Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, October 18, 2018

Wema Sepetu akana kuchepuka na mume wa Irene Uwoya

Wema Sepetu amekanusha vikali tetezi ambazo ziliibuliwa na mwanadada wa mitandaoni Mange Kimambi kwamba kuna siku alichepuka na Dogo Janja ambaye ni mume wa ndoa wa Irene Uwoya.

Mange ambaye amekuwa akilumbana kwenye mitandao ya kijamii na Wema Sepetu, siku ya jana alipost chart mtandaoni akionyesha kuzungumza na Dogo Janja kuhusiana na tetesi hizo.

Hata hivyo aliufuta ujumbe huo muda mchache huku watu wengi mtandaoni wakidai kwamba taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

Baada ya kuibua tetesi hizo, Wema ambaye siku ya jana alimtangaza mpenzi wake mpya, amedai sio kweli kwamba anatoka kimapenzi na mpenzi huyo wa Irene Umoya.

“Pale unapoona mtu anakuongelea vitu visivyo make sense ili mradi tu… Mi Arusha nimeenda Lini…??? Na Huyo Dogo nimekaa nae WAPI…???? Hata mazoea nae sina…!!!Ila Dada anakuwaga na stress za ajabu sometimes… Kimambi… Utaniacha lini nipumue in Peace…!??? You are Obsessed wallahy,” aliandika Wema Sepetu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )