
   
ENDELEA
“Sina kazi, wewe ni nani ambaye unanisimamisha kazi”
Mzee huyo alizungumza kwa ukali sana huku akinitazama usoni mwangu. Mwanasheria wa familia akasimama.
“Samahani kwa kuweza kuwaingilia katika hili, ila nina jambo ninaomba niweze kulizungumza na kuliweka sawa kwenu nyote.”
Mwanasheria akafungua brufcase yake na kutoa faili moja jeusi.
“Hili hii faili jeusi, nina amini nyinyi nyote humu ndani munaweza kutambua na kuelewa ni kitu kinacho husiana na faili hili. Huyu ni Ethan Klopp, ni mtoto wa mwisho wa mzee Ethan. Mikaka miwii iliyo pita kabla ya tarehe ya leo mzee Klopp aliweza kuniita ofisini kwake na kunipa hii fomu hapa ambayo ni nguvu ya urithi”
 
“Mzee Klopp kwa akili zake yeye mwenyewe na ufahamu wake yeye mwenyewe pasipo kulazimishwa na mtu wa aina yoyote, aliweza kuacha urithi huu kwa kijana huyu Ethan Klopp. Urithi huu unampa Ethana nguvu ya kumiliki kila mali ambayo mzee Klopp ana miliki. Makapuni na majumba yote yapo chini ya Ethan. Hivyo naomba muweze kumsikiliza kijana huyu”
Mwanasheria mara baada ya kumaliza kuzungumza na kukaa chini. Mwanasheria wa makapuni yote naye akasimama. 
“Kama alivyo tangulia kuzungumza mwenzangu, hata kwa upande wangu huku nami niliweza kuachiwa fomu ya urithi inayo muonyesha Ethan Klopp ndio mrithi wa kila mali ya mzee. Asanteni”
Mwanasheria huyo mara baada ya kuzungumza hivyo akakaa chini na kuwafanya wazee hawa hususani aliye kuwa muongeaji sana kukaa kimya huku akiwa mnyonge kabisa.
“Nimewaita hapa kutoka nahitaji kuwapa taarifa mbaya.”
Wazee wote wakanitolea macho wakionekana kustuka.
 
“Dada Mery naomba ukamuite dokta Alfonce”
“Sawa”
Dada Mery akasimama na kupandisha gorofani, baada ya dakika kama mbili havi wakarudi huku wakiwa wameongozana na daktari. Daktari Alfonce akawasalimia viongozi hawa”
“Naomba uje hapa dokta”
Nilizungumza kwa ukakamavu hadi mimi mwenyewe nikajishangaa, kwa umri wangu huu, inakuwaje ninakuwa jasiri sana.
“Dokta naomba uzungumze nao kile kinacho endelea”
“Asante Ethan”
Daktari akakohoa kidogo kisha akanitazama usoni mwangu, kwa ishara ya macho nikamuomba aweze kuzungumza kile ambacho kinaendelea.
“Mzee Joradan Klopp amefariki dunia”
Watu wote humu ndani wakastuka huku wakinitazama usoni mwangu.
“Mzee Klopp alikuwa akisumbuliwa na saratani ya damu, amefariki jioni hii. Mukiwa kama watu wa karibu kabisa na hii familia tumeona ni vyema tuweze kuwapa taarifa awali kabisa kanbla taarifa hii haijatoka kwenye vyombo vya habari. Yangu ni hayo”
 
Baada ya daktari kuzungumza hivyo akaka kwenye sofa.
“Taarifa hii ni nzito kwa kila mmoja wetu. Tunacho hitaji ni ushirikiano wenu. Kwa upande wangu nimemaliza. Dada Mery una lolote la kuzungumza?”
Dada Mery akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hana chochote cha kuzungumza.
“Daktaria ninaomba uandae utaratibu wa watu kwenda kumuona mzee kabla hatujakwenda kumuhifadhi hospitalini mwili wake”
“Sawa”
Nilipo maliza kuzungumza nikatoka nje ya nyumba hii. Nikaelekea kwenye moja ya bustani na kuanza kulia kwa uchungu sana kwa maana nimepewa jukumu moja zito nikiwa bado nina umri mdogo sana.
“Ethan”
Niliisikia sauti ya dada Mery nyuma yangu, nikegeuka na kumtazama.
 
“Ethan nahitaji kuzungumza na wewe kama itawezekana”
Nikajifuta machozi kisha nimkubalia kwa kutingisha kichwa.
“Pole kwa majukumu ambayo baba amekubebesha, natambua swala zima la kusimamia mali zake ni jambo gumu na zito na isitoshe kwamba una umri mdogo”
“Asante, ila dada wewe ndio msaada wangu mkubwa sana kwenye hili swala. Peke yangu siwezi, peke yangu nahisi nitashindwa”
Nilizungumza huku machozi yakitumwagika sote wawili. Tukakumbatiana kwa nguvu huku, baada ya muda kidogo tukaachiana mara baada ya kumuona mwanasheria wa familia akitufwata hapa tulipo simama.
“Samahani kwa kuwasumbua”
“Bila samahani”
“Je ninaweza kuwaita waandishi wa habari ili waweze kuitoa taarifa hii”
“Ndio”
“Sawa sawa”
Mwanasheria akaondoka na kutuacha wenyewe.
“Ethan kuna mtu unapaswa kumpa habari kabla ya yeye kuweza kuisikia kwenye vyombo vya habari”
“Nani?”
“Camila”
“Naomba unisaidie simu yako”
Nilizungumza kwa unyonge.
“Sijui hata nimeiacha wapi”
 
“Ngoja nikatumie simu ya ndani”
Nikaelekea ndani, nikachukua simu ya sebleni na kupiga namba ya shuleni kwa Camila. Simu yake ikapolewa na sekretari wa shule hiyo, nikajitambulisha na kutokana si mara yangu ya kwanza kupiga simu, nikakubaliwa kuongea na Camila na nikaombwa nisubiri kidogo ili aweze kwenda kuitwa.
“Ethan mama ameamka”
Daktari alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Sawa nina kuja kumuona”
“Sawa”
“Ethan”
Niliisikia sauti ya Camila akizungumza kwa furaha.
“Mambo”
“Poa mpenzi wangu, mbona unazungumza kwa unyonge hivyo kuna tatizo?”
“Ndio mpenzi wangu”
“Tatizo gani tena mpenzi wangu?”
“Baba amefariki”
“Nini!!?”
Camila aliniuliza kwa mstuko mkubwa sana.
“Ndio amefariki kama lisaa moja na nusu hivi “
“Ohoo Mungu wangu”
Camila alianza kulia taratibu.
“Amekufaje?”
 
“Ninakuomba uzungumze na mama na chukuru ruhusa uje huku”
“Sawa mume wangu, ninakuja sasa hivi”
“Sawa”
Nikakata simu, nikirudisha sehemu nilipo itoa kisha nikaelekea chumbani, nikamkuta bibi Jane Klopp akiwa amekaa pembeni ya mwili wa mume wake huku akiendelea kulia. Taratibu nikamsogelea na kulaza kichwa chake kwenye bega langu.
“Mama”
“Ethan bora ningeenda na mume wangu, kwa nini ameniacha peke yangu ehee?”
Mama alizungumza kwa uchungu sana, sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumbembeleza. Mwanasheria akasimama mlangoni na kwa ishara akaniita.
“Mama nina kuja”
“Sawa”
Nikamuachia mama na nikamfwata mwanasheria wa familia.
“Waandishi wa habari wamesha fika”
“Umewaandalia sehemu ya kuzungumza nao”
“Ndio”
“Ninakuja”
“Sawa sawa”
Nikarudi sehemu alipo mama. Nikamshika mikono yake huku nikimtazama usoni mwake.
 
“Mama”
“Mmmm”
“Ninakwenda kuzungumza na waandishi wa habari”
“Sawa naomba ujikaze mwanangu”
“Sawa mama”
Nikamtazama daktari aliye kaa kwenbye moja ya sofa humu ndani.
“Nakuomba umtazame mama”
“Sawa sawa”
Nikatoka ndani humu na kuongozana na mwana sheria hadi kwenye moja ya bustani. Nikawakuta wana habari wengi wakiwa wamekusanyika huku wakiwa wamebeba kamera za kurekodi na kupiga picha za kila tukio ambalo linaendelea katika eneo hili. Nikamuona dada Mery akiwa amesimama mbali kidogo na hapa tulipo, nikamfwata na kusimama naye.
“Unahitaji kuonekana na wewe kwenye hii taarifa”
“Hapana Ethan nina shindwa kufanya hivyo”
“Kwa nini?”
“Nenda tu Ethan”
Dada Mery alizungumza huku machozi yakimtiririka usoni mwake. Nikaruidi eneo walipo waandishi wa habari na kusimama katika sehemu niliyoa ndaliwa kusimama. Nikawatazama waandishi hawa wa habari, nikatazama saa yangu ya mkononi na kuona ina nionyesha sasa hivi ni saa moja usiku.
 
“Habari zenu”
“Salama”
“Kwa wale wasio nifahamu ninaitwa Ethan Klopp. Nina habari ambayo sio nzuri kwa familia na hata wapenzi wa soka”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Masaa mawili yaliyo pita, baba yetu mzee Klopp ametutoka duniani”
Waandishi wa habari nao wakaonekana kustuka kidogo huku kila mmoja akiweka sawa kamera yake.
“Nilikuwa shule, nikarudishwa nyumba, ila kwa bahati mbaya nilimkuta mzee akiwa katika hatua za mwisho kabsisa za maisha yake”
Nikakaa kimya huku nikijifuta machozi usoni mwangu. Waandishi wa habari wakaanza kunyoosha mikono juu ili kunihoji maswali, ila nikashindwa kumjibu yoyote kwani hali ninayo isikia sio nzuri kabisa. Nikaondoka na kumuacha mwanasheria wa familia akizungumza. Nikaingia ndani. Daktari akainiita kwa ishara na nikamfwata pale alipo.
 
“Ndio”
“Mwili wa marehemu unatakiwa kwenda kuhifadhiwa sasa, sindano tuliyo mchoma nguvu yake itaisha mara baada ya muda mchache kuanzia hivi sasa”
“Sawa gari la wagonjwa si lipo tayari?”
“Ndio hata gari za polisi zimesha fika katika eneo hili”
“Sawa munaweza kuupeleka tu hospitali”
Maandalizia ya kuutoa mwili wa mzee Klopp yaakaanza kufanyika, huku kwenye televishion taarifa zinazo samba zinahusiana na kifo cha mzee Klopp, ikiwa ni pigo kubwa kwa taifa la Ujerumani hususani kwenye tathini ya michezo, kwani mzee Klopp aliichezea timu ya taifa ya nchi hii miaka kadhaa ya nyuma iliyo pita. Waziri mkuu akatangaza msiba huu ni msiba wa taifa, na bendera ya taifa ikashushwa nusu mlingoti. Camila na mama yake wakafika nyumbani hapa majira ya saa tatu usiku. Camila moja kwa moja akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu huku akimwagikwa na mchozi usoni mwake.
“Kweli baba amekufa?”
“Ndio”
“Ethan pole sana mwanangu”
Mama Camila alizungumza huku akitukumbatia wote wawili.
“Asante sana mama”
Nilizungumza huku nikiendelea kulia kwa uchungu. Watu washuhuri na wafanya biashara kutoka maeneo mbali mbali wakafika katika jumba hili la mzee Ethan na ulinzi ukazidi kuimarishwa.
 
‘Ethan’
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu katika ufahamu wangu wa akili.
‘Vipi?’
Nilimjibu kimoyo moyo pasipo watu wengine kuweza kufahamu ni nini ninacho kizungumza.
‘Kuna watu wana mpango wa kukuua usiku huu, kuwa makini la sivyo jua la asubuhi huto weza kuliona’
Maneno ya Ethan yakanistua sana kwani watu walio fika nyumbani hapa ni wengi sana hadi sujui nani ni mzuri au nani ni mbaya, jambo lililo anza kunipa wasiwasi moyoni mwangu.

==>>ITAENDELEA KESHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )