Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, November 22, 2018

Waziri Mkuu Mjaliwa:TSN Endeleeni Kuhimiza Uendeshwaji wa Jukwaa Hili Mikoani na Fanyeni Tathimini

Na Anitha Jonas – WHUSM,Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ameutaka uongozi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuhimiza katika Mikoa mbalimbali umuhimu wa Jukwaa la fursa za biashara na Uwekezaji, ili liweze kusambaa nchi nzima na kuibua fursa  ambazo zitasaidia kufanikisha azma ya serikali ya kufikia uchumi wa Kati na Uchumi wa Viwanda.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo Mjini Tabora alipokuwa akifungua Jukwaa la Nane la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloratibiwa na TSN ambapo amewasisitiza mara watakapo maliza mzunguko wa Jukwaa hili katika ngazi ya Mkoa wa shuke katika ngazi ya Wilaya na Kisekta ili kuweza kuwafikia wajasiriamali wa chini moja kwa moja.

“TSN angalieni  namna ya kuandaa majukwaa ya namna hii katika ngazi ya Wilaya na badae Kisekta kama sekta ya Kilimo,Ujasiriamali,Ufugaji  na kwa kufanya hivi itasaidia kuwafikia wajasiriamali wadogo na pia mara baada ya Jukwaa fanyeni tathimini ili kujua changamoto na kupima mafanikio ya jukwaa,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa Jukwaa hilo Mhe.Majaliwa  alieleza kuwa serikali inafarijika na kazi inayofanywa na TSN ya kuhabarisha na kuelimisha jamii kupitia Jukwaa hilo pamoja na kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji wa biashara ambazo awali zilikuwa hazifahamiki.

Pamoja na hayo katika ufunguzi wa Jukwaa hilo Waziri Mkuu huyo alizindua pia mfumo mpya wa usambazaji wa Magazeti ya TSN kupitia simu janja za kiganjani ambapo magazeti hayo yatakuwa yanapatikana katika (Application ya Play Store.)

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alieleza kuwa baadhi ya faida ya Jukwaa hilo ni kusaidia upatikanaji mitaji, teknolojia, ajira na kuongeza mapato ya serikali hali iliyosaidia kuboresha maisha ya watu.

Kwa upande wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, alisema  kuwa Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Tabora ni Jukwaa la mfano kwa kuwa limepata bahati ya kuhudhuriwa na viongozi wengi akiwemo Kiongozi wa Juu wa Serikalini.

“Leo hapa tuna Waziri Mkuu, Mawaziri Watatu lakini pia tuna Wabunge Tisa. Hii ni fursa nzuri kwa wakazi wa Tabora kulitumia vyema Jukwaa hili,” alisema Dk Mwakyembe.

Pamoja na hayo Dkt.Mwakyembe alipongeza kazi kubwa iliyofanywa na timu ya waandishi wa HabariLeo, Mkoani Tabora na kuweza kuchapa Gazeti lenye kurasa 68 jana, huku kati hizo, kurasa 48 zikuhusu Mkoa wa Tabora pekee.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Jukwaa hilo alimwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa, kuzindua huduma rasmi ya Magazeti ya Serikali kupitia Mtandao, hatua itakayomuwezesha mtu kusoma magazeti hayo hata kwa simu yake ya kiganjani.

 Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda aliipongeza Kampuni ya TSN kwa kuandaa Jukwaa hilo, ambalo limezitangaza na kuziibua fursa za uwekezaji na biashara za Tabora.

“Nakiri mbele yako, hakuna washauri wazuri kama watalaamu katika tasnia ya habari kwani kazi yao inagusa kwa weledi kila sekta,” alisema.

Aliwataka wananchi wa Tabora kuchukua fursa ya jukwaa hilo na fursa zilizopo mkoani humo, na kuzitumia kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

“Tabora ni mkoa wa kimkakati, barabara zote zikikamilika, reli ya kisasa (SGR), kiwanja cha ndege kukarabatiwa mizigo inayopita Tabora itaongezeka kutoka tani milioni mbili ya sasa hadi kufikia tani milioni 10 hadi 15,” alisisitiza.

Alishauri mkoa huo kutumia fursa hizo na kujiandaa kujenga kanda maalumu ya uwekezaji itakayowezesha mkoa huo kuwa kituvu cha mawasiliano na uchumi.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mwita Waitara, alipongeza hatua ya kuandaliwa kwa jukwaa hilo akisema ni kutekeleza maagizo ya viongozi wakuu wan chi wa kuhakikisha kila mkoa unakuwa viwanda angalau 100.

Akimwakilisha Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Waitara alisema tathamini iliyofanywa huko nyuma ilionesha kwamba viwanda vilivyoanzishwa tulikuwa na viwanda 2,280 sawa na asilimia 46.

Alisema tathmini ya pili itafanyika Januari mwaka kesho na kwamba matarajio na matarajio ni kuwa zaidi ya asilimia 90.

 Nae  Kaimu Mhariri wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abadallah, alimpongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kulifanya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Tabora kuwa la kipekee.

Alisema TSN kama chombo cha habari, iliamua kuandaa majukwaa ili kutoa mchango wake katika kuibua fursa mbalimbali za Mkoa husika.

Alisema tangu TSN iamue kuandaa majukwaa ya biashara na Tabora umekuwa ni mkoa wa nane, imeona utayari mkubwa wa wananchi katika kujitafutia maendeleo.

Alisisitiza mbali na kuchapisha magazeti, TSN pia inatoa huduma mbalimbali kama vile za kuandaa vipindi maalumu (documentaries), huduma za kutasfiri na huduma za kuchapisha magazeti.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )