Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, November 10, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 144 na 145 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
       
Muda wa kusoma risasa ukafika, yemi akasimama na kusogela jukwa maalumu, akaanza kusoma risala ya baba yake huku akito historia ya baba yake. Hadi anamaliza machozi yakawa yanashuka kwenye uso wake nikasimama na kumsogelea hadi sehemu simama nikamkumbatia taratibu huku macho yangu yakiwaangalia wageni waalikwa. Macho yangu yakafika kwa K2 ambaye naye ananitazama, kwa ishara ya mkono akanionyeshaea ishara ya kunikata shingo yangu, jambo lililo nifanya nizidi kumchukia hadi nikahisi moyo wangu ukitaka kupasuka kwa maumivu haya ninao yasikia.
   
ENDELEA           
Taratibu nikamrudisha Yemi kwenye kiti alichokuwa amekaa, nami nikaka kwenye kiti changu huku nikiifikiria ishara ambayo K2 ameweza kunifanyia. Ratiba ya mazishi ikaendelea, ikaanza kupigwa mizinga kama kanunu ya kijeshi inavyo kuwa, endapo anakufa kiongozi wa jeshi au kiongozi wa juu katika serikali, basi mizinga kadhaa hupigwa hewani ikiwa ni heshima ya kijeshi. Muda wa kumzika mzee Okocha ukawadia, sote tulipo katika hili eneo tukasimama, na tukawashuhudia wanajeshi wanavyo shusha mwili wa mzee huyu kwenye kaburi, jambo lililo mfanya Yemi kushindwa kujiazuia na kuangua kilio kikali sana. 

Nikamkumbatia kwa nguvu kifuani mwangu huku nikimuomba atulie, sikuhitaji kushuhudia jinsi mzee huyu anavyo fukiwa kwani Yemi analia kiasi kwamba anashindwa hata kusimama. Taratibu nikamnyanyua na kuandoka naye katika hili eneo na kurudi katika jengo lenye chumba chetu.
“Peter nitaishi vipi bila baba yanguu…..”
Yemi alizungumza huku akizidi kulia kwa uchungu sana.
“Nipo mke wangu, nipo usilie tafadhali kwa maana hii yote ni kazi ya Mungu ukilia sana utamkufuru Mungu”
 
Yemi akaendelea kulia, huku kichwa chake akiwa amekiegemeza kifuani mwangu. Zaidi ya lisaa moja nikawa na kazi ya kumbeleza Yemi hadi akapitiwa na usingizi, nikamlaza vizuri kwenye sofa hili tulilo kalia, nikachukua shuka na kumfunika mwili mzima na kumuacha kichwa tu.
Nikatoka nje, huku akili yangu kwa sasa ikianza kuwaza ni jinsi gani ninaweza kumzuia K2.
“Generali”
Mwanajeshi mmoja aliniita huku akinipigia saluti, nikasimama na kumtazama.
“Ndio”   
“Kuna kikao katika chumba kikuu, wageni rasmi wanakusubiria”
“Kikao kaitisha nani?”   
“Meja”
 
Nikamtazama mwanajeshi huyu, kisha nikaanza kuongozana naye. Tukafika katika ofisi inayo fanyikia kikao, kabla ya kuingia, nikawatazama wanajeshi pamoja na walinzi mbali mbali walio jipanga nje ya hii ofisi, wakiwasubiria mabosi wao waliomo ndani ya hichi kikao, kisha nikamruhusu mwanajeshi huyu kunifungulia mlango. Nikaingia nda na kuwakuta wageni waalikwa wakiwa wamekaa kwenye viti, walipo niona wote wakasimama kwa ishara ya kuniheshimu. Ni kiti kimoja tu ambacho hakina mtu, na ndio kiti ambacho ninastahioli kukalia kwani kwenye meza kuna kibao chenye jina langu la uongo ambalo ni Peter.
Nikafika kwenye kiti changu, nikawatazama wageni walikwa wote, kisha kwa ishara nikawaruhusu kuweza kukaa chini nami nikaa. Meja katika sehemu aliyo kaa, akasimama kikakamavu huku akinitazama usoni mwangu.
“Kwanza ninaomba radhi jenerali kwa kuitisha kikao kabla sijakutaarifu ila niche ni kikao cha dharura na ningeomba uweze kusikiliza kile washirika wanao unda kundi la boko haramu wanahitaji kuzungumza na wewe. Nina imani ni mgeni kwenye jeshi hili, ila ninaimani kwa kuzidi kuelekezana utaweza kuelewa ajenda zote za kundi hili.”
 
Nikatingisha kichwa huku nikimkubalia meja msamaha hawake, watu wengi waliomo kwenye hii ofisi ni wazee walio nipita umri na wengine ni kama baba zangu.
“Kwa sasa wewe ndio  kiongozi wa boko haramu, je ni kipi unacho weza kuufanyia huu umoja ili ufanikiwe kufika malengo yake”
Mzee mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama usoni mwake.
“Nitasimama katika malengo aliyokuwa nayo mzee Okocha na nitahakikisha kwamba Boko haramu inazidi kusonge mbele na kuwa ni kundi lenye nguvu kubwa duniani kama ilivyo kwa makundi kama Alquida”
 
“Muheshimiwa jenero, imejipanga vipi kukabiliana na nchi kubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambazo kila siku zinajaribu kuongeza wataalumu wa kijeshi katika kufundisha wazawa hususani wanajeshi wa kiserikali, il badae waje kuangusha hili kundi na kulifuta kabisa kwneye ramani ya dunia?”
“Nitaanzisha mkakati wa kupandikiza watu watu katika kila jeshi la nchi hususani hapa Nigeria, Marekani na sehemu nyingine. Watu hao nitahakikisha wanafanya kazi nasi kufahamu ni kitu gani majeshi hayo yanapanga, hiyo ni moja. Mbili nitaanzisha kikosi cha mauji kwa wasaliti wote ambao watajaribu kuuza siri ya umoja huu, sinto jali ni kiongozi ndani ya kundi hili au upo nje ya kundi hili, nitakacho hakikisha ni kwamba ninakuteketeza wewe na familia yako. Swali jengine”
 
Nilizungumza kwa kujiamini na msisitizo na kuwafanya watu hawa kutazamana, hadi K2 mwenyewe, akabaki akinikodolea macho tu.
“Sisi tumewekeza pesa zetu kuhakikisha kwamba jeshi hili linaitumia pesa hiyo katika kuchukua sehemu tofauti za kibiashara na kuziweka chini ya ungalizi  na kuendesha biashara ya eneo hilo na pesa zetu ziweze kurudi, sasa wewe una mpango gani katika hilo?”
Mzee huyu alizungumza na kunifanya nimtazame kwa sekunde kadhaa kwenye macho yake hadi akatazama chini.
“Unaweza kuitoa pesa yako”
Nilizungumza kwa msisitizo na kuwafanya viongozi hawa kuanza kunong’ona nong’ona.
 
“Mimi nikijana, ninauwezo wa kuchukua silaha na kwenda kupigana na vijana wangu. Nitajitolea maisha yangu kwa ajili ya hilo. Wewe huwezi kukaa huko ulipo na familia yako na ukategemea sisi kupambana au vijana wangu wapambane kwa ajili yako na wewe upate faida na uendelee kuishi maisha ya furaha na amani ikiwa damu za wanajeshi wangu zinamwagika. Kumbukeni hawa ni watu na si kuku au ng’ombe. Na nitoe angalizo katika hilo endapo unategemea kujitoa katika huu umoja, nitahakikisha kwamba ninaipiga nchi yako na kuichukua, hususani katika vitega uchumi unavyo vitegemea”
Wazee wote wakaka kimya huku wakinitumbulia macho, kwani utaratibu nilio  kuja nao hapa ninaimani kwamb ni mpya na kila mmoja utakuwa umemuudhi kwa namna moja ama nyingine.
“Swali jengine?”   
K2 akanyanyua mkono kidogo ili kuomba nafasi ya kuzungumza, nikajikuta tumbo likinicheza kidogo kwa woga kwani sijui anataka kuzungumza kitu gani.
“Zungumza”
 
“Je tukiamua kuzitoa pesa zetu kwenye huu umoja wanajeshi wako si watakufa kwa njaa?”
Swali la K2 likanifanya nishushe pumzi taratibu huku nikiuzuia woga wangu ambao tayari ulisha nitawala mwili wangu wote.
“Kama ulisha ingia kwenye hichi chama, sinto kuruhusu utoke na hilo ninaomba liweze kujulikana kwenu nyote”
“Ila jenero hiyo sio haki na hilo sio alilo kuwa akilifanya jenero aliye pita, kwa maana hichi chama alikiendesha kwa umoja  na upendo ndio maana leo hii tumekuja kumzika?”
“Huu pia ni umoja na upendo ambao nyote mutaupenda. Malengo hayawezi kufika kwa kuchekeana au kuogopana kwa kuwekeza pesa zenu. Malengo yatafika kwa kuhakikisha kwamba heshima inatawala ndani ya hili kundi.”
Msisitizo wangu ukawafanya viongozi hawa kuonekana wakiwa wamejawa na mawazo mengi vichwani mwao nina imani nitakuwa nimependekeza hali ya kuogopwa kwa kila kiongozi.
 
“Sioni cha maana ninaondoka zangu hapa”
Mzee mmoja alizungumza huku akirudisha kiti chake nyuma, kwa haraka nikasimama na kutembea hadi sehemu aliyo simama. Watu wote ndani ya hii ofisi wakabaki wakitutazama.
“Unahitaji kufa?”
Nilimuuliza kwa sauti ya upole huku nikiwa nimemkazia macho.
“Utaongozaje jeshi kwa namna hii?”
“Unahitaji kufa?”
Nikaongeza ukali wa sauti yangu, mzee huyu akabaki akiwa amenikodolea macho, kitu ambacho kinawaogopesha viongozi hawa humu ndani  wote hawanijui uhalisia wangu kwamba mimi ni mtu wa aina gani, ila K2 pekee ndio anaye nifahamu na yeye ananijua akili yangu jinsi ilivyo.
“Kaa chini kikao bado hakijaisha”
 
Taratibu mzee huyu akaka kwenye kiti cheka, nikamsaidia kukisukuma mbele kidogo kwa mana ni kiti cha matairi.
“Ninaimani nyinyi nyote hamunitambu, na kupewa nafasi hii ya kuongoza hili kundi sijapewa kwa bahati mbaya au makusudi. Nina uwezo wa kuongoza, ninajua cha kufanya ndio maana mzee Okocha aliweza kunipatia nafasi hii. Mzee Okocha anaujua ukweli wa maisha yangu”
Ilinibidi kudanganya kidogo ili kumtoa K2 kwenye mawazo ya mpango wa kuhitaji kuelezea ukweli kuhusiana na mimi mbele ya viongozi hawa ambao tayari sasa akili na mioyo yao inachemka kwa kuwazia uongozi wangu.
“K2 naye anajua ukweli wa maisha yangu”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama nyuma ya kiti cha K2, viongozi wote wakanitazama, nikaona jinsi kifua cha K2 kinavyo shusha pumzi nyingi kwani tayari nimesha muingiza kwenye mikono yangu tofauti na alivyo kuwa akifikiria.
“Raisi Donald Bush anajua ukweli wa maisha yangu. Je wewe, wewe, wewe, wewe, wewe na wewe munaufahamu ukweli wa maisha yangu?”
 
Niliwauliza viongozi baadhi kwa kuwanyooshea kidole changu, wote wakatingisha kichwa kukiri kwamba hakuna anaye nifahamu mimi.
“K2 unaweza kuwaleza wezako mimi ni nani?”
Nilizungumza huku huku nikikaa kwenye kiti changu, nikamuona jinsi K2 anavyo pata kigugumizi cha kuzungumza, moyoni mwangu nikajikuta nikianza kushangilia kwa kumuu K2 kiakili na sasa nitahitaji kumuu kimwili.
“Haloooo K2, mbona kimya?”
“Ahaa….ahaa…….”
Meja akabaki akinitazama huku amenitolea macho ya mshangao, mshangao wake ukaendelea kwa kumtazama K2.
“Ameshindwa kuzungumza. Basi kati yenu musihitaji kunijua vizuri kwa maana nitahakikisha ninawapiga hadi vyumbani kwenye kama nilivyo fanya kwenye kundi la Al-Shabab”
Nikawaona viongozi hawa wakistuka kwa maana ninatambua kwamba wameweza kusikia habari ya kufutika kwa kundi la Al-Shabab na wengi wao ninaimani wanahisi kwamba Marekani ndio limeifuta Al-Shabab kwenye ramani ya dunia.
“Meja hakikisha kwamba hakuna kiongozi hata mmoja anaye ondoka leo, nyote nitawahitaki katika chakula cha leo usiku”
“Sawa mkuu”
 
“Swali, maoni, ushauri?”
Hapakuwa na kiongozi aliye fungua kinywa chake, wote wakaka kimya.
“Tutaonana usiku, niwatakie jioni njema”
Nikasimama na kuanza kutembea kwenye chumba hichi kwa kujiamini, viongozi wote wakabaki wakinisindikiza kwa macho, nikafungua mlango na kutoka, nikaanza kusikia minong’ono, ikanibidi kufungua mlango na kuwafanya viongozi wote walio kuwa wamesimama kukaa kwenye viti vyao kwa woga.
“K2 ninakuomba”
Taratibu K2 akanyanyuka na kunifwata mlangoni, nikamfungulia mlango na kuanza kutoka naye nje.
 
“Dany wewe ni mshenzi, mbwa mkubwa wewe”
K2 alizungumza kwa hasira japo kwa sauti ya chini isiyo sikika na mtu yoyote, sikuruhusua mlinzi yoyote kutufwata nyuma yetu, hawa walinzi wa K2 wanao pokea amri kutoka kwake, wakafwata amri yangu.
“Nikuue kwa sumu, risasi, au kukuchinja?”
Nilimuliza K2 huku tukiendelea kutembea taratibu, kwa mtu ambaye anaweza kutuona, atahisi tunazungumza mazungumzo mazuri ya amani. Tukasimama kwenye moja ya bustani ya maua.
“Nimekuuliza nikuue kwa staili gani kwa maana leo hapa kwangu huwezi kuondoka, ulihisi kwamba nitaogopa mazungumzo yako uliyo yarekodi, au ukweli ambao utakwenda kuzungumza kwa watu hawa ambao kwa sasa wanafwata amri yangu?”
“Ukiniua mimi haito kusaidia kitu”
“Hahahaa, unajidanganya, una uhakika haita nisaidia kitu?
“Ndio kwa mana mimi ndio ninajua ukweli wote”
“Ukweli gani wakati umeshindwa kwendwa kuzungumza mbele ya viongozi wezako, eti mumewekeza pesa”
 
“Ukweli kuhusiana na familia yako”
Nikakaka kimya huku nikimtazama K2 usoni mwake. Nikatamani kumzaba kibao, ila wanajeshi wanao linda hii sehemu wakanifanya nishindwe kabisa kumdhalilisha K2 mbele yao.
“Malaya mkubwa wewe unataka kuzungumza nini mbele ya familia yangu?”
“Familia yako ipo hai, hakuna hata mmoja ambaye nimemuua kama unavyo zungumz…….”
Nijikuta nikishindwa kujizuia na kumtandika kofi zito K2 hadi akapepesuka, ila akajikaza na kusimama sawa huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Peter”
Niliisikia sauti ya Yemi akiniita nikatazama pembeni na kumuona Yemi akija katika eneo nililo simama na K2.
“Ohoo samahani mama K2, mume wangu leo hayupo sawa”
Yemi alizungumza kwa sauti ya upole kwa mana hatambui ni kutu gani kinacho endelea kati yangu mimi na K2 anacho hisi yeye ni kwamba ni leo tu ndio tumekutana.
“Bila samahani mwanangu, nilikuwa ninamuelekeza jinsi ya kuongoza hili jeshi ila nikateleza baadhi ya maneno ndio maana akanidhibu kama hivi”
 
“Oohoo samahani sana mama. Peter mume wangu nakuomba utilize hasira yako”
Yemi alizungumza huku akinishika mashavu yangu,  taratibu akaanza k.. midomo yangu na kumfanya K2 kuanza kuondoka hili eneo.
“Tulia ehee mume wangu”
Yemi aliendelea kunibembeleza huku akinishika mashavu yangu. Yemi akanishika mkono na kuondoka katika eneo hili.
“Peter natambua kila mmoja anaweza kukuletea ushauri wake, ila jaribu kuzuia hasira zako kwa maana hakuna ambaye anaweza kukuletea ushauri mzuri mume wangu”
“Yemi”
“Beee”
Sikuzungumza kitu chochote baada ya kumuona meja akija mbele yangu. Akanipigia saluti, akamtazama Yemi kidogo nikampa ishara ya kuzungumza.
“Mkuu tumehakikisha kwamba hakuna kiongozi anaye ondoka”
“Helicopter zao walizo kuja nazo mume ziwekea ulinzi mzuri?”
“Ndio, nina imani kwamba hakuna itakayo urka na atakaye jaribu kufanya hivyo basi tutamuangusha”
Ehee ngojeni kwanza nyinyi wanaume. Ni kitu gani kinacho endelea hadi wageni wa watu wasiondoke katika hili eneo?”
“Ninahitaji kula nao chakula cha usiku”
 
“Kula nao chakula cha usiku ndio kifanye wasiondoke?”
“Yemi huelewi ni kitu gani kinacho endelea”
“Ndio maana ninahitaji nielekezwe mume wangu, nitaelewa vipi wakati sijaeleweshwa?”
“Kati ya hawa viongozi kuna wasaliti ambao ni lazima niwahushulikie ili jeshi lisonge mbele”
“Basi kama hakuna wasaliti waache wengine waondoke”
“Siwezi kufanya hivyo”
“Fanya hivyo”
Yemi alizungumza kwa ukali hadi meja akabaki akiwa ameshangaaa. Nikamgeukia Yemi na kumtazama usoni mwake kwa macho makali.
“Kama huitaji kusikiliza kile ninacho kifwata, nijajiudhuru cheo changu na utaongoza jeshi la baba yako peke yako”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, nikaanza kuvua kofia niliyo ivaa huku nikifwatia vyeo ambavyo vipo kwenye shati langu jambo lililo mfanya meja kwa haraka kupiga magoti chini na kunishika miguu yangu huku akilia akiniomba nisitishe maamuzi yangu ninayo yafanya.
                                                                                    
AISIIIII……….U KILL ME 145

“Jenero, bado tunakuhitaji tunahitaji muongozo wako”   
Meja alizungumza huku akiwa ameendelea kunishikilia miguu yangu. Taratibu nikamuona Yemi machozi yakimwagika usoni mwake.
“Nisamehe mume wangu”   
“Meja unaweza kusimama”
Nilizungumza huku nikimtazama Yemi usoni mwake, nikaanza kurudisha vyeo vyangu nilivyo anza kuvivua kwenye shati langu.
“Hakikiasha mpango nilio waelesza unaendelea kama nilivyo zungumza”
“Sawa mkuu”
Meja akaondoka zake, sikutaka kumjibu Yemi kitu cha aina yoyote zaidi ya kuanze kutembea kwa haraka kuelekea kilipo chumba chetu.
“Peter, Peter”
Yemi aliniita huku akinikimbilia, akaniwahi kunishika mkono wa kushoto.
“Twende tukazungumzie ndani”   
Nilizungumza huku nikiuachanisha mkono wangu na mkono wa Yemi. Tukaingia ndani huku nikiwa nimekasiria, si kwasababu ya ukali wa Yemi alio uonyesha mbele yangu na Meja, ila ni kutokana na kitu alicho kizungumza K2. Taratibu Yemi akapiga magoti chini huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake.
“Peter ninakuomba unisamehe mume wangu, sikutarajia kama ninaweza kukufokea mbele za watu, natambua utakuwa umefedheheka, ila ninakuomba sana unisamehe mume wangu”
 
Nikabaki nikimtazama Yemi usoni mwake, moyo wangu unatamani sana kumueleza ukweli wa maisha yangu ila akili yangu inakataa kabisa.
“Peter tambua wewe ndio mwanaume wa ndoto zangu, tambua wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu, tafadhali ninakuomba usije ukanichukia kwa kile nilicho kifanya”
“Mke wangu usijipe tabu ya kuniomba msamaha, sio wewe uliye nikosea”
Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimnyanyua Yemi, taratibu nikakaa naye kwenye sofa, nikaanza kumfuta machozi yake, kisha nikampiga busu katika paji la uso wake.
“Nahitaji kubadilisha mfumo wa hili jeshi”
“Kivipi mume wangu?”
“Hivi unatambua kuna watu wamewekeza pesa zao, na wao wanajipatia faida kutoka kwenye hili jeshi, ikiwa kuna wanajeshi wengi wanapoteza maisha yao pasipo kufaidika kwa kitu chochote”
“Mmmmmm. Ni kina nani hao mume wangu?”
“Wageni wote walio kuja leo. Mke wangu nishauri ni nini cha kufanya, nahisi kichwa changu kinapata moto”
Yemi akashusha pumzi nyingi sana huku akiwa kimya akinitazama usoni mwangu.
 
“Mume wangu, baba yangu amekuamini hadi kukuachia cheo hichi, naamini kila unacho kifanya ni sahihi. Hakikisha kwamba unaleta mabadiliko yatakayo mjali kila mwanajeshi ili hata akiamua kufanya kazi basi anafanya kazi kwa juhudu zote”
“Nashukuru mke wangu”
Nilizungumza huku nikimvuta Yemi karibu yangu, akakilaza kichwa chake kwenye bega langu la upande wa kulia.
“Sinto rudia tena mume wangu kukuingilia katika uongozi wako. Nimeamini kwamba una nguvu ya kuongoza kwa maana sikutegemea kama meja anaweza kukupigia magoti”
“Naamini kwamba wamesha anza kunielewa, leo usiku nitahitaji uwepo nami kwenye chakula cha usiku”
“Ni jukumu langu mume wangu siwezi kukuacha uwe mbali nami”
“Nashukuru mke wangu”
Taratibu Yemi akanigeukia na kuanza kuniny mdomo wangu, mlango wa chumba chetu ukagongwa ikanilazimu kumuachia Yemi. Nikaanza kutembea kwa kujiamini hadi mlango, nikaufungua mlango wa chumba chetu, nikakutana na meja akiwa anahema.
“Vipi  meja?”
“Raisi K2 ametoroka yeye na walinzi wake, ameua walinzi wetu kumi”
“Shitiiiii”
Yemi kwa haraka akakimbilia sehemu tuliyo simama.
“Meja unasema mama K2 ameua walinzi kumi?”
“Ndio”
“Mke wangu, K2 ni gaidi, na amejidhihirisha kwamba ni gaidi. Meja nahitaji vijana watakao mlinda mke wangu, au mpelekeni katika chumba maalu cha ulinzi kwa maana simuamini mtu mwengine zaidi yako wewe”
“Sawa mkuu”
 
“Peter wewe unakwenda wapi mume wangu”
“Nilazima nimkamate K2 na kumuangamiza mbele ya wanajeshi wangu”
“Peter tuma tu vijana waweze kwenda kumfwatilia?”
“Hakuna anaye mjua K2 zaidi yangu mimi na hakuna ambaye ataweza kumkamata K2 zaidi yangu”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimekazia macho Yemi.
“Unamfahamu?”   
“Ndio, ila huu sio muda wa maelezo juu ya hilo. Meja hakikisha viongozi wengine wote munawawaka chini ya uangalizi mkali, na hakikisheni hakuna anaye weza kutoroka tena”
“Sawa jenero”
Kwa haraka Yemi akanishika mashavu yangu, akanipiga busu mdomoni mwangu, kisha akaniachia huku akinitaza.
“Mkuu vikosi vipo katika jengo la kujiandaa wanahitaji amri yako. Wewe ongozana na jenero”
 
Meja alizungumza na kunikabidhi mwanajeshi mmoja, tukaanza kukimbia na mwanajeshi huyu na kufanikiwa kufika katika uwanja, nikakuta wanajeshi wakiwa tayari wapo kweye magari na silaha zao.
“Naomba bastola mbili, magazine za kutosha pamoja na jaketi la kuzuia risasi”
“Sawa jenero”
“Ila samahani jenero, mimi ningeona kwamba uturuuhusu sisi kumfwata huyu msaliti na wewe uendelee kulinda hii ngome isije ikakosa muangalizi”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hamuwezi kumkamata K2, na musipo angalia munaweza kujikuta nyote munakufa kama alivyo waua wezenu, sawa”
“Sawa jenero”
Nikakabidhiwa jaketi la kuzui risasi, nilalivaa kwa haraka kisha nikapoea bastola zangu mbili pamoja na magazine za kutosha. Nikaruhusu magari kuondoka, huku gari niliyo panda ikiwa imetangulia mbele.
 
“Walielekea wapi?”
Nilimuuliza dereva huku nikimtazama usoni mwake.
“Walieelekea kaskazini mwetu?”
“Wana gari au miguu?”
“Wana miguu”
“Hakuna haja ya kutumia magari, simamisha magari na wanajeshi weote waelekee upande huo”
“Sawa jenero”
Dereva wangu akawasiliana na madereva wote kwa kutumia simu ya upepo. Gari zote sita zikasimama huku mawili yakiwa nia malori mawili na yote yamejaa wanajeshi.
“Hakikisheni tunamkata K2 akiwa hai. Ila ikapo lazimika kumjeruhi vibaya, itabidi kufanya hivyo kwa maana sinto hitaji kuona damu hata ya mmoja wenu ikimwagika nikiwa kiongozi wa hichi kikosi”
 
“Ndio muheshimiwa”
Wanajeshi hawa walizungumza kwa pamoja, nikagawa vikosi vya wanajeshi kumi kumi, tukaanza kuingia msituni huku tunakimbia kwa kasi, ila kila mmoja yupo katika umakini mkubwa. Kadri tulivyo zidi kwenda mbele hatukuweza kuona dalili yoyote hata ya yazo za miguu.
“Mkuu tunazidi kwenda mbele bila mafanikio ya aina yoyote, tunafanyaje na ukitegemea giza ndio hivi linaanzakutawala anga”
Mwanajeshi ambaye muda wote tupo pamoja aliniambia huku akinitazama, hata mimi mwenyewe nimejichokea kutafuta watu wasio onekana.
“Wasiliana na vikondi vingine waulize wameona chote”
“Sawa jenero”
Kwa kutumia simu ya upepo, akawasiliana na wanajeshi nilio wagawa kwenye makundi tofauto tofauti. Ripoti aliyo toa kila mkuu wa kikundi hichi, akadai hajaona chochote.
“Waambie wengine waendele na oparesheni kisha nahitaji wanajeshi watano kurudi kambini”
 
“Sawa mkuu. Oparesheni inaendelea, tunatudi na jenerali kambini”
Wanajeshi watano wakaungana na mimi na kuanza kurudi kwenye kambi yetu. Tukatumia zaidi ya dakika arobaina na tano kufika kambini. Ulinzi mkali hapa kambini ukaendelea kuimarishwa.
“Nipelekea sehemu zilipo maiti za wanajeshi”
Nikaongozana na mwanajeshi huyu hadi kwenye chumba maalumu cha kuhifadhia maiti, nikakuta miili ya wanajeshi hawa ikiwa tayari imesha safishwa na kuweka kwenye mafriji maalumu ya kuhifadhia maiti. Kitu kilicho nishanganza ni miili ya maiti hawa kutokuwa na majeraha ya aina yoyote, ila nilicho kugundua ni shingo zao kuvunjwa.
“Alio kuja nao sio walinzi wa serikali”   
Nilijikuta nikizungumza mwenyewe huku nikimgeuza mwanajeshi mmoja shingo yake.
“Mkuu unasema?”    
 
“Walinzi wa K2 ndio wamefanya hii kazi, na wote wanatoka katika kikosi chake cha wasichana tupu ambacho kazi yao ndio hii”
Nilimuambia mwanajeshi huyu huku nikiendelea kuigeuza shingo ya ya mwanajeshi huyu.
“Unaitwa nani?”
“Martin”
“Unaipenda hii kazi?”
“Ndio mkuu”
“Upo tayari kufa kwa ajili ya mtu mwingine?”
“Ndio mkuu”
“Ninaweza kukuamini?”
“Ndio mkuu”
“Utakuwa mlinzi wangu sawa”
“Nashukuru mkuu”
Martin akanipigia saluti huku akiwa amesimama kikakamavu.
“Una muda gani kwenye hii kambi?”
“Miaka mitano mkuu”
“Basi badae nitahitaji unieleze mambo mengii juu ya hii kambi”
“Ndio mkuu”
Tukatoka katika chumba hichi cha kuhifadhia maiti, moja kwa moja nikaelekea jengo walilo hifadhiwa wageni waalikwa.
“Mke wangu yupo wapi?”
Nilimuuliza meja baada  ya kunikaribia.
“Yupo katika chumba salama”
“Mumeandaa chakula cha usiku?”
“Ndio  kipo kwenye holi la chakula”
“Kamlete mke wangu nahitaji kuzungumza na hawa watu”
“Sawa”
 
“Kuna zile maiti kule chumba cha maiti, nitahitaji ukarekodi, hakikisha kwamba kila maiti unaigeuza shingo yake kwa maana wote wamevunjwa shingo zao. Pia hakikisha huo mkanda unafika nao kwenye ukumbi wa chakula”
“Sawa jenero”
Nikafungua mlango na kuingia katika chumba hichi kikubwa, nikawakuta wageni walio hudhuria kwenye kikao hichi wengine wakiwa wamekaa kwenye masofa huku wengine wakiwa wamesimama wakijadiliana.
“Mutaendelea kutufungia humu ndani kama mateka hadi saa ngapi huu ndio uongozi ulio achiwa na mzee Okocha”
Mzee mmoja alizungumza kwa jazba hadi mate mdomoni yakawa yanamtoka. Nikamtazama kwa macho makali hadi akajistukia na kutazama pembeni.
“Tukielewana hapatokuwa na hata mmoja wenu ambaye ataumia katika hili, ila endapo mutakuwa tofauti na mimi, nina waahidi kila mmoja ninampiga risasi ya kichwa na sinto ogopa nchi zenu kuja kunivamia mimi na jeshi langu, kwa maana nyinyi nyote ni wasaliti”
 
“Wa….sa…a….aliti vi…..pi baba ye….tu?”
Mzee mmoja alizungumza huku amitetemeka mwili mzima.
“Tuna dakika kumi za kujiandaa kwenda kula, mutaongozana na wanajeshi wangu hadi kwenye eneo la tukio, narudia tena na hili lieleweke na mulindane, endapo mmoja wenu atajaribu kukimbia ninawahakikishia kwamba nitawaua nyinyi nyote, sasa kama mulipanga mbinu ya kutorika ninawaeleza mapema kwamba mbinu hiyo ife na muifute kwenye akili zenu. Mmoja atayagharimu maisha yenu wote”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno haya nikatoka ndani humu, nikamkuta Yemi akiwa amesimama mlangoni, akanikumbatia taratibu.
“Pole mume wangu”
“Asante”
“Vipi umefanikiwa kumpata?”
“Hapana wanajeshi wanaendelea na kuwasaka, ila nimeamua kurudi kwa ajili ya hawa wageni wengine”
“Sawa mume wangu”
“Umejiandaa kwa ajili ya chakula?”
“Yaa hapa mimi nipo poa”
 
“Sawa. Meja zoezi limekamilika?”
“Ndi mkuu”
“Si kuna tv kule?”
“Ndio mkuu”
“Basi hakikisha unaiweka mipango sawa”
“Ndio mkuu”
“Meja huyu kijana ni mlinzi wangu kuanzia hivi sasa, ninaimani kwamba unamfahamu vizuri?”
“Ndio mkuu ninamfahamu na hata tatizo lolote katika tabia yake na hata upambanaji wa kutumia silaha pamoja miguu na mikono yupo vizuri”
“Nashukuru kwa maelezo yako meja, andaa wanajeshi watakao wasindikiza hawa viongozi hadi kwenye eneo la chakula mimi ninatangulia na mke wangu”
“Sawa”
    Tukaanza kutembea na Yemi huku akiwa amenishika mkono wangu. Kila muda Yemi ananitazama, anaonekana anahitaji kuniuliza swali ila anashindwa.
“Mume wangu unateseka na hii kazi ehee?”
“Hapana, kwa nini umezungumza hivyo?”
“Unaona jinsi ulivyo vaa haya madude ya kuzuia risasi, lakini kama ungekuwa ni mwana mitindo sasa hivi ungekuwa umetulia bichi tu”
“Ahahaaa usijali mke wangu, yote ni maisha”
Tukafika katika holi la chakula, nikakuta meza ndefu iliyo pangwa vyakula. Nikaitazama kwa umakini, nikamuagiza Martin kuanza kukagua kiti kimoja baada ya kingine na chini ya meza, kwa maana tukio la kutegwa bomu chini ya kiti cha raisi jijini Tanga, nilipo kuwa mlinzi wake bado linajirudia kichwani mwangu.
“Kupo sawa mkuu”
“Shukrani?”
Tukaka katika viti vyetu mimi na Yemi, baada ya muda viongozi wote wakaingia ndani ya eneo hili, wengi wao walio nitazama nyuso zao zimejikunja na kama ingekuwa ni amri zao basi wangesha niua. 
 
“Karibuni”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama, hapakuwa na mtu alite itikia ukaribisho wangu, sikulijali hilo zaidi ya kukaa na wao wakaka. Nikamkonyeza meja, akawasha tv iliyopo humu ndani, ikaanza kuonekana video ya jinsi walinzi wa K2 walivyokuwa wakipambana na wanajeshi wangu hadi ikafika hatu ya kuwavunja shingo na kuwaua na kipande hichi cha video kimerekodiwa na kamera zilizo kuwa katika eneo la tukio. Video hiyo ikaendelea kuonyesha jinsi wanajeshi maiti za wanajeshi hao zikiwa katika mafriji ya kuhifadhia maiti. Wageni wote wakaanza kutetemeka.
“Niliwaambia mmoja wenu akienda kinyume nami basi nitahakikisha kwamba ninawaua kwa mkono wangu mimi wenyewe, je kuna anaye weza kujitetea juu ya hilo”
Nilizungumza huku nikitoa bastola yangu kutoka sehemu nilipo ichomeka, na kumfanya mzee aliye nifokea baada ya kuingia ndani ya chumba walicho kuwepo, kuangua kilio kikali na kuzidi kuwatisha wezake ambao nao wote sura zao zimetawaliwa na woga kwani hakuna hata mmoja anaye jua hatima ya maisha yake kutoka kwangu.
                                                                                     ITAENDELEA
“Haya sasa wageni wamewekwa kwenye kumi na nane za Dany, je kuna atakaye epuka kifo katika hili alilo lifanya K2 na walinzi wake, usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kuburudisha na kusisimua”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )