Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

Rais Magufuli Ahoji Ufukwe wa Coco (Coco Beach) kutokuwa na Choo

adv1
Rais John Magufuli ameshangazwa na ufukwe wa Coco (Coco Beach) pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam kutokuwa na choo wakati eneo hilo zinakusanywa fedha kila siku.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 20, 2018 kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la  Selander jijini Dar es Salaam, Rais amedai magari yanayoegeshwa kando ya fukwe hiyo hulipiwa Sh2,000.

“Coco Beach panatia aibu. Ifike wakati tuzizungumzie aibu zetu pale hakuna hata choo, ndio nasikia wanajenga sasa,” amesema.

“Wanakusanya mapato kila siku hatujui hizo hela zinakwenda wapi na wanashindwa hata kujenga mabanda yaliyoboreshwa.”

Hata hivyo, amesema Jiji la Dar es Salaam limebadilika na kuwa na sifa ya kuwa jiji la kibiashara, kwamba anafurahi kuhamia Dodoma akiacha Dar es Salaam ikiwa katika hali hiyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )