Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, December 11, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 172 na 173 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
 
“Wasi wasi wa nani kwa manaa hata leo nikikamatwa wewe wala huto guswa na utaokolewa kama mke wa raisi”
“Mmmmm ila kumbuka wewe ndio baba”
“Ya……”
Sikumalizia senyensi yangu nikaanza kusikia mlio wa helicopter kwa haraka nikamuachia Hawa na kukimbilia dirishani, nikafungua pazia taratibu nikaona helicopter ya jeshi la kimarekani ikishusha wanajeshi wanao tumia kwene nyumba ya tatu kutoka hapa tulipo jambo lililo niogopesha sana kwani kama wameshuka kwenye nyumba ya tatu kutoka tulipo basi kutufikia sisi hapa ni haraka sana jambo ambalo ni hatari sana kwangu na watu wanao nisaidia mimi.

ENDELEA   
“Ni kina nani?”   
Hawa aliuliza huku akikimbilia sehemu nilipo naye akionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.
“Ni wanajeshi wa kimarekani.”
“Mungu wangu wamejuaje kama tupo hapa?”
“Tulia kaa hapo ulipo na usichungulie nje sawa”
“Sawa”
Nikatoka kwa haraka, nikamkuta Martin naye akipandisha ngazi akionekana kuwa na wasiwasi mwingi sana.
“Mkuu wanajeshi wamekuja?”   
“Nimewaona”
Nilizungumza huku tukishuka kwenye ngazi hizi kwa haraka sana. Tukawakuta Babyanka na wezake wakiwa sebleni huku kila mmoja ameshika silaha yake.
 
“Jamani kuna njia ya chini kwa chini ambayo tunaweza kutoroka katika hili eneo.”
Winy alizungumza huku akitutazama usoni mwetu.
“Tuonyeshe kwa haraka tuweze kuondoka na Winy wasiliana na Livna umuelezee hali halisi inayo endelea hapa sawa”
“Sawa kaka”
Winy alizungumza huku akichomoa simu yake mfukoni mwake na kuanza kuminya minya. Nikatoka nje na kuwakuta walinzi wa Livna wakiwa wamejificha kwenye maua yaliyopo humu ndani. Kwa ishara wakaniomba nirudi ndani, nikafanya hivi kwa maana sifahamu ni kitu gani walicho kiona hadi wakaniomba nirudi ndani. Nikarudi sebleni Martin akanikabidhi bastola mbili pamoja na magazine nne.
“Njia ipo katika chumba hichi”
Winy alizungumza huku akinyooshea mkono wake kwenye moja ya chumba.
“Wastue hao wasichana huko nje sawa”
“Pao”
Nikaanza kupandisha ngazi kwenda juu, nikaingia kwenye chumba na kumkuta Hawa akiwa amejibanza kwenye ukuta pembeni ya dirisha.
 
“Wanakuja huku”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Twende huku”
Tukatoka chumbani humu na kuanza kushuka ngazi hizi kwa kasi sana, tukafanikiwa kufika sebleni.
“Livna amesemaje?”
“Amesema tutaonana katika sehemu ambayo tutatokea”
“Ni mbali na hapa?”
“Ndio”
“Poa, tangulieni na Hawa”
Nilizungumza, kwa haraka watu wote wakaelekea katika eneo la mlango wa chumba hicho huku walinzi wa Livna nao wakiwa ni miongoni mwao. Nikaifunga milango ya mbele ya hii nyumba kwa kutumia fungo zake, kishindo kikali nikakisikia kwenye geti ikionyesha mambo yamesha haribika.
“Mkuu twende?”
Martin alizungumza kwa sauti ya juu huku  akiwa amesimama mlangoni.
 
“Kichwa cha Donald kipo wapi?”
“Kipo kwenye begi, Winy ametangulia nacho”
Kwa kupipitia dirishani nikaona wanajeshi wa Marekani wakiingia kwa umakini huku wameshika bunduki zao. Nikakimbilia hadi kwenye mlango wa kuingilia katika chumba hichi. Tukasaidiana na Martin katika kuufunga mlango huu ambao ni mtizo kutokana na kutengezwa na chumba. Tukaanza kushuka kwa haraka kwenye ngazi zinazo enelea chini, tukawakuta Babyanka na wezake wakitubiria. Winy akaminya moja ya batani kubwa ya rangi ya kijani iliyopo ukutani na sehemu hii ya kuingilia ndani ikajifunga kwa ndani. Kisha kwa haraka akaminya batani nyekundu, mtetemeko mkubwa ukatokea hadi sisi tukajikuta tukianguka chini.
“Ni nini hicho?”
Niliuliza huku mapigo ya moyo yakinienda kasi sana.
“Nimeilipua nyumba yangu, na nilikuwa nimeitega mabomo kwa hiyo hapo walipo ndani wote wamekufa”
Sote tukabaki tumemtazama Winy kwani hichi kitu alicho kifanya kusema kweli ni kitu cha ujasiri mkubwa sana.
 
“Tuondokeni”
Winy alizungumza, tukaanza kumfwata Winy kwa nyuma kwa uzuri ndani ya hii njia ya chini kuna taa ndogo ambazo zinatusaidia kuweza kuona tunapo elekea.
“Jamani taratibu mwenzenu nimechoka”
Hawa alizungumza huku akiinama taratibu. Ikatulazima wote kusimama, nikamsogelea Hawa, na mimi kuinama.
“Unajisikiaje?”
“Hapa kunauma”
“Pole, jikaze tuondoke”
“Sawa mume wangu”
Hawa alizungumza kiuvivu huku taratibu akinyanyuka. Tukazidi kusonga mbele huku Winy akiwa ni kiongozi wa sehemu tunapo elekea. Tukajikuta masaa mawili yakikatika na kufika katika sehemu ya kutokea.
“Katazame juu”   
Nilimuambia Martin, kwa haraka akapandisha ngazi za zilizopo katika hii sehemu, akachungulia kwa muda huku kiwili wili chake kikiwa ndani. 
 
“Vipi?”
“Kupo salama”
“Inabidi tusubirie hapa hadi Livna atakapo fika”
“Unaweza kuwasiliana naye?”
“Naona simu yangu haishiki mtandao”
Winy alizungumza huku akiinyoosha nyoosha simu yake juu.
“Hapa ni hadi utokee huko juu”
Babyanka naye alizungumze.
“Ilete”
Martin alizungumza huku  akichungulia humu ndani, Winy akapanda kangazi kadhaa na kumkabidhi simu.
“Hembu ngojeni kwaza”
Msichana mmoja wa Livna alizungumza huku akitutazama.
“Mkuu hakuacha maagizo yoyote juu ya mawasiliano kati yenu na yake?”
“Aliicha”
“Basi ngojeni kwanza yeye mwenyewe anajua nini cha kufanya”
“Alafu ni kweli, mawasiliano yetu yanaweza kunaswa isitoshe sasa hivi mitandao ya simu itakuwa makini sana kwa kila simu zinazo ingia na kutoka katika mitandoa yao”
Babyanka alizungumza.
 
“Basi inabidi kuimarisha ulinzi huko nje. Martin mazingira yapo vipi?”
“Ni pori lenye miti mingi”
“Kuna dalili yoyote ya kuwepo na mtu?”
“Labda hadi nitoke ndio nitazame”
“Hembu chunguza hilo eneo  kwa dakika tano, zikizidi zaidi ya hizo tutatoka kukupa msaada”
“Sawa mkuu”
“Nitaongozana naye”
Msichana mmoja wa Livna alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikatingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kumkubalia. Binti huyu kwa haraka akapandisha ngazi hizi za chuma zinazo elekea juu.
 
“Erick”
Babyanka aliniita huku akisogea pembeni na kujitenga nasi, nikamfwata taratibu huku nikimtazama usoni mwake.
“Unajua hatujawasiliana na waziri mkuu?”
“Ahaaa nimesahau kabisa, ila kwa hizi ngija ngija zilizo tokea kusahau ni lazima”
“Yaa kama itawezekana kule ndio kutakuwa sehemu sahihi ya sisi kuweza kijificha tukiacha hali hii ya hatari ipungue”
“Njia si unaikumbuka?”
“Ramani yake ninayo niliitunza”
Babyanka alizungumza huku akitoa kataratsi mfukoni mwake, akanikabidhi, nikaanza kuitazama vizuri na kukumbuka njia ambayo waziri mkuu aliweza kutochorea.
“Lucy mwanaye sijui itakuwaje?”
“Na tukienda pale pasipo mwanye anaweza hata atusipokee”
“Kuna mtu ndani ya NSS, ninamuamini sana ninaimani kwamba anaweza kutusaidia”
 
“Unamuamini sana?”
“Ndio”
“Basi unaweza kufanya naye mawasiliano”
Kabla hata dakika tano hazijafika, Martina akaingia ndani sehemu tulipo.
“Tunaweza kutoka eneo lipo salama na Livna amesha fika”
Kidogo nikajikuta nikipata amani ya moyo wangu, kwa haraka nikaanza kupandisha kwenye hizi ngazi nikachungulia kwa nje, nikaoga gari mbili nyeusi zikiwa zimesimama huku Livna akiwa anazungumza na wasichana wake. Nikatoka na kuanza kutembea kuelekea walipo simama.
 
“Dany pole sana kwa kurupushani zilizo tokea”
“Asante aisee vipi lakini?”
“Ahaaa umekuwa lulu mwanangu”
“Lulu kivipi?”
“Yaani wamarekani wametoa dau la dola milioni mia moja kwa yoyote atakaye fanikisha kukamatwa kwako, Yaani huko kote unapo pita ni Dany, Dany. Yaani umekuwa maarudu kwa masaa machache mshkaji wangu”
“Mmmmm”
“Yaani Osama mwenyewe hajatafutwa hivi khaaa?”
Maneno ya Livna kwa namna moja ama nyingine yananipa wasiwasi mwingi.
“Yaani laiti ningekuwa ni mtu wa tamaa ningekuuza rafiki yangu ila lengo letu ni moja, hapa ndio nilikuwa ninawaweka sawa vijana wangu  kwamba yoyote atakaye jihisi kwamba ana tamaa ya pesa, basi tamaa yake hiyo iishie moyoni mwake na asiitoe nje ya moyo wake kwani tunaweza kumuua muda wowote na popote atakapo kwenda Duniani lazima tutampata”
 
“Shukrani”
“Ingieni kwenye magari jamani, kwa sasa Dany hutakiwi kuishi kabisa kwenye ardhi”
“Una maanisha nini?”
“Twende nitajua ni wapi kwa kukupeleka”
Livna alizungumza, nikaingia naye kwenye gari moja. Taratibu safari ikaanza ya kuondoka katika eneo hili.
“Hivi wanajeshi wa kimarekani walijuaje kama nipo pale?”
“Wamarekani wana mitandao mingi ya kumtafuta mtu, hususani kwa kupotelewa na raisi wao, kwa hilo lisikushangaze sana”
“Wametambua kwamba sisi ndio tulihusika katika kutekwa kwa raisi wao?”
“Hapana ila wanatutilia mashaka tu hii ni kutokana na rekodi  kubwa ya kigaidi ambayo unayo”
 
“Mungu wangu”
“Usiogope Dany, huwa sipendi kubadilika badilika kama kinyonga, nimekuahidhi kukusaidia na nitakusaidia hadi dakika ya mwisho katila hili”
“Shukrani Livna kwa maneno yako ambayo unayazugumza”
Safari nzima ndani ya hili pori, akilini mwangu ninawaza kuhusiana na jinsi gani maisha yangu kwa sasa yalivyo magumu sana, taratibu nikajukuta nikijilaumu kumuacha hai kwanza K2 na kushuhulika na raisi wa Marekani.
“Dany”
“Naam”
“Usiwaze sana”
“Kuwaza nilazima rafiki yangu”
“Kwa sasa dunia inakutamua kama gaidi. Itabidi kuishi kigaidi gaidi na si kuishi kwa kufikiria kulipiza kisasi”
“Daaa yaani ninayakumbuka maisha ya nyuma sana, ya Mariam na mama yake”
“Duuu hivi huyo msichana yupo?”
“Sijui kwa kweli?”
 
“Mariammmmm lilikuwa tawi zuri la K2 na masiki ya Mungu alijikuta akiiua famili yako pasipo kufahamu kwamba ni familia yako”
“Yaa silaumu sana kwa hilo kwani lilikuwa ni jukumu la kazi yake”
“Yaa pia alifanya kwa kushinikizwa, mama yake aliwekwa kizuizini. Mara ya mwisho nilisikia kwamba yupo Somalia sijuia atakuwepo hadi sasa?”
“Hapana nilikitana naye hapo katikati kipindi ninamkimbia baba Hawa, baada ya hapo aliondoka na mume wake”
“Ahaaa ameolewa?”
“Yaa ameolewa”
“Mungu amsaidie kwenye maisha yake nina imani kwamba atakuwa anajutia maisha haya tunayo ishi sasa”
“Ni kweli, natamani hata itokee ndoto, miaka irudi nyuma. Na niishi yale maisha ya nyumba za kapanga kama vile nilivyokuwa ninaishi kwa mama Mariam””
 
“Ahaaa hilo jambo haliwezekani rafiki yangu, kikubwa ni kupambana hadi mwisho wa mwisho wa maisha yako”
“Nikimua K2 ninajisalimisha mikononi mwa serikali”
“Acha ufala wewe, ukimuua K2 tafute sehemu ukaishi na Hawa wako, leeni mtoto wenu mambo yatakuwa yameishi kiaina hiyo. Ila usiniambie kwamba utajisalimisha kwenye serikali ambazo hazijui ukweli wa mambo kwamba hao wanao waamrisha kufanya hivyo ndio magaidi namba moja”
Nikaka kimya huku nikimtazam Livna usoni mwake. Gari hizi zikafika mwisho wa msitu huu na kusimama, mbele kuna ufukwe mkubwa wa bahari.
“Majira ya saa mbili usiku kuna boti yangu itafika hapa itatuchukua hadi yalipo makao mkuu yangu”
“Sawa sawa”
“Nina imani kwamba siku zote ulikuwa unatamani sana kuweza kuyaona makao makuu yangu”
 
“Huko kwenye meli yako”
“Ndio, ila watu wako tutawafunga vitambaa vyeusi kwenye macho yao nisingependa wafahamu ni wapi wanaelekea”
“Sawa hilo kwangu halina shaka”
“Sawa, ila Dany kumbuka kwamba ninakuhitaji uishi kama gaidi, na niataka kukufanya uwe GAIDI mkubwa zaidi ya magaidi ambao walisha wahi kutokea duniani hapa, si Osama, si nani ila kwa sasa dunia nzima inakwenda kusikia jina la DANYYYY, na hata ukihitaji tuipike Marekani uwezo huo tunaoa na utaweza kuipiga nchi hiyo na yoyote itakayo jaribu kukusogelea ikiwemo Tanzania”
Livna alizungumza kwa msisitizo mkubwa sana huku akinitazama usoni mwangu, nikabaki nikiwa ninamshangaa kwani maneno anayo yazungumza hata siku moja sikuwahi kuyafikiria kichwani mwangu kwani kichwa changu hadi sasa kimetawaliwa na mtu mmoja ambaye ni K2 adui tunaye sakana miaka nenda rudi.

AISIIIII……….U KILL ME 173 

Tukazidi kusubiri masaa yazidi kusonga mbele huku wasichana wa Livna wakizidi kuimarisha ulinzi katika eneo hili. Marija ya saa mbili usiku kama alivyo zungumza Livna, boti moja ikafika katika fukwe hizi, wasichana wawili walio tokea kwenye boti wakafika hadi sehemu tulipo. Livna akaniomba tushuke kwenye gari. Nikashuka kwenye gari huku nikiwa makini sana, Livna akanitambulisha kwa wasichana hawa, kisha sote tukaingia kwenye boti hii.
“Haya magri”   
“Tunayeteketeza”
Livna alizungumza huku akitoa rimoti ndogo kwenye mfuko wake. Akaminya batani nyekundu gari hizi zikalipuka huku nasi tukiondoka eneo hili na kuzidi kutokomea baharini. Martin na wezake wote wakaanza kufungwa vitambaa vyeusi kwenye macho yao.
“Dany”
Livna aliniita huku nikiwatazama jinsi wezangu wanavyo fungwa vitambaa vyeusi na wasichana hawa walio kuja kutuchukua.
 
“Naam”
“Njoo”
Tukatoka eneo hili na kupanda juu kabisa ya boti hii, na kuanza kutazama jinsi maji haya ya bahari yanavyo changuka kila tunapo pita kwenye hii bahari.
“Kwenye maisha yangu huwa sipendi kufanya dhambi ikiwa nina haki ya mtu mikononi mwake”
“Sijakuelewa kivpivi?”
“Baba yako aliacha haki yake kwenye kikosi hichi ninacho kimilili, nimekaa nikafikiri na nilivyo kutana na Martin naye alivyo nishauri japo nilimpatia kichapo, nikaona hapana. Peke yako huwezi, nikaona kwamba nilazima niweze kukupatia msaada japo mimi na baba yako tulitengana kwa ubaya ila siwezi kuendelea ubaya wetu kwako”
 
Livna alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwa ameinamia kwenye bomba zilizopo pembezoni mwa hii boti.
“Nashukuru kwa kuweza kuona hali ninayo pitia”
“Usijali kwa hilo Dany, hembu nieleze ukweli”
“Ukweli gani?”
“Kati ya Hawa na Yemi ni nani unaye mpenda?”
Nnikaka kimya kwa muda huku nikishusha pumzi taratibu.
“Ninampenda Yemi. Hawa imetokea kumsamehe kwa ajili ya kiumbe chake alicho kibeba tumboni na laiti ingekuwa sio hivyo ningemuua”
 
“Usimuue”
“Kwa nini?”
“Mpe nafasi ya kuzaa mtoto ambeye atakuwa ni msaada kwako, kwani tunamkuza kwenye mazingira kama walivyo kua wasichana hawa wengine ambao wote ni bikra kwa hiyo hawajua mwanaume. Wewe na Martin huko tuendapo munatakiwa kuwa makini sana musije mukanivunjia bikra za wasichana wangu.”
“Hahaaaaa, sasa hivi sio kit*** tena”
“Wapi, wakati umetukimbia kidogo, tukajua mwenzetu unakwenda kuua, umeturudia ukiwa umevaa boksa”
“Hahaaa hembu acha kunichekesha”
“Ila unatakiwa kuwa makini na Hawa, kama aliweza kukubadilikia mara ya kwanza basi hata mara ya pili anaweza kukubadilikia”
“Hilo nimelielewa, ila hata wewe inabidi usibadilike kama mara ya kwanza”
“Kwa sasa siwezi Dany, nipo tayari hata kuweka kiapo cha damu”
 
“Una uhakika?”
“Ndio hata ukihitajio niweke sasa hivi nitaweka”
“ Basi ninaomba tuweke”
Livna akanitazama kwa muda kisha akaniaga kushuka chini, hakuchukua muda mrefu akarudi akwia ameshika kisu kidogo, akasimama mbele yangu na taratiba akajichana sehemu ya kiganja chake cha kushoto, kisha akanikabidhi na mimi kisu.
“Nawe unaweza kufanya hivi nilivyo fanya”
Sikuwa na hiyana zaidi ya kuchukua kisu hichi na kujichana kwenye sehemu ya kiganja changu. Taratibu Livna akfungua kinywa chake na kunimba nimnyunyize vipande vya damu8 mdomoni mwake, nikafanya hivyo kisha akavimeza, na mimi akaninyunyizia vipande vya damu mdomoni mwangu na nikavimeza;
“Umeamini kwamba sinto weza kukusaliti?”
“Ndio, ulisha wahi kuweka kiapo kama hichi kwa mtu?”
“Hapana sikuwahi kufanya kwa mtu yoyote na wewe ndio mtu wa kwanza kuinywa damu yangu na mimi kunywa damu yako”
Maneno na vitendo vya Livna vikaanza kunioa ujasirina na kuanza kumuamini, japo si sana kwani kauli ya mama yangu ya kuniambia kwamba nisimuamini mtu bado inaendelea kuishi moyoni mwangu na ninaikumbuka kila ninapo anza kufanya kazi na mtu yoyote hususani yule ambaye alisha wahi kunisaliti kipindi cha nyuma.
 
“Kiapo chetu hichi nina ninakuomba kiwe ni kati yetu mimi na wewe ninakuomba usimuambie mtu”
“Sinto wesa kufanya hivyo nina imani kwamba una nifahamu vizuri”
“Yaa”
“Tutachukua muda gani kuweza kufika huko tuendapo?”
“Masaa kama manne, ni mbali sana”
“Duuu”
Safari ikazidi kusonga mbele huku tukiendelea kuzungumza mambo mengi na Livna huku akiendelea kunipa siri nyingi kuhuaisna na K2 na ili tuweze kumuangusha K2 nilazima kuna mizizi tunatakiwa kuikata kwani nikimuangusha yeye kama yeye basi wapo watu nyuma yake ambao watakuja kulipiza kisasi kwa ajili yake. Majira ya saa nane usiku tukafika kwenye meli kubwa ambayo katika maisha yangu ninaweza kuifananisha na meli ya Titanic iliyo zama miaka mingi ya nyuma, 
 
“Tumesha fika nyumbani kwanagu, hapa hakuna mtu anaye weza kuingia kuanzia chini ya maji, kwenye usawa huu wa maji hata angani, ndio maana ulijaribu kuitafuta sana hii sehemu ila ulishindwa”
Livna alizungumza huku tukishuka juu huku tulipo, boti hii ikasimama pembezoni mwa hii meli, tukashushiwa ngazi na taratibu tukaanza kupanda huku Martin na wezake wakifunguliwa vitambaa walivyo fungwa soni mwao.
Katika hii meli kuna wasichana wengi walio valia nguo nnyeusi zilizo wabana vizuri miili yao. Wasichana baadhi wakabaki wakinishangaa.
 
“Hao hawajawahi kumuona mwanaume uso wa kuso kwa maana tuliwachukua kuanzi walivyokuwa wachanga sana”
“Mmmmmm hiyo kazi aalikuwa anaifanya naani?”
“”Kazi gani?”
“Kazi ya kuwateka?”
“Hao watoto tuliwachukua hospitalini na wengine tulikuwa tunawachukua kwenye vituo va yatima”
“Huko hospitalini huwa munawawaiba au munawachukua tu?”
“Yaa huwa wanaibiwa kwenye vile vyumba vya kuhifadhiwa watoto baada ya kuazaliwa”
“Ahaaa”
Livna akatukaribisha sehemu maalumu ya watu kupata chakula kabla ya utambulisho alio niambia ataufanya mbele ya wasichana wake ambao ni wengi kusema kweli. Tukaanza kupata chakula taratibu, tukamaliza na Livna akaamuru msichana mmoja kuwasanya wezake haraka iwezekanavyo
Mlio maalumu akaanza kusikika.
 
‘Ni nini?”
“Hiyo ni kama kengele, hapo wanakusanyika katika kiwanja namba moja kilichopo gorofa ya kati”
“Hivi wapo wangapi hawa wasichana?”
“”Idadi yao ukitoa wasichana wenye umri kuanzia miaka tisa kushuka chini. Walio bakia wapo laiki moja na tisini elfu na hawa wasichana wadogo wapo kama elfu  kumi”
“Mmmmmmm Livna una hatari, sasa malezi wanayapata vipi hao wasichna wadogo?”
“Usijali kesho nitakutembeza sehemu muhimu kwenye hii meli ila nyengine hatuto weza kuzimaliza kwaaajili ya ukubwa wa hii meli?”
“Ukubwa wake si sawa na Titanic?”
“Weee Titanic ndogo katika hii, wajapani walio jenga meli hii, hawakujenga kwa ajili ya safari. Ipo husasni kwa uzalishaji wa wasichana ambao ni majasusi wa kufa mtu”
“Hivi si wapo ambao wanamjua K2 sasa wakiniona si inaweza kuwa ni shida?”
 
“Hakuna anaye weza kutoboa siri, hawa wasichana tunawafundisha mambo mengi sana moja wapi ikiwa ni kuwa ni utunzaji wa siri za kikosi hichi”
Tulizungumza huku tukipandisha ngazi kuelekea kwenye gorofa ya pili. Tukaingia kwenye ukumbi mkubwa ambao kusema kweli idadi ya wasichaana tulio wakuta humu ni wengi sana. Livna akakabidhiwa kipaza sauti na mmoja wa wakuu wa wasichana hawa. Akaanza kwa kuwasalimia wasichana hawa.
“Leo tuna ugeni ambao kwa sasa watakwenda kuishi nasi hapa kama ndugu zetu. Kikubwa ni heshima, ushirikiano. Ila kuna mmoja wenu nina imani kwamba mumwezeza kumsikia na kama si kumsikia basi mumeweza kumuona hata picha yake. Anaitwa Dany, nina imani kwamba mutakuwa munashangaa kumuona mwanaume hapa au kumuona yeye hapa, ikiwa ni mara kadhaa baadhi yetu niliwaagiza katika kumtafuta”
Livna akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akinitazama kwa jicho la kuiba.
“Japo alipandikiziwa mbegu ya kuonekana yeye ni mbaya, mbegu iliyo mfanya leo hii kuonekana kwamba ni gaidi ila si kweli na ukweli wa kila jambo mimi mkuu wenu ndio naufahamu. Nitaomba muheshimu yeye na timu yake aliyo kuja nayo, na siku za mbeleni nitawaeleza ni nini cha kufanya”
 
Katika kuwatazama tazama hawa viongozi nikamuona msichana mmoja ambaye alishikiriki katika kutuvmia mimi na Mariam kipindi tulipo agizwa kufanya kazi moja na baba yangu ytulivyokuwa nchini Japani. Livna akanikabidhi kipaza sauti kwa ajili ya kuwasalimia wasichana hawa, nikakohoa kidogo li kuliweka koo langu sawa kisha nikawasalimia wasichana hawa wote wakaniitikia kwa furaha kuliko hata walimvyo muitikia Livna.
“Ninaitwa Dany, ninaomba ushirikiano wenu katika kuishi hapa, kusema kweli nimependa usikivu wenu na ukarimu wenu kwangu. Ninawashukuru sana”
Baada ya kujitambulisha nikampatia Hawa kipaza sauti hichi naye akawasalimia, baada ya sote kusalmia na kujitambulisha mbele ya hawa wasichana, tukapelekwa katika vyumba vya kulala.
“Nitalala na Hawa kwa ajili ya kumuangalia”
Babyanka alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Sawa hakuna tabu. Martin ninakuomba kwa muda tuzungumze”
 
“Sawa mkuu”
Martin akaingia chumba ninacho lala. Nichumba kizuri ambacho ukuta wake mmoja ni wa kioo kikubwa na kipo chini ya maji na baadhi ya samaki kwa usiku huu ninawaona wakikatiza katiza eneo la karibu.
“Umeyaonaje mandhari hapa?”
“Nimeyapenda kwa kweli watoto ni wazuri sana aisee”
“Wote hao unavyo waoana ni bikra”
“Bikra?”
“Ndio na hilo ndio jambo nililo kuitia. Tumekuja na hawa magube gube wetu ambao hapa ni mmoja tu ambaye nimeivunja bikra yake ambaye ni Hawa, hao wengine wala sifahamu bikra zao zimevunjwa na kina nani. Kitu ambacho ninahitaji kukusisitoizaia ni kuhusiana na hifadhi hii ambayo tumepewa”
Nilizungumza huku nikimtazama Martin usoni mwake kwa macho makali huku nikiendelea kuisoma tamaa na uchu wake wa mapenzi ulio mvaa baada ya kuwaona wasichana hawa.
 
“Wasichana wote ni bikra, wasichana wote hao wanajua kupambana kulilo unavyo fikiria, mziki wao ninahisi umeupayta kutoka kwa Livna aliyekuwa mke wako. Wewe m** Winy, Livna mwenyewe au Babayanka, ila nisije kusikia kwamba umevunja mtoto wa watu bikra sijui nitakufanya nini, kwa maana sisi huko nje ni wakimbizi na hii ndio hifadhi yetu ya  pekee ambayo tumekabidhi kwa hiyo hado hado bwana mdogo tusije kufukuzwa humu kwa tamaa zetu za ngono na ubaya mimi na wewe ndio wanaume kwenye hii meli hakuna wanaume wengine, sasa ishu ya mimba ikitokea kwa mmoja wao mimi na wewe tutawajibika sawa?”
 
“Sawa muu nimekuelewa sinto wagusa hao watoto wa watu jao nilisha anza kuwamezea mate kusema kweli?”
“Hayo mate yako yaishir tu mdomoni huku nje wala yasitoke”
“Sawa mkuu nipo kwa ajili ya kuifwata amri yako”
:Sawa nashukuru kwa hilo. Unaweza kwenda”
“Sawa mkuu”
Martin akasimama wima na kunipigia saluti kisha akageuka kikakamavu na kuanza kuelekea mlangoni.
“Unakwenda ku Winy?”
Martin akageuka na kutabaamu tu, hilo likawa jibu tosha ya swali langu, akafungua mlango na kutoka chumbani humu. Nikaanza kukichunguza chumba hichi  huku nikitazama mapamba yaliyo wekwa humu ndani. Nilipo jiridhisha na uchunguzi wangu nikapanda kitanda huku nikiwa nimevalia nguo zangu, Kutokana na ucovu mkubwa na kusahau hata kulala kwa siku kadhaa sasa, usingizi mzito taratibu  ukanichukua na kulala fofofo.
                        ***
      Asubuhi na mapema Livna akaingia kwenye chumba changu huku akiwa amevalia nguo za jeshi, kwa bahati nzuri akanikuta nami nipo kwenye harakati za kuamka kitandani.
“Vipi umepata usingizi mwanana?”
“Yaaa umeamkaje?”
“Nipo poa tu, nimekuja kukuamsha nikakuonyeshe eneo la mazoezi”
“Sawa”
“Kumbe hukupata nguo za kubadilisha?”
“Ndio”
“Ngoja nikakuletee, utaoga kisha utabadilisha nguo hizo”
“Sawa sawa”
 
Livna akatoka chumbani humu na kuniacha peke yangu, nikanyanyuka kitandani na kufungua mlango wa bafu na choo uliopo humu ndani. Nikavua nguo zangu na kuoga haraka haraka, nikarudi chumbani huku nikiwa nimevalia boksa, nikamkuta Livna akiwa ameweka kombati za jeshi juu ya kitandani huku yeye akiwa amesimama pembeni.
“Ngoja nitoke mie nisije nikaingia majaribuni”
“Ahaa wapi?”
“Ohoo Dany mimi nikitazama hicho kifua chako, kisimi kinanicheza sasa ya nini kumsaligti Hawa ikiwa yupo humu humu ndani?”
“Hawa mapenzi naye yamekwisha”
“Ahaa wapi, hadi kakubebea mimba unasema kwamba mapenzi yamekwisha?”
“Kweli vile”
“Kwa hiyo nikihitaji kidogo unanipatia?”
“Sio kdogo tu hata kingi nitakupatia”
Tukatazamana na Livna kwa macho yaliyo jaa mahaba, taratibu akausogele mlango na kufunga kwa ndani, kisha kwa haraka akanisogelea na kunishika mashavu yangu kwa viganja vya mikono yake na kaunza ku denda. Tukiwa katika harakati za kuvuana nguo, mlango ukagongwa kwa nguvu, sote tukajikuta tukiutazama mlango huu.
“Vaa”
Livna alizungumza huku akianza kueleka mlangoni, nikavua boksa hii na kuvaa boksa aliyo ni;etea Livna, nilipo vaa suruali yangu, Livna akafungua mlango.
“Mkuu kuna tatizo”
Nilisikia sauti ya msichana.
 
“Tatizo gani?”
Msichana huyu akamkabidhi Livna simu, akatazama kitu kinacho onyeshwa, nikamuona sura yake ikijaa makunyanzi baadhi yatokanayo na hasira, taratibu nikamsogela na kutazamaa anacho kitazama, nikaona wasichana wawili wakiwa wamefungwa gundi maalumu midomoni mwao huku wakiwa katika ulinzi mkali wa kikosi cha F.B.I kutoka nchini Marekani.
“K2 amewauza walinzi wangu nilio muachia kwa Wamarekanai, wakifa basi na yeye amekufaa poamoja na hao Wamarekani”
Livna alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake akionekana kujawa na hasira kali dhini ya hili jambo lililo tokea kwa wasichana wake ambao hata mmoja akifarikia basi ni kosa kubwa sana kwa yule aliye msababishia mauti msichana huyo kwani naye ni lazima atakufa
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa wasichana wa Livna wameingia mikononi mwa F.B.I je wasichana hao waliokuwa wakimlinda K2 je wanaweza kutoa siri ya sehemu kambi yao ilipo? Usikose sehemu inayo fwata ya hadithi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )