Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 19, 2018

Alichokisema Waziri Mwakyembe Baada ya Taifa Stars Kufungwa 1-0 na Lesotho

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyemba amesema akifika Tanzania atamueleza Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa kilichotokea kwenye mchezo dhidi ya Lesotho kuwa ni bahati mbaya na kumuahidi kuwa kwenye mechi dhidi ya Uganda Taifa Stars itaibuka na ushindi.

Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo baada ya  mchezo dhidi ya timu ya Lesotho  na Taifa Stars  jana Novemba 18,  ambapo Taifa Stars ilifungwa bao 1-0.

Akizungumza na waandishi wa habari Nchini Lesotho Waziri Mwakyembe amesema; “ Raisa alisema turudi na ushindi, nitamwambia tumefungwa moja na tunasubiri mechi ya Uganda ambayo lazima tushinde, huu ndiyo moyo wa kimchezo,  ukijikunyata utakuwa unadundwa ngumi kila wakati.

“Milioni 50 tulizopewa zimetusaidia kufungwa bao moja tu pengine tungefungwa hata sita ila tumefungwa sawa ndiyo mchezo tunaendelea kutafuta ushindi, tumejitahidi sana ila kwa sasa sio kichwa cha mwendawazimu tena,” ameongeza Mwakyembe.

Jana Rais Magufuli alieleza kuufatilia mchezo baina ya timu ya Taifa dhidi ya Lesotho ambapo  katika mtandao wa Twitter aliandika; "vijana wangu Taifa Stars, muda mfupi ujao nitakuwa nikitazama mchezo kati yenu na timu ya taifa ya Lesotho, mimi na Watanzania wenzangu tunawatakia mchezo mwema, mrudi na ushindi,".
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )