Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 23, 2018

Upelelezi Kesi Ya Mfanyabiashara Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Dakika Bado Haujakamilika

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa  kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Mohamed Mustafa Yusufali aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika pamoja na wenzake wanne.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Novemba 23, 2018  na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa Serikali, Tulia Holela  kueleza kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya  kutajwa.

“Kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika naomba mahakama kuipangia kesi tarehe nyingine ya kutajwa,” amesema Holela.

Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Shaidi ameutaka upande wa mashtaka kufanya bidii katika jambo hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 7, 2018.

Mbali na Yusufali ambaye anakabiliwa na mashtaka 198 peke yake,  washtakiwa wengine wanaokabiliwa na shtaka moja la utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni ni Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )