Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 28, 2018

Zitto Kabwe Awataka Wananchi Waendelee Kukemea Matukio ya Utekaji

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewataka wananchi kutokaa kimya yanapotokea matukio ya utekaji nchini Tanzania, akibainisha kuwa kukemea kunasaidia ukweli kujulikana na hata wahusika kupatikana.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari unaofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Kijitonyama, Dar es Salaam.

Amesema Watanzania kupaza sauti baada ya kutekwa na kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ kumeonyesha jinsi walivyoanza kuchoshwa na vitendo hivyo.

“Haya tumekuwa tukiyasema ndani na nje ya Bunge na tutaendelea kusisitiza kwa sababu tunafahamu umuhimu wa vyombo hivi (vya Serikali). Kama wapo wachache wanaochafua taswira ya vyombo hivi ni lazima tuseme,” amesema Zitto.

“Kama vyombo hivi haviambiwi sisi ni lazima tuseme, hatua zichukuliwe kwa matukio ya awali.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )