Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, December 25, 2018

Alikiba Atoa Ofa kwa Mwanadada Aliyemlilia Wakati wa Tamasha la Tigo Fiesta

Msanii Alikiba ameamua kutoa ofa kwa mwanadada Emiliana Mgema aliyemlilia juzi  kwenye tamasha la Tigo Fiesta

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ali Kiba ametangaza ofa hiyo huku akiwa ameweka video ya dada huyo akiwa anahojiwa huku analia na kueleza hisia zake jinsi anavyompenda msanii huyo.

Ali Kiba ameandika “Asante sana dada anayemjua huyu dada amwambie nina tiketi yake ya bure na mofaya zake za kutosha tarehe 29 /12 Next Door Arena,” aliandika Kiba wakati anatangaza ofa hiyo kwa Emilina ambapo anatarajia kufanya shoo yake aliyoipa jina la ‘Funga mwaka na KingKiba.’

Emy amesema ameanza kumpenda Ali Kiba tangu alipotoa kibao chake cha Macmuga ambapo kipindi hicho alikuwa akisoma darasa la saba Shule ya Msingi Nata mkoani Tabora na kuanzia hapo amekuwa akimfuatilia hadi leo na hakuna ngoma yake hata moja aliyowahi kuiona mbaya.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...