Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

Mrema Agoma Kurudi CCM

adv1
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP na Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Agustine Mrema amesema kuwa hawezi kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa kumfuata ndani ya chama chake bali atafanya hivyo akiwa upinzani.

Mrema ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo cha EATV  ambacho kilitaka kupata maoni yake juu ya hamahama ya waliokuwa wabunge wa vyama vya upinzani ambao walieleza sababu kuu ya kufanya hivyo kuwa ni kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mrema amesema, "sina sababu ya kurejea CCM, na ningetaka kurudi CCM hakuna wa kunizuia, ila narudi kufanya nini kwa sababu Rais aliniona nikiwa TLP, nirejee CCM kutafuta nini kama kazi nimepata na nawatumikia watanzania."

"Kuhusu kumuunga mkono Rais mimi nilimuunga mkono akiwa hajachaguliwa licha ya wenzangu wa upinzani walikuwa wamenitenga, kwa hiyo sirudi CCM kwa sababu Rais wangu hajaniambia nirudi CCM," ameongeza.

"Siamini kumfuata Rais CCM ndiyo kumuunga mkono, mbona mimi niko TLP na namuunga mkono, nampenda nitaendelea kuwaambia watanzania wamchague," amesema Mrema.

Mrema alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambaye alijibebea umaarufu kwa utendaji kazi wake lakini pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo ambapo mwaka 2015 kiongozi huyo alienguliwa na Mbunge wa sasa James Mbatia.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )