Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 25, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 18

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

“Kila mmoja aweke mikono yake juu ya meza”
Wote wakatii amri hadi mwanaume ambaye naye anahusika na mpango huu wa kumteka dada Mery na kuhitaji kuchukua mali kiurahisi. Nikaanza kuwapiga fimbo za mikono kwa kutumia fimbo hii ambayo imetengezwa kwa chuma. Mamenaja hawa wakazidi kulia kwa uchungu sana ila hapakuwa na hata mmoja wao ambaye alithubutu kufanya ujinga wa kunishambulia kwani kilicho tokea kwa mchungaji feki kila mmoja amekishuhudia, kwani ni jambo ambalo binadamu wa kawaida hawezi kulifanya na tukio kama hilo nahisi walisha liona kwenye baadhi ya filamu za Kimarekani kama Spider Men.
       
ENDELEA
“Ni nani aliye mteka dada yangu”
“Ni yule kule mkuu”
Menjea mmoja alizungumza huku machozi yakimwagika kama mtoto mdogo. Nikamtazama mchungaji aliye mnyooshea mkono, kwa haraka nikamfwata mchungaji huyu na kumnyanyua kwa mkono mmoja hadi wote wakashangaa, kwani kwa umri wangu, sina nguvu ya kunyanyua mwanaume kama huyu.
Nikamkalisha mchungaji juu ya kiti chake huku akionekana kuona mawenge mawenge. Nikaanza kumpapasa kwenye suruali yaka na nikatoa simu, nikaiweka mezani huku nikimtazama usoni mwake.
“Wapigie vijana wako wamrudishe dada yangu ndani ya dakika kumi, la sivyo nitavuja kichwa chako na weka loud speaker”
Mchungaji huku akitetemeka mwili mzima, akaichukua simu yake na kuanza kuiminya minya. Akataka kuiweka sikioni mwake, ila kwa ishara nikamuamrisha kuiweka mezani, ila hata anacho kizungumza watu wote waweze kukielewa.
“Ndio boss”
“Mark mrudisheni huyo binti sasa hivi”
“Boss”
“Nimesema mrudisheni sasa hivi sihitaji maswali pumbavu wewe”
“Nahitaji kungumza na Mery nijue yupo salama”
“Wewe ni nani?”
“Acha kuuliza, fanya ulicho ulizwa”
“Ethan”
“Ndio dada yangu upo salama”
“Ndio, ila naona wanageuza gari sijui wanaelekea wapi?”
“Wanakurudisha nyumbani, ikitokea mtu akakushika hata ziwa lako niambie itamgarimu”
“Sawa Ethan”
Nikaichukua simu hiyo na kuikata, kisha nikaibwaga mezani.
“Kuna jambo moja nahitaji niliweke wazi kwenu. Mimi sio mjinga na musijidanganye mukahisi mali hizi nilizo achiwa siwezi kuziongoza, ninaweza tena mara kumi ya hata sasa hivi kwa maana mzee alisha niandaa kuwa kiongozi toka nikiwa nia miaka saba, sijui tunaelewana”
 
“Ndio Boss”
Waliitikiwa kwa unyonge huku wengine wakijipangusa macho kwenye mashavu yao.
“Leo nitawaandishika mkataba wa kifo.”
Wote macho yakawatoka huku wakinitazama kwa umakini.
“Mkataba huu, yoyote atakaye kiuka masharti, basi kama mkataba unavyo sema. Basi adhabu yake ni kifo cha aina yoyote ambacho siku hiyo nitaamua kumpatia sijui tumeelewana?”
“Ndio mkuu”
Waliitikia huku wakilia kwa uchungu sana. Nikafungua mlango wa kutokea ukumbinu humu, nikamuita mwanasheria kwa iashara.
“Ndio”
“Unaweza kuniandalia mikataba muhimu”
“Sasa hivi?”
“Ndio”
“Ngoja nikachukue laptop”
“Fanya hivyo”
Mwanasheria akaondoka kisha nami nikarudi kwenye kiti changu.
 
“Haya yaliyo tokea humu, endapo nitayasikia nje ya hapa basi sinto muacha hata mmoja wenu hai, sinto jali ni wewe, au wewe, au wewe ambaye ulitoa siri. Akifa samaki mmoja basi ni wote wanakufa”
Maneno yangu yakazidi kuwaogopesha mameneja hawa, baada ya muda mwanasheria akarudi huku akiwa ameongozana na dada yangu Mery.
Wote wakaonekanekana kujawa na mshangao kwa maana watu waliomo humu ndani sura zao zimejawa na huzuni kubwa kuliko hata sisi wenye msiba wetu. Nikanyanyuka na kumfwata Mery sehemu alipo simama, nikakumkumbatia kwa nguvu huku kichwa chake akikilza begani mwangu.
“Pole saana dada yangu”
Nilizungumze huku nikiendelea kumkumbatia kwa nguvu.
“Asante. Ethan ni nini kinacho endelea?”
“Tutuzungumza baade, naomba ukakae chumbani pamoja na mama”
“Ethan naogopa”
“Usijali dada yangu, kila kitu kitakwend vizuri, sawa”
“Sawa, alafu yule mchungaji pale ndio mwenye vijana wake walio niteka”
 
Dada Mery alizungumza kwa sauti ya kuninong’oneza huku akinitazama usoni mwangu.
“Usijali nitalishuhulikia, wewe fanya kama nilivyo kuambia dada yangu”
“Sawa, ila inabidi tuwafahamishe askari kwa maana yule mchungaji sio mtu mzuri kabisa”
“Hakuna haja”
“Kwa nini?”
“Kila kitu niachie mimi”
Dada Mery akanikazia macho huku aki akinitazama usoni mwangu.
 
“Sawa”
Dada Mery akamtazama mchungaji kwa jicho kali kisha akatoka ndani humu, nikaufunga mlango kwa ndani na kurudi kwenye kiti changu nilicho kuwa nimekaa.
“Samahani mwana sheria kwa kukusumbua”
“Bila samahani mkuu”
“Nahitaji uandike mkata utao sainiwa na kila mtu humu ndani ya hichi chumba. Mkataba huo ni wa mwaka mmoja katika kuiongoza kampuni anayo iongoza. Masharti ya mkabata huo, nahitaji hadi inafika tarehe ya kama leo na mwezi kama wa leo, mwaka ujao, kila mmoja kwenye kampuni yake awe ameingiza mapato mara mbili ya mapato anayo ingiza hivi sasa hivi. Kwa yoyote atakaye shindwa, adhabu yake ni KIFO”
 
Mwanasheria macho yakamtoka huku akionekana ni jambo jipya kwa yeye kulisikia.
“Ethan pasipo kukuvunjia heshima, ila hili swala halipo katika sheria yoyote hapa nchini Ujerumani”
Mwanasheria alizungumza huku akinitazama, mameneja wote pamoja na mchungaji na mwezake wamekaa kimya kwani wanatambua ni kitu gani nilicho wafanya.
“Hiyo ni sheria yangu na mali zangu. Unatambu kwamba huyo mchungaji leo alihitaji kuniua na ndio aliye mteka Mery”
“Mery alitekwa….!!?”
“Ndio na mchungaji ndio mtekaji, huyo jamaa mwenye manywele yake, naye ni mshawishi kwa hawa wajinga sita hapa ili kila mmoja ajimilikishe kampuni anayo iongoza.”
Maneno yangu yakazidi kumshangaza mwana sheria pamoja na hawa watu wengine kwa maana nina hisi kitu wanacho jiuliza sana, nimejuaje juu ya mipango yao ya siri.
“Ninajua kila mpango wenu na ninajua munacho kifikiria juu ya kutoka hapa. Sasa ole wake mtu yoyote afanye ubadhilifu hawa wa dola moja ndani ya kampuni, mkataba wako utaisha siku ambayo utaonana na mimi nikiwa katika sura nyingine”
“Kwa aliye iba pesa za kampuni na kuhamishia pesa Uingereza, Uswiz, na sehemu nyingine duniani. Nahitaji hadi inatimia saa moja asubuhi pesa muwe mumezirudisha kwenye akaunti za viwanda.”
Baada ya kumaliza kuwapa mameneja maagizo yangu, nikamgeukia mchungaji na mwenzake.
“Wewe una jishuhulisha na kitu gani?”
“Ni…ni ni muuzaji wa magari kwa nchi za Asia na Afrika”
“Nahitaji asilimia sabini ya hisa zako za kampuni yako kabla ya saa moja asubuhi, ila kama huitaji nilicho mfanya mchungaji ni mara mbili na kile nitakacho kufanya wewe”
“Asilimia sabini?”
“Ndio au nimezungumza kilugha.”
“Samahani mkuu”
“Mchungaji una miliki nini, ole wako unidanganye?”
“Nina kasino moja lipo Munich, nina hotel ipo London na nina kanisa lina matawi mia moja na hamsini ndani na nje ya Ujerumani”
“Nahitaji asilimia sabini ya kipato kitokanacho na makanisa yako yote kingie katika mashirika ya kusaidia watoto yatima barani Afrika hususani Tanzania”
“Sawa mkuu”
“Tena, mwanasheria utanisaidia kufungua shirika ambalo nitaliita Ethna Childrean Foundation”
“Sawa sawa”
 
“Pesa yote ingiza kwenye shirika nitakalo lifungua, sijui umenielewa?”
“Nimekuelewa mkuu”
“Mwanasheria kufungua shirika inachukua muda gani?”
“Kama wiki hivi mkuu, kwani tutafwata sheria zote za kiserika na kutokana ni shirika ambalo ni la msaada kwa mataifa yote duniani, ndio maana litachukua muda hivyo”
“Nashukuru”
Nikajilaza vizuri kwenye kiti changu hichi cha kuzunguka huku nikiwatazama watu wote humu ndani.
‘Hii ndio nguvu niliyo kuwa nikikueleza toka ulivyo kuwa mtoto’
‘Kweli nime iona hiyo nguvu’
‘Kwa umri wako ila wana kuogopa kuliko hata simba’
‘Hivi kweli hawato nisaliti?’
‘Kwa sasa hakuna ambaye ata kusaliti. Wameshika adabu yao’
‘Hahaaa, ila nashukuru sana msaada wako’
Nilizungumza kimoyo moyo na hakuna hata mmoja ambaye anasikia mazungumzao yangu mimi na Ethan’
‘Usijali ni jukumu langu na niliweka ahadi toka usiku ule ulivyo weza kutupwa mtoni’
 
‘Ehee nimekumbuka’
‘Umekumbuka nini?’
‘Ni kina nani walio nitupa mtoni na ilikuwaje?’
‘Usijali, nitakuelea kila jambo pale nitakapo pata muda’
‘Leo huwezi nieleza?’
‘Maliza kwanza kitu kimoja, ndio ufwate jambo jengine.’
‘Sawa sawa’
“Nimemaliza mkuu”
Mwanasheria alizungumza huku akinyanyuka kweye kiti chake. Akabeba laptop yake hadi kwenye mashine ya kutolea kopi, akatoa kopi ya karatasi kadhaa kisha akaanza kuzitandaza mezani kwa kila mmoja. Akanikabidhi na mimi karatasi moja. Nikaisoma, kila nilicho muhitaji aandike amekifanya kama vile ninavyo hitaji.
 
“Mikataba yetu, inaeleweka na inasomeka vizuri na muna saini tukiwa na mwana sheria wa kampuni zote. Haya sasa kazi kwenu, muna kalamu au tuwa azime”
“Mimi ninayo”
Mzee mmoja alizungumza huku akito kalamu kwenye mfuko wake wa koti. Akasaini sehemu anayo takiwa kusaini, inayo mpa kiapo kwamba amekubaliana na masharti ya mkataba wangu. Baada ya kila mtu kutia saini ya mkataba, mwanasheria akaikusanya na kunipatia. Nikaanza kuupitia mkabata mmoja baada ya mwengine huku nami nikitia saini kama mtoaji masharti hayo.
“Naona tumemaliza na asanteni sana baba zangu na babu zangu. Niwatakie usiku mwema”
Nilizunugmza huku nikimkabidhi mwana sheria kalamu ambayo aliitoa meneja mmoja.
 
‘Ethan kalamu hiyo ina ushahidi wa kila kitu milicho kizungumza’
‘Kalamu gani?’
‘Hiyo muliyo saini’
Nikageuka nyuma na kumuona mwana sheria akimkabidhi meneja huyo kalamu hiyo na taratibu mzee akaaweka katika mfuko wake wa suti, huku sura yake kidogo ikonyesha kuwa na furaha. Nikarudi hadi katika kiti alicho kaa, akanitazama kwa wasiwasi, nikamnyooshea mkono huku nikimtazama usoni mwake.
“Nini mkuu?”
“Kalamu”
Mzee huyu nikamuona jinsi anavyo babaika, wasiwasi mwingi ukamjaa na kujikuta akinisukuma na kuanza kukimbilia mlangoni, kwa kasi ambayo hata mimi mwenyewe sifahamu nimeitolea wapi nikajikuta nikiwa nimesimama mlangoni huku nikimsubiria kufika hapa mlangoni. Nikamshika mzee huyu shingoni mwake na kumnyanyua juu kwa mkono mmoja hadi mimi mwenyewe nikajishangaa hii nguvu niliyo nayo.
 
“Naomba kalamu”
Meneja huyu akatoa kalamu na kunikabidhi mkononi mwangu huku mwili mzima ukimtetemeka.
‘Ethan huyu amenisaliti nimfanyaje?’
‘Mrushie kwenye meza kule’
Nikamrusha mzee huyu hadi mezani ambapo ni mita kama ishirini kutoka hadi hapa nilipo simama. Watu wote wakaka kimya wakimshuhudia mwenzo jinsi anavyo angukia katika viti. Nikashusha pumzi taratibu huku nikiminya kalamu hii katika eneo la kifuniko, mazungumzo niliyo kuwa nikiyazungumza ndani humu yote yakaanza kusikia kwa kila mtu.
 
“Yoyote mwenye ujinga kama huu, labda umeurekodi kwenye simu yako. Toa simu yako sasa hivi na ufute kile kitu mbele yangu. Mameneja na mchungaji wakaanza kutazamana.
‘Hakuna aliye fanya hivyo’
‘Kweli Ethan?’
‘Niamini mimi’
NIkamuona meneja akijitahidi kunyanyuka kwenye viti hivyo alivyo vivunja.
“Nenda kamsaidieni mwenzenu”
Nilizungumza kisha nikafungua mlango na nikatoka ndani humu, huku mwanasheria akinifwata kwa nyuma kwa mwendo wa haraka.
“Ethan”
“Naam”
“Hembu niambie ni wewe au ni macho yangu yaliona vibaya kitu ulicho kifanya”
Nikasimama na kumgeukia mwana sheria.
“Ulicho kiona ndani ya ofisi nahitaji kibaki ndani ya ofisi. Umenielewa?”
“Sawa sawa mkuu”
Tukarudi katika jumba ambalo watu mbalimbal wamakusanyika na wapo kwa ajili ya kutupatia pole kwa msiba ulio tupata.
“Ethan”
Muandishi wa habari wa BBC aliniita, nikakumbuka ahadi niliyo mpatia, nikasimama na akanifwata nilipo.
“Samahani naona nusu saa nililo kuahidi lilipita dada yangu”
“Usijali, sijui tunaweza kufanya mahujiano?”
“Ndio tunaweza, kutoka nilikuahidi inabidi nitimize ahadi yangu niliyo kuambia”
 
“Nashukuru kusikia hivyo. Tunaweza kutoka nje na kuelekea katika gari letu la kurusha matangazo”
“Sawa”
Nikaongozana na dada huyu hadi kwenye gari lao kubwa la kurusha matangazo. Vijana wake wakasha kamera, akachukua maiki yake, akajiweka vizuri kwenye zake. Kamera man, akaanza kuhesabu vidole vyake kuanzia moja hadi tatu.
“Habari za muda huu watazamaji wa BBC, tupo katika nyumba ya mzee Klopp, mchezaji wa zamani wa nchi ya Ujerumani na timu ya B. Dotmund. Hapa nipo na mwanaye wa kiume, Ethan Klopp atatuelezea ni kitu gani kilicho tokea hadi baba yake mzaza akapoteza maisha. Karibu sana”
 
Kabla sijalijibu swali la muandishi wa habari huyu, nikashuhudia gari la wagonjwa likisimamishwa kwa haraka aneo la mbele la nyumba hii. Wauguzi wakashuka kwa haraka kwenye gari hilo huku wakiwa na kitanda cha kusukuma na kukimbilia ndani ya nyumba hii. Wasiwasi mwingi ukanijaa moyoni mwangu, makamera man wakageuzia kamera zao katika eneo lilipo gari hilo la wagonjwa. Nikaanza kutembea kueleka katika eneo hilo la gari huku nikifwata kwa nyuma na waandishi hao wa habari. Kabla sijalifikia gari hili nikawaona wauguzi wakitoka ndani humu huku juu ya kitanda wakiwa wamemlaza bibi Jane Klopp huku akihemea pumzi ya oksijeni jambo lililo nistusha sana kwani sifahamu ni kitu gani ambacho kimempata mama yangu, bi Jane Klopp.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )