Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 12, 2018

Upelelezi Kesi Ya Uhujumu Uchumi Inayomkabili Mdogo Wake Rostam Azizi Haujakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Elia Athanas ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, tunaiomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa" amedai wakili Athanas.

Kufuatia malezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Mshtakiwa Azizi anakabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na Silaha za aina mbali mbali mbali, utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 9018.

Pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 108, risasi 6496 na pia anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati, Kilogramu 65 yenye thamani ya Shilingi Mil 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 huko Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )