Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, November 6, 2018

Mbunge wa CUF Ataka Mwenge usikimbizwe Kwa Madai Kwamba Umepoteza Mvuto

adv1
Leo Jumanne Novemba 6, 2018, mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameuliza kama Serikali haioni kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa sasa hakuna umuhimu tena kwani umekuwa ukisababisha mambo mengi ikiwemo magonjwa ya zinaa ikiwamo HIV.

Akiuliza swali katika kikao cha kwanza, mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma, Mtolea alielekeza swali hilo kwa Waziri Mkuu kuwa kama Mwalimu Nyerere alisema anawasha mwenge ili uwekwe juu ya mlima Kilimanjaro kwanini serikali inaendelea kuutembeza.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde amesema "kuwa lengo la mwenge ni kujenga misingi ya binadamu na utu wa mtanzania, pia umelenga kuhamasisha ukombozi wa bara la Afrika, kupitia utaratibu huu, mwenge ni chombo muhimu kwa kuimarisha nchi yetu.”

Mara baada ya majibu hayo Mbunge huyo wa jimbo la Temeke alidai mwenge huo kwa sasa unapokelewa na baadhi ya watumishi wa serikali, wakiwemo madiwani pamoja wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari pekee akidai kuwa wananchi wamechoshwa kuuona kila mwaka.

Kufuatia swali hilo la Nyongeza Spika Ndugai aliamua kumkatisha mbunge huyo wa Temeke kwa kile alichokisema kuwa swali lake halikuwa la msingi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )