Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, November 26, 2018

Amber Rutty na Mpenzi wake Wakosa Dhamana kwa Mara ya Tatu, Warudishwa Segerea

adv1
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ na mpenzi wake Said Bakary Kitomali wamekosa tena dhamana kwa mara ya tatu katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na Amber Ruth na Said Bakary, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.

Mshtakiwa Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi imeahirisha hadi December 10,2018.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

Ili Amber Rutty na mpenzi wakewadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti yavkuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 1
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )