Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, December 6, 2018

Putin: Urusi itatengeneza makombora Mapya Iwapo Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo

Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo, ameonya rais Vladimir Putin.

Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri.

Rais wa Putin amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

Katika tamko hilo lililoangaziwa kwenye televisheni, kiongozi huyo alisema mataifa mengi yanaunda silaha zilizopigwa marufuku katika mkataba wa INF

"Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaonelea ni lazima wao pia wawe na silaha ," alisema.

"Jibu letu ni nini? Bila shaka - sisi pia tutafuata mkondo huo."
 
Rais wa Marekani Donald Trump siku za hivi karibuni aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba huo kutokana na mienendo ya Urusi.

Wadadisi wanasema Urusi unachukulia suala la uundaji wa silaha hizo kama mbinu mbadala ya kuimarisha vikosi vyake na gharama yake ni nafuu.

Alipowasili kwa mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa EU, Kiongozi wa muungano wa Ulaya anayesimamia sera za nje Federica Mogherini ametoa wito kwa mataifa hayo mawili kudumisha mkataba huo akiongeza kuwa "Umekuwa hakikisho la amani na usalama barani Ulaya kwa miaka 30 sasa".

-BBC
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )