Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 10, 2018

Darasa Aibuka Upya Baada ya Ukimya wa Muda Mrefu

adv1
Msanii  nyota wa muziki wa bongo fleva, Darasa amekuja na ujio mpya kwa nyimbo mbili Kali ambazo ataziachia rasmi Jumatano.

Darasa ambaye anatamba na nyimbo zake moto ukiwamo 'Muziki' ambao umefanya vizuri, amesema ukimya wake ulikuwa na maana kubwa licha ya kuzushiwa mambo mengi mabaya.

"Wasanii hatupendani, unapofanya vizuri badala ya mtu kukuchalenji kwa kutoa nyimbo nzuri wenyewe wanazusha vitu tofauti, muziki umekuwa na siasa sana, nilikuwa kimya na 'projekiti' zangu na nimekamilisha sasa naziachia," amesema Darasa.

Amesema Jumatano ataachia wimbo mpya wa 'Pisha Njia" ambayo tayari ameufanyia video.

"Huu wimbo video yake nimeifanyia Afrika Kusini..., nimetumia mtindo wangu ninaoutumia katika kuimba, naamini utakuwa aibu kwa wote ambao hawanitakii mema na kunizushia uongo," amesema Darasa
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )