Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 8, 2018

Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Toka Kwa Mabalozi Wapya Wa Uae, Canada Na Spain Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

adv1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 3 walioteuliwa kuziwakilisha nchi za Hispania, Canada na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini, baada ya Mabalozi waliokuwepo kumaliza muda wao.

Waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Francisco Pedros Carretero – Balozi wa Hispania hapa nchini, Pamela O’donnel – Balozi wa Canada hapa nchini na Khalifa Abdulrahaman Mohamed Al-Marzooqi – Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini.

Pamoja na kuwakaribisha Mabalozi hao Rais Magufuli amewahakikishia kuwa Tanzania inathamini uhusiano na ushirikiano mzuri kati yake na nchi hizo na ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kukuza uhusiano huo kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote.

Rais Magufuli amewaambia Mabalozi hao kuwa Serikali inatarajia kuona shughuli mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo iliyokuwa ikisimamiwa na Mabalozi waliotangulia inaendelezwa na kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo uwekezaji katika viwanda.

Kwa upande wao Mabalozi hao wameahidi kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na nchi wanazoziwakilisha na wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kukuza uchumi, kupiga vita rushwa na kuimarisha ustawi wa jamii.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )