Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 7, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 140 na 141 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA     
  
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, nikabeba koti langu begani, kisha nikaichukua saa yangu na taratibu nikaanza kuondoka hili eneo, nikasikia mlio mdogo wa bastola inayo kokiwa, taratibu nikageuka na kumkuta mzee Okocha akiwa ameninyooshea bastola yake huku sura yake ikizidi kutisha kwa kukasirika.
“Wewe ni nani na unataka nini kwangu?”
Mzee Okocha alizungumza kwa sauti nzito ambayo hainitishi kabisa, kwani nikiwa katika hasira huwa ninajiamini kuliko muda wowote ambao ninakuwa tofauti. Taratibu nikaanza kumsogelea mzee Okocha huku akilini mwangu nikitaka kumueleza ukweli kwamba mimi ni Dany na nipo hapa kuhakikisha kwamba ninamkamata yeye na kundi lake lote la boko haramu.
       
ENDELEA   
“Mimi ni mkwe wako mpya na ninacho kihitaji kwako ni mwanao tu, kuna laziada?”
 
Nilimuuliza Mzee Okocha kwa sauti nzito huku nikimkazia macho na yeye, tukatazamana kwa sekunde kadhaa, taratibu mzee Okocha akatabasamu, akaishusha chini bastola yake kisha akaichomeka kiunoni mwake.
“Nimekupenda sana Peter kwa kujiamini kwako”
Mzee Okocha alizungumza huku akinishika bega lang, tukaanza kutembea kurudi sebleni.
“Naamini mwaangu amepata mwanaume sahihi ambaye anaweza kumlinda kwa kila jambo, shida na raha”
“Nashukuru kwa kuligundua hilo”
“Umejifunzia wapi mbinu za kupigana hivyo kwa maana ni watu wachache ambao wanafanya hivyo. Na Upepo ndio kijana wangu mwenye mafunzo ya juu katika jeshi langu hili, na wewe umempiga imekuwaje hapo?”
 
“Mama yangu alipenda kunipeleka katika mafunzo ya karate tangu nilipokuwa mtoto, ukitegemea Kenya kule amani kwa kipindi fulani ilikuwa ni tete, kwa hiyo kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo nilivyo zidi kujifunza na kukomaa kwenye upambanaji tangu nikiwa mtoto mdogo sana”
Niliendelea kumdanganya mzee Okocha, na uongo wangu ninahakikisha kwamba unaendana na ukweli na sihitaji kusahau chochote ninacho kidanganya.
“Kwa sasa ni mapema sana, nitahitaji kuweza kukujua na nitakupatia nafasi katika jeshi langu”
“Kwani mzee una jeshi lako mwenyewe”
“Ahaa siwezi kuzungumza kwa sasa Peter, nitahitaji kukujua wewe vizuri kwanza sawa”
 
“Nimekuelewa”
Tukaingia sebleni, Yemi akasimama kwa haraka kwenye sofa alilo kalia huku akinishangaa nikajitazama shati langu nikakuta likiwa limejaa damu na limechafuka kwa kiasi kikubwa.
“Ni kitu gani kimekupata mume wangu?”
Yemi alizungumza huku akinifwata, mzee Okocha akatuacha wawili na kuelekea kukaa kwenye sofa.
“Ahaa…kuna mazoezi nilikuwa ninayafanya”
“Mazoezi, baba niambie ni kitu gani kinacho endelea”
Yemi alizidi kuhoji maswali huku akiwa katik hali ya kushangaa sana.
“Nilikuwa ninampima mume wako”       
“Unampima kivipi?”
“Nimempambanisha na kijana wangu na amefanikiwa kumpiga”
 
“Nini……baba hivi kweli unaweza kumapambanisha mwanaume ninaye mpanda na hao watu wako wa ajabu ajabu”
“Nimefanya hivyo kwa ajili ninahitaji kumjua Peter, ni mwanaume wa aina gani unahisi ninaweza kukukadhibi kwa mwanaume mjinga mjinga ambaye hata yeye mwenyewe anashindwa kujilinda?”
Mzee Okocha alizungumza kwa ukali kidogo huku akisimama kwenye sofa kwani Yemi anaonekana kukasirika kwa jambo hili.
“Hata kama baba unahitaji kumpima mwanaume huyu, ila unatakiwa kunijulisha mimi kwanza. Je angekufa au angeumia?”
 
“Haujaumia na wala hajakufa”
“Baba hii sio haki kabisa, sinto penda Peter ajihusishe kwenye biashara zako na watu wako”
“Lazima Peter ardhi kiti changu na hakuna mwengine wa kukirithi ikiwa wewe ni mtoto wa kike na hauna wazo lolote juu ya hili jeshi langu ninalo endelea kuliunda siku hadi siku”
Kukaripiana kwa Yemi na baba yake kunaanza kunipa picha halisi ambayo nilisha simuliwa na Hawa.
“Baba siwezi kuruhusu Peter kujiunga na yeye, tuachie maisha yetu. Tuache tuishi sisi wawili, niachie mwanaume ninaye mpenda aishi kwa amani”
Yemi alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakimwagika usoni mwake.
 
“Nakupenda mwanangu na ninawapenda nyinyi nyote wawili, ila sina jinsi ni lazima Peter awe”
“Kwa nini huja jinsi baba yangu eheeheee?”
“Kwa sababu ninakufa”
Maneno haya yakastua mimi na Yemi, taratibu Yemi akaanza kumsogelea baba yake huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Nina miezi michache ya kuishi mwanangu, nimeishi na sataratni ya damu kwa damu kwa mwaka sasa, daktari ameniambia kwamba siwezi kumaliza huu mwaka ni lazima nitakufa. Ni nani atakuwa muangalizi wa hili jeshi, nani atatimiza ndogo zangu za kuikomboa hii nchi kutoka mikononi mwa viongozi wala rushwa, viongozi wabinafsi, ni nani mwamngu?”
Mzee Okocha alizungumza huku machozi yakimwagika, taratibu nikajikuta nikimuonea huruma mzee huyu.
“Baba kwa nini unakuwa msiri kwa kipindi chote hicho na huniambii ukweli?”
 
“Sikuhitaji kukupa hofu mwangu, sikuhitaji uishi kwa mawazo ukinifikiria mimi, nilihitaji kujiua tu mimi mwenyewe, ili nisife nikiwa kitandani. Tafadhali Yemi elewa hichi ninacho kuambia mwanangu, mumeo Peter ndio anajukumu la kuiongoza hili jeshi”
Taratibu Yemi akamkumbatia baba yake huku wote wakilia kwa uchungu, nikajikuta machozi na mimi yakinimwagika, ila taratibu nikajifuta huku nikitazama chini.
“Peter”
Niliisikia sauti ya mzee Okocha akiniita, taratibu nikanyanyua sura yangu na kumtaza, kwa ishara ya mkuno akaniita, nikatembea kwa hatua za taratibu hadi sehemu walipo simama.
“Umesikia mambo mengi ambayo kwa sasa sikuhitaji uweze kuyasikia, ila umeweza kuyasikia, je ninaweza kumuamini?”
Mzee Okocha na Yemi wakabaki wakinitazama usoni mwangu kwa sura zilizo jaa majonzi.
“Ndio mzee unaweza kuniamini”
“Nahitaji kesho Mungu akibariki tuzungumze mambo mengi sana juu yengu. Kwa sasa ninawaomba nikapumzike”
Mzee Okocha akamuachia mkono Yemi na kuanza kuondoka katika hili eneo, taratibu tukamsindikiza kwa macho akipandisha gorofani hadi akapotea kwenye usawa wa macho yetu.
 
Yemi akanikumbatia kwa nguvu huku akilia, sikuwa na jinsi zaidi ya kuhakikisha kwamba ninambembeleza Yemi. Taratibu tukaelekea katika chumba tulicho andaliwa kulala. Yemi hakuwa na furaha yoyote zaidi ya kukaa kwenye sofa huku amejikunyata sana. Taratibu nikavua shati langu lenye damu iliuyo kauka, nikaingia bafuni, huku nikiwa na mawazo mengi kichwani mwangu, kwani kazi ambayo imenilete huku tayari imesha ingia doa.
 
‘…..Je ninaweza kukuamini?’
Kauli ya mzee Okocha ikajirudia kichwani mwangu, nikajikuta nikifumba macho huku nikiwa nimesimama mbele ya kioo kikuba kilichopo humu bafani.
‘Mungu nisaidie katika hili’
Nikafumbua macho yangu, nikaanza kunawa mikono yangu pamoja na uso wangu, nikamaliza, nikatoka bafuni humu, nikamkuta Yemi akiwa bado amejikunyata kwenye sofa huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Mpenzi wangu”
Nilimuuita Yemi kwa sauti ya upole na unyonge huku nikikaa pembeni yake, Yemi akanitazama tu usoni mwangu, taratibu nikamsogeza karibu yangu na kichwa chake akakilaza kifuani mwangu.
“Peter baba yangu anakwenda kufaa, nitabaki peke yangu”
“Shiiiiiii….nipo kwa ajili yako mke wangu”
“Peter, natambua sijakueleza ukweli wowote kuhusiana na maisha ya hii familia yangu, najua utaniacha ukiujua ukweli”
“Siwezi kukuacha mke wangu, nipo hapa kwa ajili yako sawa”
 
“Kweli mume wangu?”
“Kweli”
“Nahuahidi nitakuwa pembeni yako hadi mwisho wa uhai wan…….”
Sikumalizia sentensi yangu mlango wa chumbani kwetu ukangogwa kwa nguvu. Tukatazamana na Yemi, kwa haraka nikanyanyuka na kuanza kutembea kuelekea mlangoni, nikaufungua mlango kwa umaikini mkubwa, nikakutana na na mwanajeshi mmoja, akanipigia saluti.
“Muheshimiwa mzee amenguka ndani kwake na hali yake ni mbaya”
“Nini”
Nikamuona Yemi akinyanyuka kwa haraka kwenye sofa na kuja mlangoni nilipo simama.
“Unasema baba yangu amenguka?”
“Ndio muheshimiwa, daktari anajitahidi kumuhudumia”
“Ohooo Mungu wangu”
Tukatoka kwa kasi huku mweanajeshi huyu akituongoza, tukafika chumbani kwa mzee Okocha tukakuta baadhi ya wanajeshi wakimnyanyua na kumuweka katika kitanda cha matairi.
 
“Imekuwaje”
Niliuliza huku nikimwa nimemshika Yemi mkono wa kulia, kwani pasipo kufanya hivi anaweza kuanguka na yeye.
“Hali yake ni imezidi kuwa mbaya inabidi kumuwahisha hospitalini haraka iwezekanavyo”
“Baba…. Baba”
Yemi aliita huk machozi yakimwagika, wanajeshi hawa wakaanza kukisukuma kitanda cha mzee Okocha huku nasi tukifwata kwa nyuma. Mwajeshi mmoja akanipatia tisheti ya jeshi, nikaivaa kwa haraka kw amaana nipo tumbo wazi. Tukaingia kwenye gari la wangonjwa huku tukiwa na daktari wa jeshi.
 
“Baba yangu nini nini kimempata dokta?”
“Presha imepanda”
“Presha tu ndio inapelekea hivi?”
Ilinibidi kumuuliza daktari. Daktari akatutazama kwa macho ya wasiwasi, nikaweza kuitambua hali aliyo kuwa nayo, nilicho kifanya ni kumkonyeza tu asizungumze chochote mbele ya Yemi. Tukafanikiwa kufika kwenye hospitali ambayo wala sikuifahamu inaitwaje huku tukiwa na ulizi wa wajeshi zaidi ya ishirini. Mzee Okocha akapokelewa na madkatari wa hii hospitali, na moja kwa moja akakimbizwa kwenye chumba cha duma ya matibabu.
“Baba atapona kweli?”
Yemi aliniuliza huku akiendelea kuliaa.
“Atapona mke wangu, kikubwa tumuombe Mungu katika hili”
“Ohoo Mungu wangu msaidie baba yangu mie”
Yemi alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu, simu yangu mfukoni ikaita taratibu nikamuchia Yemi, na kumuomba niweze kupokea simu hii.  Nikasogea pembeni umbali kidogo kutoka kwenye chumba alicho ingizwa mzee Okocha, ila ni kwenye kordo hii hii tuliyopo. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta ni namba ya meja ndio anaye nipigia.
 
“Ndio meja?”
“Dany upo kwenye hatari”
“Hatari?”
“Ndio muheshimiwa raisi ametuma kikosi cha  makomandoo sita na amawaagiza waweze kukuangamiza, ni kutu gani kinacho endelea Dany kwa maana nashindwa kuelewa”
Taarifa hii ikanistua sana jambo lililo nifanya nigeuke na kumtazama Yemi, nikamuona akiwa amekaa kwenye kiti huku amejiinamia chini akiendelea kulia. Nikawatazama wanajeshi hawa walio jipanga nje ya mlango wa hii hospitali.
“Dany unanisikia?”
“Ndio meja ninakusikia”
“Ni kitu gani kinacho endelea?”
“Raisi ana mahusiano na mke wangu”
“Nini?”
 
“Nilipiga simu asubuhi, kwa bahati nzuri kwangu, raisi alipoke pasipo kufahamu kama amepokea simu yangu, niliweza kusikia miguno ya kimapenzi, na inavyo onyesha walikuwa katika hatua ya mwisho mwisho kumalizia kufanya mapenzi. Raisi alimuomba mke wangu aweze kunishuhulikia na kuniondoa duniani japo Hawa alimsisitizia aniache peke yangu ila ndio hivyo ameamua kufanya maamuzi yake”
“Na alitambua kwamba umewasikia?”
“Ndio”
“Shitiiitiii, ni ujinga gani anao ufanya sasa”
“Meja nisiwe muongo kwako wala mnafki, nimeamua kuachana na hii kazi, kama ameamua kuniua basi acha aniue, ila sinto kufa kijinga kiasi hicho anacho fikiria nitahakikisha kwamba kila anaye mtuma kwangu ni lazima na mimi niweze kumuua”
 
Nikamsikia meja akishusha pumzi nyingi
“Muheshimiwa raisi ametusaliti, na siwezi kupinga katika hilo, ninatakia maisha mema Dany ila hakikisha kwamba unakuwa salama”
“Nashukuru Meja na Mungu akubariki katika hili, kwani taarifa yangu itayaokoa mausha yangu”
Nikakata simu, kitendo cha kuirudisha mfukoni nikaanza kusikia milio ya risasi ikirindima kwa nje jambo lililo wafanya wanajeshi walipo katika eneo hili kujiweka sawa kwa mashambulizi. Nikakimbilia hadi sehemu alipo kaa Yemi anaye shangaa shangaa. Nikamshika mkono na kumnyanyua, nikaufungua mlango wa chumba cha alicho ingizwa mzee Okama tukawakuta madaktari wakiendelea kutoa huduma kwa mzee Okama.
“Hamtakiwi kuingia humu ndani kwa sasa”
Daktari alizungumza huku akitutazama kwa mshangao.
“Tunatakiwa kumuondoa mzee hapa sasa hivi”
“Siwezi”
Nikamuachia Yemi mkono, nikamshika daktari na kumvuta daktari hadi nje ya chumba alipo sikia milio ya risasi akabaki akiwa anatetemeka kwani hali ya usalama katika eneo la hii hospitali inazidi kuwa mbaya kadri muda unavyo zidi kwenda.
                                                                                    
AISIIIII……….U KILL ME 141

   
“Sasa fanya iwezekanavyo, ninaihitaji kuondoka na mzee hivi sasa”
“Sawa sawa”
Daktari alizungumza huku akizidi kutetemeka, mwanajeshi mmoja akachomo bastola yake kiunoni na kinipatia.
“Hakikisheni munawazuia”
“Sawa mkuu”
Nikaingia ndani ya chumba, daktari wakamuandaa mzee haraka haraka.
“Mke wangu ninakuomba ujikaze sawa”
Nilizungumza huku nikimshika Yemi mashavu yake huku nikiwa nimekazia macho kwani muda wote huu anatetemeka mwili wake. 
 
“Umeniaelewa?”
“Ndio honey”
Nikaikoku bunduki yangu vizuri, nikafungua mlango na kuchungulia nje, wanajeshi wote nilio waacha nje dakika kadhaa wote nikakuta wamefariki dunia, na kwenye hii kordo hakuna mtu yoyote jambo lililo nifanya nirudi ndani huku nikiwa na wasiwasi mwingi.
“Kuna nini?”   
Yemi aliniuliza huku akitetemeka mwili wake.
“Wanajeshi wote wamekufa”   
“Ohoo Mungu wangu”
“Shiiiiii”
Nilimnyamazisha Yemi baada ya kusikia miguu ya watu wakinyata, kwa haraka nikatazama ndani ya hichi chumba, nikaona mtungi wa gesi. Nikauchukua kwa haraka, kila mtu ndani ya chumba hichi akabaki akinishangaa.
 
“Jificheni”
Nilizungumza huku nikimtazama Yemi usoni mwake. Kwa haraa kila mtu akajibanza kwneye sehemu yake, nikabaki nikiwa nimesimama mlangoni, kwa haraka nikauufiringisha mtingi huu wa gesi chini, kuelekea kwneye kordo. Wavamizi hao wakaanza kushambulia kwa risasi.
“Musipige risasi”
Nilisikia sauti kubwa ya mmoja ya wavamizi hawa, kwa uwazi mdogo wa mlango nilio ucha, unaifanya kuuona mtungi wa gesi, taratibu nikafumba jicho moja huku nikiwa nimeunyooshea bastola yangu, kwa risasi mbili za uhakika zilizo tua juu ya mtingi huu wa gesi, ukaufanya kulipuka, na kusababisha mttemeko mkubwa huku vilio vya wavamizi hawa vikisikika, kwa haraka nikafungua mlango, kila mvamizi aliye hai, nikaahakikisha ninampiga risasi risasi ya kichwa na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake. Wavamizi hawa wapo sita na wamefunika nyuso zao na kubakisha macho yao tu, kwa haraka nikaanza kumvu mvua mmoja baada ya mwengine kinyago alicho jifunika usoni mwake. Kila niliye mfunua ana sura ya kimarekani, hapa ndipo nikaamini kwamba raisi Donald Bush amaeamua kutangaza vita na mimi. 
 
Nikaanza kugagua eneo zima la kutoka nje ya hii hospitali, nilipo hakikisha kwamba usalama upo wa uhakika nikarudi katika chumba walipo Yemi madaktari pamoja na baba yake.
“Tuondokeni”
Nilizungumza huku nikikishika kitanda cha Mzee Okocha, tukaanza kukivuta kuelekea nje, huku nikiwa makini sana. Tukafika sehemu yenye lilipo gari la wagonjwa, tukamuingiza mzee Okocha ndani ya gari.
 
“Mke wangu tangulieni nyumbani, kuna kazi nina imalizia hapa”
“Unasemaje Peter?”
“Umenisikia Yemi tangulieni nyumbani na baba kuna kazi ninaimalizia kukaa kwenu hapa kutahatarisha hali ya baba. Wewe dokta endesha gari”
“Sawa mkuu”
“P…..”
“Tafadhali Yemi nenda nyumbani”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimuingiza Yemi ndani ya gari na kuufunga mlango, daktari akawasha gari na kuondoka eneo hili. Nikato simu yangu mfukoni na kurudi nayo ndani huku nikiwa makini sana. Nikaanza kuchukua video ya maiti za Wamarekani hawa pamoja na wanajeshi wa mzee Okocha kisha nikajirekodi na mimi.
 
“Najua sina hatia katika hili, ila muheshimiwa raisi umenisukuma katika hili. Sikutarajia kwamba unaweza kutembea na mke wangu Hawa, kisha ukanitumia wanajeshi wako waje kuniangamiza, ila waliweza kuwaua wanajeshi hawa, wakiamini kwamba hata mimi wataweza kuniua kirahisi. Muheshimiwa raisi, usihitaji kuirudisha nchi yako katika dhama za Osama Bin Laden kwa maana kwa ujinga wako utapelekea melfu ya watu wako kuweza kuangamia kisa mwanamke, kama unajipenda ni bora kuachana na hii vita. Ulinituma kufanya kazi ya upelelezi, ila kuanzia sasa hivi muheshimiwa raisi, sinto weza kufanya hiyo kazi, nitaishi maisha yangu ya kawaida, na sinto hitaji kabisa kujihusisha na maisha ya kulipiza visasi, yaliyo pita acha yapite. Niawatakie maisha mema wewe na Hawa”
 
Baada ya kumaliza kuzungumza hivi, video hii nikamtumia raisi Donald Bush kupitia mtandao wa WhatsApp.  Nikatoka nje na kuingia kwenye moja ya gari na kuanza kufukuzia gari la wagonjwa huku akilini mwangu nikiwa na mawazo mengi sana ya kufikiria kitu alicho kifanya raisi Donald Bush.
‘Sinto mlipizia kisasi’
Nilijikuta nikizungumza hivyo, huku nikizidi kuendesha gari langu kwa kasi sana. Nikafanikiwa kuwafikia, nilicho kifanya ni kulipita kwa kasi na kuongoza msafara huu mfupi, uzuri wa kichwa changu huwa nikipita sehemu mara moja ni ngumu kunitoka kichwani mwangu. Tukafika katika jumba la mzee Okocha na kukuta wanajeshi wake wakiimarisha ulinzi mkali, wanajeshi wakisaidiana na madaktari hawa wawili tulio kuja nao, wakamshusha mzee na kumpeleka ndani, huku Yemi akifwata kwa nyuma.
“Muheshimiwa”
Mwanajeshi mmoja aliniita huku akisimama mbele yangu, akanipigia saluti kwa ukakamava.
“Ndio kaka unahitaji nini?”
“Kuanzia hivi sasa wewe ndio mkuu wa jeshi letu”
“Nani kasema hivyo?”
Mwanajeshi huyu akanikabidhi simu ndano yenye video inayo muonyesha mzee Okocha akizungumza.
 
“Watu wangu wa Boko haramu, ninaimani kwamba nimetengeneza hichi kikosi kwa miaka zaidi ya kumi na tano sasa. Nimekuwa nikiliongoza kuhakikisha ninapambana na rusha zote zinzo endelea ndani ya nchi hii. Kwa sasa hali yangu ni mbaya, muda wowote na siku yoyote ninaweza kufa. Baada ya kifo changu, nitahitaji Peter mkwe wangu achukue nafasi yangu. Ninaimani kupitia yeye malengo ya boko haramu yatasonga mbele na atapigania haki kama nilivyo kuwa ninapigania mimi. Ninawaomba muweze kufwata amri yake na kila kitu atakacho waeleza muweze kufwata. Niwatakie mafanikio mema”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi huku nikimalizia kuitazama video hii.
“Mkuu turuhusu tuweze kuvamia kwenye kambi ya jeshi la nchi hii”
“Bado mapema, tuangalie afya ya mzee”
Nilizungumza huku nikimkabidhi jamaa huyu simu yake, nikaanza kutembea kwa kujiamini kuelekea ndani, nikamkuta Yemi akiwa amesimama sebleni huku uso wake ukiwa umelowana kwa machozi. Nikamsogelea na kumkumbatia taratibu.
“Mungu atasaidia baba atapona”
“Kweli Peter?”
“Ndio niamini mke wangu, baba atapona”
Tukaendelea kukumbatiana na Yemi huku kila mmoja akiwa katika hisia za majozi. Tukaachiana taratibu na kukaa kwenye sofa huku sote tukiwa tunashauku ya kuhitaji kufahamu hali ya mgonjwa inaendeleaje.
 
“Peter”   
“Naam”
“Ndani ya hospitali ulirudi kufanya nini?”
“Tutazungumza badaye mke wangu, kwa sasa tumuombee baba sawa mke wangu”
“Sawa mume wangu, ila nilikuwa ninahitaji niweze kufahamu tu, kwa maana kwa sasa nina ogopa, kwani sijajua ni kwa nini tulivam……..”
Tukajikuta tukikaa kimya huku tukinyanyuka kwenye sofa, macho yetu yote tukawa tumeyatupia usoni mwa daktari huyu aliye toka katika chumba alicho lazwa baba.
“Dokta baba yangu anaendeleaje?”
Daktari uso wake unaonekana kujawa na huzuni kubwa, taratibu akavua miwani yake na kujifuta machozi yanayo mlenga lenga. Kwa upande wangu nikawa nimegundua kwamba tayari mzee ameiaga dunia.
 
“Dokta niambie baba yangu anaendeleaje?”
Yemi alizungumza kwa sauti kubwa huku akimshika daktari, koti lake na kuanza kumtingisha kwa nguvu.
“Muheshimiwa hatupo naye tena duniani”
Yemi akamtazama daktari huyu kwa sekunde kadhaa, gadla akalegea na kuanza kwenda chini, kabla hjafika chini nikamuwahi kumdaka asianguke. Nikamnyanyua kwa haraka na kuamlaza kwenye sofa,  nikamfungua kifungo cha suruali yake.
“Amepoteza tu fahamu, la atakuwa sawa”
Daktari alizungumza huku akimtazama Yemi usoni mwake. Sikuweza kuzungumza kitu chochote kwani siku ya leo kwangu imekuwa ni ndefu sana tangu jana usiku, nikajikuta nikikaa kwenye sofa huku nikimtazama Yemi aliye lala tuli.
“Samahani tulijitahidi kadri ya uwezo wetu ila imeshindikana kabisa, ninakuomba unisamehe katika hilo”
Daktari aliendelea kuzungumza kwa sauti ya upole na unyeyekevu. Nikasimama wima na kutoka nje, nikamuita mwanajeshi mmoja.
 
“Ninaomba unikusanyie wanajeshi wote sehemu husika, nina mazungumzo nao”
“Sawa mkuu”
Nikarudi ndani, kwa haraka na kueleka katika chumba ilipo maiti ya mzee Okocha. Nikamkuta daktari akiwa amesimama pembeni huku amejawa na huzuni kubwa.
“Alizungumza neno gani kabla ya kufa kwake?”
Daktari akatingisha kichwa akiniashiria kwamba mzee hakuzungumza kitu chochote kabla ya kufa kwake. Nikampima mzee Okocha kwa vidole vyangu pambenizoni mwa shingo yake, na nikadhibitisha kwamba mzee Okocha amefariki dunia.
“Muandaeni mzee”
“Sawa mkuu”
Nikatoka nje ya hichi chumba, nikawakuta wanajeshi wawili wakiwa wamesimama wakinisubiria.
“Mkuu tayari tumesha kusanyika”
“Wewe baki hapa mlinde mke wangu, wewe tuongozane”
“Sawa mkuu”
Tukatoka nje na mwanajeshi huyu, tukaelekea kwenye kiwanja kimoja na kuwakuta wanajeshi zaidi ya elfu moja wakiwa wamesimama kwenye mistari iliyo nyooka. Nikasimama sehemu ya juu ambayo wanajeshi waote wanaweza kutuona.
 
“Hivi hapa ndio makao makuu ya hili jeshi?”
“Hapana makao makuu yapo nje ya mji huu”
“Kuna wanajeshi wangapi?”
“Zaidi ya laki mbili na nusu”
“Safi”
“Hapa utachukuliwa video moja kwa moja na itarushwa kwenye makao makuu na wanajeshi wote huko pia watakuwa wanakuona muheshimiwa”
“Sawa”
Baada ya kumaliza kuzungumza na huyu mwanajeshi niliyte kuja naye hili eneo. Nikawatazama kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari ni nini ninaaweza kuzungumza.
“Wanajeshi wezangu, ninaimani hili ninalo kwenda kulizungumza litakwenda kuumiza moyo wa kila mmoja ila hakuna budi zaidi ya kulizungumza.”
Nikameza mate kidogo huku nikiwa nimesimama kikamavu.
“Mzee wetu, mkuu wetu amefariki dunia dakika kumi zilizo pita, kufariki kwake dunia kumesababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu aliyo kuwa anaishi nayo kwa mwaka mmoja sasa”
 
Nikaona baadhi ya wanajeshi wakidondokwa na machozi, ila hawakutingishika wala kulaza vichwa vyao chini na wamesimama kwa ukakamavu ule ule nilio wakuta nao.
“Mzee ameniachia kiti chake, si kwasababu mimi ni bora zaidi yenu au kwasababu ni mkwe wake. Ila ni Mungu mwenyewe ndio amenilete hapa. Nitahakikisha kwamba ninaongoza jeshi la Boko haramu kuwaangusha viongozi wote mafisadi, wala rushwa na ving’ang’anizi wa madaraka. Na vifo vya wanajeshi walio kufa hospitalini ni lazima wamarekani waweze kulipa hilo”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwatzama wanajeshi hawa.
“BOKO HARAMUUUUUUUUUU”   
Nilizungumza huku nikinyoosha mkono wangu wa kulia juu, wanajeshi wote wakaitikia kwa sauti ya pamoja iliyo nipa matumaini na kujiamini kwamba nina uwezo wa kuongoza wanajeshi hawa katika kutimiza ndoto alizo kuwa nazo mzee Okocha na zikatimia.
                                                                                     ITAENDELEA
“Je raisi Donald Bush ataweza kumuacha Dany katika vita hii ya mapenzi, usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimua”

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )