Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 2, 2018

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Aendelea Kushikiliwa na Jeshi la Polisi

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita jana Jumamosi Desemba Mosi, 2018 alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na hadi leo saa 9:25 alasiri alkuwa bado anaendelea kushikiliwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo kuwa sababu ya Mwita kukamatwa ni kitendo chake cha kuongoza maandamano bila kuwa na kibali. Manadamano hayo yalifanyika jana katika kata ya Vijibweni wilayani Kigamboni kuelekea daraja la Mwalimu Nyerere.

Mwita pia ni diwani wa kata ya Vijibweni Kigamboni kwa tiketi ya Chadema.

“Tulipomkamata akaeleza alikuwa anakwenda kuzindua kisima cha maji ambacho hakukijenga yeye kilijengwa na Serikali kupitia kwa mheshimiwa DC aliyehamia Ruangwa,” amesema Mambosasa.

“Sasa yeye alikuwa anataka kupora ili kutafuta sifa kwamba alijenga yeye wakati mradi ni wa Serikali, aliokuwa amewaalika walikimbia wote.”

Amesema polisi wanaendelea kumshikilia hadi upelelezi utakapokamilika, baadaye atafikishwa mahakamani.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema meya huyo jana alikuwa na mkutano na baadhi ya wananchi wa kata ya Vijibweni kabla ya kuzindua matawi mapya.

Amesema walipokuwa wakielekea katika uzinduzi wa matawi hayo polisi waliwavamia na kuwakamata.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )