Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 17, 2018

Serikali kulifuta shirika la Ndege la Fast jet....Yatoa Notisi ya Siku 28

adv1
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania  (TCAA) imesema Shirika la Ndege la Fastjet limepoteza sifa ya kufanya biashara nchini, hivyo limezuia ndege moja ya shirika hilo kuruka kutokana na matatizo ya mara kwa mara na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Hamza Johari leo Jumatatu Desemba 17, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema tayari TCAA imetoa notisi ya siku 28 kuanzia leo ya kusudio la kufuta leseni ya shirika hilo.

"Tumekuwa tukiwaandikia barua ya kuwataka watueleze kuhusu mwenendo wao wa biashara tangu Fastjet Plc wajiondoe lakini pia shirika limekuwa na madeni mbalimbali ambayo hayajalipwa. Tukiomba watupe mpango wao wa fedha na biashara kwa mujibu wa sheria hawafanyi hivyo," amesema Johari.

Amesema shirika hilo linadaiwa na watoa huduma wake wengi ikiwemo TCAA inayolidai Sh1.4 bilioni lakini pia halina meneja mwajibikaji ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ndege anayepaswa kutoa majibu ya hali ya ndege.

"Kwa sasa fastjet hawana ndege. Ndege yao tangu jana tumeizuia kuruka kwa kuwa imekuwa ikipata hitilafu mara kwa mara na hawana mtu ambaye anaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wake jambo ambalo linahatarisha usalama endapo itaruka," amesema Johari.


==>Msikilize hapo chini
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )