Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 23, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 158 na 159 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
               
“Nimewapakiza ndege mbili tofauti na Yemi. Yemi amapenda katika ndege yangu binafsi na mwili  wa mwanaye, jamaa na watu wake nao wamependa kwenye ndege nyingine na wale wajinga wake watatu. Kwenye ndege waliyo panda, kuna bomu liliko tengwa, na nitahitaji maamuzi yako kwamba tuwalipue wafie hewani au tuwaache waendelea na maisha yao?”
Swali la meja likanifanya nitazamane na Martin, taratibu nikamtazama meja usoni mwake, huku nikikumbuka uwenda wazimu ulio nipata jana usiku kutokana na ukweli walio uzungumza mume mwenzangu kwa Yemi na kujikuta nikisikia sauti moyoni mwangu ikihitaji niweze kumuangamizaa jamaa huyu kwani amenipotezea mwanamke aliye nipa furaha maishani mwangu.

ENDELEA   
 Taratibu nikajiku nikiyang’ata meno yangu kwa hasira huku sauti ninayo isikia moyoni mwangu ikiendelea kunipa uchochezi wa kufanya mauaji haya.
“Dany nasubiria jibu lako?”   
“Samahani meja kama ninawaingilia, ila ninaomba nishauri katika hilo”
 
Sote tukamtazama Martin aliye zungumza kwa sauti ya upole.
“Kwa jinsi nilivyo agana na Yemi leo asubuhi, aliniomba nimlinde Dany hadi mwisho wa maisha yangu. Sikuhitaji kulizungumza hapo awali kwako mkuu, ila ukweli ni kwamba Yemi bado anakupenda. Tukimuua mume wake huyu ni lazima atajawa na chuki ambayo itapaelekea yeye kulipiza kisasi kwako jambo ambalo litakuzidishia maadui hapa duniani ikiwa hawa maadui waliopo mbele yetu hatujawamaliza”
 
Martina alizunguzma kwa upole na usikivu mkubwa sana, taratibu nikajikuta moyo wangu ukianza kutulia.
“Sasa hivi tunatakiwa kuwaangalia maadui hawa watatu walipo mbele yetu, inabidi kuwazuia kwa manaa hao wana nguvu ya kiserikali, wana nguvu ya kuendelea kukutangaza Dany wewe kama gaidi, hembu tuangalie hili sasa”
“Kwa hiyo Martin unapendekeza bosi wako amuachilie mbali mwanaume aliye mpokonya mke?”
 
“Mimi ndio nilimpokonya mke wake”
Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama meja usoni mwake na kumfanya anishangae.
“Nilimpokonya jamaa mke wake kwa kumpiga na pia nimepelekea mtoto wao kufa, yote ni kwa ajili yangu. Nina hisi hata nikimuua jamaa damu yake itenililia maishani mwangu na pia inaweza kupeleka kuto kukamilisha hili zoezi la kulipiza kisasi”
Nilizidi kuzungumza kwa upole huku n ikijitahidi hasira na sauti ya uchochozi inayo endelea moyoni kuipinga ili kutoa maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye kwa maana Yemi hajanifanyia jambo lolote bada.
 
“Sawa kama umeridhia rafiki yangu siwezi kuendana kinyume na makubaliano yako, ngoja nimpigie simu rubabi niliye mpa jukumu la kujitoa muhanga kwa ajili hili”
“Kumbe ulikuwa umemtoa mtu muhanga?”
“Ndio nimemkabidhi kiasi kikubwa cha pesa kitakacho isaidia familia yake kwa miaka mingi tu baada ya kifo chake”
“Mmmmmmm”
Nilijikuta nikihema kwani maamuzi aliyo kuwa ameyachukua meja katika kunisaidia ni magumu sana. Meja akatoa simu yake mfukoni akaminya minya juu ya kioo kisha akaiweka sikioni.
“Zoezi nimelisitisha”
“Sawa”
Meja akakata simu huku akitabasamu.
“Jaamaa ameshusha pumzi sana, masikini wee”
“Nani?”
 
“Rubani, emeshusha pumzi nina imani hapo alikuwa anaomba zoezi lisikamilike”
“Hivi kumbe kuna watu wanaweza kujitoa muhanga kwa ajili ya pesa?”
“Ohoo rafiki yanu umasikini mbaya sana, kwa maana nimemlipa jamaa pesa ya mshahara wake kwa mawaka mara mbili nikazidisha kwa miaka kumi mbele”
“Ni sawa na kiasi gani?”
“Dola milioni tano, ni utajiri mkubwa sana”
“Pesa yote hio utamuacha ande nayo?”
“Yaa ni dili, wewe ndio umemuakoa, itabidi nije kumuambia kwamba wewe ndio umeweza kuyaokoa maosha iyake atajua ni jinsi gani atakushukuru”
“Usimuambie bwana kwa maana sijafahamu anaweza kunichukulia vipi, isitoshe nina imani atakuwa amesikia habari zangu”
“Sidhani, unajua huku Madagasca watu sio wafwatiliaji sana wa mambo, ndio  maana juzi tuliweza kutembea barabani kwa kujiamini na wala hakuna hata polisi aliye weza kukutilia mashaka”
 
“Kweli. Sasa ni muda wa kujua tunaanzai katika hii kazi iliyo bakia mbale yetu”
Nilizungumza huku nikimtazama meja usoni mwake.
“Jambo la kwanza ambalo tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba unaingia nchini Tanzania pasipo mtu yoyote kuweza kukufahamu, kwani nina imani kwa sasa ulinzi nchini Tanzania utakuwa ni mkali sana kutokana na ujio wa raisi Donald Bush”
“Tutatumia ndege au?”
“Hatuwezi kutumia ndege kwa maana kila ndege inayo ingia katika angala la Tanzania ni lazima ikaguliwe na wewe nina imani picha yako itakuwa imesambazwa kwenye vituo vyote vya usifiri.
 
Meja aliendelea kusisitiza huku akitutazama.
“Njia  ya usalama itakayo kuwezesha wewe kufika nchini Tanzania ni kutumia bahari?”
“Unahitaji tutumie meli?”
“Hapana nina boti za mwendo kasi ambazo zinaweza kuwafikisha Tanzania katika masaa machache sana ila itabidi kuwaacha japo maili moja kabla ya kuingia Tanzania, na mutazamia majini hadi kufika Tanzania.”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi huku nikimtazama meja usoni mwake.
 
“Hapo ni lazima kuogela rafiki yangu, pasipo kufanya hivyo unakwenda kuingia mikononi mwa Wamarekani na wakikukamata ndugu yangu kwa sasa hawato kuacha na watakuua haya kwa kukuchoma sindano ya sumu”
“Hilo halita weza kutokea”
 Martin alizungumza kwa kujiamini.
“Yaa mukiwa makini nina imani kwamba hilo halito weza kutokea”
“Mukiwa makini basi halito weza kutokea. Tanzania mutakwenda kukutana na kijana wangu anaotwa Godlove, atawapokea katika fukwe ambayo mutatokea”
“Kwa Dar es Salaam ni fukwe gani ambayo haina ulinzi sana?”
 
Nilizungumza huku nikikmtazama meja.
“Wewe ndio mwenyeji mwenzetu unatuuliza na sisi tena?”
“Nimeondoka muda sana Tanzania kwa hiyo siwezi kuelewa kama mambo yamebadilika au laa”
“Ngona nimpigie Godlov”   
Meja akampigia kijana wake baada ya sekunde kadhaa akaiweka simu mezani huku akiwa ameweka loudspeaker.
“Mkuu habari yako?”
“Salama meja”
“Hii laini yako ina usalama wa kuweza kuzungumza?”
“Ndio mkuu hakuna anaye weza kupata mawasiliano yetu”
“Sawa ni bichi gani kwa jijini Dar es Salaam hapo mulipo ina ulinzi dhaifu?”
 
“Koko bichi ipo dhaifu, japo kwa wiki hii umeimarishwa ulinzi kwa ajili ya ujio wa raisi wetu ila bado ulinzi wake ni wa kusua sua”
“Sasa Dany na mwenzake watakuja Tanzania nina imani watakuwepo huko majira ya saa tisa usiku nina imani kwamba ume waandalia mazingira mazuri?”
“Hilo usijali mkuu nimeanda kila kitu kipo sawa, na nitawasubiria katika ufukwe huo hadi wafike”
“Itakuwa vizuri, nina imani utawapa ratiba nzima ya shereha na ziara za Donald pamoja na K2”
“Ndio mkuu”
 
“Basi nikutakie asubuhi njema”
“Nashukuru mkuu”
Meja akakata simu na kututazama usoni mwangu.
“Kazi ni raisi sana kilicho baki ni nyinyi kuanza safari muda wowote mukiwa tayari”
“Shukrani sana meja sijajua hata nikulipe kitu gani kwani kwa msaada wako ulio nipatia sijawahi kuupata kutoka kwa mtu yoyote duniani”
“Usijali Dany haya ni maisha na pesa inatafutwa, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hilli”
“Kitu kingine ninakuomba umlinde Yemi, ninajua baada ya haya matukio ambayo nitakwenda kuyafanya nina imani kwamba kuna watu watakao mfwatilia na kumuua”
“Unampenda?”
 
Meja aliniuliza kwa sauti ya upole huku akinikazia macho.
“Ndio nina mpenda, upendo hauwezi kufutika kwa siku moja na…..”
“Usijali Dany huna jaya ya kujieleza sana katika hilo ikiwa hata mii ninazielewa hisia zako”
“Shurkani meja kwa kuweza kinielewa”
“Sawa ngoja niwaache muzungumze mawili matatu, niandae mpango mzima wa safari”
“Sawa meja”
Meja akasimama na kuondoka katika eneo hili na kuniacha na Martin.
“Mkuu isije ikatokea siku ukamkosea huyu mzee”
“Kwa nini?”
“Amekusaidia kwa asilimia kubwa sana na pasipo yeye nina imani kwamba tungekuwa tumesha kufa ile siku tuliyo tekwa na Wamarekani”
 
“Yaa ni mtu mwenye thamani kubwa kwangu nina mthamini sana. Sasa jiandae kama kuna cha kuchukua chukua safari itaanza asubuhi hii”
“Sawa mkuu”
Nikanayuka na kuelekea chumbani kwangu kwangu, nikaingia bafuni na kuaoga, japo ninayakumbuka matukio machache niliyo yafanya humu bafuni na Yemi ila sina jinsi zaidi ya kuvumilia na kuweka hisia za mapenzi pembeni na kuimalizia kazi iliyopo mbele yangu.
Nikava jinsi, tisheti na raba, nilipo hakikisha kwamba nimekamilika, nikachukua  pete ya Yemi na kuivaa katika kidole changu cha mwisho cha mkono wangu wa kushoto kisha nikatoka humu chumbani. Nikamkita Martin akiwa amesimama sebleni na meja.
 
“Boti ipo tayari kwa ajili ya safari”
“Sawa meja”
Tukaanza kutoka na kuelekea katika kingo za fukwe ya bahari iliyopo pembezoni mwa jumba la meja.
“Hakikisheni kazi munaifanya kikamilifu na safari hii Dany usifanye makosa yoyote ambayo yatakugarimu”
“Usijali meja, nikishindwa kufanya sasa hivi nina imani kwamba sinto weza kufanya tena hii kazi”
“Sawa sawa nakuamini katika hili”
“Pia meja nina shukuru sana kwa kila kitu ulicho nifanyia na unacho endele kunisaidia”
 
“Usijali rafiki yangu, niwatakie safari njema”
“Asante”
Tukaingia kwneye boti moja kubwa ya kifahari.
“Mukifika Tanzania, Godlove atawaeleza jinsi ya kuwasiliana nami”
“Sawa meja”
Taratibu boti hii ikaanza kuondoka eneo hili huku tukiwa tumekabidhiwa vijana wawili wa meja pamoja na nahodha wa hii boti. Safari ikazidi kusonga mbele huku boti hii ikienda kwa mwendo kasi sana.
“Mkuu unahitaji tuwaue vipi maadui  zako?”
“Hilo tutalijua tukifika nchini Tanzania kwa sasa ni vigumu kulizungumzia kwani bado hatujajua wamejipanga vipi katika hilli swala”
“Sawa”
Nahodha wahii boti kusema kweli ni mtaalamu kwania kasi anayo kwenda nayo ni kibwa na muda mwengine tunakutana na mawimbi makubwa ya maji ila tunafanikiwa kupita. Masaa yakazidi kwenda hadi giza likaingia.
 
“Tuna masaa kadhaa mbele, kuna maelezo tunatakiwa kuwapatia”
Kijana mmoja wa meja alizungumza huku akitutazama kwenye siti tulizo kaa. Nikanyanyuka na kumsogelea.
“Sawa”
“Kuna nguo maalumu za kuzamia kwenye maji pamoja na mitungi maalumu nina imani kwamba munaweza kuitumia?”
“Kwa mimi ninaweza, Martin unaweza?”
“Ndio ninaweza mkuu”
“Basi hii mitungi inagesi itakayo wawezesha kukaa chini ya maji kwa masaa zaidi ya kumi. Pia kuna hii simu haiingii maji na inatumika hata ukiwa ndani ya bahari. Itawasaidia katika swala zima la kutazama muelekeo wa wapi munakwenda, kwani tumeambiwa kuwaacha maili moja kutoka Tanzania ilipo”
 
“Sawa”
Kijana huyu akanikabidhi simu hii nikaitazama vizuri, kisha nikamkabidhi Martin.
“Kuna swali munahitaji kuniuliza?”
“Hapana”
“Basi niwatakie kazi njema na karibuni Madagascar”
“Asante”
“Tukiwa tunakaribi kufika basi tutawaambia muweze kuvaa mavazi hayo?”
“Tunaweza kuvaa juu ya hizi nguo zetu?”
“Hapana labda muziweke kwenye begi maalumu ambalo lipo hapa na haliingii maji?”
“Sawa sawa na sehemu ambayo munatuacha haina samaki wakali?”
“Hapana samaki wake ni wa kawaida. Na kuna tochi maalimu mutazitumia mikiwa chini ya maji ila munatakiwa kuwa makini sana”
 
“Shukrani kaka”
“Niite Michael”
“Sawa asante sana Michael”
Nikarudi kwenye siti yangu baada ya kupata maelekezo hayo, huku kichwani mwangu nikifikiria jinsi nilivyo poteza uhuru katika nchi yangu na nina rudi kama mvamizi ambaye endapo nitaonekana basi ninaweza kupoteza maisha yangu.
‘Mungu nisaidie katika hili’
Nilijikuta nikizungumza maneno hayo huku nikiwa nimeyafumba macho yangu. Baada ya masaa mawili, Michael akaingia tena kwenye hichi chumba tulipo kaa huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.
 
“Vipi?”
“Tumepata tatizo”
“Tatizo gani?”
Boti yetu inafukuziwa na boti za jeshi la majini na wanamlazimisha nahodha kusimamisha boti la sivyo wanakwenda kutulipua na hadi sasa wametupa onyo la pili tunasubiria amri yako tusimamishe boti au tusonge mbele ili tulipuliwe”
Michael alizungumza haraka haraka na kunifanya ninyanyuke kwa haraka hukun ikiwa nimejawa na wasiwasi mwingi, kwani hili ni tatizo jengine ambalo sikulitarajia litokee kwenye safari yangu hii.

AISIIIII……….U KILL ME 159  

“Boti zipo ngapi za hao wanajeshi?”
“Zipo boti nne”
“Muambie nadhodha asimamishe boti”
“Sawa mkuu”
Michael akatoka katika chumba hichi, na kutuacha mimi na Martin tukiwa tumesimama huku wasiwasi mwingi ukiwa umetutawala. 
 
“Tutafanyaje mkuu wakitukuta humu ndani?”
“Ni lazima tufanye jambo”
Nilizungumza huku nikitoka ndani ya hichi chumba, nikawakutua Michael na wezake wakiwa wamesimama wakitazama jinsi boti hizi za jeshi zikiizunguka boti hii tuliyo panda.
“Michael njoo”
Michael akanifwata sehemu nilipo jibanza.
“Kuna silaha humu ndani ya hili boti”
“Ndio mkuu”
“Zipo wapi?”
Tukarudi kwenye chumba tulichopo, Michael akafungua moja ya kabati lililomo humu ndani akasogeza nguo zilizopo kwenye hili eneo, akaanza kutoa bunduki moja baada ya nyingine na kutukabidhi. Nikachukua bunduki moja iliyo jaa risasi za kutosha.
 
“Wanajeshi wakileta shida tutawashambulia”
“Sawa mkuu”
Michael akatoka ndani humu na kutuacha mimi na Martin kila mmoja akiwa na bunduki yake na tumejibanza kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa mtu wa nje kuwea kutuona ila sisi ni rahisi kuweza kumuona mtu wa nje hii ni kutokana na vioo vigumu viliyomo kwenye kuta za hichi chumba.
Tukawashuhudia wanajeshi watatu wakiingia kwenye boti hii huku wakiwa wameshika bunduki zao, ila katika kuwatazama sare zao sio za wanajeshi wa jeshi la maji Tanzania.
 
“Hawa wanajeshi ni wa wapi?”
Nilimuuliza Martin huku nikiendela kuwatazama wanajeshi hawa.
“Ni wanajeshi wa Msumbiji”
“Ina maana bado hatujaingia Tanzania?”
“Yaa”
Tukaendelea kuwatazama wanajeshi hawa walio anza kugaua vibali vya hii boti huku wakiwatazama Michael na mwenzake, wakazungumza nao kwa dakika kadhaa, Michael akatoa kibunda cha dola za kimarekani na kumkabidhi mwanajeshi mmoja aliye anza kuhesabu pesahii haraka haraka kisha akamtazama Michael huku akitingisha kichwa. Taratibu nikawaona wakishuka kwenye boti kisha wakaruhusu boti yetu kuondoka. Nikajikuta nikishusha pumzi nyijngi kisha nikarudi kukaa kwenye siti yangu. Michael akaingia kwenye chumba chetu.
 
“Walihitaji nini hao wanajeshi?”
“Walikuwa wanafoka foka tu kwa nini tumepita kweney ukanda wa nchi yao, pasipo kuw ana kibali”
“Wana vichaa kweli”
“Nimewapa dola elfu tano, ndio maana wametuachia”
“Sawa tumebakisha muda gani hadi kufika nchini Tanzania?”
“Tumesha ingia kwenye ukanda wa nchi ya Tanzania, hapa tutatumia muda mchache kufika usawa wa Dar es Salaam”
“Sawa sawa”
 
Michael akaanza kurudisha silaha ndani ya kabati hili huku akisaidia na Martin. Baada ya muda wa kama dakika aroboini na tano Michael akatuommba tuweze kuvaa nguo maalumu za kuogelea kwani muda kuzama baharini umefika.
Tukaanza kujiandaa mimi na Martina hatukuchukau muda mrefu tukawa tumefanikiwa kuvaa nguo hizi pamoja na mitungi maalimu ya gesi ya oksijeni tuliyo ivaa mgononi. Tukavaa miwani maalimu, kisha Michaela katukabidhi tochi.
“Niwatakie kazi njema”
 
“Shukrani na murudi salama. Martin mbona umemeba begi?”
“Nimeweka nguo zetu na vifaa vichache”
“Sawa”
Nikampa mkono wa shukrani Michael na mwenzake kisha taratibu tukajitosha kwenye maji. Tukaanza kushuka chini huku tukiwa tumewasha tochi zetu. Tulipo fika katika usawa ambao tunaamini hata mmtu awe kwa juu hatoweza kuona mwanga wa tochi tulizo ziwasha, tukaanza kuogelea kwenda mbele huku Martin akiongoza kwa kufwata malekezo kwenye simu aliyo ishika, tukazidi kusonga mbele huku tukiwa makini sana hadi tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyavu kubwa ya chuma. Martin akanikabidhi simu aliyo ishika kisha akavua begi na kutoa koleo kubwa la kukatia njavu hii. Taratibu akaanza kukata njavu hii huku mimi nikiwa makini kutazama tunapo toka na tuendapo. 
 
Alipo maliza kukata taratibu tukaanza kuingia kwenye uwazi alio kata na tukaendelea na safari yetu. Hadi inatimu saa tisa usiku tukafanikiwa kufika katika ufukwe wa koko bichi huku tukiwa tumechoka sana. Tukatoka ndani ya maji na kukaa chini ya mwamba mmoja ulipo hapa pembezoni.
“Ohooo kukaa kwenye maji ni kazi kweli kweli”
Nilizungumza huku nikihema sana.
“Yaani wee acha tu”
“Huyu jamaa sijui atakuwa amesha fika”
“Ngoja nikamtazame”
Martib alizungumza huku akinyyanyuka, akavua viatu maalumu vya kuvulia, akaivua na tochi na kuizima, akatoka kwenye mwamba huu ambao umeingia ndani, hata hazikupita dakika mbili nikiaiskia milio ya risasi iliyo nistua sana, kwa haraka nikachungulia kwenye mwamba huu, nikamuona Martin akiwa amezungukwa na watu walio valia nguo nyeusi.
 
Nikatamani kujitokea ila sina silaha amabayo itawezesha kushambuliana na watu hawa. Nikamuona Martin akipigishwa magoti chini huku mikono yake akiweka nyuma na kufungwa pingu. Akanyanyuliwa kwa haraka na watu hawa wakaondoka naye katika hili eneo.
“Shitiii”
Nilizungumza huku nikiwa nimekasirika sana kwani sijajua mpango huu umevurugwa na nani na mtu ambaye tumeambia kwamba atakuja katika hili eneo ni Godlove ambaye hata sura yake siifahamu. Nikafungua begi lenye nguo, kwa haraka nikaanza kubadilisha nguo nilizo zivaa na kuvaa nguo za kawaida, nilizo kuwa nimezivaa nilipo toka katika kisiwa cha Madagasca.
 
Nikachunguza hili eneo kwa umakini na nikaanza kutoka katika huu mwamba sikuelekea katika usawa alio kuwa amekwenda Martin. Nikaanza kutembea huku nikiwa makini sana katika kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye weza kunifwatilia au kuniona. Nikiwa katika moja ya barabara iliyo tulia nikaona gari aina ya Toyota Mark X ikiwa imefunuliwa boneti ya mbele huku ikitoa moshi mwingi na mlango wa dereva nao umefunguliwa. 
 
Nikataza hili eneo nikagundua kwamba hakuna sehemua mbayo askari wanaweza kujificha na ikawa ni mtego kwangu. Nikaanza kulisogelea hili gari hadi nikanikiwa kufika, nikamkuta msichachan mmoja akiwa amejilaza kwenye siti yake akionekana kuchoka sana na kwenye zake zimefunika sehemu ya uso wake. Mkononi ameshika chupa ya wyne na inaonyesha amelewa sana.
“Hei”
Nilimuita huku nikiendeleak kutazama eneo hili kwa umakini sana. Binti huyu akakurupuka na kunitazama huku akiziweka nywele zake sawa. Sote tukabaki tukishangaana kwani huyu binti ninamfahamu sana.
“Dany!!”
“Lucy!!”
Nilimuita huku sote tukishangaana. Lucy akatoka kwenye siti aliyo kaa na kusimama, akanikumbatia kwa haraka, tukajikuta tukiwa tumejawa na furaha.
“Oohoo Dany ni miaka mimi sasa hatujaonana, upo wapi wewe?”
 
Lucy alizungumza huku akiwa ametanasamu.
“Maisha tu, gari lako lina tatizo gani?”
“Sijui ninaona limenizimia tu hapa”
Nikamuachia Lucy huku nikitembea hadi mbele ya hili gari, nikaanza kutazama tazama tatizo la hili gari, mwanga mkali wa gari inayo kuja nyuma yetu ukanifanya nisigeuke na kujifanya nipo bize ninaendela kutengeneza hili gari. Gari hili likasimama karibu kabisa na gari hili, taa za gari hilo zikazimwa na kunipa nafasi ya kugeka kidogo, nikajikuta nikistuka baada ya kuona platenamba za hili gari inaonyesha ni gari ya polisi.
‘Nitawaua’   
Nilijikuta nikiapia huku nikiendelea kuinama kugusa gusa baadhi ya vitu viluyopo kwenye hii bonet.
“Mbona mumechelewa?”
Nilisikia sauti ya Lucy akizungumza na polisi hawa, jambo lililo nifanya moyo wangu kunistuka sana na kuhisi kwamba Lucy ameniuza kwa askari hawa. Nikataka kugeka ila nikajikuta nikiwa mvumilivu nikisikilizia kauli ya askari yoyote atakaye jibu swalli la Lucy mtoto wa Mzee Jogoo, niliye wahi kumsaidia mikaa mingi katika ajali ya moto kipindi nilipo kuwa ninaishi Sinza.
 
“Kidogo tulikuwa kwenye patroo Ubungo ndio maana tumechelewa samahani”
“Ahaa gari limenibumia hapa”
“Huyo anaye kusaidia ni nani?”
Kwa jicho la kona nikamuona Lucy akigeuka na kunitazama, akatabasamu na kunisogela nilipo simama na kuendelea kujifanya nina tengeneza gari hili.
“Ni mpenzi  wangu”
Nikashusha pumzi kidogo kwani tayari nilisha anza kujiandaa kiakili jinsi ya kupambana na askari hawa wanne.
“Ingia ndani ya gari ujaribu kuwasha”
Nilizungumza huku nikaza moja ya nati ambayo nimeikuta imelegea. Lucy akatembea kwa madoido hadi ndani ya gari akajaribu kuwasha na gari ikawaka.
“Waooooooooooo”
Lucy alishangilia huku akishuka kwenye gari.
“Asante mpenzi wangu”
Lucy alizungumza huku akinifwata na kunikumbatia, sikutaka kabisa kuigeuza sura yangu kuwatazama hawa askari kwani nina imani wataingia kwenye msiba ambao sihitaji niwe chanzo cha vifo vyao.
 
“Ngoda mumaweza kuondoka tu gari langu tayari”
“Mkuu ametuagiza tukusindikize hadi nyumbani”
“Mumbieni baba kwamba mimi ninaendelea kula bata weekend ndio imeanza hivi”
“Ila ni kwa ajili ya usalama wako”
“Nipo salama si munamuona shemeji yenu hapa”
“Mbona shemeji haitaji kututazama”
“Eheee kwani ni lazima jamani. Ngoda ondoka na watu wako bwana”
“Sawa”
Askari hawa wakarudi kwenye gari lao, wakapanda na kuondoka eneo hili na kutuacha tukiwa tumesimama tukisindikza gari lao kwa macho.
“Asante”   
Nilizungumza huku nikielekea katika mlango wa pili wa hili gari, Lucy akazunguka hadi katika mlango wa dereva na sote tukaingia ndani, tukafunga milango na kuanza kuondoka eneo hili.
 
“Dany ni kwa nini wewe?”
Lucy alizungumza kwa sauti ya chini huku akinitazama.
“Tunaelekea wapi kwanza?”
“Jibu swali langu kwanza”
“Unahisi ni kweli ni mimi?”
“Ndio maana nina hitaji kujua ukweli kuhusu wewe kwa kipindi chote ambacho unatafutwa na kutangazwa kama Gaidi tena wa kimataifa?”
“Mimi sio gaidi ila hao wanao watangazia wao ndio magaidi”
“Nitakuamini vipi ikiwa nimesikia umeua watu wengi sana na hapa Tanzania unatafutwa kama shahabu na endapo mtu atafanikishwa kukamatwa kwako basi yeye na umaiskini ndio kwaheri”
 
“Lucy”
“Beee”
“Una niamini?”
“Ndio ninakuamini, ndio maana sikuhitaji kukuchomesha kwa wale askari pale kwani bado sijakaa na wewe kufahamu ukweli ulio pelekea kuitwa gaidi na kuwindwa sana”
“Nashukuru, baba yako yupo wapi?”
“Baba ni waziri mkuu”
“Ananizungumziaje mimi katika hili swala”
“Baba yangu nina imani amejazwa chuki kubwa na anakuchukia sana na anatamani hata leo akukamate na kukuadhibu kwa makosa yako yote uliyo yafanya”
“Asijaribu kufanya hivyo kwani na yeye nitamua”
Gafla nikastukia Lucy akifunga breki za gari lake huku akinitazama kwa macho makali akionekana kushangaa kauli yangu niliyo itoa kwani ni kauli ambayo nina amini kwamba ni mbaya sana kwake ila ndio ukweli kutoka moyoni mwangu.
 
ITAENDELEA
“Haya sasa Lucy ameweza kukutana na Dany ambaye ameahidi kumuua baba yake endapo ataamua kuingia kwenye kumi na nane zake na Lucy ndio mtu wa pekee anaye tambua kwamba Dany yupo nchini Tanzania, je ni kitu gani kitakcho endelea. Usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimua
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )