Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, November 5, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 138 na 139 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
 
“Baba umefwata nini chumbani kwangu!!”
Niliisikia sauti ya Yemi Okocha akizungumza kwa mshangao, nikahisi labda yupo usingizini.
“Huyu ndio aliye kufanya umsaliti mumeo?”
Sauti nzito ya mwanaume ikanifanya nifumbue macho yangu, nikakutana na sura ya baba Yemi ambaye ni gaidi niliye tumwa kuja kumtafuta nchini hapa Ningeria, pembeni yake wamesimama wanajeshi wawili wakiwa na bunduki mkononi mwao, na mlangoni nikamuona mume wa Yemi Okocha akitutazama kwa hasira kali huku Yemi naye amekaa pembeni yangu huku amejifunika kwa shuka kuficha maungo yake ya ndani.
       
ENDELEA   
“Baba sio kosa la huju kijana kulala na mimi au kumsaliti huyo mshenzi hapo”
Yemi Okocha alizungumza kwa kujiamini sana huku akimtazama baba yeke usoni, mwili mzima ukaanza kunitetemeka kwa maana hili kosa ni saawa na kufuniwa na mke wa mtu.
“Mume wako amenieleza kila kitu, kwamba amekukuta na huyu kijana na mukamvamia na kumpiga kisha hapa mumelala pamoja”
“Ni muongo, baba unajua ni jinsi gani nilivyokuwa ninampenda Thomas, unatambua ni jinsi gani nilivyo yatoa maisha yangu kwa ajili yake, hadi hii hoteli alijenga kwa pesa yangu ambayo wewe umenipatia. Leo hii nimsaliti kirahisi pasipo yeye kuanza ujiang”
 
Yemi alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Sikuhitaji hata kujitingisha kwa maana kunaweza kuniletea matatizo na isitoshe kwamba nimepoteza ujasiri kabisa na sina uwezo wa kupambana kabisa.
“Baba mimi ni mwanao wa pekee. Haya ni mahusiano na maamuzi yangu binafsi, sinto penda wewe uyaingilie”
“Lakini mwanangu hii ni aibu, kulala na mwanaume mwengine namna hii”
“Baba yeye amelala na wahudumu wawili wa hoteli yangu, ninawalipa pesa yangu. Wamelala kwenye kitanda changu ambacho ni mali yangu. Hapo kweli kuna ubaya wa mimi kuamua kufanya maamuzi tofauti na yeye. Sinto jali baba kaishi maisha yangu mimi ukiendelea kunishawishi kurudiana na Thomas, simpendi na ukimuacha aendele kunisogelea ninakuahidi nitamuua”
Yemi Okocha alizungumza kwa ujasiri mkubwa huku akiendelea kumtazama baba yake, baba Yemi akashusha pumzi nyingi sana, akanitazama usoni mwangu kwa macho makali yaliyo nipa woga fulani.
“Kijana unaitwa nani?”   
“Peter”
Nilizungumza huku nikiendelea kutetemeka mwili wangu. Naamini kutetemeka huku pia kunanisaidia kuficha uhalisia wangu juu ya kazi ya upelelezi iliyo nilete hapa Nigeria.
“Vaa nguo zako”
“Baba Peter haondoki hapa pasipo mimi na kama unahitaji avae nguo zake wacha mimi nivae kwanza.”
“Yemi alizungumza huku akitaka kutoa shuka alilo lifunika, baba yake kwa haraka akageuka na kutupa mgongo kwani haitaji kuona maungo ya ndani ya mwanae.
“Acha kuvaa tafadhali. Wewe na huyo rafiki yako saa mbili usiku hakikisheni munakuja nyumbani kwa ajili ya chakula cha usiku ninahitaji kumfahamu zaidi ya hapa”
 
“Sawa baba”
“Na wewe uongozana na mimi”
Baba Yemi alizungumza huku akimnyooshea Thomas kidole, wakatoka kwenye chumba hichi na kunifanya nishushe pumzi nyingi huku jasho likinitoka usoni mwangu.
“Samahani kw ahili lililo tokea Peter”   
“Mmmm”
“Natambua unaogo ila usihofu juu ya hili, kila jambo litakwenda jinsi ninavyo weza isitoshe kwamba baba yangu ananipenda ndio maana ameweza kunisikiliza mawazo yangu juu ya maisha, kikubwa ninahitaji uwe na amani”
“Ila baba yako ni mwanajeshi ataniua mimi”
“Hawezi kufanya hivyo, namjua baba yangu ana roho njema, niamini Peter”
Yemi alizungumza huku akiwa amenishika mashavu yangu kwa viganja vyake viwili. Taratibu akanibusu mdomoni mwangu, tukatazamana kwa ukaribu sana wa nyuso zetu kwa sekunde kadhaa kisha tukajikuta tukianza kunyonyana lipsi zetu. 
 
‘Asante Mungu kazi yangu inakwenda vizuri’
Nilizungumza huku nikikilaza kichwa cha Yemi kwenye mtu, huku tukiendelea kunyonyana mdomo yetu. Woga na wasiwasi vyote vikanipotea, sikutaka kuwa mchoyo kwa Yemi kwa kumpa kile anacho kihitaji kwa asubuhi hii. Hatukuchukua muda mwingi tukajikuta sote tukimaliza mechi hii kwa pamoja.
“Asante Peter, sijui kwa nini siku zote sikuweza kukufahamu”
“Kivipi?”
“Wewe ni mwanaume ambaye umenionyesha ni jinsi gani mwanamke anatakiwa kut na mwanaume, sikutarajia kama siku ninaweza kukutana na mkuno ambao umeweza kunioatia jina usiku na leo asubuhi.”
“Kwani..aha…..mume alikuwa akufanyii hichi ninacho kufanyia?”
“Alikuwa hajiwezi, ila tuachane na hayo mambo sipendi kuyazungumzia sana. Ila tujiandae tukapate kifungua kinywa”
“Sawa”
“Au tupike humu humu?”
“Ni wewe tu”
“Ok sawa”
Tukashuka kitandani na kuingia bafuni pamoja, tukaingia katika sinki la kuga na taratibu tukaanza kuoga huku sote tukiwa katika furaha nzuri.
 
“Peter”
“Naam”
“Wewe ni mzuri”
“Hapana mimi wa kawaida sana”
“Nakuambia ukweli wewe ni mzuri, hivi umetokea wapi hapa Nigeria?”
Swali la Yemi likanifanya ninyamaze kimya kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama usoni mwake. Kichwani mwangu ninapangilia ni sehemu gani ambayo ninaweza kuitaja kwa haraka haraka ili aweze kunielewa.
“Kwetu sio hapa Nigeria”
Nillizungumza kwa sauti ya upole kidogo na kumfanya Yemi kukaa vizuri kwenye sinki hili huku akinitazama kwa macho malegevu.
“Umetokea wapi?”
“Familia yangu ilikuwa nchini Kenya, na ndipo nilipo zaliwa. Nimesoma huko hadi nikamaliza, nikaajiriwa kwenye shirika moja la simu linaitwa Safaricom, nikafanya fanya kazi hapo ila baada ya mama yangu kufariki basi nikaamua kuja hapa Nigeria kwa maana mama aliniambia kwamba baba yangu ni mnageria na ndipo asili yangu ilipo, basi ikanibidi kuja hapa ili kumtafuta baba yangu”
 
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga ili kuukamilisha uongo wangu vizuri sana. Taratibu Yemi akanisogelea na kunishika mashavu yangu.
“Shii….usilie mpenzi wangu. Je ulisha wahi kumuona baba yako?”
“Hapana sikuwahi muona kabisa wala hata kuja kwangu sidhani kama ninaweza kufanikiwa kwani aliondoka Kenya tangu nipo tumboni mwa mama yangu na wala baba yangu hakuwahi kujua kwamba ameacha mtoto nchini Kenya”
Nilizungumza uongo ambao hata tukisema tuanze kazi ya kumtafuta baba yangu basi itakuwa ni kibarua kigumu kwetu.
“Ohooo pole mpenzi wangu, sasa utaweza kweli kumtafuta baba yako?”
“Sidhani kwa maana sijui hata sura yake ipo vipi”
“Je jina mama alisha wahi kukutajia labada tunaweza kumtafuta”
Yemi aliendelea kuzungumza kwa suti ya upole huku akinishika mashavuni mwangu.
 
“Aliniambia anaitwa Popoola”
“Duuu kuna majina mengi ya watu wanaitwa Popoola, ila tutajaribu kufwatilia kwenye mtandao na tunaweza kupata japo mtu hata anaye weza kuendana nawe”
“Nitashukuru sana”
Yemi akanipiga busu la mdomoni, tukamaliza kuoga na kutoka bafuni. Tukavaa nguo zetu na kuanza kuandaa kifungua kinywa. Hatukuchua muda sana tukawa tumemaliza kuanda akifungua kinywa.
“Wanamitindo wezangu watafika saa ngapi hapa?”
“Sio wezako tena”
“Kwa nini?”
“Peter naomba uelewe, japo ni haraka sana kwa hili jambo. Ninakupenda, si kwasababu nimeachana na mume wangu, la hasha. Tangu nilipo kuona kwenye mashindano nilitokea kuvutiwa na wewe, ila nilijitahidi kuuzuia moyo wangu katika kukupenda kwa maana nilitambua nina mume wangu wa ndoa na ninaheshimu ndoa yangu. Haikuwa hivyo kama nilivyo tarajia ndoa yangu iwe, naamini wewe mwenyewe umeweza kuhushudia kila kilicho tokea””
 
“Yaaa, labda ni kitu gani kimekufanya unipende?”
“Hahaaa hilo swali utanieleza badae tunywe chai kwanza kisha kama huyo jali tutaingia gym kufanya mazoezi”
“Sawa, sasa sina nguo za mazoezi?”
“Itabid kwenda kufanya manunuzi ya nguo madukani, mazoezi tunaweza kufanya hata usiku”
“Hapo sawa, japo umesahau kwamba usiku leo baba yako anatuhitaji nyumbani kwake”
“Ohoo Mungu wangu, kichwa changu kimesahau kabisa jamani, daaa nauona uzee unanikabili”
“Haha sio uzee, mawazo tu, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba mawazo hayo yanakwenda kufutika kichwani mwako”
 
“Nitashukuru sana mpenzi wang”
    Tukajiandaa na kuanza safari ya kuelekea katika maduka ya nguo, kila tunapo pita Yemi hakusita kunishika mkono, jambo lililo nifanya niwe na wasiwasi mwingi sana kwani kwa kipindi hichi mitandao ya kijamii inarusha habari kwa haraka sana na ninaelewa ni lazima Hawa atakuwa anaifwatilia oparesheni hii kwa ukaribu wa hali ya juu. Umaarufu wa Yemi unazidi kuihatarisha kazi yangu kwani kila sehemua watu walimuomba kupiga picha nasi na aliweza kuwakubali.
“Baby”
“Mmmm”
“Huwa sipendi kupiga picha mbele za watu”
“Kwa nini mume wangu”
“Bado mapema sana kwa watu kuweza kufahamu kwamba mimi na wewe tuna mahusiano”
“Peter, tafadhali mpenzi wangu, nimesha fanya maamuzi yangu mimi mwenyewe niakuomba uwe na amani wewe kwa sasa ndio mume wangu”
“Sawa nalitambua hilo ila sinto penda kuishi maisha ya umaarufu”
 
“Kweli mume wangu?”
“Ndio”
Yemi akanipiga busu la mdomo, na baadhi ya watu walio tuzunguka wakapiga picha kadhaa kwa kutumia simu zao. Tukaingia kwenye gari tulilo jia na kuondoka eneo hili.
“Kwa nini hupendi kuishi maisha ya umaarufu?”
“Kwa sababu sikuzaliwa kuwa mtu maarufu”
“Kumbuka ulikuja kwenye shindano la uwana mitindo, na utambue kwamba video yako inaendelea kutazamwa na watu wengi duniani, umesha kuwa maarufu Peter”
Yemi alizungumza huku akikunja kona, tukaingia kwenye moja ya mtaa wenye maduka mazuri ya nguo za kiume.
“Nalitambua sana ila nilifanya hivyo kwa ajili ya kujaribu tu ili kuona kama na mimi ninaweza kuwa mwanamitindo na hata kama anikipata pesa basi zitanitosheleza katika kipindi chote nitakacho kaa hapa Nigeria nikimtafuta baba yangu.”
 
“Ohooo sawa mpenzi wangu, nimekuelewa”
Yemi akasimamisha gari kwenye moja ya duka lenye midoli ya kiume iliyo valishwa suti. Tukashuka kwenye gari na kuingia ndani ya duka hili, tukanunua suti nne zinazo nitosha kisha baada ya hapa tukaanza safari ya kuelekea hotelini.
    Japo ninatambua kwamba ni maisha ya muda mfupi ya kufurahia na Yemi ila kusema kweli ninafurahi sana kwa maana Yemi ana tabia ambayo nimeikosa kwa wasichana wengi katika maisha yangu. Kila muda Yemi kwake ni furaha, ananijitahidi kadri anavyo weza kunifurahisha.
“Unatambua ni nini Peter”
“Eheee”
“Tukifika nyumbani kwa baba yangu, ninakuomba ujiamini, ule woga wako kama wa asubuhi sinto hitaji kuuona leo usiku”
“Usijali”
“Sawa ngoja nikaonane na washiriki, hapa nimeambiwa kwamba wamefika. Kama unahitaji unaweza kujumuika nami?”
“Hapana nenda kaonane nao tu”
“Poa”
Yemi akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu, kabla hajatoka nikampatia namba yangu ya simu kisha naye akanipatia ya kwake na akatoka chumbani humu. Nikapiga hatua hadi kwenye moja ya dirisha niksimama na kuchungulia nje. Nikatoa simu yangu na kumpigia raisi Donald Bush. Simu yake ikapokelewa ila sikusikia akizungumza zaidi ya kusikia miguno ya mapenzi. Nikataka kukata simu ila nikasubiria kidogo kusikilia.
‘Nakojoaaaaa’
Niliisikia sauti ya Hawa na kujikuta nikistuka sana, mwili ukaanza kunicheza wivu wa mapenzi ukaanza kunitawala moyoni mwangu. Hasira kali ikazidi kunipanda na swali kubwa nikajiuliza ni kwa nini raisi amemua kunisaliti.
 
“Kwa penzi hili ulilo nipa nitahakikisha kwamba mume wako nina mshughulikia”
“Hapana muache Dany peke yake, upo na mimi hakuna haja ya kumfwatilia muache aendelee na maisha yake”
“Una uhakika na unacho kizungumza?”
“Ndio, kwa picha nilizo ziona leo, Dany akiwa na Yemi zina dhihirisha kabisa wapo kwenye mapenzi matamu, nimekufungulia moyo wangu muheshimiwa raisi, ninajitahidi kukupenda”
“Nashukuru Hawa, sikufamu kama wasichana wa kiafrika muna mapenzi matamu kiasi hichi”
“Ila na wewe hakikisha mke wako unamueleza ukweli kuhusiana nasi”
“Usijali nitamueleza ukweli sawa baby”
“Mbona kama simu yako ipo hewani”
“Shitii”
Simu ikakatwa, jambo lililo nifanya nijikute nikimwagikwa na machozi usoni mwangu. Taratibu nikaizima simu yangu na kuirudisha mfukoni mwangu.
 
‘Hawa kwanini unataka kutengeneza uadui mwingine juu yangu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku machozi yakiendelea kunimwagika, kazi ambayo imenileta huku taratibu ninaanza kuichukia kwani mwanaume niliye muamini na kumpa jukumu la kumlinda mke wangu leo hii yupo chumbani na mwanamke wangu.
Mlango ukafunguliwa, kwa haraka nikafuta machozi yangu huku nikiwa ninatizama dirishani, nikageuka nyuma na kumkuta Yemi akiwa amesimama huku tabasamu pana limemjaa usoni mwake.
“Vipi mbona umerudi?”   
“Ahaa nimewapa maelekezo nimeona nije nitulie na wewe mpenzi wangu, vipi mbona kama unaonekana haupo sawa?”
“Kichwa kidogo kinaniuma”
“Ohoo pole sana”
Taratibu nikajikuta nikimsogelea Yemi na kumkumbatia kwa nguvu, machozi nikashindwa kuyazuia na kujikuta nikiangua kilio kikali sana hadi Yemi akabaki akishangaa ikambidi aanze kazi ya kunibembelea huku akiniuliza maswali ya kutaka kufahamu ni kutu gani kinacho endelea  kwangu.

AISIIIII……….U KILL ME 139
 
“Peter tafadhali ninaomba uniambie ni kitu gani kinacho kuliza mpenzi wangu?”
 
Yemi Okocha aliendelea kuniuliza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge ndani yake.
“Namkumbuka sana mama yangu”
Ilinibidi kuzungumza uongo.
“Shiii usilie mume wangu, kwa sasa nitakuwa mama, baba kwako nitakujali kwa kila jambo katika maisha yangu sawa”
“Nimekuelewa mke wangu ninashukuru sana”
“Vipi tutakula mchana?”
“Hapana nipo vizuri”
Taratibu tukaka kwenye sofa, Yemi akaniomba nilaze kichwa changu kwenye miguu yake na nikafanya hivyo.
“Mama yangu alikuwa ni mwanamke mpambanaji sana, kwenye maisha yake hakuhitaji kumtegemea mwanaume. Alijitahidi kuhakikisha kwamba ninapata elimu bora ili ije kunisaidie mbeleni”
Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama Yemi usoni mwake, na viganja vya mikono yake vinakazi ya kukatiza katiza katika mwili wangu.
 
“Mama alisumbuliwa na nini hadi akafariki?”
“Saratani”
“Daaa pole sana”
“Nashukuru, nilijaribu kumpeleka katika kila hospitali kubwa nchini Kenya ila ilishindikana na Mungu aliweza kumchukua”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga tena ili kuzidi kumpumbaza  Yemi Okocha.
“Kikubwa ni kumshukuru Mungu mpenzi wangu sawa baba”
“Sawa”
    Tukaanza kujiandaa kwa ajili ya kueleka katika nyumbani kwa baba Yemi. Nikavaa moja ya suti ambayo nimetokea kuipenda sana.
“Mke wangu kesho unikumbushe kuelekea katika hoteli niliyo toka nikachukue begi langu la nguo”
“Sawa hakuna tabu katika hilo”   
Imetulazimu kuondoka mapema kutokana na foleni kubwa iliyopo hapa katika jiji la Lagos Nigeria. Ikatuchukua saa moja na nusu kufika katika jumba kubwa la kifhari la baba Yemi. Nyumba hii inalindwa na wanajeshi wenye silaha kubwa zenye uwezo mkubwa katika upambanaji.
“Mkewangu tafahali usishuke kwanza kwenye gari”   
“Kwa nini?”
“Mbona kuna wanajeshi wengi hivi?”
“Baba yangu ni kamanda mkuu wa jeshi, ni lazima nyumbani kwake walinde wanajeshi”
 
“Huoni kama inaweza kuniletea shida kwangu kama anakuwa amejazwa sumu na mume wako uliye achana naye?”
“Baba yangu ni muelewa mkubwa sana na anapenda kunipa uhuru kwa kila jambo ambalo ninalotaka kulifanya kwa hiyo katika hili wala usiwe na wasiwasi mume wangu sawa?”
“Sawa”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikishuka kwenye gari, tukapokelewa na wafanyakazi wawili wa kike na moja kwa moja tukaeelekea ndani. Tukaingia kwenye seble moja kubwa sana ambayo ukubwa wake kwa nchi yetu ya Tanzania unaweza kujenga nyumba hata ya vyumba vinne vya kulala.
“Waooo karibu mwanangu”
Baba Yemi alizungumza huku akinyoosha mikono yake na kumkumbatia mwanaye. Wakazungumza kilugha ambacho sikuweza kukielewa. Yemi akanigeukia na kunishika mkono wangu.
 
“Baba huyu anaitwa Peter ni mume wangu mtarajiwa”
“Peter huyu ni baba yangu Mzee Okocha”
“Nashukuru kukufahamu”
Mzee Okocha akanipatia mkono huku  akiutingisha na kunitazama usoni mwangu kwa macho makali ila anatabasamu. Tukakaribishwa kwenye meza ambayo imejaa vyakula vingi  vya kila aina huku kukiwa na majagi makubwa ya juisi. Wafanyakazi walio simama pembeni ya hii juisi nilisihi kwamba wanaweza kukaa nasi kwenye hii meza kubwa wajumuike kula nasi, ila hadi ninaanza kula sikuona hata mmfanyakazi mmoja akigusa kijiko kwa ajili ya chakula.
“Mwanangu laiti kwamba Peter asinge kuwa kijana mwenye muonekano basi ningekukatalia katu katu kuwa naye kimahusiano”
“Hahahaa, kwahiyo baba unapenda kijana mwenye muonekano mzuri?”
 
“Ndio, kwani mimi mbaya. Hata siku ambayo nilimpata mama yako nilikuwa nimevalia vizuri, sikupata shida ya kuzungumza maneno mengi, nilijikuta namchukua kiulaini sana”
Maneno ya Mzee Okocha yakatufanya tucheke sana kwani mbwembwe zake ni sawa sawa na marehemu baba yangu kwani nakumbua kwamba alisha wahi kuniadisia kwamba alimpata mama yangu kutokana na uzuri wake.
“Ila mama alikuwa mzuri sana”
“Ahaahaa ndio maana nikawa naye, wewe ulitaka awe mbaya ili nipate mtoto mbaya. Tazama wewe jinsi unavyo vutia naamini hata Peter umemependa mwanagu?”
“Ndio mzee”
Nilizungumza huku nikitabasamu, ila moyoni mwangu nina wasiwasi na woga mkubwa.
“Hicho ndicho nilicho kihitaji kutoka kwako Peter. Yule mshenzi Thomasi amekuja kunitoa hapa asubuhi asubuhi amenionyesha sikio lake nusu, nikakua kweli bwana kumbe ni mshenzi sana”
 
“Yaani baba laiti kama uneng’ang’ania niendelee kuwa na Thomas, basi muda kama huu ungekuwa umesha ipata maiti yake”
“Hahahaaa nililiona hilo mapema”
Mazungumzo ya Yemi na baba yake, kwa mtu mwenye uelewa wa hali ya juu, nilazima utahisi kuna jambo linalo endelea chini ya hii familia.
“Peter baada ya hapa ninahitaji kuzungumza na wewe maneno mawili matatu nje huko”
“Jamani baba munataka kuwa ninyi peke yenu?”
“Ahaaa kuna mambo mengine ninatakiwa kuzungumza na mkwe wangu peke yetu”
“Sawa”
Tukamaliza kula, mimi na mzee Okocha tukaanza kutembea kutoka katika hii nyumba. Tukatokea kwenye moja ya bustani kubwa na pembezoni kuna bwawa moja kubwa.
“Ahaa Peter wewe umetokea wapi?”
“Nimetokea Kenya mzee”
 
“Sawa sawa, unataka kuniambia kwamab wewe ni mkenya?”
“Ndio ila kwa historia ya mama yangu aliniambia kwamba uhalisia wangu ni hapa Nigeria kwa maana baba yangu alikuwa ni mnigeria”
“Ahaaa sawa sawa, sasa baba yako umeweza kuonana naye?”
“Hapana mama aliniambia kipindi baba anaondoka Kenya, alimuacha akiwa na mimba ya mwezi mmoja na baba wala hakuweza kulitambua hilo. Na kila alipo msubiria aweze kurejea baba hakurejea, hadi nikazaliwa na kuwa mtu mzima kabisa”
“Na mama yupo wapi?”
“Kwa sasa mama amesha fariki”
“Daaa pole sana, unajua kipindi ambacho mke wangu alifariki na kuniacha na Yemi, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa maana tulipendana sana na mama yake”
Mzee Okocha kwa jinsi anavyo zungumza unaweza ukamdhania kwamba ni mtu mwema sana asiye na tabu na mtu ila kwa historia ambayo niliipata yeye na kundi lake basi ni mtu mmoja gaidi sana.
“Thomas aliniambia uwezo wako wa kupambana je ni kweli?”
“Kivipi baba”
“Aliniambia kwamba unajua kurusha ngumi, mateke. Unajua jinsi ya kumzuia adui je ni kweli?”
“Kidogo japo sio sana”
“Sio sana!!?”
Mzee Okocha alizungumza huku akinitazama vizuri usoni mwangu.
 
“Ndio baba”
“Nitahitaji unionyeshe uwezo wako”
“Baba sio sana”
“Huo huo wa sio sana ndio nitahitaji unionyeshe kwa maana nahitaji kukujua wewe vizuri. Kwa maana binti yangu ni mzuri sana, anahitaji kupata mwanaume atakaye mlinda na kumpenda. Endapo mwanangu atakufa mikononi mwako basi nitahakikisha kwamba na wewe ninakuua. Na binti yangu akimuumiza na mimi nitahakikisha ninakuumiza.”
Mzee Okocha alizungumza kwa sauti nzito aliyo zungumza nayo asubuhi, nikabaki nikiwa nimemkazia macho.
“Sawa baba nimekuelewa”
“Na kitu kingine kuna mitihani yangu mitano nitakupatia ukifanikiwa kuipta hiyo basi utaishi na mwanangu na nitawapa kila kitu changu, ila ukishindwa basi nitakuua kimya kimya pasipo mtu yoyote kufahamu, umenipata Peter?”
 
“Ndio nimekupata mzee”
Tukafika kwenye moja ya kiwanja cha mpira wa mikono, mzee Okocha akaka kwenye moja ya kiti, nikataka kukaa akanizuia kwa ishara huku akinitazama usoni mwangu.
“Nahitaji kuuona uwezo wako wa kupigana”
“Ahaa mzee hapa mbona tupo sisi wawili tu nitapigana na nani?”
“Unaweza kupigana na upepo”
“Upepo!!?”
Niliuliza huku nikiwa nimeshangaa, bado nusu tu nimtukane mzee huyu kwani ninamuona ni mwenda wazimu japo nimetumwa kumpeleleza, nimeamua kuikatisha kazi hiyo kutokana na usaliti wa Hawa na raisi Donald Bush.
“Ndio”
Nikasimama huku nikimtazama mzee Okocha vizuri usoni mwake. Nikahisi hatua za mtu akija nyuma yangu kwa haraka nikageuka na kukutana na mwanajeshi mmoja mwembamba na ana urefu kama wangu.
 
“Huyo anaitwa upepo sasa unaweza kupambana naye”
Hapa ndio nikapata maana ya mzee huyu kuzungumza kwamba nitapambana na upepo, taratibu nikavua koti langu la suti pamoja na saa yangu ya kononi, nikaviweka kwenye moja ya kiti kisha nikamgeukia huyu mwanajeshi. Nikamtazama Mzee Okocha, akanikonyeza, nikstukia teke zito la kifua lililo niangusha chini mzima mzima, mwajashi huyu akaanza kunishambulia kwa kasi sana, uwezo wake unaweza kusema ni kama mchina aliye fuzu mafunzo ya kung fu.
Kila nilipo jaribu kujipanga, upepo aliweza kupangua mipango yangu. Sikuweza kurusha ngumi wala teke hata moja, sikuwa na ujanja zaidi ya kuanza kumsoma huyu upepo kuanzia urushaji wake wa mateke hadi ngumi. Kitu nilicho kigundua kwamba mikono yake ndio ina kasi sana kuliko miguu. 
 
“Kwa mtindo huo siwezi kukuachia mwanangu, mwanaume gani wewe”
Mzee Okocha alizungumza maneno ya kejeli huku akinitazama jinsi ninavyo jizoa zoa kunyanyuka chini nilipo anguka, shati langu lote jeuepe limeshafuka kwa fumbi la hichi kiwanja.
    Nikasimama kimtego upepo akajaribu kunikabili kwa mateke ya kuruka hewani, ila nikamkwepa na kumsindikiza kwa teke la mgongo lililo mfanya aanguke kifudifudi kama mzigo, upepo akanyanyuka kwa kasi, pasipo kufikiria kwamba nimemgundua siri ya upiganaji wake, akaanza kunishambulia kama mwanzo. Laiti kama kungekuwa na mashabiki pembeni wanao nishabikia basi wangeweza kunishabikia kwa nderemo na vifijo.
 
Huku si kupiga bali ni kumbuta mwanajeshi huyu anaye itwa upepo, kila alivyo jaribu kurusha ngumi, mimi nilicho kifany ni kuudaka mkono wake na kuhakikisha kwamba ninavunja japo kidole kimoja, upepe alijitahidi kujikaza kuonyesha ukakamavu mbele ya bosi wake ila mbinu na mipango yake yote nilisha itunza kwenye akili yangu.
 
“Khaaghaaaaaa……..”
Upepo alitoa ukelele mkali baada ya kumvuja mkono wake wa kulia hadi mfupa ukatoka nje, nikakamsukuma pembeni upepo na kumfanya mzee Okocha kubaki akiwa ameduwaa, kuona kijana wake anavyo garagara chini. Nikaanza kutembea kwa kujiamini hadi kwenye kiti alicho kalia mzee Okocha, huku nikiwa nimejawa na hasira kali. Nikameza funda zito la mate, taratibu mzee Okocha akasimama huku akiwa ameikunja sura yake.
 
“Usinijaribu tena na vijana wako nitawaua”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, nikabeba koti langu begani, kisha nikaichukua saa yangu na taratibu nikaanza kuondoka hili eneo, nikasikia mlio mdogo wa bastola inayo kokiwa, taratibu nikageuka na kumkuta mzee Okocha akiwa ameninyooshea bastola yake huku sura yake ikizidi kutisha kwa kukasirika.
“Wewe ni nani na unataka nini kwangu”
Mzee Okocha alizungumza kwa sauti nzito ambayo hainitishi kabisa, kwani nikiwa katika hasira huwa ninajiamini kuliko muda wowote ambao ninakuwa tofauti. Taratibu nikaanza kumsogelea mzee Okocha huku akilini mwangu nikitaka kumueleza ukweli kwamba mimi ni Dany na nipo hapa kuhakikisha kwamba ninamkamata yeye na kundi lake lote la boko haramu.
                                                                                     ITAENDELEA
“Je Dany atazungumza ukweli wa yeye ni nani, basi usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimu”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )