Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, October 25, 2018

TAKUKURU Kuchukua Harbinder Sethi Mahakamani

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumchukua mshtakiwa Harbinder Sethi ili ikamilishe kuchukuliwa maelezo yake.

Ombi hilo limetolewa leo saa 3:03 asubuhi na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huduma Shaidi.

Kabla ya kueleza hayo, Wakili Swai alidai kesi hiyo ilipangwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Swai aliitaarifu Mahakama kuwa wachunguzi wa Takukuru wataenda kumchukua Sethi gerezani kwa ajili ya kumuhoji.

Kwa upande wa wakili wa utetezi, Dorah Mallaba aliieleza Mahakama kuwa Sethi wakati akichukuliwa maelezo wakili wake lazima awepo.

Hata hivyo, mawakili wa utetezi, Mallaba na Paschal Kamala waliusisitiza upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo mapema na kwa wakati.

Baada ya mawakili hao  kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )