Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 25, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 178 na 179 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
   
K2 akamshika kichwa Lucy na kukilaza kwa lazima kwenye meza. Akamnyooshea mkono mlinzi wake, akachomoa bastola na kukabidhi, K2 akaiweka bastola hii kwenye sikio la Lucy huku akinitazama kwa macho makali.
“Ninamuua huyu malaya wako uliye mtoa bikra na kikukaribisha nchini kwangu, sasa utajia kwamba nina uwezo wa kukufanya wewe chochote.”
Baada ya K2 kuzungumza maneno hayo, pasipo na huruma akafyatua risasi iliyo ingia sikioni mwa Lucy na kusababisha damu nyingi kusambaa kwenye meza yake jambo lililo nifanya nifumbe macho yangu kwa hasira kali na kujikuta nikijilaumu  ni kwa nini nimemuacha K2 hai kipindi nilipo pata nafasi ya kumuua.

ENDELEA
K2 akamsukuma Lucy pembeni kisha bastola akamrudishia mlinzi wake.
“Jinsi nilivyo mfanya huyu kunguni, ndipo siku nitakavyo kufanya wewe mwehu”
 
K2 baada ya kumaliza kuzungumza maneno yake akazima tv yake na kusasabisha giza kwenye Tv hii ninayo itumia.
“K2 amechanganyikiwa, alikuwa na haja gani ya kumuua msichana wa watu”
Livna alizungumza huku akikaaa kwenye kiti cha pembeni yangu. Nikakaa kimya huku nikiwa nimekosa jibu la kumjibu Livna. Moyo wangu ukazidi kujilamu kwa kusababisha mauaji ya Lucy ambaye nina imani kwamba amekufa kwa ajili yangu.
“Mazungumzo haya ninaweza kuyapata?”
“Kivipi?”
“Yaa unaweza kuyapata”
Ester alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Naomba niyapate”
 
“Unahitaji na hili pia ulirushe kwenye mtandao?”
“Ndio, tena ikiwezekana munaweza kuutoa upande wangu na kuuacha upande wa K2?”
“Inawezekana kila kitu tuna Edit”
“Naomba mufanye hivyo kama inawezekana”
Ester akaanza kufanya kazi ya kuweka sawa mauzungumzo yangu na K2, alipo maliza akanigeuzia upande wangu na kuonyesha upande wa K2 ambao anaonekana anazungumza na mtu asiye onekana.
“Unaweza kurusha hewani sasa hivi?”
“Ndio”
“Kwa video hii itakuwa ni rahisi kwa K2 kwenda kutolewa madarakani, na itakuwa ninafasi yapekee kuhakikisha kwamba nina mkamata na kumshuhulikia ipasavyo”
“Ila huyu si mtoto wa waziri mkuu?”
“Ndio”
“Hahaaaa, K2 sijui atafanywa nini na hawa watu jamani”
“Mwisho wa ubaya ni aibu”
“Tayari, japo Twiter aliifuta akaunti yetu ila nimeweza kuirudisha hewani”
“Waliifuta?”
“Ndio, akaunti nyingi za watu wanao jihusisha na ugaidi zimefutwa, ikiwemo na ya kwetu”
Ester alizungumza hukua kiendelea kuminya minya batani za laptop yake. 
 
“Sasa ukiirudisha tena si itafutwa tena?”
“Hapana mkuu, nimewapa onyo endapo wataifuta, basi na mimi nitaufuta mtandao wao unao waingiazia mabilioni ya pesa kwa siku”
“Imerudi na idadi ya watu wake?”
“Tena watu wameongezeka kutoka bilioni moja hadi watu bilioni mbili, duniani kote na akaunti yetu ndio inashika nafasi ya kwanza kuwa na watu wengi”
“Duuuu”
“Ninaimani kwamba Watanzia wataamua kufanya maamuzi sahihi ya kumtoa raisi wao madarakani”
Nilizungumza huku nikiitazama video hii, baada ya muda mlango ukafunguliwa akaingia msichana mmoja, akamfwata Livna sehemu alipo kaa, akamnong’oneza na kumfanya Livna kuchukua rimoti na kuwasha tv ambayo ninatumia kuzungumza na viongozi.
 
“Dany kiongozi wa kikundi cha Al-Quida anahitaji kuzungumza nawe”
Livna alizungumza huku akiwa ameishika ritoni na kidole kimoja kipo kwenye batani ambayo inaweza kuruhusu vidoe hiyo kuonekana.
“Al-Quida?”
“Ndio”
“Anaitwa nani huyo kiongozi?”
“Sijajua ila kama upo tayari tuwasiliane naye”
“Sawa muweke tuwasiliane naye”
Mtu aliye ifunika sura yake na kuacha macho yake tu, anaonekana mbele yetu huku, Ester akanipatia earphone fupi za kuvaa sikio moja.
“Akizungumza lugha yake huko utasikia kwa kiswahili”
“Habari yako bwana Eddy”
Sauti hii nzito yenye lafudhi ya kiarabu, ikanifanya nikae kimya kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama.
 
“Asalam ghaleykum?”
“Walyakum Mslam”
“Nimefurahishwa na utendaji wako wa kazi, niliamini kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuiangaisha Marekani, japo sisi tunajaribu  kila siku ila tunaishia kupoteza vijana wetu ila wewe hadi sasa hivi sijasikia jina la kikundi chako wala kukamatwa kw amtu wako zaidi ya kukusikia upo peke yako, una uwezo gani Dany”
“Kabla sijakujibu maswali yako ninahitaji kuiona sura yako na pia itakuwa sio mbaya kama nitalifahamu jina lako”
Taratibu mwanaume huyu akaanza kuvua kitambaa kilicho ifunika sura yake, sote hapa chumbani tukastuka kwani mtu tunaye muona, tulisha sikia habari zake zamani sana kwamba alisha uwawa.
 
“Mimi ni OSAMA BIN LADEN”
Nikatamani kunyanyuka ila miguu ikaishiwa nguvu, kwani kipindi gaidi huyu anatamba kwenye vyombo vya habari, nilikuwa shuleni ninasoma na wala sikuwahi kufikiria kwamba ipo siku nitakuja kuonana naye.
“Nimesikia kwamba wewe umekufa?”
“Hapana, Wamarekani wameidanganya dunia, ila sijakufa. Nipo hai ninapanga mashambulizi mapya, ila wewe umeniwahi”
“Ndio yeye”
Ester alizungumza huku akitugeuzia laptop yake mimi na Livna na kweli sura hii tunayo iona kwenye hii tv ni sawa na sura anayo tuonyesha Ester.
“Mwili wako wako ulitolewa hadharani na kusemekena kwamba umeuwawa?”
“Nitakufa kwa kudra za Allah”
“Inshalah”
 
“Dany nitahitaji kushirikiana nawe kwenye mipango mingi. Mmarekani amenitesa kwa miaka mingi sana, ninaishia mafichoni nikijitahidi kuandaa jeshi jipya litakalo songa mbele kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nina lipiza kisasi kwa Mmarekani. Kulipua magorofa yake ya twin tower bado haitoshi, nahitaji kufanya dunia inikumbuke tena na kufahamu kwamba nipo na nina weza kuibadili dunia”
“Kama ni kushirikiana ninahiaji kuonana kwanza na wewe, nami nitakubali kushirikiana nawe”
“Karibu sana, niambie ni lini unahitaji kuonana nami nami nikutajie muda na saa ya kuonana?”
“Baada ya siku mbili hizi tuonane”
“Sawa kesho jioni tutawasiliana nami nitakuambia ni sehemu gani ambayo tunaweza kuonana” 
 
“Sawa”
Video hii ikazimwa, taartibu nikajikuta nikishusha pumzi huku nikimtazama Livna usoni mwake.
 “Hili nalo jipya jamani”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti changu kwani hichi nilicho kiona kusema kweli maishani mwangu ni kipya kabisa, kwani Osama Bin Laden kipindi anatamba duninai mimi nilikuwa bado kijana mdogo sana tena mwanafunzi.
“Ni kweli unahitaji kuonana na Osama?”
Livna aliniuliza kwa sauti ya chini sana, huku akinitazama usoni mwangu.
“Ndio”
“Ila huoni kwamba inaweza kuwa hatari sana kwa maana satelaiti zote duniani zinaitafuta sura yako?”
“Tutajua jinsi ya kufanya ila nitahitaji kuonana naye”
“Ester DNA ya Osama tuliye zungumza naye na hiyo picha zipo sawa?”
 
“Ndio mkuu, Osama hajakufa na vipimo vinaonyeshe ni yeye”
“Kwa hiyo Marekani ilidanganya watu?”
“Yaaa, walihitaji kujipatia umaarufu nahisi”
“Ila mwenzenu ninahisi kwamba huu ni mtego, wasije huyu akawa ni mtu wa kupandikiza na mwisho wa siku ikala kwetu?”
Livna alizidi kushauri kuliwekea msisitizo hili swala.
“Mkuu kwa hili sidhani kama inawezekana ikawa ni uongo, kwa maana hapa nimaengalia DNA test ina fanana”
“Na yule aliye uwawa na Wamarekani ni Osama gani, jamani roho yangu ina mashaka mwenzenu”
“Tungoje hadi kesho akiwasiliana nasi basi tunatujua ukweli wa mambo”
“Mmmmm haya”
“Hembu wasiliana na Marekani, nahitaji kuzungumza nao juu ya kumchukua Yemi”
 
“Hapana kwa sasa hembu waache kwanza kwa maana nina imani nguvu yao wameielekeza katika kutafuta mawasiliano haya yanapo  tokea, na wakiipata ujue tumekwisha”
“Sawa”
“Ila hili la kuonana na Osama tuwashirikishe na kina Martin”
“Sawa, kama inawezekana wakaja humu chumbani”
Livna akamuagiza msichana mmoja baada ya muda Martin na wezake wakaingia kwenye hichi chumba.
“Mama kijacho mbona hajaja jamani?”
“Amelala”
“Amepata chakula cha mchana?”
“Bado hajapata, ila hajisikia vizuri”
Bayanka alijibu huku akikaa kwenye moja ya kiti.
“Eheee hao Wamarekani wamepatwa na nini tena?”
Winy aliuliza huku macho yake yakiwa kwenye Tv inayo onyesha vikosi vya uokoaji jinsi wanavyo okoa watu ambao wamesalimika katika milipuko ya visima vya kutengenezea nyuklia ambavyo ni muda mchache nimetoka kuvilipua.
“Kazi ya Dany”
 
“DANY……!!”
“Unashangaa nini Babyanka?”
“Ila jamani si tumekubaliana kuachana na swala la kuanzisha vita?”
“Hujajua ni kitu gani kilicho tokea katika masaa haya machache”
“Wamefanyaje?”
“Wamekataa kumuachia Yemi, na wameonyesha utovu wa nidhamu wa kunikoromea”
“Hata kama Dany, ila si kulipua hivyo visima vya nyuklia, hivi unajua ni madhara gani yametokea kwa raia ambao hawana hatia?”
“Babyanka sasa hivi tambua tunaishi kwenye maisha ya aina gani, hakuna muda wa huruma, hakuna muda wa msamaha, hakuna muda wa kuogopana. Hapa ni ubaya kwa ubaya mpenzi wangu”
“Kusema kweli Dany maamuzi hayo sijayapenda”
“Ester muonyeshe video”
“Ipi?”
 
“Anza na video ya K2”
Ester kwa haraka akaanza kuminya minya batani zake, baada dakika moja Tv ikaanza kuonyesha video jinsi K2 anavyo muua Lucy kwa kumpiga risasi, jinsi video hii inavyo endelea kazi yangu ni kumtazama Babyanka usoni mwake.
“Hao watu ndio unahitaji waonewe huruma. Binti wa watu amefanya kitu gani hadi kumpa hukumu kama hiyo. Baba yake yupo kule mafichoni na tulimuahidi kwamba tunamrudisha mwanaye salama mikononi mwake. Sasa angalia alicho fanywa, bado tu unahitaji kuwaonea huruma viongozi kama hao. Wananchini wanaingia matatizoni kwa ajili yao, nilimshawishi aachie madaraka ila bado anang’ang’ania je kuna kitu ambacho unaweza kunishauri na kukulewa hapo?”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Babyanka machoni mwake.
 
“Lucy anadhambi gani inayo mstahili kuuwawa kinyama kama hivyo. Leo K2 anatumia jeshi kunitafuta mimi, anajificha kwa muamvuli wa uraisi, unahisi nikihitaji kumuangamizi, nitakwenda ikulu kumkamata eheee?”
Nikaendelea kufoka na kuwafanya watu wote humu ofisini kukaa kimya.
“Ninarudia tena, tunaishi kama magaidi, sura yangu nimeitangaza kwenye vyombo vya habari na ninajulikana kama gaidi, ila wamenifanya niwe gaidi, sikuzaliwa kuwa gaidi, sikuzaliwa kuwaua watu wasio na hatia.”
Machozi  yalinilenga lenga kwa uchungu ulio changanyikana na hasira kali sana.
“Dany nakuomba utulie”
Livna alizungumza kwa sauti ya upole huku akinishika mabega yangu.
“Babyanka ninahitaji uwe na roho ya kikatili, ninahitaji uwe na roho ngumu kama ilivyo yangu, sihitaji kushauriwa vitu ambavyo mwisho wa siku nitakwenda kuanguka. Nitafeli kwenye hili”
 
“Samahani Dany kama nimekukosea”
“Ok jamani kitu nilicho muagiza binti aje kuwaita ni kuhusiana na taarifa ya kuonana na Osama Bin Laden”
“Hahaa Livna ngoja kwanza, huu ni mchana hakuna aliyopo usingizini kusema kweli, kwa hiyo hembu rudisha akili yako hapa kwanza ndio uzungumze kilicho tuleta hapa”
Martin alizungumza huku akitabasamu, kwa jicho kali nililo muangalia Martin yeye mwenyewe akajikuta akikaa kimya hata tabasamua lilo lijenga usoni mwake likafutika kwani anatambua kwamba nimekasiriaka na sasa sio muda wa masihara kabisa.
“Ndio leo tumewasiliana na Osam Bin Laden”
“Jamani ila Osama amekufa?”
“Ni kweli Winy, kwa jinsi unavyo fikiria wewe nasi ndivyo hivyo tulivyo kuwa tunajua”
 
“Sasa amewasilana nanyi kwa simu au kwa njia gani kwa manaa hamuwezi kusema mumewasiliana na Osama kwa simu, sisi tutaamini vipi?”
“Ester wawekee video”
Ester akafanya kile alicho elekezwa na Livna. Martin na wezake wote wakaonekana kustushwa na video wanayo iona hapa. Wakasikiliza mazungumzo ambayo nilikuwa ninayafanya na gaidi huyu aliye hesabikia kwamba ni gaidi namba moja Dunia, japo kwa sasa inasemekana kwamba nimeichukua nafasi yake ya gaidi namba moja duniani, katika kizazi hichi cha karne ya ishirini na moja.
“Jamani sio mtu aliye vaa sura ya bandia, akawa ni muarabu aliyetumiwa na Wamarekani katika kuhakikisha kwamba wanakukamata mkuu?”
“Ester ametudhibitishia kwamba ni Osama mwenyewe”
“Amedhibitisha kivipi?”
 
“Kila kitu kwa sasa kinawezekana kupitia mtandao, nimeweza kui scan sura yake tuliyo kuwa tunaiona hapo, zimeendana na sura yake halisi na DNA, zinafanan kabisa.”
Ester alijibu na kutusaidia katika kumjibu Martin swali lake.
“Kazi iliyopo mbele yetu ni kuonana Osma Bin Laden, kikubwa ambacho tunachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha kwamba Dany anakuwa katika mikono salama na kama atatoka atarudi salama, je ulinzi wake tutaumarisha vipi?”
Kila mtu akaka kimya akifikiria ni kitu gani cha kuzungumza katika hili.
“Mimi ninafikiria nitengenezewe sura inayo fanana na Dany nivishwe mimi kisha niende kuonana naye ili hata likitokea la kutokea tujue kwamba Dany halisi yupo”
“Martin wazo lako zuri sijui Dany mwenyewe unasemeje katika hilo”
“SIHITAJI KUONANA NAYE”
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo ya hasira ambayo imetoka kunipanda muda mchache, watu wote wakabaki na mshangao, kwani mimi ndio nilipanga kuonana naye ila nimebadilisha maamuzi yangu na nina imani kila mmoja niliye kaa naye humu ndani anahitaji kufahamu ni kwa nini nimekataa kuonana na Osama Bin Laden.


AISIIIII……….U KILL ME 179

“Kwa nini….!!?”
Livna aliuliza huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao.
“Ninahitaji kumpatia kazi moja kabla hajakutana nami”
“Kazi gani?”
“Nahitaji amtafute Yemi, baada ya hapo ndio nitaweza kuonana naye”
Watu wakaka kimya huku wakinitazama mimi usoni mwangu.
“Ester hembu fanya mawasiliano naye”   
“Sawa”
Ester akaanza kuminya minya laptop yake.
 
“Hayupo hewani”
“Basi hiyo kesho akiwasiliana nami basi nitamueleza.”
Baada ya kuzungumza maneno hayo nikanyanyuka kwenye kiti changu na kuanza kujinyoosha kwa maana nimechoka sana kutokana na mechi niliyo ifanya na Livna.
“Jamani nina njaa mwenzenu”
“Hata mimi inabidi tukapate chakula”
Tukatoka chumbani humu na kuwaacha Martin na wezake wakitutazama kwa mshangao  kwani kikao tulicho waita ndio kimekwisha kwa mfumo huo.
“Dany inabidi K2 tumshuhulike kabla  hajaleta matatizo zaidi kwenye nchi ?”
“Unaweza kutuma vijana kwenda kumshuhulikia?”
“Kwa sasa ni hatari na vijana wangu anawajua wengi so inaweza kuleta matatizo”
“Hivi mtoto wake yupo wapi, si ana mtoto wa kiume mmoja?”
“Ndio anaye”
“Ninamuhitaji mtoto wake”
“Leo?”
“Hata ikiwezekana leo ninahitaji kumpata”
“Sawa ngoja niwape kazi ya kumtafuta”
“Tupate chakula kwanza ili tukiingia kwenye kazi ya kumtafuta basi  tunajua tunamtafuta mwanaye”
Tukaingia katika ukumbi maalumu ambao unatumika kwa ajili ya watu kupata chakula. Tukajitengea chakula cha kutosha, kisha tukaka kwenye moja ya meza na kuanza kula taratibu.
“Dany nikuulize kitu”
 
“Niulize”
“Kwa nini ulikuwa unanipa mikito ya namna ile?”
“Kwa nimefanya vibaya?”
“Hapana hujafanya vibaya, ila kusema kweli umenifanya nijihisi kufa, yaani hapana”
“Tuachane na hizo mada bwana, tule twende tukamtafute mtoto wa K2”
“Sawa”
Hata kabla hatujamaliza kupata chakula, akaingia Ester akiwa ameshika laptop yake, akaiweka mezani na kuifunua.
“Ninaona Wamarekani wanajiandaa kwa mashambulizi ya kivita”
Ester alizungumza huku akituonyesha video ya jinsi  ndege za kivita pamoja na meli za kijeshi zikianza safari yake.
“Hii video umeipata saa ngapi?”
“Dakika moja na sekunde kadhaa, sijajua sasa hizi ndege zao wanazipeleka wapi pamoja na meli”
“Isije wakawa wamegundua sehemu tulipo?”
Niliuliza huku macho yakiwa yamenitoka, kwani kufahamika nilipo ni kosa kubwa sana kwangu, kwani nitasababisha vifo vya watu watu wengi ikiwemo watoto wadogo sana waliopo kwenye hii meli.
“Sio  raisi”
Livna alinitoa wasiwasi.
“Ester hujajua hizo ndege zinakwenda wapi?”
“Sijajua nimeona zimeruka tu kutoka katika kambi zao”
“Hii ni nafasi”
 
Nilizungumza huku nikimtazama Livna usoni mwake.
“Nafasi ya nini?”
“Kuiingiza Marekani mikononi mwa Korea Kusini”
“Nimefwatilia nimeona Korea Kusini hawana uhasama na Marekani. Wenye uhasama na Marekani ni Korea ya Kaskazini”
“Kumbeee!!”
“Ndio, unataka kufanyaje?”
“Ester si unaweza kuyaandaa mabomu ya nyuklia yaliyopo  nchini Marekani?”
“Ndio, ila hadi nipate msaada wa wale wezangu wawili”
“Waite”
Ester akatoka hapa huku akikimbia, baada ya dakika mbili akarudi na wasichana anao shirikiana nao kwenye kufanya kazi za kimitandao ambao  wana ujuzi mkubwa sana katika mambo hayo. Kila mmoja ana laptop yake, wakaanza kufanya kazi ya kuandaa mambomu kadhaa ya nyuklia ambayo yapo nchini Marekani.
“Tayari”
 
Ester alizungumza hukua kinigeuzia laptop yake.
“Umeyaelekezea Korea Kaskazini?”
“Ndio”
“Ila ikiwezekana hayo mabomu musiyapeleke kwenye miji yenye watu”
“Unataka tuyapeleke wapi?”
“Nionyesheni ramani”
Msichana mmoja akamgeuzia Livna laptop yake na kumuonyesha ramani ya Korea Kaskazini. Livna akaitazama kwa muda kisha akahgua moja ya eneo.
“Yaelekezeni katika milima ya Paektu huko  ninaimani kwamba hakuna watu na kama wapo wanao ishi niwachahe sana”
“Samahani mkuu ila milima hiyo ni milima inayo toa Volcano kubwa sasa na hayo mabomu inakuwaje?”
“Hapa tunajenga uchonganishi, ninaimani nilazima Korea Kaskazini atajibu mashambulizi hayo”
“Sawa”
Ester akachukua laptop yake na kuanza kiminya minya tena batani kwa kasi kubwa, baada ya kufanikisha alichoa mbiwa akanigeuzia laptop yake.
“Unaweza kushambulia sasa”
“Ni mabomu mangapi?”
“Manne?”
 
“Dany ngoja kwanza”
“Ningoje kwanza kwa nini?”
“Ester hujatambua ni wapi ndege hizo zinaelekea, kwa maana tusije tukaingiza nchi hizi mbili kwenye vita na mwisho wa siku tukajilaumu jamani”
“Logate umeweza kujua ndege za Marekani zinaelekea wapi?”
“Ndio, zinaelekea Pakistani”
“Pakistani kufanya nini?”
“Ngoja niangalie”
Logate naye alizungumza hukua kiendelea kuminya minya laptop yake.
“Ohoo wameweza kunasa mawasiliano yako na Osama Bin Laden, ila wewe hawajaweza kujua upo wapi ila yeye ndio wameweza kujua yeye yupo wapi”
“Ester jaribu kufanya mawasiliano na Osama”
“Sawa”
Ester akaanza kufanya kazi hiyo.
“Nimempata, earphone hii hapa”
Ester baada ya kuzungumza hiyo akanipatia earphone maalumu ambayo inauwezo wa kubadilisha mazungumzo na kutoka katika lugha ya kiarabu hadi kuja katika lugha ya Kiswahili.
 
“Vipi tena Dany?”
“Wamarekani wameweza kusana mawasiliano yangu na yako, ila wewe ndio wameweza kujulikana upo wapi, sasa wameandaa ndege zao za kijeshi pamoja na meli kubwa za kivita zinakuja kukushambulia seheu ulipo, kama inawezekana wewe na vikosi vyako hakikisheni muonaondoka nchini Pakistani haraka iwezekanavyo”
Nilizungumza kwa haraka huku nikimtazama Osama Bin Laden usoni mwake. Akaonekana kustuka sana kwani ni taarifa ambayo hakuwa nayo na kama kukamatwa basi atakamatwa muda wowote kuanzia hivi sasa.
 
“Shukrani rafiki yangu Dady. Allah akubariki”
“Ukifanikiwa kupata sehemu iliyo tulia basi utanijulisha na nina imani kwamba mawasiliano haya wameyapata wamarekani”
“Nashukuru, ninaondoka sasa hivi”
“Sawa”
Wawasiliano haya ya video yakaishia hapa.
“Tuwasaidieni jamani”
Livna alizungumza kwa sauti ya upole.
“Kwa nini?”
“Mzee wa watu anatia huruma, unaona jinsi alivyo stuka, na nina imani hapo Wamarekani wamecharukwa kwa kumuona Osam Bin Laden tena akiwasiliana nawe”
 
“Tutawasaidia vipi wakati ndege ndio zipo njiani kwenda kumteketeza”
“Tunaweza kuzidungua”
Ester alizungumza huku akiwa amesimama.
“Kuzidungua zinawezekana?”
“Ndio, kila kitu tutatumia Satelaiti, ku activaite mabomu yao wao wenyewe na kuanza kushambuliana marubani kwa marubani”
“Sijakuelewa”
“Ngoja”
Ester alizungumza huku akivuta kiti tena na kukaa, nikamtazama Ester usoni mwake na kuona umakini wake katika kazi.
“Minya allpa huko kwako”
Ester alimuambia Logate, kila kitu wanacho kifanya kusema kweli sielewi hata kimoja. Kazi ikawachukua kama dakika saba wakawa wameshamaliza.
 
“Unaweza kuwasiliana na marubani na kuwapa onyo la kurudisha ndege zao sehemu wanapo tokea”
“Kwani zipo ndege ngapi?”
“Ndege kumi na mbili, zote ni jet F-22 Raptor, hizo ni ndege zenye uwezo mkubwa sana wa kushambulia kutokea angani, na sifa yake nyingine haziwezi kushambuliwa na ndege yoyote ya kivita wala bomu lolote ziidi ya wao kwa wao kushambuliana na hizi Jeti zipo Marekani tu na ukiona wameziachia leo  ujue ni mashambulizi makubwa sana wanayo kwenda kuyafanya”
 
Ester alitupa maelekezo huku akituonyesha ndege hizi za kijeshi zinazo itwa F-22 Raptor, muonekano wake tu zinaonyesha ni jinsi gani zilivyo hatari.
“Wamebakisha muda gani kufika Pakistani?”
“Dakika arobaini na tatu”
“Zina spidi kubwa kiasi gani?”
“Sijui nizifananishe na super concod labda, maada spidi yake ni kubwa mmono”
“Watanisikiao hao Marubani?”
“Ndio tuwasiliane nao kwa video call”
“Fany hiyo”
Ester akaiweka laptop yake mbele yangu na kuniweke usawa wangu. Nikaona video za marubani kumi na mbili wakiwa katika kazi ya kuziongoza ndege hizo.
“Habari zenu, nina imani kwamba mumenisikia. Sihitaji kujitambulisha kwenu, ninacho kihitaji sasa hivi kama munaipenda nchi yenu hakikisheni kwamba munageuza ndege zenu na kurudi kwenye kambi zenu nchini Marekani la sivyo hakuna hata mmoja wenu atakaye fika nchini Pakistani.
“Wewe ni nani?”
Rubani mmoja alizungumza huku akinitazama.
“Dany”
 
“Hatusikilizi amri kutoka kwa kwako, amri inatoka kwa raisi wa Marekani”
Rubabi huyo anaye onyesha ndio kiherehere alizungumza kwa kujiamini sana. Nikaifunika laptop hii na kuwafanya watu wote kushangaa.
“Twendeni chumba kile hapa siwaoni vizuri hawa, wajinga. Pia wasilianeneni na makamu wao wa raisi”
“Tayari amesha apishwa sasa hivi ni raisi”
“Vyoyote wasilina naye”
Nilizungumza huku tukitembea kwa kasi kuelekea katika chumba hicho. Tukakuwakuta Martin na wezake wakitazama Tv.
“Jamani kuna kazi muhimu, ninawaomba wote munyanyuke kwenye vitu na mukae pembeni”
Nilizungumza huku nikikifwata kiti ambacho ninapenda kukaa na kipo mbeke ya video ambayo huwa ndio nina wasiliana nao. Hapakuwa na mtu hata mmoja aliye bisha wote wakanyanyuka na kusimama pembeni ili kuto onekana kwenye video hii.
 
“Umewaunganisha kwenye tv?”
“Ndio tv namba moja na mbili zitatumika zote”
Ester alizungumza huku akibadilisha mfumo wa tv inayo onyesha taarifa ya habari. Na ikaonyesha marubani hawa nilio kuwa nina wasiliana nao, huku tv namba moja ikiwaonyesh viongozi  wa Marekani walio kaa kwenye kikao cha pamoja akiwemo na raisi wao bwana Sound.
“Nimewapa amri vijana wako kurudisha ndege zao na kusitisha zoezi la kwenda kumshambulia Osam Bin Laden nchini Pakistani ila bado wanasonga mbele. Sasa wewe ndio mtu wa pekee unaye weza kudilisha maamuzi kwa maana wamedi kwamba wewe ndio umewapa amri”
 
Viongozi wote wa Marekani wakabaki wakiwa wameshangaa, kwani nina imani kwamba hawajui ni jinsi gani nimeweza kufahamu siri yao ya mashambulizi wanayo kwenda kuifanya kwa Osama.
 
“Dany siwezi kubadilisha maamuzi yangu”
“Muheshimiwa raisi, ninakuheshimu na hao vijana wako wanao endendesha hizo F-22 Raptor wana familia zao zinazo wategemea. Wewe na hao wajinga wezako mumekaa hapo hamjui maumivu yoyote ambayo watayapata. Sasa ni ombi langu la mwisho kwako, waambie warudishe ndege kwenye kambi zao”
“Siwezi kumsikiliza Muafrika mjinga kama wewe, huwezi kuitawala Dunia kwa kauli zako za kipumbavu na kizembe nitahakikisha ninakukamata”
 
“Sawa muheshimiwa raisi. Mimi ni Muamfrika mjinga ila nilazima niiangushe Marekani chini”
Nilizungumza kwa msisitizo, kisha nikamgeukia Ester ambaye yupo pembeni yangu na haonekani kwenye hizi tv. Kwa ishara ya macho ikatosha kumuelewesha Ester ni nini anacho takiwa kukifanya. Ester na wezake wakaanza kazi ya kuziongoza wao hizi ndege. Haikuchukua hata sekunde kumi, ndege ya rubani namba moja ikaanza kuonyesha chenga kwenye kipande chake cha video ikimaanisha kwamba tayari amesha lipuliwa na mwenzake. 
 
Nikaendelea kumtazama raisi huyu mpya wa Marekani bwana Sound usoni mwake, ambaye yeye naye na viongozi wezake wanawaona marubani wao kwenye Tv kubwa lililopo katika ukumbi wao wa mikutano. Ndege ya pili nay a tatu nazo zikalipuka, na kuzidi kuwapa hofu viongozi wa Marekani. Ndege ya tato nayo ikalipuka na kuzidisha idadi ya vifo vya marubani hawa kuongezeka, hata ukaaji wa raisi kwenye kiti chake ukawa ni wa kuhangaika. 
 
‘Nyinyi si ndio taifa kubwa duniani, sasa mimi ndio nitakuwa mkubwa kwenu. Shenzi’
Nilizungumza kimoyo moyo huku  nikiendelea kuwaangalia viongozi hawa. Ndege ya sita na saba nazo zikalipuka, ndege ya nane nayo ikalipuka na zikabaki ndege nne, nikamuoan mzee mmoja aliye valia nguo za jeshi zenye vyeo vingi akisimama kwenye kiti chake. Taratibu akapanda kwenye meza yao ambayo ni kubwa, akapiga magoti chini huku akinitazama mimi.
“Dany ninakuomba usiendeleze vifo vya marubani hawa wasio na hatia”
 
“Una fanya nini jeneral?”
Raisi alizungumza kwa ukali sana huku akimtazama jeneral huyo ambaye sijui ni wa kitengo gani cha jeshi.
“Dany mimi ni jeneral wa jeshi la anga, hao ni vijana wangu ninakuomba usiwateketeze zaidi”
“Mtoeni hapa, nchi yangu haiwezi kuingia mikataba wala kumsujudia Gaidi tena mtu mweusi”
Raisi alizungumza, wanajeshi wengine wakataka kumshika jeneral wao, ila akanyoosha mkono kwao na kuwazuia.
“Muheshimiwa raisi, nchi yetu ni kubwa sikatai ina kila aina ya uwezo wa kumuangamiza gaidi yoyote duniani, ila kwa Dany, kubali yaishe. Makosa ambayo aliyefanya marehemu Donald Bush tumuombe Dany yaishe mambo sasa hivi yapo ifuani yakifika shingoni, hakuna hata mmoja ambaye atatoka katika hili jego”
Baada ya jeneral huyo wa jeshi kuzungumza hivyo akashuka mezani na kutolewa eneo hilo. Viongozi wote sura zao zikabaki zimejawa na wasiwasi.
 
“Endeleni kusonga mbelee”
Raisi Sound akili zake wala sijui zipo vipi, kwani alicho kizungumza sikielewi kabisa, nikamtazama Ester sikumpa ishara yoyote.
“Siwaui marubani wako, sasa wewe ndio utawaua kwani mashambulizi sasa hivi yatakuja kwako hapo Washington D.C ulipo, jiandae muheshimiwa raisi”
Viongozi  wote wakaanza minong’ono wengi wakionekana kugopa sana kwa kile kitakacho kwenda kutokea hapo baada ya muda mchache. Ester na wezake ambao kwa sasa ndio wana uwezo wa kuziongoza ndege hizo wakafanya kile nilicho kizungumza, na ndege hizo zikageuzwa badala ya kueleke Pakistani zikaanza kueleke Marekani kwenye mji wa Washington D.C na zikifika hapo nilazima zifanye mashambulizi za kulichangua jengo hilo la serikali alipo raisi Sound na viongozi wengine wote na inchi itakosa kiongozi wa kisiasa kwani nilazima wafe.
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa DANY anazidi kuwa tishio kubwa kwa nchi kubwa DUNIANI Marekani, Je ndege hizo zitafanikiwa kushambulia jengo hilo la kiserikali alipo raisi Sound aliye chukua madaraka baada ya raisi Donald Bush kuuwawa kikatili na Dany? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )