Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 14, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 188 na 189 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Akaingia msichana mrefu, mweupe amevalia gauni jeusi lenye mpasuo mkubwa hadi karibi kabisa na kiuno chake, paja lote la mguu wa kulia lipo wazi. Nywele zake ni ndefu zinaning’inia mgongoni mwake na baadhi zimeficha jicho lake la kushoto kidogo. Umbo lake ni namba nane yenyewe, kwani ana hispi ambazo kusema kweli zinanitamanisha.
“Dany huyu anaiwa Magreti, ndio utakuwa naye kwenye kazi unayo kwenda kuifanya ya kumkamata Osama Bin Laden”
‘Mmmmm kweli lazi itafanyika hapa?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama binti huyu aliye jaribu kunipa mkono wake wa kulia ila nikabaki nikimazama kwani ni mzuri kupindukia hata Livna mwenyewe hamfikii msicha huyu hata nusu yake.
   
ENDELEA
“Dany si unapewa mkono?”
Livna alizungumza huku akinigonga kidogo kwenye bega kangu an kujukuta nitoka kwenye dibwi la mawazo la kumfikiria msichana huyu.
 
“Ndio habari yako”   
Nilizungumza huku nikimabidhi mkono msichana huyu, akatabasamu na kunifanya nizidi kujawa na bumbuwazi  kwani kwenye maisha yangu sijawahi kukutana na msichana mzuri kama huyu, japo nilio wahi kukutana nao ni waziru ila huyu amewazidi wezake kwa asilimi zote mia moja.
“Salama”
Nikashindwa hata kuijibu salamu yake kwani msisimko ninao upata hapa ukaanza kumuamsha jogoo wangu taratibu. Nikameza funda zito la mate kisha nikauachia mkono wa huyu msichana.
“Bado Osama yupo Tanzania?”
Niliuliza ili kuipoteza hali ya uchu wa mapenzi nilio nao juu ya huyu msichana ambaye kusema kweli ni kibarua kikubwa cha kupambana na hisia zangu.
 
“Bado hajaondoka Tanzania na leo usiku kutakuwa na sherea ya mtoto wa shemeji yake anaoa. Na harusi hiyo ndio iliyo mfanya kubaki nchini Tanania”
“Amejiingiza machinjioni”
”Hatari moja ni kwamba katika hiyo ulinzi ni mkali sana, ukiachilia mbali tu watu wake basi kuna NSS ya Taania na wana FBI kutoka Marekani”
“Wote wanafanya nini?”
Niliuliza huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.
“Wanamlinda Osama, sasa itakuwa ni ngumu sana kuweza kumteka katika hiyo harusi”
 
Ester aliendelea kunipatia maelekezo huku akinitazama usoni mwangu.
“Na hapo Dany humuwezi kutumia bunduki ni lazima itakuwa ni hatari kwenu”
Livna naye alisisitizia katika hilo.
“Ila kuna njia ambayo munaweza kuitumia”
Logate alizungumza huku akinikabidhi simu aina ya iphone 7.
“Kupitia hiyo simu tutakusaidia kukutumia video za kamera zote ambazo zipo ndani ya huo ukumbi. Mbili kuna hivi viji layer vya macho ya bandia, unatakiwa kuyavaa, ili hata kukitoke kukafanyika ukaguzi  wa macho basi hakuna anaye weza kukugundua kwamba wewe ndio Dany”
Logate alizungumza huku akitoa viji leyer vya macho na kunivisha katika macho yangu. Akanikabidhi kioo, macho yangu yangu yamebadilika mboni yake na kuwa mboni ya kijani kwa mbali jambo lililo zidi kunipendezesha.
“Ingia upande wa wa picha katika hiyo simu”
Logate alinipatia maelekezo na nikafanya hivyo.
“Jicho lako la upande wa kushoto utaweza kuona jinsi muonekano wa watu kwa ndani, it’s mean unaweza kutuona sote hapa nguo zetu za ndani”
“Kweli bwana”
Nikata kumgeuzia Logate simu hii ila Livna akaniwahi.
“Hembu acha utoto Dady, sikiliza maelekezo”
“Unataka nikuone wewe tu ehee?”
“Ndio”
“Sawa mama, mwalimu wangu ehee endelea”
“Lengo la kuweza kuitumia program hiyo ni nini haswa, ni kuhakikisha kwamba unaweza kumuona kila mlinzi mwenye silaha ndani ya ukumbi mzima, pili utaweza kuiona sura ya Osama vizuri kwani kuna watu watakuwa wamejifunga vilemba usoni mwao na kubakisha macho ilimradi kutoweza kumtambua Osama ni yupi”
 
“Sawa sawa”
“Magreti si unanielewa vizuri?”
“Ninakuelewa Logate”
“Na wewe Magreti simu yako hiyo hapo, na ina uwezo kama huu wa Dany hapo. Na wewe itakulazimu kuvaa hivi viji leyers vya macho kwa maana kupitia macho yako nawe rekodi zako wakizidaka basi utatiliwa mashaka. Hapa tumewatengenezea vitambulisho vya uraiAi nchini , ambavyo kwa Dady utatumia jina la Mpoki Samweli na Magreti utatumia jina la Nagenjwa Petro”
“Wewe Logate majina ya wapi haya jamani?”
Niliuliza huku nikitazama kitambulisho changu.
“Wewe ni Muhaya na Magreti weweni Mpare sawa?”
“Sawa ila hili jina la Mpoki ahaaa sio haki jamani”
“Dany be serious”
 
Livna alizungumza huku akinikazia macho.
“Tuendelee, nina imani kwamba kila mmoja ana silaha zake, ila katika ukumbi ambao mutaingia nilazima gari zetu zitakaguliwa, sio kukaguliwa kwa kutazamwa kwa macho. Ila computer ndio itakuwa na kazi ya kukagua gari lenu. Sasa kuna gari aina Aud A7, ambayo ipo huko  chini ya meli, mutaondoka nayo sasa hivi”
“Usiniambie kwamba ina uwezo wa kutembea juu ya maji?”
“Hapana, munaondoka na boti kubwa, mutapelekwa hadi katika fukwe za Kigamboni, kisha mutapita katika daraja na kuitokea katikati ya jiji. Sasa maana yangu ni kwamba mutaacha silaha zenu ndani ya gari, mukiwa munaingia ukumbini, na hakuna program yoyote ya kukagulia magari itakayo weza kuona silaha zenu, japo itawaonyesha nyinyi katika mfumo wa mafuvu ya watu pale munapo kaguliwa”
“Kwa hiyo watauona nguo za ndani?”
“Hapana, watawaona nyinyi katika mfumo wa mafumfu tu kwa ndani”
 
“Sisi nasi tutajiona?”
“Hapana, mtaalamu atakaye kaa kwenye computer hiyo ndii atakaye weza kuona kila kitu, si nyinyi tu bali wageni wote watakao ingia kwa miguu, magari wataonekana hivyo”
“Hapo nimekupata”
“Kuna hii kadi, hapa. Ukiitazama unaweza kusema kwamba ni kadi ya benki, ila hii ndio kadi ya harusi sasa. Ukifika mlangoni utawakabidhi hii kadi wakaguzi nao wataweza kuipitisha kwenye mashine ya ukaguzi na majina yenu yataokea. Kumbuka kwamba Dany unaitwa Mpoki Samweli na Mage”
“Nagwenjwa”
Magreti alimuwahi kumjibu Logate na kunifanya nimtazame kisha nikatabasamu.
“Picha zenu zitatokea katika kadi hiyo”
“Picha mulinipiga saa ngapi?”
“Sasa hivi ulivyo simama hapo”
Nikamtazama Ester nikamuona akininyooshea dole gumba ikionyesha kwamba yeye ndio aliye nipiga picha anayo izungumzia Logate.
“Kuna hivi vinasa sauti kila mmoja avae kwenye sikio lake, mutaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja”
“Nimevimisije hivi vidumwana, nakumbuka nilivivaa kipindi nilipokuwa nina oparesheni ya kuliangamizi kundi la Al-Shabab”
“Dany mbona unaongea sana leo, unafuraha. Hembu tilia maanani kwa kazi unayokwenda kuifanya basi”
Livna alizungumza kwa kulalamika kidogo, nikamkonyeza huku nikitabasamu na kumfanya akenue midomo yake akionyesha kupuuzia mkonyezo wangu.
“Kuna hii sindano ndogo, Magreti unaweza kuficha kwenye nywele zako, hiyo sindano utamchoma nayo Osama na italewesha, na atakusikiliza kila utakacho muambia. Hakikisha kwamba unautumia uzuri wako kumteka mzee huyo”
 
“Sawa”
Magreti akapokea kisindano kidoho na kichomeka katika nywele zake na si rahisi kwa mtu kuweza kufahamu kwamba ana sindano ndogo.
“Baada ya hapo nina imani kwamba kila kitu kitakuwa kimekamilika kwa upande wenu. Sisi kazi yetu itakuwa ni kuwapa maelekezo kuhakikisha kwamba munakwenda salama na kurudi salama kama tulivyo kubaliana”
“Tunashukuru”
“Ninawatakia kazi njema”
“Asante Ester”
“Twende tukawaonyeshe gari mutakayo tumia”
Ester alizungumza, tukatoka katika chumba hichi huku Livna akitufwata.
“Dany mpenzi wangu ninakuomba uwe serious katika hii kazi, kumbuka tayari umesha pandikiza kitu kwangu, sinto kubali kukuona unaingia kwenye matatizo”
 
“Mungu nisaidie, nitakuwa serious nitahakikisha kwamba ninarudi salama sawa”
“Sawa mpenzi wangu mimi ninakuombea kwa Mungu. Magreti hakikisha kwamba unamlinda huyu”
“Sawa mkuu”
Tukafika katika sehemu maalumu ambayo boti maalumu huwa ndipi zinapo tokea, tukakuta boti moja ikiwa tayari imesha andaliwa huku kukiwa na gari nzuri yenye rangi nyekundu.
“Dany hembu shika kioo cha upande wa dereva”
Nikauweka mkono wangu. Logate akaanza kuminya minya tablate yake kubwa, mlango ukafunguka.
“Utaweza kuifungua hiyo gari kwa mkono wako wa kulia. Mage na wewe weka mkono wako kwenye mlango upande wa dereva. Dady wewe funga mlango”
 
Nikaufunga mlango, kusema kweli dunia inazidi kukua na tecknologia inazidi kuchukua nafasi kwenye maisha ya watu.
“Tayari, sasa nyinyi kupitia mikono yetu ya kulia munaweza kufungua mlango wa hilo gari, hakuna mtu mwengine atakaye weza kufungua. Gari unawasha kwa hiyo batani iliyo andikwa start engine. Itawaka na utaweza kuendesha”
“Halina funguo?”
“Hakuna funguo. Ingieni ndani ya gari”
Tukaingia ndani ya gari huku nikikaa upande wa dereva.
“Angalizo, ambaye hatofunga mkanda wa siti aliyo kalia awe dereva ama abiria wa siti ya mbele wala nyuma, gari haliwaki sasa muwe waangalifu katika hilo”
“Mmmmmm kazi kweli kweli”
“Yaa ndio magari ya kisasa. Kitu kingine, hii gari haiingii sirasi, pia ina uwezo wa kubadilisha mfumo wa rangi yake ya nje, hapo kuna rangi tatu. Hii nyekundu, nyeupe na  nyeusi. Kila rangi ina namba zake za usajili sasa inaweza kuwa rahisi kwenu kubadilisha muonekano wa gari lenu pale endapo kutakuwa na hatari itakayo wafanya mufanye hivyo.”
“Tunabadilishia wapi hiyo rangi?”
 
“Mimi ninafahamu”
“Magreti anafahamu, so vitu vya ndani ya gari atakuelekeza kama wewe ndio utakuwa dereva?”
“Mfuno wake ni manuel au automatics?”
“Ina mifumo yote miwili chaguo ni lako wewe mwenyewe”
“Ohoooo sawa sawa”
“Kwa mimi nimemaliza, nami nitawakie safari njema”
“Tunashukuru”
Livna akainama kwenye dirisha langu, akanitazama kwa muda huku akitabasamu kinyonge.
“Dany fanya hii kazi ila kumbuka kwamba huku nyuma umeacha watu wawili wenye viumbe vyako, watatu ni Yemi ambaye amekwenda kuchukuliwa, hakikisha kwamab hii kazi unaifanya kiumakini mpenzi wangu sawa”
 
“Usijali mama”
“Mungu awatangulie”
Livna bila kujali wasichana wake hawa wawili waliopo katika hili eneo, akaninyonya midomo yangu taratibu huku akinitazama usoni mwangu kwa macho malagevu.
“Mage, mlinde huyu”
“Sawa mkuu, atarudi salama”
“Jamani kushuka je, kuna haja ya kuweka mkono kwenye kioo?”
“Hapana, unafungua mlango kama kawaida”
“Ahaaaa hapo sawa”
Livna na Logate wakatoka katika boti hii ambayo ni kubwa kiasi yenye uwezo wa kubeba gari hili la kifahari ikaanza safari huku ikiendeshwa na msichana mmoja.
“Tutachukua masaa mangapi kufika Tanzania?”
“Masaa kama manne au matano”
“Duu kumbe kuna umbali ehee?”
“Ndio”
Nikabaki kumtazama Magreti kwa macho ya matamanio. Hakulijali hilo, kwani anatambua kwamba mimi ni mume wa bosi wake. Ili hali ya matamanio isiendelee humu ndani, nikafungua mlango na kutoka, nikaanza kutazama mandhari ya hii bahari kwani tangu siku nifike hapa sijawahi kutoka kabisa. Magreti naye baada ya muda kidogo akashuka kwenye gari na kunifwata sehemu nilipo simama.
“Kwa mavazi yako utaweza kupambana kweli?”
“Yaa tena yananipa uhuru mzuri sana wa kufanya chochote ninacho jisikia”
“Upo vizuri”
“Kwenye nini?”
Nikatamani kumsifia ila ninashindwa kwani mazungumzo yetu yote Livna na watu wake wanayasikia.
“Kupambana na nguo hizo”
“Kawaida, ukiwa unaifanya hii kazi inabidi uwe unaweza kupamba kwa kila vazi, liwe ni shele, suruali, baibui. Chochote unatakiwa kuweza kupambana”
“Kweli, nina imani kwamba mke wangu amenichagulia mtu sahihi”
“Hajakosea kabisa.”
Meli ikazidi kusonga mbele, huku tukipata kifungua kinywa. Baada ya masaa kadhaa tukafanikiwa kufika katika fukwe za mji wa Kigamboni. Tukaagana na msichana alite tulete kisha tukaingia kwenye gari hili, nikafwata maelekezo kama jinsi  alivyo nieleza Logate, nikawasha gari hili. Taratibu nikaanza kulitoa ndani ya boti hii, nikaanza kuondoka taratibu kwenye eneo hili, japo kuna mchanga mwigi wa bahari ila gari hii haititii chini wala kuyumbishwa na mchanga huu. Tukafanikwia kuingia barabarani na kuianza safari ya kuelekea katikati ya jiji.
Tukafanikiwa kufika darajani na kukuta mlolongo mrefu wa magari yanayo elekea Dar es Salaam. Ikatulazimu na sisi kupanga foleni. Tataratibu gari ikaanza kusogea mbele hadi tukafika katika sehemu ya ukaguzi, mwanajeshi mmoja akaniomba nishushe kioo cha gari langu, nikafanya hivi, akachungulia ndani na kututazama.
 
“Habari yako kiongozi”
Nilimsalimia mara baada ya kutuona anatutazama sana, hakunijibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kunikazia macho mimi na Magreti jambo lililo anza kunipa mashaka, akaiwasha simu yake ya upepo iliyo anza kukoroma kwa sauti ya juu. Kwa kupitia kioo changu cha pembeni nikaanza kuona wanajeshi wengine wawili wakilisogela gari letu huku wakiwa wamezishika bunduki  kwa  umakini wakionekana wakiwa na mashaka nasi jambo lililo nifanya nianze kuupeleka mkono wangu katika sehemu nilipo ichomeka bastola yangu kujiandaa na lolote litakalo jitokeza mbele yetu.
 
AISIIIII……….U KILL ME 189
   
Magret taratibu akanishika mkono wangu na kwa ishara ya macho akaniomba nisifanye kitu chochote.
“Tunaomba vitambulisho vyenu”
Mwanajeshi huyu alizungumza, taratibu nikachia tabasamu. Nikaingiza mkono wangu mfukoni na kutoa kitambulisbo changu. Magreti naye akanipatia kitambulisho chake na kwapamoja nikamkabidhi huyu mwanajeshi. Wanajeshi wawili waliokuwa wanakuja nyuma yetu wakachungulia chungulia ndani ya gari.
“Habari zenu”
“Salama tu, munaelekea wapi?”
“Posta hapo”
“Ohooo, aisee dada Mungu amekujalia. Kama ni manzi wako kusema kweli umepata mwanamke”
“Shukrani kiongozi”
“Munaweza kwenda”
Askari tuliye mpatia vitambulisho vyetu alizungumza huku akinirudishia. Taratibu nikafunga kioo cha upande wangu na kuondoka eneo hili.
 
“Huwa una maamuzi ya haraka eheehee”
“Yaa nilidhani wanahitaji kutuzingua”
“Siku  nyingine usijaribu kufanya hivyo. Inaweza kuharibi mipango yote tuliyo nayo”
“Sawa bosi, au uliwapagawisha kwa uzuri wako”
“Shauri yao ila kikubwa ni kufanya kazi iliyo tuleta huku”
“Poa, sasa harusi si inafanyika usiku na muda huu, tutafanyaje?”
“Tutafute hoteli ambayo tunaweza kupumzika”
“Mimi sina pesa yoyote”
“Usijali”
“Unazo wewe?”
“Wewe twende”
“Sawa.”
Tukafika katika hoteli moja ya kitalii, iliyopo maeneo ya hapa Posta.
“Silaha zetu tunatakiwa kuziacha ndani ya gari tukifika kwenye hiyo hoteli unayo kwenda”
Magreti alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Poa poa”
Nikasimamisha gari sehemu ya maegesho na kushuka. Nikajiweka vizuri koti langu la suti na kuanza kutembea kuelekea ndani, Magreti taratibu akaingiza mkono wake wa kulia katikati ya nafasi iliyo achwa na mkono wangu wa kushoto, nikamtazama kwa macho ya mshangao.
“Tunatakiwa kutembea kama mume na mke”
“Una uhakika?”
“Ndio upo huru kwangu kwa muda huu”
“Weeeee”
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na tabasamu. Kila tunapo pita watu hawakusita kututazama hususani Magret kwani anavutia kwa kila macho ya kila mwanaume. Tukachagua sehemu iliyo tulia na iliyo jificha kidogo, tukakaa huku sote macho yetu yakiwa na kazi ya kutazama tazama eneo hili kwa umakini.
 
“Habari zenu”
Dada mmoja muhudumu alizungumza huku amesimama pembeni yetu kwa heshima kubwa sana.
“Salama tu dada, tunaomba menu ya chakula”
“Sawa”
Dada huyu akaondoka, baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameshika vitabu viliwi. Akatukabidhi kila mtu cha kwake, nikaanza kutazama orodha ya vyakula hivi, vilivyo orodheshwa na bei zake.
“Niletee chipsi na miskaki na juisi ya embe”
“Na mimi niletee hicho alicho kiagiza mume wangu”
“Sawa karibuni”
Dada huyu akaondoka.
“Unapenda sana nionekane kama kama mume wako”
“Ni kama, na hii nikazi na ninacho kizungumza sikimaanishi”
“Sawa mwaya”
“Ila umependeza na wewe, ninaona wadada wakikushangaa shangaa”
Tukaendelea kuzungumza mambo mengi hadi chakula kikaletwa pamoja na vinywaji. Tukaanza kula tartaibu huku kkwa mara kadhaa nikiwa na kazi ya kumtazama Magret usoni mwake.
 
“Hivi tunakula tutalipa na nini?”
“Mbona una wasiwasi, tukishindwa kulipa si tutaosha vyombo vya hii hoteli”
“Hahahaaa wewe acha masihara”
“Eheee tunaosha, tunasogeza sogeza muda mbele”
“Oya kama huna pesa seme nianze kufikiria njia ya kuondoka hapa”
“Usiwe na wasiwasi”
Magreti alizungumza huku akifungua kipochi yake kidogo, akanionyesha jinsi noti za dola mia mia zikiwa zimejipanga vizuri kwenye hii pochi.
“Tuna uwezo wa kula chochote na kunywa chochote”
“Daaa hapo nina amani, inabidi tule kwa maana kazi tunayo kwenda kuifanya ni kubwa sana”
“Ukila ukishiba utashindwa kufanya kazi, kula wastani”
Kusema kweli Magreti ni mchangamfu sana na endapo anatokea mtu ambeye hatufahamu katika huu moango anaweza kusema kwamba sisi ni wapenzi wa muda mrefu sana.
“Unajua katika haya mahusiano yetu feki kilicho kosekana ni pete. Hapa hata tukimuambia mtu sisi ni mke na mume inaweza kula kwetu, atakapo hiji kuhusiana na pete”
Magreti alizungumza alizungumza huku akinitazama kwa macho malegevu kiasi, japo tupo kazini ila kuna kitu ambacho tayari nimesha kihisi kwa Magreti, ninaimani kwamba kuna chembechembe za hisia za penzi langu vimeingia moyoni mwake. Nikaitazama saa yangu ya mkononi mwa sekunde kadhaa.
“Hivi sasa ni saa kumi kasoro, tunaweza kutafuta pete za kofoji”
“Sawa”
Magreti akamuita muhudumu aliye tuhudumia.
“Dada naomba bili”
“Sawa”
Dada huyu akaondoka na kurudi akiwa na kijitabu kidogo akamuwekea Magreti pembeni yake. Akakifunua na kutoa kararasi ndogo.
“Elfu thelathini na mbili eheee?”
“Ndio”
Magreti akafungua pochi yake na kutoa noti ya dola mia.
“Si ninaweza kulipa hata kwa dola?”
“Ndio dada unaweza kulipia”
Magreti akaiweka noti hiyo kwenye kijitabu hichi tulicho letewa.
“Chechi itakayo baki chukua mdogo wangu”
“Asante sana dada yangu”
Binti huyu  aliondoka huku akiwa amejawa na tabasamu pana. Tukasimama na kutoka nje huku tukiwa tumeshikana mikono.
 
“Unajua umemuachia pesa nyingi sana”
“Ahahaa hembu acha ubaili kama mpare bwana”
“Ohoo pesa ni nyingi ile”
“Muache bwana”
“Hembu nipe kiasi kidogo cha pesa, maswala ya wewe kutoa pesa ninaonekana mimi ni boya bwana”
Magreti akaanza kucheka hadi tunaingia ndani ya gari bado anacheka.
“Wewe mwanaume sijui mwanamke utakaye muoa atapataje tabu”
Magreti alizungumza huku akifungua kipichi chake akachomoa noti kumi za dola mia mia na kunikabidhi, nikazikunja vizuri na kuziweka kwenye mfuko wa suti.
“Hapo sawa, ngoja tumtafute sonara kwanza”
“Hakia ya Mungu, Dany unanipa raha una vituko hadi basi”
Tukafika katika duka moja kubwa la sonara, tukashuka kwenye gari na kuingia ndani. Tukachagua ni pete gani ambazo tunahitaji kuchongeshewa kisha nikafanya malipo na kila pete moja ina thamani ya milioni moja na nusu na ikamlazimu Magreti kuongeza kiasi cha pesa kwani alichonipatia kimekwisha.
 
“Ndugu zitachukua muda gani?”
“Nusu saa muheshimiwa”
“Sawa, fanyeni fanyeni kwa maana tuna haraka”
Simu yangu ikata nikaitoa mfukoni na kukuta namba isiyo na jina, nikamuonyesha Magreti kwa sauti ya chini akaniambia kwamba ni Livna. Nikaipokea na kuiweka sikioni
“Mume wangu?”
“Niambie”
“Munaendeleaje?”
“Tunaendelea vizuri tu, vipi”
“Nimekumiss tu ndio maana nikakupigia”
“Kwani husikii tunacho kizungumza?”
“Mimi sipo chumba cha mawasiliano, kidogo ninajisikia sikia joto mwilini. Nipo chumbani nimepumzila”
“Umepata sawa?”
“Yaa dokta ndio amenitazama muda huu, ameniambia ni mabadiliko ya hali ya hewa”
 
“Pole mama”
“Nashukuru. Ninakuomba uwe makini”
“Usijaki nitakuwa makini sana”
“Ninakupenda Dany wangu”
Nikawatazama waty walipo karibu nasi ambao nao wamekaa kwenye viti wakisubiri huduma zao.
“Na mimi pia”
Nikakata simu na kuirudisha hewani.
“Mr na Mrs Mpoki ninawaomba munifwate”
Dada mmoja wa kiarabu alizungumza, tukaingia kwenye moja ya chumba na kukutana na muarabu mmoja menene akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa cha kuzunguka.
“Habari zenu”
“Salama tu”
“Pete zenu zipo tayari, nina imani kwamba zitawapendeza”
Muhindi huyu alizungumza huku akitukabidhi pete zetu za dhahabu na zimechonga vile tulivyo hitaji. Nikaichukua pete ya Magreti, nikamtazama muhindi huyu, kisha nikauchukua mkono wa kushoto wa Magretu na nikamvisha  pete hii kwenye kidole husika cha pete ya ndoa.
“Mulikuwa bado hamjavishana pete?”
“Hapana, pete zetu za ndoa, kuna sehemu kidogo tuliziacha”
“Ahaaaa, ila mumependezana. Dada na wewe mvishe mwenzio”
Magreti kwa tabasamu pana, akaichukau pete yangu ambayo nilipanga kujivisha mimi mwenyewe, akanivisha kidole changu cha pete. Taratibu nikamsogelea na kumbusu mdomoni jambo lililo nifanya nipate msisimko mkali sana. Magreti hakuonekana kuchukizwa na lolote zaidi ya kufurahi kwa kile nilicho kifanya kwake.
“Tunashukuru ndugu”
“Karibuni sana”
Tukatoka katika ofisi hii na kuridi ndani ya gari letu. Magreti akanitazama kwa macho ya matamanio, taratibu nikamshika mkono wake wa kulia, nikamsogeza kichwa chake karibu yangu, tukatazama kwa sekunde kadhaa huku nikizilamba lamba lipsi zangu tararibu. Nikausogeza mdomo wangu hadi sehemu ulipo mdomo wake.
“Mmmmmm”
Magreti alizungumza huku  akikaa sawa kwenye siti yake akafunga mkanda wa siti.
“Tuondoke, tuna kazi ya kufanya”
Safari ya kuelekea ukumbini ikaanza huku  nikihakikisha kwamba ninafuta mawazo yote ya kijinga ninayo muwazia Magreti na ninahitaji kukakikisha kwamba ninawaza kazi iliyopo nbele yetu. Kutokana na foleni kubwa ya barabarani. Tukafika ukumbi muda husika,, gari letu likakaguliwa mlangoni kisha tukaruhusiwa kuingia ndani.
 
“Tupo kazini sasa, tuwe makini, kila kilicho tokea muda ulio pita tupotezee, hakikisha kwamba unajilengesha kwa Osama Bin Laden ninahitaji akiwa hai”
“Nimekuelewa”
“Sawa”
Sote tukashuka kwenye gari huku kadi ya mualiko nikiwa nayo mimi. Nikamshika kiuono Magrerti hadi mlangoni. Walinzi kusema kweli wapo wengi sana katika huu ukumbi huu, nikatoa kadi hii na kumkabidbi jamaa ambaye ndio mkabidi, akaipitisha katika mashine ya ugaguzi na macho yake akayatupia kwenye computer iliyopo pembeni yake. Akanirudishia kadi yangu huku akiwa ametabasamu.
“Karibuni sana”
“Shukrani ndugu”
Tukaingia ndani humu ambapo kumejaa watu wengi sana wakiwa na wamependeza sana.
“Hakikisha kwamba hugusi sikio lako sawa”
Magreti alizungumza kwa sauti ya kunining’oneza.
“Usijali katika hilo ninaelewa kila kitu”
Tukatafuta viti ambavyo tunaweza kuliona jukwaa vizuri na tukaa.
“Mungu wangu tunamuonaje hapa”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikiwa nimesogelea karibu sana Magreti.
“Tutamuona, Logate unatusikia?”
“Ndio ninawaiskia tangu mulipo ondoka hapa”
“Basi tunakuomba utusaidie katika hili”
“Nipo kwa ajili yenu”
Sherehe ikaanza huku tukiendelea kuwatazama watu waliomo humu ndani. Wakaingia watu wapatao nane wakiwa wamevalia kanzu na wamejifunika nyuso zao na kubakisha macho tu
‘Osama ameingia ukumbini’
Tuliisikia  sauti ya Logate akitupatia maelekezo.
“Ni yupi sasa kati ya hawa watu tisa?”
‘Tumieni simu zenu kifanyeni kama munapiga picha’
Tulaemdelea kutazama walinzi walipo katika eneo hili. Bibi harusi na bwana harusi walipo anza kuingia ukumbini hapa, watu wote wakanyanyuka huku  wenye simu zao wakijitahidi kuchukua video kwa kile kinacho endelea katika eneo hili. Na sisi tukatoa simu zetu mifukoni na kuanza kuchupiga picha maharusi hawa wanao ingia kwa mbembe kubwa za kucheza.
Nikaweka upande wa video na kuigeuza simu yangu sehemu alipo Osam Bin Laden na kundi lake, nikajikuta macho yakiwa yamenitoka kwani watu wote walio zifunika sura zao kwa vitambaa ni sura ya Osama Bin Laden.
“Mage umeona hichi kinacho tokea hapa?”
“Mbona wamefanana jamani?”
“Logate hii inakuwaje?”
“Hata sisi tunashangaa huku hatujui Osama ni nani kati yao kwa maana wote wanafanana”
Hatukujua ni nini cha kufanya hadi watu wote tulipo ruhusiwa na muongoza sherehe(MC) tukae kwenye viti vyetu.
 
 ITAENDELEA
‘Haya sasa DANY na MAGRETI hadi sasa wameshindwa kumtambua Osaman ni nani kati ya watu walio ingia kwenye ukumbi huo. Ni nini watakacho kifanya? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
ad
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )