Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 22, 2018

Wanawake Wanne Wavamiwa na Kubakwa Usiku wa Manane

adv1
Wanawake wanne (majina yamehifadhiwa) wakazi wa kijiji cha Buganzu kata ya Lunzewe Mashariki, Wilayani Bukombe Mkoani Geita wamebakwa na wanaume zaidi ya mmoja baada ya kuvamiwa na watu hao wakiwa majumbani mwao.

Tukio la kubakwa wanawake hao limetokea Desemba 11 majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho, walipovamiwa na wanaume wanne wakiwa wamelala kisha kubakwa na kila mmoja na kupelekea kuwasababishia maumivu makali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa waliofanya unyama huo wamekwishakamatwa ambapo amewataja kuwa ni pamoja na George Deogratius(42) maarufu (Tolu) mkazi wa Ibamba, Josephat Emmanuel(25) mkazi wa Kabuhima, Rashid Maganga(18)) na Albert Makisio maarufu Kamkono wote wakazi wa  Ibamba.

Kwa mjibu wa Kamanda Mponjoli, matukio mengine ni pamoja na watu wawili kuuawa Desemba 19 majira ya usiku, na wananchi wenye hasira kali wakiwa katika jaribio la kutenda uhalifu katika kijiji cha Nyakahengere kata ya Lukalanga Mjini Geita.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )