Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 10, 2018

Rais Magufuli atoa vitambulisho maalumu kwa wafanyabiashara wadogo Wenye Mitaji Chini ya Milioni 4

adv1
Rais John Magufuli, amezindua vitambulisho maalumu 670,000 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo ili viwasaidie kuzitambulisha biashara zao.

Rais Magufuli amegawa vitambulisho hivyo leo Jumatatu Desemba 10, alipokuwa katika mkutano wake na viongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wakuu wa mikoa ambapo amesema vitambulisho hivyo ni maalumu kwa wafanyabiashara ambao mtaji wao hauzidi Sh milioni nne.

Baada ya kugawa vitambulisho hivyo maalumu kwa wakuu wa mikoa ili wakawapatie wafanyabiashara katika maeneo yao, Rais Magufuli ametaka wafanyabiashara hao wasisumbuliwe na mtu yeyote.

“Nimefikia hatua ya kutoa vitambulisho hivyo mimi mwenyewe kwa sababu nimeona mamlaka husika inachelewesha na wafanyabiashara wadogo wanaendelea kusumbuliwa.

Rais Magufuli amesema vitambulisho hivyo viko 670,000 na kila mkuu wa mkoa atapewa vitambulisho 25, 000 ili wakavigawe kwa wafanyabiashara wa maeneo yao na fedha watakazopewa wakazilipe TRA.

“Vitambulisho hivi navitoa bure ila wafanyabishara watachangia 20,000 kila mmoja, kama kurudisha gharama ya utengenezwaji wake ili fedha hizo zikatumike kutengenezea vitambulisho vingine na kianze kutumika mara tu anapokipata.

“Kama vitambulisho hivi navitoa mimi mwenyewe sijaona mtu wa kuwasumbua, na mfanyabiashara mwenye mtaji wa chini ya Sh 4,000,000 na ana kitambulisho nasisitiza asisumbuliwe,” amesema.

Aidha Rais Magufuli ametoa rai kwa wafanyabiashara watakaopata vitambulisho hivyo kuvitumia kwa matumizi yao na si kuvichukua kisha wakawafanyie biashara wafanyabiashara wakubwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )