Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 19, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 34

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

Hadi ninamaliza kumuadisia, macho yakwa yamemtoka sana.
“Kaka kwa matatizo yako una haja ya kupata muda wa kupumzika, uwanjani si unafahamu kwamba mtu hutakiwi kuwa na mambo mengi kichwani”
“Usijali nitacheza, ila tambua watu ninao waamini kwa sasa ni wachache sana.”
“Pole sana ndugu yangu, ila kama alivyo kuambia mwana sheria wako, usimuamini Camila kama alikufanya yale yote na bado akaamua kurudi basi kuwa makini”
“Kweli, hapa ni mwendo wa kuchezeana akili, akileta ujinga sasa hivi nakuapia haki ya Mungu, nitahakikisha kwamba ninamuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”

ENDELEA
“Kaka kama ukimuua kwa mikono yako huoni kwamba itakuwa ni kesi ya dunia. Baba yake anakwenda kuwa raisi hii hii nchi, ulitambua hilo”
“Nalitambua”
“Na kumbuka wewe ni maarufu. Una makampuni mengi, una kipaji kizuri cha mpira. Utatakiwa siku moja uwe na mtoto wako naye afwate nyayo zako. Hakikisha kwamba hufanyi maamuzi ya kipuuzi Ethan”
 
Frenando alizungumza kwa upole sana huku akinitazama usoni mwangu. Siku zote huwa ninampenda Frenando kwani ni mtu ambaye akili yake imetulia sana na hata akikushauri jambo basi anakushauri kwa ajili ya maisha ya baadae.
“Nimekuelewa kaka, ila leo usiku ninaweza kutoka”
“Unakwenda wapi?”
“Nitakuambia safari kama itakuwepo kwa maana nimekaa mguu mmoja ndani mguu mmoja nje”
“Sawa, tuongozane?”
“Nitakujulisha”
“Poa poa kaka. Mwanangu nimepata kitoto cha Kimerxco hapa hotelini yaani weee acha tu kitamu kishenzi”
“Weee umesha mla?”
“Oohoo unahisi kwamba ninachelewa jamaa yangu. Kitoto ni kihudumu, leo kataingia shifti ya usiku. Yaani asikuambie mtu”
 
“Hahaaa rafiki yangu wee mbaya”
Tulizungumza huku tukiwa tumejawa na furaha sana. Tukaendelea kuzungumza mazungumzo mbalimbali. Kocha akajumuika nasi huku akionekana kuwa mtu wa furahas ana.
“Ethan nina habari nzuri, ila ni mbaya kwa wapinzani wetu”
“Ehee tuambie kocha”
“Leo niliweka hii picha yako kwenye akaunti yangu ya Twitter, na nikaangindika. ‘Mashine yangu imerudi’ Weee wapinzani wamejawa na presha balaa”
“Hahaaa kocha ungewaacha tuwafanyie suprize bwana”
“Tungewafanyia Suprize wangekufa kwa presha, kwa maana si kwa kukuogopa huku”
“Hahaa kazi wanayo”
 
“Kocha una mipango gani baada ya hapa?”
Frenando alimuuliza kocha huku akimtazama usoni mwake.
“Mipango ipo mingi sana. Kama mukichukua kombe, basi ninakwenda kuongeza taaluma yangu ya ukocha na ninampango wa kufindisha timu kubwa duniani”
“Ni mipango mizuri kocha, siku ukipata nafasi kwenye timu yoyote, tungependa kucheza chini yako”
“Haki ya Mungu, lazima niwachukue kwa garama yoyote na nitakuwa tayari hata kuvunja rekodi ya Pogba katika manunuzi yenu”
“Sawa kocha tutakuunga mkono, ila ningependa upate timu kama za Uingereza hivi kwa maana ligi ya hapa Ujerumani mimi naona kama haina changamoto kiviele”
“Ni kweli unacho kizungumza Ethan, ligi ya ujerumani, ina mtawala mmoja ambaye ni Munich. Ila Uingereza kwa sasa hakuna mbabe, kila mwenye kisu kikali basi ndio anaye kula nyama”
“Kweli kocha, natamani siku moja tubebe kombe mikononi mwako”
“Hahaa muta beba tu wala musijali”
“Sawa kocha”
Simu niliyo achiwa na mwanasheria ikaingia ujumbe mfupi wa maneno. Nikaufungua na kuusoma kwa umakini.
‘TUMEMPATA, SAA NNE USIKU NITAKUJA KUKUCHUKUA’
Nilipo maliza kusoma ujumbe huu, nikaufuta kwenye simu yangu.
 
“Vipi kuna tatizo?”
Frenando aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hapana hakuna tatizo”
“Sawa”
“Kocha kesho mazoezi yataanza saa ngapi?”
“Majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi”
“Sawa”
“Mechi ya kesho kutwa nina waomba muweze kujituma sana. Kumbukeni kwamba mechi iliyo pita hamkuwepo na tulifunga goli moja tu. Goli ambalo lilizua maneno mengi kwenye mtando huku watu wengine wakitukashifu kwamba bila nyinyi timu haina uwezo wowote”
“Usijali kocha kila kitu kitakwenda sawa. Unataka nikufungie goli ngapi?”
“Sita”
“Mmmmm”
“Unaguna nini Frenando, mbona ina wezekana”
“Haya mwaya, mimi langu ni goli. Nitazuia kuto kufungwa kwa uwezo wangu wote”
“Ulinde vidole vyako wasije wakakutengua tena”
“Tena sasa hivi nipo makini sana kwa maana kuan watu kama vile wanachezea timu ya taifa. Yaani kazi yako ni kudungua tu mashuti utadhani aliye kaa golini ni roboti”
Maneno ya Frenando yakatufanya tucheke. Nikawaaga wezangu na kurudi chumbani. Nikamkuta Camila akiwa amelala kitandani, nikajilaza pembeni yake huku nikimkumbatia.
 
“Niambie”
Nilizungumza huku nikimbusu shavuni mwake.
“Safi tuu mume wangu”
“Usiku kuna sehemu nitakwenda mpenzi wangu”
“Wapi tena Ethan?”
“Yule mzee amapatikana”
“Kweli?”
“Ndio, nitahitaji kwenda kuzungumza naye uso kwa uso”
“Mume wangu huoni kwamba inaweza kuwa hatari sana kwako?”
“Usijali kila kitu kimewekwa chini ya uangalizi mzuri.”
Camila akanitazama usoni mwangu kisha akaninyonya midomo yangu kwa muda kidogo huku akishusha pumzi taratibu.
“Nitapenda usimfungulie mlango mtu yoyote zaidi yangu”
“Usijali mume wangu, siwezi kumfungulia mtu mlango na nitawamfahamisha baba aweze kunitumia walinzi wake waje kunilinda”
 
“Itakuwa ni vizuri”
Masaa yakazidi kwenda. Usiku ukawadia, tukapa chakula cha usiku, mwanasheria wangu akafika hotelini hapa na helicopter. Tukaagana na Camila huku nikimkabidhi Frenando jukumu la kumlinda shemeji yake kisha mimi nikaondoka. Tukiwa ndani ya helicopter, mwana sheria akanikabidhi bahasha kubwa kidogo ya kaki.
“Humo ndani ya bahasha kuna taarifa za mzee huyo. Tumeweza kufwatilia hadi familia yake iliyopo nchini China”
“Kazi nzuri, kazi umeifanya na nani?”
“Kuna vijana wangu nimewatumia. Wapo wanne wao ni wapelelezi maalumu na wenye uwezo wa juu sana na huwa wanafanya kazi zao wao kama wao”
“Ahaaa sawa sawa”
Nilizungumza huku nikitazama picha kadhaa za mzee huyu, huku nyingine zikimuonyesha famili yake. Tukafika katika moja ya msitu, tukaona kiwanja kidogo cha helicopter ambacho kwa pembezoni mwake kimewashwa moto.
“Ni wapi hapa?”
 
“Hapa ndipo walipo vijana wangu”
Mwanasheria wa familia alizungumza huku helicopter ikishuka taratibu. Helicopter ilipo fika ardhini. Tukafunguliwa mlango na jamaa mmoja mrefu aliye jazia mwili wake. Akanisalimia kwa kunipa mkono kisha tukaanza kuongozana kuingia msituni. Tukakuta mfuniko mzito wa chuma, kijana huyu akaufungua kisha akanza kuingia ndani humu huku akiwa amewasha taa. Wasiwasi kwa mbali ukaanza kunitawala huku nikijifikiria endapo kama mwana sheria ataamua kunigeuka basi, ataniulia humu ndani na hakutokuwa na mtu wa aina yoyote ambaye atafahamu kuhusiana na kifo changu.
 
‘Ehee Mungu nisaidie’
Nilizungumza kimoyo moyo huku tukishuka kwenye ngazi hizi, zipatazo hamsini. Tukakuta kordo ndefu iliyo washwa taa zenye mwanga hafifu kidogo. Tukaendelea kutembea huku tukimfwata kijana huyu nyuma nyuma. Tukatokea kwenye ukumbi mkubwa ambao umejaa tv kubwa sana zipatano kumi. Katika ukumbi huu kuna vijana watatu pamoja na mzee yule wa kichini akiwa amekalishwa kwenye kiti huku amefungwa kamba za mikononi mwake na miguuni. Usoni mwake anamwagikwa na damu na inaonyesha kwamba amepata kipigo kimoja kikali sana. Nikasalimiana na vijana hawa huku wakionekana kujawa na furaha sana ya kuniona.
“Mtu wako mkuu huyu hapa. Tumeweza kumuhoji na ametupa ushirikiano wa kutosha”
 
“Amewaeleza juu ya sehemu alipo huyo mwana mama aliye mteka?”
“Ndio amesema kwamba mwana mama huyu yupo katika nchi moja inaitwa Tanzania katika bara la Afrika Mashariki”
Kidogo nikastuka huku nikimtazama mzee huyu wa kichina. Taratibu nikamsogela na kumtazama usoni mwake.
“Nimewahi kufika kabla ya wewe kufika. Nahitaji kufahamu mwanamke huyo yupo wapi ndani ya Tanzania?”
Mzee huyu akanitazama kwa muda kisha akanitemea mate jambo ambali lilimfanya kijana mmoja atake kumpiga ila nikamzui kwa ishara ya mkono. Nikajifuta mate yake usoni mwangu, kisha taratibu nikavua koti langu hili kubwa na kumkabidhi mwana sheria anishikie.
 
“Yupo wapi mama yangu”
Nilizungumza kwa kauli hii kwa maana tayari mwili wangu umesha anaza kupata hisia ya kutambua kwamba mwanamke huyu ni mama yangu.
“Yupo Tanzania, ila sinto kuambia ni wapi alipo hata uniue”
‘Ethan naomba nguvu’
Nilizungumza kimoyo moyo pasipo mtu yoyote kuweza kusikia. Mwili wangu ukapata msisimko ambao siku zote nikihitaji kuwa na nguvu basi Ethan hunipa nguvu kwa njia hiyo. Nikakinyanyua kiti hichi na mzee akiwa amekikalia jambo lililo washangaza watu wote humu ndani, kwani kwa umri wangu sina nguvu ya kumnyanyua mzee huu na kiti chake. Nilipo mpikisha kimo cha kama ng’ombe dume hivi. Nikamtupa chini kwa nguvu mzee huyu hadi kiti chote kikapasuka vipande vipande.
“Yupo wapi mama yangu?”
 
Nilizungumza kwa ukali na sauti iliyo jaa besi kidogo. Mzee huyu mwili mzima ukazidi kumtemeka. Nikaokota moja ya koande cha mbao ya kiti kilicho chongeka kiasi. Nikamkita nacho kwenye paja la mguu wake wa kulia na kumfanya mzee huyu kupiga ukunga mmoja mzito sana.
“Nitakutajiaaaa…….”
Mzee huyu alizungumza hukua kilia kwa uchungu sana.
“Wapi alipo….”
“Tanzania katika mkoa mmoja uaitwa Tanga…..”
“Itafuteni Arusha hapo”
Nilimuambia kijana mmoja aliye kaa katika kiti huku pembe yake kukiw ana computer ya kampuni ya Apple. Kijana huyu akautafuta mji huo wa Tanga na baada ya muda kidogo, akafanikiwa kuupata.
“Tanga sehemu gani?”
“Katika mji Mmoja unaitwa Lushoto”
“Umeipata Lushoto”
“Ndio mkuu”
“Lushoto eneo gani?”
“Kuna mji mdogo unaitwa Lukozi”
“Lukozi?”
“Ndio”
 
Mzee alizungumza huku akilia kwa maumivu makali sana kwani bado nina endelea kumshindilia ubao huu ambao hadi sasa umezama kama nusu hivi. Nikauchomoa ubao huu huku nikimtazama mwanasheria usoni mwake.
“Nahitaji lifanyike kila linalo wezekana ndani ya siku mbili hizi mama yangu awe amepatikana. Utawapa kiasi chochote ambacho watakihitaji kwenye hii kazi. Mutakwenda Tanzania, sasa sijui mutakwenda wangapi?”
“Tutakwenda sisi wawii mkuu”
“Basi nawaombeni muwe makini na endapo mutampata basi nawaomba muweze kumleta hapa Ujerumani. Natamani sana kuzungumza naye mambo mengi sana”
 
“Sawa mkuu kazi itaisha ndani ya siku nne”
“Nashukuru kwa umoja wenu na ushirikiano wenu”
Nilizungumza huku nikitoa kitambaa changu mkononi. Nikajifuta damu za mzee huyu.
“Mkuu kuna swala moja hatujakujilisha”       
“Swala gani?”
“Huyu mzee ana bosi wake ni mwanamama tajiri sana kutoka nchini Nigeria katika viwango vya utajiri kwa wanawake barani Afrika yeye ni namba moja na kidunia kwa wanawake yeye ni namba nane”
“Anaitwa nani?”
“Yemi. Hilo ndio jina lake linalo pendelewa na watu wengi kuitwa”
“Ina maana bosi wake ndio aliye mtuma hilo boksi jeusi?”
“Ndio mkuu”
Nikashusha pumzi taratibu, nikamsogelea mwana sheria na kumtaza usoni mwake.
“Hii ni vita ambayo tumesha ianzisha. Ni lazima damu za watu ziweze kumwagika. Nahitaji kuwa pamoja nawe kwenye kila jambo”
 
“Usijali mkuu, baba yako alinipa jukumu la kukuangalia nami nitakuangalia hadi mwisho wa maisha yangu”
“Sawa nashukuru kusikia hivyo. Huyo mwana mama tunamfanyaje?”
“Kwa sasa ngoja tumtafute kwanza mamam mzazi. Tukisha mpata tunamgeukia na yeye”
“Nashukuru”
“Huyu mzee mkuu tunamfanya nini?”
Kijana mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwake. Nikamuonyesha ishara ya kuchinja, kijana huyu akachomoa bastoka yake na kumpiga risasi nne za kifua mzee huyu na kumfanya afe hapo hapo.

ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )