Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 2, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 134 na 135 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

Ndani ya muda alio niambia dereva tukawa tumefika katika hoteli moja kubwa, nikakuta mlolongo wa vijana wakike na wakiume wakiwa wamepanga mistari kwa ajili ya kwenda kujisajili katika mashindano haya ya kutafuta wana mitindo, na mimi nikapanga mstari nikiwa ni mshirikia wa elfu moja na mia mbili. Muda ukazidi kwenda na foleni ikazidi kosogea, vijana walipo katika eneo hili wapo wengi wamependeza, nikajitazama mweyewe nilivyo vaa na kimoyo moyo nikajishauri na kujiambia kwamba nina vigezo vya kuweza kushinda katika shindano hili.
   
ENDELEA       
Vijana wengi walio ingia katika chumba cha usahili wengi walitoka wakiwa katika hali ya huzuni, huku wengine wakilalamika kwamba majaji wanaringa. Hali hii ikaanza kunitisha kwani kazi yangu iliyo nileta hapa ni kuhakikisha kwamba ninakuwa karibu na Yemi Okocha. Ikafika zamu yangu, na mimi nikaingia katika chumba cha ushahili, nikakuta majaji wanne watatu wakiwa wa kiume na mmoja akiwa ndio Yemi mwenyewe niliye weza kumuona kwenye picha niliyo onyesha kipindi nilipokuwa kwenye kambi ya jeshi ya Wamarekani nchini Somalia.
“Peter umetuletea nini leo”
Yemi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, swali la Yemi naamini kwamba hili ndio alio wauliza vijana wengi na wameshindwa kwani wengine wao ambao wameweza kushindwa wamevalia vizuri sana.
 
“Peter, Peter”       
Yemi aliniita baada ya kuniona nikiwa nimeduwaa kwa sekunde kadhaa huku nikijishauri ni kitu gani ambacho ninaweza kukijibu.
“Naam”
“Umetuletea nini kipya hapa kama mwanamitindo chipukizi”
“Nimewaletea mbinu na namna ambavyo walinzi wa tajiri wanavyo takiwa kumlinda tajiri wao pale anapo vamiwa”
“Mmmmm kivipi?”
Jaji mmoja wa kiume aliniuliza huku akionekana kushangazwa sana kwa kile ambacho nimekizungumza.
“Ningemuomba jaji mmoja”
Majaji wakatazamana, akasimama jaji mmoja wa kiume aliye jazia mwili wake, akapiga hatua mbili mbele, ila Yemi akasimama na kumuomba jaji huyo arudi alipo kuwa amekaa kisha akanisogelea yeye.
 
“Haya nionyeshe ni jinsi gani unavyo weza kunilinda pale ninapokuwa nimevamiwa?”
Nikatazama kamera zaidi ya sita zilizopo ndani ya hichi chumba na zote zinachukua tukio hili. Nikasimama nyuma ya Yemi, ambaye kusema kweli ameumbika, umbo lake limejazia makalio ya wastani, amebarikiwa urefu wa futi kama sita na nukta zake.
“Mwanamitindo anatakiwa kuwa mbunifu wa hali ya juu, hili ninalo kwenda kulifanya hapa nitakuomba uwe makini sana kwani kidogo ni hatari”
“Wewe kuwa huru tu”
“Kwa mfano adui anatokea mbele yako na mimi ndio mlizi na nipo nyuma yako. Ninatakiwa kufanya hivi”
 
Kwa haraka nikamshika Yemi Okocha mabega yake na kumgeuza huku nikiwa nimemshika, akaangalia nilipo kuwa mimi, kisha na mimi nikawa sehemu alipo kuwa yeye huku mguu wangu wa kulia nikiwa nimeunyoosha usawa wa kiuno changu, nikimaanisha kwamba nimeweza kumzuia adui mwenye kisu. Yemi akiwa katika kushanga shangaa, nikampiga mtama huku nikutangulia kulala chini na akaniangukia kifuani mwangu, na kwa haraka nikamgeuza na kumlaza chini, ila nikahakikisha kwamba nguo yake hata moja haigusi chini kwani mkono yangu ilijitahidi kumshika kiunoni mwake. 
 
“Hapa ni pale gaidi anapokuwa amefyatua risasi na mlinzi anatakiwa kuhakikisha kwamba bosi wake anaanguka chini kwa usalama”
Nikamnyanyua Yemi Okocha juu na kumfanya ashushe pumzi kwani matukio yote hayo nimeyafanya katika sekunde ambazo nina uhakika hazizidi sitini. Jaji mmoja akaanza kupiga makofi, na kuwafanya wezake kumtazama kwa mshangaa kwa maana hata Yemi Okocha na yeye yupo katika hali ya mshangao mkubwa.
 
“Peter una kitu kikubwa ambacho vijana wengine walio kuja hapa sijapata kukiona”
“Kitu gani wakati alihitaji kumuangusha jaji mkuu?”
“Hapana jaji Ode. Peter anambinu ambazo vijana wengi wa kiume hapa wameingia wamejazia vifua, wamejazia mikono na kukata matumbo yao na kuwa six pack, ila hakuna anaye weza kufanya kama hichi anacho kifanya Peter. Chifu mkuu Peter ni aina ya wanamitindo wachache ambao tunawahitaji, yaani kwa mfano mdogo tu kama tukisema kwamba tunamtengenezea filamu Peter, kampuni yako jaji mkuu ninaamini kwamba itakwenda kuwa mara dufu na na hapa tulipo”
Yemi akanitazama kwa sekunde kadhaa usoni mwangu, kisha taratibu akaanza kutembea kuelekea kwenye kiti chake, akaka huku akihema kidogo.
 
“Jaji mkuu hapa sijaona kitu chochote kutoka kwa huyu Peter”
“Jaji Ode hicho unacho kizungumza ni ufinyu wa fikra, kama hamuamini, fundi mitambo hembu rudisha hili tukio niamini kwamba mutakuwa mumelirekodi vizuri”
“Jaji mkuu hakuna haja ya kurudisha nyuma sijui tukio alilo lifanya, kuna watu wengine nje wanahitaji kuingia ndani”
“Jamani nasema hivi kama hamjaona kitu kutoka kwa Peter na mukashindwa kunielewa kwa kile ninacho kizungumza basi ninawaambia, mimi nitajivua rasmi sasa hivi kisha nitamchukua mimi na nitamtengeneza chini ya kampuni yangu na mutaona ni kitu gani ambacho jamaa ayakifanya”
Yemi Okocha akanyanyua mikono yake juu kidogo usawa wa meza ikiwa ni ishara ya kuwanyamazisha majaji hawa wawili wanao bishana kuhusiana na mimi.
 
“Fundi mitambo hembu rudisha tukio alilo lifanya Peter”
Watu wote humu ndani tukaigeukia Tv kubwa iliyopo kwenye moja ya ukuta. Tukio nililo lifanya likaanza kuonyeshwa tena likiwa limepambwa na mziki mdogo wa filamu. Kusema kweli unaweza kusema ni tukio fulani ambalo lipo kwenye filamu, kwani hata makamera mani waliweza kutingisha vichwa vyao kwa kubaliana na tukio hilo.
 
“Mumeona, mumeonaa. Tazama jaji mkuu pale jinsi ulivyo geuzwa, tazama ulivyo lazwa chini pasipo wewe mwenyewe kujijua na wala kijiandaa. Tazama jinsi alivyo kushika kwa nguvu, hakuna hata nguo yako iliyo husa chini. Sasa hapo munasema munataka mwana mitindo wa ina gani jamani ahaaaaa”
Jaji huyu ambaye hadi sasa sijamjua jina lake ameonekana kunikubali kwa asilimia kubwa sana.
“Peter”
“Naam jaji mkuu”
“Sijapata ona, una kipaji cha hali ya juu. Safi sana”
Yemi Okocha alizungumza na kumfanya jaji huyu mwengine anaye nishabikia kunyanyuka na kushangilia sana, akanifwata sehemu nilipo simama, akanikumbatia huku akinipiga piga mgongoni mwangu.
 
“Nilisema huyu ni genius. Ode ulitaka watu wanao tukatizia katizia miguu hapa huku wakidunda dunda hahahaaaa”
“Umeshinda Joo”
“Peter elekea mlango ule”
Yemi Okacha alizungumza huku akionionyesha mlango ambao ni tofauti na mlango wa kutokea. Nikawashukuru huku nikiwa nimetabasamu, nikaingia katika chumba nilicho onyeshwa, nikawakuta washiriki wengine walio shinda na kuchaguliwa, huku nao wakitazama matukio yanayo tokea kwenye chumba walipo majaji. Kila kijana humu alinitazama sana, nikatafuta kiti na kukaa huku nikiwa nimejawa na furaha ila moyoni mwangu nikijipongeza kwani kazi yangu sasa imesha anza.
 
Kila alipo toka mshiriki mmoja kwenye chumba cha majaji, kipande cha video ya tukio langu na Yemi Okocha kinaonyeshwa kwenye hii tv kubwa tuliyonayo humu ndani.
    Baada ya masaa manne washiriki wakawa wamekwisha, ndani ya chumba hichi kwa haraka haraka tupo wanamitindo thelathini, wanawake wakiwa ni kumi na sita huku wanaume tukiwa kumi na nne. Yemi Okocha na jopo lake la majaji wakaingia ndani ya chumba hichi huku wakionekana wakiwa wamechoka sana.
“Tunamshukuru Mungu tumeweza kumaliza mchujo wetu kwa usalama, pia ninawashukuru nyinyi nyote kwa kuweza kufika leo na kupata nafasi hii ya kuwa chini ya kampuni yangu”
 
Yemi alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaka kimya kidogo na kuendelea kuzungumza.
“Kwa leo mutaweza kulala katika hii hoteli, kesho tutaondoka hapa na tunawaambia ni wapi ambapo mutakwenda. Ila kumbukeni kwamba nyinyi ni wamaitindo ambao ni wabunifu kama rafiki yangu Peter hapo, hadi sasa kipande chake cha ubunifu wake alio nionyesha kimetazamwa na watu zaidi ya milioni kumi katika chaneli yetu iliyopo katika mtandao wa YouTube.”
Wamaitindo waote wakapiga makofi ikiwemo na mimi, ila akilini mwangu ninatambua kwamba ni jambo la hatari kwani maadui zangu tayari wamesha weza kugundua ni eneo gani ambalo nipo.
“Yaani sikutegemea sana, ndani ya masaa matano kupata watazamaji wengi kama hao. Wazo la jaji Joo kwamba tumepata mtu kweli hapa tumepata mwanamitindo”
 
Jaji Joo akanikonyeza huku akitingisha kichwa, akionekana akiwa anafurahia uwepo wangu uliopo katika eneo hili.
“Basi sisi tuawatkie usiku mwema, jaji Joo atawaongoza hadi kwenye vyumba vyenu na baada ya hapo mutapelekwa kwenye sehemu ya kula”
“Tunashukuru”
Jamaa mmoja alizungumza, tukatoka katika chumba hichi na kuongozana na jaji Joo, na moja kwa moj tuaanza kuonyeshwa kila mtu chumba chake.
“Peter”
Jaji Joo aliniita baada ya kuingia katika chumba changu huku mimi nikiwa ndio mtu wa mwisho kabisa kuonyeshwa chumba changu cha kulala.
“Ndioo Jaji”
“Hongera sana kwa kile ulicho tuonyesha, hivi ulitoa wapi wazo hili?”
“Ahaa nimefikiria kwa haraka haraka, nikaona mbinu hiyo kidogo inaweza kunisaidia na kweli imenisaidia”
“Kazi nzuri Peter, ninauhakika ukijitahidi tutatengeneza pesa nyingi sana kupitia wewe. Ila kitu cha kuangalia hakikisha kwamba unasimamia kwenye maslai mazuri pale unapo ingia mkataba”
 
“Nimekuelewa katika hilo”
“Basi tuelekee eneo la chakula”
“Sawa”
Tukaongozana na jaji Joo hadi kwenye ukumbi wa chakula ambapo nikawakuta wanamitindo wezangu wakiendelea kula taratibu.
“Kaa tu hapa”
Jaji Joo alizungumza, nikaka kiti cha pembeni yake, nikaletewa chakula nilicho kihitaji, taratibu nikaanza kula huku kazi yangu ikiwa ni kuwasoma tabia zao wana mitindo wote waliomo ndani ya hichi chumba. Nilipo jirizisha na upelelezi wangu wa kimya kimya pasipo mtu kuelewa nikanyanyuka kwenye meza niliyo kalia na kuanza kueleka chumbani kwangu kujipumzisha kwani nimesha maliza kula.
“Hei Peter”
Dada mmoja mwembaba aliniita huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kalia. Nikasimama kumtazama jinsi anavyo nifwata.
“Ndio”
“Naitwa Calx, kusema kweli nimevutiwa sana na wewe”
“Ninashukuru Calx”
“Ahaa naweza kupata namba yako ya simu?”
“Nitakupatia asubuhi kama huto jali”
“Kwa nini isiwe sasa?”
“Sawa unaweza kunipatia namba yako ya simu kisha nikakutafuta mimi?”
“Ndio”
 
Calx akanipatia namba yake ya simu kisha nikaondoka eneo hili na kurudi chumbani kwangu. Nikaufunga mlango kwa ndani, nikazima taa ya chumbani kwangu na kutazama kwenye kuta zote kama kuna taa nyekundu ya kamera yoyote ambayo inaweza kutegwa humu ndani. Nikainama hadi chini ya uvungu wa kitanda kutazama kama kuna maera, ila sikufanikiwa kuona chochote. Nikawasha taa na kuanza kutafuta kama kuna kinasa sauti chochote cha kutegwa, kwani katika hoteli kubwa kama hizi hususani kwenye mashindao ya namna hii vitu hivi hutegwa kwenye vyumba vya washiriki ili kufwatilai nyendo zao. Sikuweza kufanikiwa kupata chochote, ikanibidi kuanza kukipanga vizuri chumba hichi kwani nikekichagua vibaya.
 
Nikataka kupiga simu Marekai ila nikasita kwani bado nafsi yangu inakataa kabisa kuweza kuamini hichi chumba kwani watu ninao shuhulika nao wana akili nyingi sana na pasipo kuwa mjanja basi ninaweza kujikuta nikistukiwa mapema sana.
Nikavua nguo zangu, nikachukua taulo na kujifunga kiunoni mwangu, nikaeleka bafuni na kuanza kuoga taratibu huku nikipanga ni jinsi gani ninaweza kujifanya nionekane bora na kuaminika mbele ya macho ya Yemi Okocha ili kuhakikisha kwamba ninafanikiwa kumteka kiakili na kufahamu kile kilicho nileta huku Nigeria.
 
Nikafungua mlango wa bafuni na kutoka, nikasimama mbele ya kioo kikubwa huku nikiwa sin nguo hata moja, taratibu nikaanza kujifuta maji yangu kwenye jogoo langu, huku nikiendelea kujitazama. Gafla taa ya chumbani kwangu ikazima, pasipo hata mimi kuizima, kioo cha dirishani kikavunjika na akaingia mtu aliye valia nguo nyeusi tupu huku ameficha sura yamebaki macho tu huku mkononi mwake akiwa amshika panga refu jambo lililo nifanya nijipange kwa kujihami haraka iwezekanavyo.

AISIIIII……….U KILL ME 135


Mtu huyu akaanza kupiga hatua za kunizunguka jambo ambalo lililo nifanya na mimi nianze kuzunguka taratibu taratibu. Mtu huyu akaanza kunishambulia kwa kasi sana jambo lililo nifanya na mimi nianze kumkwepa kwa kasi sana huku nikiepuka sana asinikate na panga lake alilo lishika.
Katika kurupushani hizi na mtu huyu nikafanikiwa kumpiga teke la kifua nililo mfanya aanguke chini kama mzigo huku panga lake likiangukia pembeni. Sikutaka kumpa nafasi ya kunyanyuka, nikamuwahi na kumpiga kabali ya shingo huku nikijitahidi kuhakikisha kwamba ninamvua kitambaa alicho jifunika uso wake. Nikakutana na sura ya kiume ambayo sikuwahi kuiona kabisa tangu niweza kufika nchini hapa Nigeria.
 
“Ni nani aliye kutuma”   
Nilimuuliza huku nikiendelea kumkaba kwa nguvu.
“Sii……..”   
Ikanibidi kuendelea kuminya shingo yake hadi akapoteza fahamu. Kwa haraka nikanyanyuka  huku jasho jingi likinimwagika, nikapiga hatua hadi swichi, nikawasha taa ya chumbani humu, mandhari ya chumba hichi yamebadilika sana kwani ni vitu vingi vimeanguka na kuchanguka changuka. Nikajikota hadi lilipo taulo langu nikajifunga na kuingia bafuni. Nikanawa uso wangu na maji ya baridi huku nikipikijitazama kwenye kioo.
Nikarudi chumbani, nikaichukua simu yangu aina ya samsung na kumpigia Calix.
“Peter hapa”
 
“Waooo Peter, mambo vipi?”
“Nahitaji msaada wako”
“Msaada gani?”
“Njoo chumbani kwangu”
“Chumbani kwako?”
“Ndio ninakuomba msaada wako”
“Upo chumba namba ngapi?”
“Ahaa ni chumba namba………”   
Nilizungumza huku nikitembea kuelekea mlangoni, nikafungua mlango na kuchungulia kwenye kordo, sikuona mtu yoyote, nikatazama namba ya mlango wangu na kukuta ni namba mia tatu na tatu
“Nipo chumba namba mia tatu na tatu”
“Ok ninakuja”
“Sawa”
Nikaufunga mlango na kusimama pembeni ya mlango huku nikimtazama jamaa huyu aliye lala chini. Hazikupita hata dakika tano, malango ukagongwa kwa nje.
“Nani?”   
“Calx”
“Ok”
Nikafungua mlango na Calx akaingia, akaanza kushangaa jinsi vitu vilivyo changuka humu ndani, akamshangaa na mtu ambaye amelala chini.
 
“Mungu wangu, Peter kimetokea kitu gani hapa?”
“Nimevamiwa na huyu mtu hapa”
“Hajakumiza”
Calx alizungumza huku akinishika mwili wangu, akauchunguza vizuri huku akionekana kunishangaa.
“Hapana hajaniumiza”
“Itabidi tuwasiliane na uongozi wa hii hoteli”
“Unaonaje tukawasiliana na majaji walio tuleta hapa kwa maana mtu huyu ni jambazi kwa kweli”
“Sawa tena nina namba ya jaji mkkuu Yemi Okocha”
“Ninaomba umpigie”
Calx akatoa simu yake mfukoni na kumpigia jaji Yemi ambaye kwangu yeye ndio mtu muhimu aliye nifanya mimi kuweza kufika hapa.
“Habari madam unazungumza na Calx”   
“Sahamani kwa kukupigia simu usiku”
“Kuna jamaa sijui ni nani amemvami Peter”
“Ndio chumbani kwake na alikuja na panga kabisa”
“Sawa madam”
 
Calix akakata simu na kunitazama usoni mwangu.
“Madam anakuja sasa hivi”
“Sawa nashukuru kwa kumpigia simu”
“Usijali maisha ni ni kusaidianana”
“Kweli kweli”
Haukupita muda mrefu Yemi na walinzi wake wakaingia ndani ya chumba changu, nao pia wakaonekana kushangaa kuona jinsi chumba kilivyo changuka na jamaa huyu aliye lala chini na hadi sasa hivi hajapata nafuu.
“Upo salama kweli Peter?”
“Ndio jaji mkuu nipi solama”
“Ahaa pole sana”
Yemi Okocha akawapigia simu uongozi wa hii hoteli, ambao nao pia hawakuchukua muda mwingi awkafika katika chumba changu.
“Huyu mtu mbona kama ninamfahamu”
Muhudumu mmoja wa hoteli alizungumza huku akimtazama mtu huyu usoni mwake. Sote tukamtazama mtu huyu.
“Unamfahamu vipi?”
 
“Anaishi mtaani kwangu na ninasikia sikia kwamba ni jambazi na leo kama hivi amekamatwa”
“Hili swala inabidi tuwashirikishe polisi kwa maana hakuna mtu ambate anafahamu kwamba washiriki wangu kwa leo wanalala hapa”
Yemi Okocha alizungumza huku akimtazama meneja wa hii hoteli. Meneja huyu taratibua kamshika mkono Yemi na kusogea naye pembeni, mazungumzo yao hapakuwa na mtu aliye weza kuyasikia, ila mimi kazi yangu ikawa ni kutazama lipsi zao za midomo na nikafahamu kabisa ni kitu gani wanacho kizungumza. Meneja anaonekana kumuomba sana Yemi Okocha asilifikishe swala hili kwenye vyombo vya sheria, kwani linaweza kuiweka hoteli katika hali ya uchunguzi. Yemi akaniangalia kisha akanita kwa ishara taratibu nikawasogelea sehemu walipo simama.
 
“Peter meneja hapa ana aombi kwako, japo ameniomba mimi ila nikaona si vyema mimi kulichukulia maamuzi moja kwa moja nikaona ni vyema kukushirikisha”
“Zungumza tu hakuna tatizo”
“Kaka natambua kwamba umeweza kumdhibiti huyu jambazi, ila hili swala kama ikitokea tukawakabidhi askari linaweza kutuletea hali ngumu ya kibiashara. Wageni wataogopa kulala hapa watahofia kwamba ulinzi wa hii hoteli ni mdogo sana”
 
“Na kweli ni mdogo, hivi meneja, inakuwaje mtu anatoka huko alipo toka hadi hapa chumbani kwangu tena na kuvunja dirisha hili la kioo pasipo kuwa na mtu ambaye yumo ndani ya hii hoteli yako na ametoa mchongo kwa huyu jamaa na akihahisi kwamba kuna pesa kwa hawa washiriki?”
 
Swali langu likamfanya meneja kupatwa na kigugumizi na akakopoteza ujasiri wa kunijibu kabisa.
“Isitoshe kabla ya mtu huyu kuingia humu ndani alizima taa ya hichi chumba akiwa kwa nje, na kwa uelewa wangu tu wa kawaida, katika mahoteli makubwa kama haya, lazima kuna chumba kimoja ambacho kinashuhulika na maswala yote umeme, na hapa inaonekana kwamba muhusika wa kupanga mpango wa mimi kuvamiwa yumo ndani ya hii hoteli yako ukubali ama ukatae”
Nilizungumza kw amsisitizo huku nikimtazama meneja huyu.
“Meneja naona hadi sasa hivi hujazungumza kitu cha muhimu kinacho weza kumshawishi Peter na mimi nikisema kwamba nikutete, unaweza kumfanya Peter kunifikiria mimi vibaya wakati mimi wala sipo hivyo”
 
“Kweli ni…nimeelewa hapa, ila ninacho waomba huyu mtu mumshuhulikie nyinyi wenyewe kama mutaweza”
“Ahaa mimi ni mwana mitindo sio askari wala sio mwanajeshi, na walinzi wangu hawawezi kuifanya hiyo kazi, sasa unavyo hitaji tumshuhulikie unakosea meneja”
Yemi Okocha alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama meneja usoni mwake.
“Jaji mkuu huyu tunaweza kumuhoji humu humu ndani”
“Peter utaweza kufanya hivyo?”
“Ndio jaji mkuu”
“Sawa”
Tukarudi alipo lala huyu jamaa, mlango ukafungwa kwa ndani na watu wote wakawa na kazi ya kunitazama mimi kuona ni kitu gani ninakwenda kukifanya. Nikamkalisha mtu huyu kwenye kiti nikashukua upanga  wake na kuushika mkononi mwake. 
 
“Niletee maji ya baridi”
Muhudumu wa hoteli hii akakimbilia hadi sehemu iliyo na friji ndogo humu ndani, akachukua chupa ndogo ya maji na kurudi nayo nilipo kaa, nikachomoa mkanda wa suruali yangu na kumfunga mikono yake kwa nyuma jamaa huyu kwenye kiti alicho kikalia.
Nikaifungua chupa ya maji na kuanza kumwagia usoni mwake, jamaa akakurupuka kwa haraka huku akihema, ikajaribu kunyanyuka ila akashindwa, akanza kutazama mtu mmoja ndani ya hichi chumba, alipo fikisha macho yake kwa muhudumu ambaye alisema kwamba amemtambua akastuka sana. 
 
“Moses”       
Muhudumu huyu alimuuita huku akiendelea kumshangaa. Jamaa kwa aibu akajikuta akitazama chini.
“Hei Moses”
Nilimuita huku nikimnyanyua uso wake, akajaribi kukikaza kichwa chake, nikamtazama Yemi Okocha, akanikonyeza na kuniruhusu kutumia nguvu ili azungumze ni nani ambaye amemtua kuja kunivamia mimi. Nikamyanyua tena sura yake ili anitazame ila akakikaza kichwa chake, sasa hivi sikuhitaki kumbembeleza zaidi ya kutandika kofi zito la shavu lililo wastusha watu wote humu ndani ya hichi chumba. Nikamnyanyua kwa nguvu uso wake na kumtazama usoni mwake.
“Ni nani aliye kuagiza kuja kufanya uvamizi humu ndani?”
“Nenda ka....  mama yako”
Jamaa alinitukana tusi lililo nifanya nitazame chini kwa sekunde kadhaa huku nikishusha pumzi kwani hatambui ni wapi mama yangu alipo, nikanyanyua uso wangu huku ukiwa umejaa tabasamu panasana jambo ambalo natambua halikutegemewa na watu wengi ndani ya hichi chumba.
 
“Nashukuru, na nitafanya hivyo Moses. Hembu tuambie ni nani aliye kutuma?”
Moses akakaka kimya, nikalitazama panga lake nililo lichika mkononi mwangu. Pasipo na huruma nikalipitisha kwa nguvu kwenye paja lake la mguu wake wa kulia huku nikiyagandamiza makali ya upanga wake kwenye hili paja lake jambo lililo mfanya apige kelele, Calx na muhudumu wakabaki wakifumba macho yao ila Yemi, meneja na walinzi wawili wa Yemi wakabaki wakiwa wamemkazia macho Moses.
“Ni nani aliye kituma uje kunivamia  mimi?”
Moses akaendelea kulia kwa uchungu huku damu zikizidi kumwagika, nikazidi kumkata paja lake huku nikigandamiza panga hili kwa nguvu kadri niwezavyo.
 
“Ni nani aliye kutuma?”
“NI…….ME…E……NEJA”
Watu wote ndani ya hichi chumba tukamgeukia meneja aliye anza kushangaa shangaaa huku akionekana woga umemtawala usoni mwake.
“Meneja?”
Yemi Okocha alizungumza huku akimtazama meneja kwa macho ya mshangao. Kwnai hili lililo tokea hapa ni jambo lililo tushangaza sisi sote. Kwa haraka meneja akamkaba Yemi Okocha kabali kwa nyuma huku akitoa kisu kidogo mfukoni mwake na kumuwekea Yemi Okocha shingoni mwake.
“Mtu yoyote akinisogelea nitamuua jaji wenu”
Meneja alizungumza kwa msisitizo, walinzi wa Yemi wakabaki wakiwa ameduwaa tu wasijue ni nini cha kufanya kwa kitisho walicho patiwa na meneja huyu ambaye hadi sasa hivi hatujui lengo lake ni nini haswa.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )