Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, November 1, 2018

Zitto Kabwe Aondolewa Osyterbay na Kudishwa Mahabusu Mburahati

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe leo Novemba 1, 2018 ameondolewa kituo cha Oysterbay alikokuwa amehifadhiwa na kupelekwa Mahabusu ya kituo cha polisi Mburahati kilichopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo umekuja baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake kuanzia saa 2:20 asubuhi hadi saa 5:45 na kumrudisha tena kituo cha Oysterbay.

Wakili wa Zitto, Jebra Kambole amesema kwamba wapo kwenye mchakato wa kuwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili mteja wao apate dhamana.

“Tupo kwenye hatua za mwisho za kuwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili mgeja wetu aweze kupewa dhamana,” ameeleza Kambole.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema hadi sasa kiongozi wake hajapewa dhamana badala yake anazungushwa kila kona.

“Hatuna jinsi tunafuata polisi wanavyotaka maana sasa hivi kiongozi wangu amerudishwa Mburahati," amesema Ado .

Zitto alikamatwa na polisi siku moja baada ya Polisi mkoani Kigoma kumtaka awasilishe vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amesema tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )