Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, November 22, 2018

Lori la JWTZ lenye Magunia ta Korosho Lapata Ajali

Gari la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambalo lilikuwa limebeba tani 15 za korosho likitokea wilayani Tandaimba kuelekea Mtwara mjini limepata ajali jana Novemba 21, 2018 na kusababisha korosho zote kumwagika barabarani.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo chanzo chake kilitokana na breki za gari hiyo kufeli, ambapo dereva na wengine waliokuwepo kwenye gari hilo wanaendelea vizuri.

“Gari hilo lilipata ajali jana jioni Novemba 21, chanzo chake ni kufeli breki kwa gari hilo la jeshi“, amesema RC Byakanwa.
 
Novemba 12, 2018 Rais John Magufuli alisema Serikali ya Tanzania itanunua korosho zote za wakulima zilizolimwa mwaka huu 2018 na itachukua dhamana ya kuzitafutia soko.

Alitangaza uamuzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa Jumamosi ya Novemba 10, 2018.

Alisema JWTZ ndio watakuwa na jukumu la kusimamia kuhakikisha ulinzi kwenye maghala, korosho zinapimwa na wakulima wanalipwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )