Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, November 13, 2018

Neno la DC Jokate Mwegelo kwa Rais Magufuli Kuhusu Uteuzi Anaoufanya

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,  Jokate Mwegelo amempongeza Mkurugenzi Mkuu mteule wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine Sayi ambapo amemtaka awawawakilishe vijana vizuri.

DC Jokate pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Jokate ametoa ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ambapo ameandika  kuwa ana ufahamu uwezo wa Japhet na kuamini kuwa suala la Korosho atalisimamia vyema.

"Rais kaomba leo Ikulu uthibitishwe kijana mdogo uwe Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. - TADB. 

"Tunaamini kwa akili na uwezo wako mkubwa sasa wakulima watafutwa machozi yao na hili la korosho utalisimamia vyema. Sina shaka na uwezo wako kabisa. Mwenyezi Mungu aendelee kukuongoza . 

"Asante Mhe Rais kwa kuendelea kuamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu," ameandika Jokate kupitia ukurasa wake wa Instagram leo.

Japhet Justine Sayi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo kabla ya jana Rais Magufuli kuelelekeza Waziri husika anayeshughulikia benki hiyo kumthibitisha Rasmi kuwa Mkurugenzi mkuu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )