Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 12, 2018

Breaking News: Makampuni 13 Yajitokeza Kununua Korosho...Kampuni Moja Linataka Korosho Tani Laki 2

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya serikali.

Majaliwa ametoa kauli hii leo Jumatatu November 12 wakati wa zoezi la kuwaapisha mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Magufuli.

Amesema, makampuni matano yalipeleka barua ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam huku makampuni 8 yakipeleka Dodoma.

Waziri Mkuu ameyataja makampuni hayo kuwa  ni Mega movers  ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )