Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 27, 2018

Waziri Mkuu Atoa Maagizo Kwa Wakandarasi Majengo ya Serikali Dodoma

adv1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza makandarasi wanaosimamia majengo ya Serikali kufanya kazi usiku na mchana ili kwenda na kasi ya muda uliowekwa.

Amesema ni lazima wafanye kazi kwa kasi kwa sababu Rais John Magufuli hataki visingizio.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 27, 2018 alipotembelea jengo la Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) ambalo limeanza kujengwa mkoani humo.

Wizara ya Utumishi na Utawala Bora ambalo ndilo jengo pekee lililoanza kunyanyuliwa kati ya wizara zote.

"Visingizio havitakiwi tunataka watumishi kuhamia hapa katika muda tuliopanga ndiyo maana naagiza mfanye kazi usiku na mchana," amesema Majaliwa.

Kaimu meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),  Herman Tanguye amesema muda waliopewa unatosha kwa maelezo kuwa hadi sasa wapo mbele kwa mujibu wa mpango kazi wa Serikali.

Tanguye amesema ratiba inaonyesha leo walipaswa kuwa kwenye jamvi lakini wao wameshanyanyua ukuta.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )