Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 31, 2018

Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Pancras Ndejembi Kuzikwa Kesho

adv1
Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Pancras Ndejembi unatarajia kuzikwa kesho Jumanne Januari Mosi, 2019 katika  kitongoji cha Chizomoche kijiji cha Bihawana Jijini Dodoma.

Ndejembi (90) alifariki dunia Jumamosi Desemba 29, 2018 saa 2  asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Mweyekiti wa kamati ya mazishi, David Mzuri amesema leo Jumatatu Desemba 31, 2018 kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo watoto wa marehemu ambao walikuwa wanasubiriwa kutoka nje ya nchi.

Mzuri amesema mwili wa marehemu ulitarajia kuchukuliwa hospitali leo na kulala nyumbani kwake mtaa wa Uzunguni kata ya Kilimani.

“Kesho  saa sita mchana tutapeleka mwili wa mpendwa wetu Kanisa la Mtakatifu Paul wa Msalaba na ibada itafanyika pale kisha msafara utaelekea Chizomoche kwa ajili ya mazishi,” amesema.

Baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu ni mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda na John Malecela. Viongozi wengine wastaafu ni Balozi Job Lusinde, Joseph Butiku, William Kusila na Hezekia Chibulunje.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )