Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 7, 2018

Mahakama Kuu Yamwachia Huru Aliyemuua Mtu Aliyekuwa Akimbaka Mkewe

adv1
Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora, John Utamwa amemwachia bila masharti mkazi wa kijiji cha Mahene Wilaya ya Nzega aliyekiri kumuua bila kukusudia mtu anayedaiwa kumbaka mkewe.

Kabla ya uamuzi huo upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili Tito Mwakalinga umedai Oktoba 12, 2016 mshitakiwa alisababisha kifo cha Mabula Ngassa kwa kumpiga  fimbo na kumsababishia majeraha mwilini.

Wakili Mwakalinga amesema siku hiyo mshtakiwa alirejea nyumbani kutoka katika harusi ya jirani yake na kukuta mlango wa nyumba yake umevunjwa huku sauti ya mkewe ikisikika akiomba msaada.

Ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuta mkewe akibakwa huku watu wengine wawili wakiwa wamemshikilia, kuamua kutumia fimbo kumpiga aliyekuwa akifanya kitendo hicho.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo,  Jaji Utamwa amesema  baada ya kusikiliza pande zote mahakama imezingatia kwamba mazingira ya mauaji yalitokana na mshitakiwa  kukuta mkewe akiomba msaada wake kwani alikuwa anabakwa.

Ameeleza kuwa mahakama imekubali maelezo ya wakili wa utetezi,  Chombala Kanani kwamba mshitakiwa alisababisha kifo kwa kwenda kufanya kosa kubwa la jinai ambalo hata adhabu yake ni kubwa kisheria.

Amebainisha kuwa mshtakiwa alikuwa anachukua hatua ya kumlinda mkewe  kwa kumtetea dhidi ya hatari aliyokuwa anakabiliana nayo ya kubakwa kosa ambalo lilikuwa linafanywa na watu ambao asingeweza kupimana nao nguvu.

Jaji  Utamwa amesema alitumia fimbo aliyoiokota eneo la tukio tena kwa kuirusha ikiwa ni njia ya kujihami kwa ikizingatiwa kuwa ilikuwa usiku.

Chombala aliiomba mahakama itoe adhabu ndogo  hata kwa kumwachia kwa masharti mshitakiwa kwani  ni mkosaji wa mara ya kwanza, ana familia   na watoto wanaomtegemea.

Pia wakili huyo alieleza kwamba mshitakiwa tayari alikiri tangu siku ya kwanza alipokamatwa na hakuisumbua mahakama hivyo amepunguza gharama na muda.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )