Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, December 1, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 164 na 165 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       
“Kwa nini umefunga kifaa hicho?”
“Niliamua tu kufunga kwa usalama wangu binafsi”
Waziri mkuu na Martin wakaingia ndani ya gari hili aina ya Toyota TX. Taratibu geti likafunguka nikaanza kutoa gari hili taratibu. Kabla hata sijakunja kona ya kuingia barabarani gari zipatazao nne kutoka katika kitengo cha NSS, nikaziona zikija kwa kasi jambo lililo nifanya nianze kufikiria kwa haraka ni kitu gani ninaweza kukifanya ili kuhakikisha kwamba ninawakimbia askari hawa wa kikosi cha NSS, mabao tayari wamesha gundua kwamba mkuu wao pamoja na waziri mkuu wapo mikononi mwangu jambo ambalo nina imani wanaamini kwamba ni hatari kwao.

ENDELEA   
“Wewe twende”   
Babyanka alizungumza huku naye akitazama gari hizi zinavyo kuja kwa kasi katika eneo hili, kwa taratibu nikaanza kuingia barabarani gari hizi nazo zikakatiza katika njia ambayo tumetokea, njia inayo elekea nyumbani kwa Babyanka.
 
“Mzee ni wapi tunapo elekea?”   
“Elekea hii njia ya Bagamoyo tukifika mbele huko nitakuambia ni wapi pa kuelekea”
Nikaanza kuongeza mwendo kasi wa hili gari huku nikikimbizana na muda ambao tupo nao kwani tayari hali ya hatari imesha tangazwa kwenye vyombo vya usalama na ninatambua ni lazima hadi  kuna pambazuka ni lazima kutakuwa na vizuizi vingi barabarani.
“Hembu simu yangu”
Babyanka alizungumza kwa haraka nikatoa simu yake mfukoni na kumkabidhi.
 
“Unataka kufanya nini?”   
“Nahitaji kufunga kila kitu wasinione kwenye satelaiti”
“Sawa”
Babyanka akaanza kuminya minya kioo cha simu yake, mimi kazi yangu ni kuhakikisha kwamba ninafika Bagamoyo mapema sana.
“Hawawezi kutufwatilia”
“Umezima?”
“Hapana nimeonyesha muelekeo tofauti na ninapo kwenda”
“Kivipi yaani?”
“Kwa sasa wanaona tunaelekea Mbagala”
“Haiwezi kulete hatari wakastukia?”
“Hapana hakuna mwenye ujuzi  huo ofisi nzima”
“Sawa”
 
Hadi inatimu saa kumi na mbili alfajiri tayari tukawa tumefanikiwa kufika mji Bagamoyo. Waziri mkuu akaanza kunielekeza kuelekea kuelekea katika shamba lake. Japo barabara sio nzuri ila gari hili kidogo linaweza kuhimili mashimo mashimo yaliyopo barabani.
“Kunja sasa kulia nenda moja kwa moja kwenye huo msitu”
“Sawa mzee”
Kusema kweli hii sehemu tunayo elekea kweli ni porini na wala sidhani kama kuna mtu yoyote ambaye anaweza kutupata kirahisi kwani kuna pori kubwa lililo jaa misitu  mingi sana.
 
“Waziri mkuu hivi huku kweli kuna dalili ya watu kiishi?”
Babyanka alimuliza waziri mkuu huku akigeuka na kumtazama siti ya nyuma.
“Wee acha huku nimepapata siku nyingi sana, hata kabla ya kuwa waziri mkuu”
“Mmmmm kazi kweli kweli yaani na hivi ninavyo jisikia ninajihisi kunyong’onyea kabisa”
“Tumebakisha kama kilomita moja hivi?”
“Mmmmmm, kilomota moja!!?”
Martin naye aliuliza kwa kushangaa, kwani hata mimi mwenyewe dereva ninahisi mikono yangu kuniuma.
“Ndio tuvumilie tu kidogo tutafika”
“Huku pia ni Tanzania?”
“Ndio ni Tanzania”
“Mmmmmm kweli Tanzania ni kubwa”
“Yaa”
 
“Ila Martin hata Nigeria ni kubwa”
“Sio kubwa snaa kama Tanzania mkuu”
Mazungumzo ya hapa na pale ndani ya gari, tukajikuta hata mawazo ya uchovu wa hii safari ya kipotea na watu wakazidi kuzoeana sana hususani kwa Martin. Hadi inatimu saa mbili na nusu asubuhi tukafanikiwa kufika eneo la shamba kubwa la huyu mzee, ambapo tumekuta nyumba moja ndogo iliyo tengenezwa kuta zake kwa mbao.
“Karibuni jamani”
Waziri mkuu alizungumza huku tukishuka kwenye gari. Taratibu nikaanza kujinyoosha viungo vyangu vya mwili.
“Karibuni ndani”
Waziri mkuu  alizungumza huku akianza kutangulia mbele, Babayanka akaanza kumfwata kwa nyuma.
“Mkuuu”
“Ndio”
 
“Hivi una waaamini sana hawa watu?”
“Asilimia kumi, vipi wewe?”
“Mini hata moja siwaamini, kwa maana sijajua ni kwa nini wamemaua kukubali kuungana nawe kirahisi hivi?”
“Ninawafahamu na wananifahamu, ila kwa watu ambao walipanga kuniangamiza sio rahisi kuwaamini”
“Jamani karibuni”
Waziri mkuu alizungumza kwa sauti ya juu huku akiwa amesimama nje ya mlango wa kijumba chake hichi. Tukaanza kutembea kuelekea walipo huku bunduki zetu tukiwa tumezishika vizuri sana.
Waziri mkuu akafungua mlango na taratibu tukaingia ndani, japo kuna giza kiasi ila mwanga unapita katika sehemu ndogo zenye uwezo.
“Itabidi tushuke huku chini”
Waziri mkuu alizungumza huku akiwasha iliyo tufanya tuweze kuona vizuri eneo hili la ndani mwa hii nyumba. Nyumba hii haina chumba chochote zaidi ya seble yenye viti viwili pamoja meza moja tu. Waziri mkuu akasogeza meza pembeni, Martin akamsaidia kusogeza viti hivyo viwili, akafunua kapeti zito, tukaona malango wa kuingilia chini, waziri mkuu akaufungua mlango huu na tukaonga ngazi zinzo elekea chini.
“Huku ndipo ilipo nyumba yangu”
Waziri mkuu alizungumza huku akianza kushuka chini, nasi tukaanza kumfwata kwa nyuma, akawasha taa iliyo tufanya tuweze kuona eneo zuri lililo pambwa kwa vitu vingi vya thamani.
 
“Kwa nini uliamua kujenga chini ya ardhi?”
Martina alimuuliza waziri mkuu huku akitazama eneo hili la hii seble.
“Nilipenda sana staili ya majengo haya niliipata nchini Ujerumani”
“Sasa walio jenga hivi ni kina nani?”
“Nilichukua mafundi kutoka nchini Ujerumani na wao ndio walio ifanya hii kazi iliwachukua miezi zaidi ya kumi na sita”
“Duuu”
Waziri mkuu akawasha tv kubwa iliyopo hapa sebleni.
“Hapa huduma zote za ndani zipo”
Taratibu Babyanka akakaa kwneye moja sofa huku akiwa ameshika tumbo lake. Nikamsogelea na kuchuchumaa mbele yake.
“Unajisikiaje”
“Tumbo langu kwa hapa linauma kidogo”
Babyanka alinionyesha sehemu ya chini ya kitovu chake.
“Pole. Mzee kuna dawa za kutuliza maumivu?”
“Ndio zipo?”
 
“Ninaomba umpatie Babyanka”
Waziri mkuu akaingia kwenye moja ya chumba na kutuacha hapa sebleni.
“Raisi Donald Bush anakuja saa ngapi Tanzania?”
“Leo saa moja moja hivi atakuwa amesha tua uwanja wa ndege”
“Tunatakiwa kumuangusha leo”
“Kivipi Dany?”
“Tunatakiwa kumuua raisi Donald, mke wake pamoja na K2?”
“Dany umechanganyikiwa, hivi unajua ni ulinzi wa wana usalama wangapi ambao wnaamlinda raisi Donald?”
“Hilo kwangu sio dili, ninacho kihitaji mimi ni kuhakikisha kwamba ninawaua”
“Hivi vitu Dany usichukulie hasira utafeli na wewe peke yako huwezi kukamilisha hilo unalo lihitaji kulikamilisha”
Babyanka alizungumza kwa msisitizo, waziri mkuu akatoka huku akiwa ameshika kisanduku chenye rangi nyeupe huku kikiwa na msalaba mwekundu.
 
“Unasikia maumivu sehemu gani?”
Waziri mkuu alimuuliza Babyanka ambaye akamuonyesha sehemu anayo hisi maumivu. Waziri mkuu akafungua kisanduku hichi na kuto sindano pamoja na kichupa kidogo cha dawa.
“Hii dawa itatuliza maumivu kwa kipindi fulani”
“Kwa muda gani?
“Masaa ishirini na nne hadi sabini na mbili”
“Sawa nichome tu”
“Mkuu”
martin alinita, nikamtazama kwa ishara ya kidole akanionyesha Tv na sote tukajikuta tukiitazama. Tukaona picha zangu na Martin zikitangazwa kwamba sisi ni magaidi tuliopo nchini Tanzania na atakaye fanikisha kukamatwa kwetu basi atazawadiwa dola milio moja sawa na bilioni mbili za Kitanzania. Sote tukakaa kimya huku tukiendelea kumtazama mtangazaji wa tangazo hili.
“Inabidi kumtoa madarakani kinguvu K2 amefanya mengi maovu”
 
Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo jambo lililo nifanya nimtazame kwa macho ya mshangao.
“Umetambua uovu wa raisi wako leo?”
“Kwa mfanyakazi wa kawaida kama mimi unahisi ni rahisi kuweza kufahamu kwamba bosi wangu yeye ndio gaidi?”
“Mimi ninafahamu”
Babyanka alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kalia.
“Una muda gani tangu ufahamu kwamba K2 ni gaidi?”
“Kabla hata hajawa raisi, mimi na Dany ndio watu wa pekee tuliye gundua uovu wake hadi akamuua raisi aliye pita ambaye ni kaka yake hii yote ni kwa uroho wa madaraka”
“Sawa ni kwa nini ukuzungumza kabla hajachukua hii nchi?”
“Unahisi maisha anayo ishi Dany kwa mimi mtoto wa kike ngingeweza kuishi.?”
 
Babyanka alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Waziri mkuu alibaki mdomo wazi lile alilo tamani kulizungumza alijikuta akishindwa kabisa kulizungumza.
“Nilikiongoza hichi kikosi cha NSS kwa amri kutoka kwa K2, na jana usiku kama ingekuwa ni kumkamata Dany ningeweza kumkamata kwa maana nilikuwa ni mtu wa kwanza kumuona tangu wakiwa kwenye fukwe za bahari ila kutokana mulikuwa mupo wawili nilihitaji akamatwe mwenzako ili wewe nije kukutana nawe”
 
“Kwa nini uliamua kunishambulia?”
“Kwa sababu ya waziri mkuu, sikuhitaji afahamu kujua kwangu kitu chochote kuhusiana na wewe”
Mimi na Martin tukatazama kwani maneno ya Babyanka kidogo yanaendana na ukweli ila sina imani naye kwa asilimia zote.
“Tuachane na melezo mengi. Tunahitaji kumuua K2”
“Kwa leo itakuwa ngumu”
“Kwa nini?”
“Walinzi wake wanao mlinda si NSS”
“Ni nani?”
“Kikosi chake cha wasichana wauaji, hao leo ndio wanamlinda”
Babyanka alizungumza huku akinikazia macho usoni mwangu. Wasichana hao ninawafahamu vizuri kwani Livna ndio kiongozi msaidizi.
 
“Kikosi cha wasichana?”
Waziri mkuu aliuliza kwa mshangao huku akimtazama Babyanka.
“Ndio, na kikoasi hichi kiongozi wao anaitwa Livna Livba”
“Nina mjua”
Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka
“Yupoje huyo msichana?”
Waziri mkuu aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu
“Chotara fulani hivi”
“Hemb ngoja”
Waziri mkuu akakimbilia ndani kwake kisha akarudi na laptop yake mkononi, akaifungua, akaiwasha na baada ya muda akaanza kuminya minya batani za laptop hiyo kisha taratibu akatugeuzia.
 
“Msichana huyu?”
Waziri mkuu alizungumza huku akituonyesha picha ya Livna. Taratibu Martin akaanza kutembea huku akisogelea laptop ya waziri mkuu, taratibu akachuchumaa na kuitazama vizuri picha ya Livna.
“Martin vipi?”
“Ninamfahamu huyu  msichana”
“Unamfahamu vipi?”
Martin akanigeukia na kunitazama kwa macho ya yaliyo jaa wasiwasi mwingi hata swali langu ambalo nimemuuliza anashindwa kulijibu jambo lililo nifanya nijiulize maswali mengi juu ya hili.
“Martin mbona kimya?”
“Huyu msichana ni mke wangu wa ndoa”
Nikabaki nikimshangaa Martin kwani kwa kipindi chote ambacho nimeweza kumfahamu hajawahi kunieleza kwamba alisha wahi kuoa msichana yoyote isitoshe huyo msichana wake nillisha wahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi miaka kadhaa nyuma.
 
AISIIIII……….U KILL ME 165

“Mke wako wa ndoa!!?”   
Nilimuuliza Martin huku nikimshangaa usoni mwake.
“Ndio nimemuoa miaka miwili iliyo pita, ila tulikuja kutengena”
“Kutengena kwa sababu gani?”
“Aligundua kwamba nipo katika kikosi cha Boko Haramu”
“Yeye alikuwa anafanya kazi gani?”
“Yeye alikuwa ni mwana chuo cha ualimu pale Lagos”
“Basi sio mwanachuo ni gaidi, tena gaidi kukushinda hata wewe, na ili tumpate K2 ni lazima kumpata Livna la sivyo hatutafanikiwa”
 
Nilizungumza huku  nikikaa kwenye moja ya sofa.
“Mimi ninajua jinsi ya kumpata”
Martin alizungumza huku akinitazama.
“Tutampataje?”
“Kama yupo Dar es Salaam ni lazima turudi Dar es Salaam”
“Dar ulinzi ni mkali kijana na kitendo cha kurudi ni lazima mutakamatwa na watanzania jinsi walivyo na njaa unahisi hiyo dola milioni moja watashindwa kutoboa siri pale watakapo waona?”
“Nitaenda nao, nitaweza kuwakinga pale nitakapo kutana na vizuizi”
 
“Kitambulisho chako unacho?”
“Ndio ninancho”
“Kama unacho unaweza kwenda nao”
“Wewe utakaa hapa?”
“Ndio sihitaji kurudi Dar es Salaam kwa sasa, nahitaji kupanga mipango ya kumpindua K2”
“Mipango hiyo utaipanga wewe mwenyewe?”
“Hapana ninategemea msaada wenu pia nitawawezesha huko muendapo kukutana na watu ambao  wanaweza kuwasaidia”
“Kwa mimi sihitaji mtu wa kutusaidia”
Nilizungumza huku nikimtazama waziri mkuu usoni mwake.
“Kwa nini?”
“Simuamini mtu hata wewe sikuamini mzee wangu, hii oparesheni nitaiendsha mimi na kijana wangu.”
Maneno yangu yakamFanya waziri mkuu kukaa kimya.
“Tutaondoka saa ngapi hapa mkuu”
Martin aliniuliza.
“Saa kumi na mbili jioni tutaianza safari kama kuna chakula mzee tunahitaji kuandaa”
“Njoo huku”
Waziri mkuu alizungumza huku akisimama, taratibu tukaingia kwenye moja ya chumba.
“Hapa ndio jikoni huwa marehemu mke wangu alikuwa anapenda sana kupatumia kupika pika vyakula vyake tukija mapumzikoni huku”
“Ninaweza kukuamini?”
“Unasema?”
“Mzee ninaweza kukuamini kama mwanao alivyo jitunza katika kuilinda bikra yake?”
Waziri mkuu  alinitazama usoni mwangu huku akinitumbulia macho.
 
“Ina maana umemtoa mwanangu usichana wake?”
“Ila ulisha wahi kuniambia hicho kitu “
“Kwamba?”
“Mwanao bado ni bikra, nihakikishe ninaitoa au umesahau”
“Wewe mwana haramu unadhani mwanangu anaweze kuishi na mwanaume kama wewe unaye tafutwa kila kona?”
“Analitambu hilo na nilimtahadharisha ila alikubaliana nami”
Waziri mkuu akatoa mchele kwenye moja ya droo ya kabati kubwa lililopo humu ndani.
“Hiyo si pete ya ndoa?”
“Ndio”
“Umeoa?”
“Ndio maana nimeivaa”
“Hakikisha mwanangu unamtoa mikononi mwa K2, na baada ya hapo ninakuomba uachane naye kabisa, sinto hitaji umuumize moyo kwa mambo ya kihuni huni sawa”
Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo huku  akiwanikazia macho.
“Mzee acha hasira mambo mengine hayahitaji hasira”
“Hapa ninazungumzia kuhusiana na mwanangu, kwenye hilo swala ni lazima niwe na hasira”
 
“Haya nimekuelewa mkuu”
Tukasaidia na waziri mkuu hadi tukamaliza kupika wali  maharage. Tukaandaa chakula hichi na kurudi nacho sebleni na kuwakuta Martin na Babyanka wakizungumza kwa kucheka sana wakionekana kuzoeana sana.
“Jamani nimeshindwa hata kuja kuwasaidia ikiwa mimi ndio mwanamek niliyopo humu ndani”
“Usijali tumesha korofisha msosi. Kuna jipya lolote lililo tangazwa kuhisiana na kupotea kwenu?”
“Mimi na waziri mkuu?”
“Ndio?”
 
“Hapana ila nyinyi ndio munatafutwa kila dakika mutatangazwa”
“Je simu umepigiwa?”
“Hapana simu nimeifunga na si rahisi kwa mtu kuweza kunipata hewani ila mimi ndio ninaweza kumpigia simu mtu”
“Poa”
Tukaaanza kula chakula hichi tulicho kiweka kwenye sinia kubwa. Hatukuchukua muda mwingi tukamaliza kula chakula. Waziri mkuu akaanza kutuchorea ranami na barabara ya kutokea huku shamhbani kwake kwani hata mimi siikumbuki vizuri. Akatupatia namba yake ya siri ambayoa naitumia huku porini. Tukaanza kuzishuhulikia silaha zilizopo kwenye begii kwa kuzisafisha na kuzipanga vizuri kwa ajili ya kazi ambayo tunaiendea mbele yetu.
“Dany hakikisha kwamba unampata Lucy na kunirudi naye huku porini”
 
“Sawa mzee”
“Niwatakie safari njema, na kazi njema na nina imani kwamba baada ya maasaa machache ninaweza kupata habari nzuri”
“Usijali nina imani  utakwenda kuwa raisi ajaye”
Nilizungumza kwa utani na kumfanya waziri mkuu kucheka kidogo kisha akatupa mikono ya kutuaga. Nikazichomeaka kiunoni bastola zangu mbili ambazo zina risasi za kutosha, kisha bunduki yangu kubwa nikaishika vizuri. Martin akabeba begi lenye silaha na tukaanza kutoka humu ndani. Waziri mkuu akatusindikiza hadi lilipo gari.
“Jamani umakini ndio kitu cha muhimu. Tumieni ujuzi wenu wote kuhakikisha kwamba munamuangusha K2 na nina imani kwamba mutaweka historia kubwa kwenye hii nchi”
“Shukrani mzee”
Tukaingia kwenye gari huku Babyanka akiwa amekaas iti ya mbele. Taratibu nikawasha gari na kuanza kuondoka hili eneo. Sikuweza kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kutokana na kuwangalia angalia barabara hiii ambayo kusema kweli inachanganya.
“Jamani haya maharage yananipa usingizi”
Martin alizungumza huku akijinyoosha viongo vya mwili wake.
 
“Pole sana, lala tukifika barabarani nitakustua”
“Asante mkuu”
Safari ikazidi kusonga mbele huku  kazi ya Babyanka ni kunisomea ramani ya kutokea kwenye huu msitu. Hadi inatimi saa mbili usiku tukafnikiwa kutoka katika huu msitu na kuingia kwenye barabara ya lami. Safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza.
“Dany”
“Naam”
“Uumeoa?”
Babyanka alizungumza huku akinitazama kidole cha upande wa kushoto cha mkono wangu wa kushoto.
 
“Ndio nimeoa”
“Mke wako yupo wapi?”
“Nigeria”
“Ahanafahamu uwepo wako huku Tanzania?”
“Ndio japo tumetengana kwa sasa”
“Kisa nini?”
“Maisha ya hapa na pale”
“Pole”
“Asante. Vipi wewe?”
“Nilibahatika kupata mtoto mmoja wa kike ila alifariki akiwa na miaka miwili”
“Ohoo pole aisee”
“Asante”
“Alifariki na nini?”
“Malaria ilichangia sana kifo chake”
“Pole sana”
“Kuna ukaguzi hapo punguza mwendo”
Nikatazama mbele nikaona kizuizi cha jeshi la polisi. Taratibu nikapunguza mwendo kasi wa gari. 
 
“Martin”
“Mmmmm”
“Amka jiweka sawa”
“Tumefika barabarani?”
“Muda mwingi sana”
Askari aliye valia koti jeupe alitusimamisha, taratibu nikasimamisha gari pembeni, sikushusha kioo upande wangu ila Babyanka aliweza kushusha.
“Njoo huku”
Babyanka alizungumza na kumfanya askari huyo kuzunguka upande alipo yeye, nikatazaama askari wengine waliopo kando kando ya barabara huku wameshika bundiki zao aina ya SMG.
“Habari yako”
Babyanka alizungumza huku akimtazama askari huyu.
“Salama, ninaomba vitambulisho vyeni”
Babyanka akatoa kitambulisho chake, nikamuona askari mmoja akilikagua gari letu akafika katika upande wa kioo changu, taratibu akagonga dirisha taratibu na kuniomba nifungue.
“Mkuu waambie dereva wako afungue kioo”
“Kwani kuna tatizo?”
 
“Tupo kwenye msako mkali wa kuwatafuta magaidi wawili hatari sana”
“Sasa mimi mwenyewe na kitengo changu cha NSS, tupo kwenye mpango wa kuwatafuta hao magaidi, kama umeona kitambulisho changu basi turuhusu tuondoke unatupotezea muda”
Babyanka  alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama askari huyu.
“Mmkuu”
Askari huyu alimuita mkuu wake aliyopo pembezoni mwa barabara upande wa pili.
“Mart”
“Ndio”
“Umakini”
“Sawa mkuu”
 
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikianza kuivuta taratibu bunduki yangu iliyopo pembeni yangu. Tukamuona mzee mmoja akija kwa mwendo wa haraka, akafika sehemu alipo askari wake, akamkabidhi kitambulisho cha Babyanka, mkuu huyo akatazama kitambulisho hicho kwa sekunde kadhaa, kisha akatoa simu yake mfukoni mwake na kuanza kiminya minya batani zake.
“Mkuu unataka kufanya nini?”
Babyanka alizungumza huku akimtazama kuu huyu wa polisi, ila cha ajabu mkuu huyu wa polisi ndio kwanza akasogea mbali kidogo na gari. Nikaminya batani maalumu ya kutoa ‘lock’ za milango, mlio wa lock za milango kufunguka ikawa ishara tosha kwa Martin kuelewa ni kitu gani kinacho takiwa kufanyika kwa wakati huu. 
 
Tukafungua milango ya gari na kushuka kwa kasi na kuanza kuwashambulia askari wote walio shika bunduki. Shambulizi letu halikuchukua hata dakika mbili tukawa tumewashambulia askari wote wenye silaha na kumbakisha mkuu wao aliye pata kiwewe na bumbuwazi kubwa huku simu yake akiwa bado ameishika mkononi mwake.
“Chukau simu yake”
Nilizungumza na kumfanya Martin kumpokonya mzee huyu simu yake akaikuta ipo hewani, nikaitazama jina la namba aliyo ipigia simu nikakuta jina lililo andikwa  ‘mke wangu’. Nikaminya batani ya kukata simu na kumtazama vizuri mzee huyu.
 
“Dany kwa nini mumewaua hawa?”
Babyanka alizungumza huku akishuka kwenye gari kwani hata hili shambulizi wala hakuhusina na kipindi linaendelea nina imani alikuwa anashangaa shangaa.
“Mzee amewaponza wenzake”
“Ulikuwa unazungumza na nani mzee?”
“Mmmm, mke wangu”
“Hembu simu”
Babyanka alizungumza huku akiichukua simu niliyo ishika, akaanza kuikagua. Nikaona sura ya Babyanka ikibadilika kidogo akionekana kama ana wasiwasi.
“Vipi?”
“Mzee ulikuwa unazungumza na mke wako kweli?”
“Ndio”
“Raisi ni mke wako?”
Babyanka alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mzee huyu. Hata kabla mzee huyu hajajibu kitu chochote simu yake ikaita na Babyanka akanigeuzia simu hiyo na kuiona namba aliyo  kuwa anazungumza nayo mkuu huyu wa polisi, taratibu nikaichukua simu hii na kuipokea.
 
“Mume wangu”
Sauti ya K2 ikanifanya nimgeukie mzee huyu na taratibu nikasimama mbele yake.
“Sikuhizi umeanzisha mahusiano hadi na wazee?”
“DAANY?”
“Waziri mkuu, na mkuu wa NSS hukuona thamani yao hata  nikiwaua kwako ilikuwa ni POA tuu, sasa huyu mume wako nitamuua kama nilivyo fanya kwa waziri mkuu wako”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiichomoa bastola yangu moja kiunoni mwangu na kuielekeza kwenye kichwa cha mzee huyu aliye zidi kutetemeka hadi mikojo ikaanza kulowanisha suruali yake.
 
“Dany Dany ninakuomba, ninakuomba mpenzi wangu usimuue huyo mwanaumee tafadhalii…………………!!”
K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa woga na majonzi hapa ndipo nikagundua udhaifu wa K2 upo kwa huyu mkuu wa polisi ambaye kwa muonekano wa nje ni mbaya mbaya tu na sijui amempa nini K2 hadi leo hii analia kwa ajili yake.
 
ITAENDELEA
“Haya sasa Dany ameugundua udhaifu wa K2 ambao ni mkuu wa polisi... je Dany atamfanya nini mkuu huyu wa polisi, atamuua au atamuacha hai. Usikose sehemu inayo fwata ya hadithi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )