Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 23, 2018

Waziri Afanya Ziara ya Kushtukiza Ubungo na Kukuta Nauli Zimepandishwa Kiholela

adv1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mkioani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam na kubaini wamiliki kupandisha nauli.
 
Kitendo cha wamiliki hao wa mabasi kimefanywa licha ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kupiga marufuku kupandisha bei za nauli wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya,

Kamwelwe aliyabaini hayo jana alfajiri alipofanya ziara kituoni hapo na kushuhudia nauli zikiwa zimepandishwa na madalali.

Mbali na nauli kupandishwa, pia abiria wanaokwenda mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mbeya na Kilimanjaro, wamekumbwa na adha ya usafiri kutokana na wingi wa abiria na uchache wa mabasi hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo, Waziri Kamwelwe alisema abiria wanapandishiwa nauli hali inayowafanya kulipa zaidi ya nauli iliyopangwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

“Nimefika kituoni hapa saa 11:15 alfajiri na kuzunguka kwenye baadhi ya mabasi nikabaini kuwa baadhi ya abiria wanalipishwa nauli tofauti na bei elekezi ya serikali,” alisema.

Pia alisema amebaini kuwapo kwa madalali wanaochangia kupanda kwa nauli wakati huu wa sikukuu.

Kamwelwe alisema kuna haja ya kupekeka mapendekezo bungeni ili kuwe na tiketi za kieletroniki zitakazosaidia kuondokana na ulanguzi unaoumiza abiria.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima, aliwataka abiria kutoa taarifa pindi wanapokuta nauli zimepandishwa ili wamiliki wa mabasi wachukuliwe hatua.

Pia alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi ya kufanya ukaguzi wa mabasi kabla ya kutoka kituoni hapo kwa ajili ya usalama wa abiria.
 
Meneja wa Kituo cha Ubungo, Imani Kasagala, alisema mabasi yote yanapaswa kuingia ndani ya kituo hicho badala ya wamiliki kupaki nje na kutafuta madalali ambao ndio chanzo cha nauli hizo kupanda.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )