Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, November 27, 2018

Ajali Mbaya ya Gari Yaua Watu 16 Tarime

Watu 16 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali mbaya iliyotokea jana katika eneo la Komaswa maarufu kama kwa Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuzikutanisha gari mbili za abiria aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na kisha kuteketea kwa moto. 

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo  itazikwa katika eneo ilipotokea ajali hiyo .

Akizungumza leo Jumanne Novemba 27, 2918 mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema uamuzi huo umechukuliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kutokana na ushauri uliotolewa na kamati ya Taifa ya maafa.

Amesema hadi sasa majina  12 kati ya 16 ya waliofariki dunia yamejulikana licha ya miili yao kutotambulika kutokana na jinsi ilivyoungua.

“Isipokuwa miili miwili  ambayo ilitambuliwa ukiwemo wa dereva na mwingine uliotambulika baada ya kukutwa na cheni shingoni,” amesema Malima.

Amesema mazishi hayo yatafanyika kesho Novemba 28, 2019 saa nne asubuhi, kwamba mabaki yaliyotokana na miili kuungua yatakusanywa na kuzikwa eneo hilo.

Amesema baada ya mazishi eneo hilo utajengwa mnara kwa ajili ya kumbukumbu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )