Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 23, 2018

Ali Kiba amliza Amtoa Machozi Shabiki Tamasha la Tigo Fiesta

Msanii wa kizazi kipya, Ali Kiba, amejikuta akimtoa machozi mwananamke mmoja kuanzia mwanzo hadi mwisho baada ya kupanda jukwaani
 
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:00 usiku , msanii huyo alipoitwa kuimba jukwaani wakati wa kilele cha tamasha la Fiesta, lilofanyika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
 
Mara ya kwanza ilianza kama utani dada huyo aliyejulikana kwa kwa jina moja la Ene, kuonyesha hisia baada ya Kiba kupanda na wimbo wa ‘Seduce’, na baadaye alipoendelea kushusha vibao vingine mfululizo mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 30 na kuendelea, alichomoka alipokuwa amekaa na kuvamia jukwaa.
 
Askari waliokuwa wanaimarisha ulinzi eneo hilo walionekana kumkamata kwa ajili ya kumrudisha, lakini Kiba alipomuona aliwaambia wamwachie na kuweza kusalimiana naye huku akiwa anabubujikwa machozi na kumuongelesha, kitendo kilichochukua kama dakika tatu kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
 
Ali[ou;izwa dada huyo kisa cha kuangua kilio namna hiyo, alidai kwamba anampenda sana Kiba, na kumuona uso kwa uso na kuweza kushikana naye mkono ni tukio ambalo bado hajaliamini.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...