Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 17, 2018

Tutatumia Mbinu na Nguvu Zote Kulinda Maeneo Inakopita Miradi ya Serikali

adv1
Serikali  imesema iko katika mpango wa kujenga kituo cha polisi katika Halmashauri ya Itigi kwa ajili ya kudhibiti hujuma na uhalifu katika ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) na mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).
 
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wavamizi kuingia eneo la hifadhi ya Rungwa ambayo kuna mito 18, ambayo ni chanzo cha Mto Rufiji ambako mradi wa umeme unajengwa.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitembelea na kukagua mradi wa kituo kipya cha polisi cha Wilaya ya Manyoni mkoani Singida na kukagua eneo linarotarajiwa kujengwa Kituo cha Polisi Itigi lengo likiwa kudhibiti matukio ya uhalifu.

Akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni, Naibu Waziri Masauni, alisema kuwa serikali iko tayari kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha miradi mikubwa ambayo serikali ya awamu ya tano imeianza, inakamilika bila kufanyiwa hujuma zozote na wahalifu.

“Miradi mikubwa ambayo Rais wetu Dk. John Magufuli na serikali anayoiongoza ameianzisha ni muhimu ikalindwa ili ilete manufaa kwa nchi itakapokamilika na sisi kama wizara tutahakikisha tunasogeza huduma za ulinzi na usalama katika maeneo yote ambayo miradi hiyo inapitia, ndio maana leo nimetembelea ujenzi wa kituo cha polisi Manyoni ambacho kiko mbioni kukamilika, lengo ikiwa ni kulinda miradi hiyo mikubwa,” alisema Masauni.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka, alikiri kuwapo na haja ya kituo katika wilaya za Manyoni na Itigi ili kuboresha usalama katika maeneo hayo ambayo yanapitiwa na miradi hiyo mikubwa miwili, huku akiiomba wizara kupeleka askari katika vituo hivyo vya ujenzi utakapokamilika.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )