Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, January 19, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 196 na 197 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA     
  
Swali la Jojo likanifanya niyanyanyue macho yangu taratibu hadi kwenye kioo kidogo kilichopo mbele yangu na kumtazama Magreti kwa nyuma.
“Unaogopa kujibu kisa Magreti, usimfiche bwana. Magreti mimi baba yangu ni malaya, sasa kama unampenda jiandae kuumia tu”
Nikajikuta nikikausha kimya, hata kufungua kinywa changu ninashindwa.
“Yaani kama baba angekupata leo, wewe ungekuwa msichana wa mia moja”
“Mungu wangu”
Magreti alizungumza huku akinitazama vizuri kwa kunichukungulia usoni.
“Hivi Dany huna ukimwi kweli wewe?”
Swali la Magreti likazidi kuninyong’onyeza kiasi kwamba nikashindwa kujibu chochote na kuendelea kukaa kimya

ENDELEA   
“Huwezi kuamini nikikuambia baba yangu hana Ukimwi kabisa, japo amekuwa na wanawake wengi sana”
“Mmmmm”
 
“Kweli vile hata ukisema umpime hapo sasa hivi hana, japo alitembea na wanawake ambao wana maambukizi ya magonjwa hayo”
“Munanitania nyinyi”   
“Kweli vile, damu ya baba yangu ni toafuti sana na damu za watu wenginene, haipokei maradhi kabisa”
“Mmmmmmm”
“Hembu hizo mada zife”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kuwafanya Magret na Jojo kutabasamu. Tukasimamishwa kwenye moja ya kwenye moja ya kituo cha ukaguzi. Nikataka kutoa bastola yangu ila Jojo akatingisha kichwa.
“Musiogope najua nini cha kufanya”
Tukatulia tu kwenye siti zetu, Jojo akafungua kioo chake.
“Habari yako binti”
Askari huyu alizungumza huku akimtazama Jojo.
“Salama tu kaka, shikamoo”
“Marahaba, una umri  gani binti?”
“Miaka ishirini”
“Ninaomba leseni yako”
Jojo akatoa leseni yake, askari huyu akaitazama kwa muda, kisha akamrudishia Jojo.
“Unaelekea wapi?”
“Ninakwenda Dar”
“Kuwa makini barabarani, kwa maana kwa msichana mdogo kama wewe kuendesha masafa marefu ni hatari kidogo”
“Sawa kaka afande nitajitahidi kuwa makini”
“Sawa binti, je ninaweza kuipata namba yako ya simu”
“Hahahaa hapana”
 
“Basi chukua ya kwangu ili hata huko mbele usisumbuliwe sumbuliwe na askari wengine”
“Mmmmm sawa naomba uniandikie kwenye karatasi”
“Huna simu nikaiandika namba yangu haraka haraka”
Polisi huyu alizungumza huku akitazama tazama humu ndani ya gari kitu nilicho kigundua kwa uharaka ni kwamba askari huyu hajagundua uwepo wetu ndani ya hili gari. Jojo akampatia askari huyu simu yake, askari huyu akaiandika kwa haraka huku akitazama wezake kama wanao tukio hili kishaa kamrudishia Jojo.
“Niaitwa afande Mweta, utanipigia mtoto mzuri”
“Asante Afande Mweta”
 
“Karibu sana, wewe wakikusimamisha tu nipigie”
“Sawa afanye”
“Una pesa ya mafuta?”
“Mmmm ninayo”
“Ok nilijua huna nikupatie japo kidogo mtoto mzuri”
“Unaweza kunipatia?”
Askari huyu akarudi kutazama tazama wezake kisha akafungua mfuko wake wa shati na kutoa dola mia na kumpatia Jojo.
“Hiyo utabadilisha, mtoto mzuri, hakikisha unanipigia basi sawa Jojo”
“Sawa afande”
“Safari njema mrembo”
Afande Mweta alizungumza huku meno yote thelathini yakionekana. Jojo akafunga kioo cha gari na tukaondoka eneo hili.
“Hivi unataka kusema kwamba huyo afande hajatuona?”
Nilimuuliza Jojo huku nikimtazama usoni mwake.
“Nimewapoteza ndio maana akawa anajishebedua”
“Yaani wanaume nyinyi, utakuta yule mbaba ana mke na watoto, ila kamuona Jojo hapa kashoboka laiti ungemuonyeshea kama ulivyo nionyeshea mimi vituko ninahisi angekufa kwa presha”
 
“Weee sio kufa tu angeacha hata hiyo kazi yenyewe”
“Hahaaa”
Nilijikuta nikicheka tu, huku nikimtazama Jojo na Magret ambao tayari wamesha onekana kuzoeana. Tukafika jijini Dar es Salaam majira ya usiku, hatakuona haja ya kusimama sehemu yoyote na tukaelekea Kigamboni kwenye fukwe ambayo ndipo yalipo maficho yetu, tukakuta boti ikitusubiria huku wasichna wawili wa Livna ndio wanao linda hili eneo.
Safari ikaanza huku wasichana hawa wawili wakimtazama Jojo, simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kukuta Livna akinipigia, nikamtazama Jojo kisha nikaosogea pembeni na kuipokea.
 
“Niambie”
“Huyo aliye ongezeka ni nani?”
“Tutakuja kuzungumza?
“Dady usijiokotee okotee watu tu ukawaleta huku ikiwezekana muue”
“Livna nimekuambia kwamba tutakuja kuzungumza nikifika, mimi sio kichaa wakusema sielewi kile kitu ninacho kifanya, wewe tulio utajua kila kitu nikifika”
Livna akaka kimya kwa sekunde kadhaa akionekana kujifikiria.
 
“Dany kumbuka kwamba haya ni maficho muhimu sana, huyo msichana utamuamini vipi au umemjulia wapi?”
“Livna hivi hunielewi ninavyokuambia  kwamba nitakuamia kila kitu nikifika huko au huniamini?”
Ilinibidi kuzungumza kwa ukali kidogo ili kusisitizia msimamo wangu kwa Livna ambaye tayari nimesha ziteka hisia zake za mapenzi.
“Ninakuamini”
“Sasa maswali mengi ya nini, unahisi kwamba mimi ni mjinga niokote okote watu?
“Naomba unisamehe mpenzi wangu”
“Poa”
 
Nikakata simu, Jojo akanisogelea huku akinitazama usoni mwangu.
“Kumbe baba yangu na wewe unakoromea watu”
“Kwa nini?”
“Ninaona jinsi unavyo mkoromea Livna hapo kisa mimi?”
“Usujali mwangu ni mambo ya kawaida tu”
“Ila kama hawato nihitaji tunaondoka kwenye meli yao kwa manaa siwezi kuishi mbali na wewe baba yangu, nilikusubiria kwa muda mrefu japo nilifahamu ni  sehemu gani upo ila nilishindwa kukufwata”
“Kwa nini ulishindwa kunifwata?”
“Mama aliniambia kwamba nitakutana na wewe siku fulani, katika eneo fulani na katika hali fulani na ndivyo ilivyo tokea”
“Sawa”
 
“Ni kweli mama alikuwa na maana yake kwa maana ningekufwata kwa njia ya kawaida tu hivi na kukuambia kwamba mimi ni mwanao ungenikubali?”
“Ningealia na maelezo yako kisha ningekupima kwa maswali kadhaa kama usinge nijubu kama ninavyo hitaji ningekukataa”
“Ila kwa nini ulinikubali haraka?”
“Kwa sababu mama yako aliniambia kwamba mwanangu atakuja kunisaidia nikiwa na matatizo”
“Ahaaa sawa”
 
“Baba na mwana munazungumza nini?”
“Ahaaa stori za kawaida tu”
“Ila Dany umejitahidi kumpata Jojo ni mzuri sana”
“Hahaaaa, unajua ni nini Magreti”
“Eheee”
“Unaonaje kuaolewa na baba yangu?”
“Weee ongea taratibu nisije nikasikiwa nikauwawa bure”
“Nani akuue?”
“Huyo ni mume wa mkuu wangu Livna”
“Mmmmm mbona baba Livna amekupita umri, hembu mchukue Magreti anaendana na wee”
“Sasa nitamchukuaje ikiwa ana ujauzito wangu?”
“Mmmm hana mimba, kizazi chake hakina uwezo wa kushika ujauzito?”
 
“Acha kunitani?”
“Kweli kabisa baba yangu, yule mwanamke anakupotezea muda, na yeye anajijua kabisa kwamba hana uwezo wa kubeba ujauzito”
“Hayo makubwa, ila jamani zungumzeni taratibu hawa wapambe watatusikia?”
“Hapana hawatusikii, niwewaziba masikio yao na wakizungumza wao kwa wao wanasikiana”
“Hivi unawezaje kufanya hayo yote?”
“Hahaaaa, ninaweza ila tukienda nyumbani nitaweza kukufundisha”
“Sawa”
“Jamani na mimi ninataka kwenda, kusema kweli kwa siku hizi kadhaa nilizo kuwa nje ya ile meli nimefurahia sana maisha. Sikuwahi kukumbatiwa na mwanaume ila baba yako ameweza kufanya hivyo”
“Hahaa masikini weee kumba ndio umekumbatiwa leo?”
“Ndio”
 
“Mkumbatie sasa hivi?”
“Nyie hembu acheni ujinga”
“Hahaaa baba ujinga gani, unamridhisha kidogo tu”
“Hayo mambo yataendelea muda mwengine sio sasa”
Tukafanikiwa kufika katika meli salama Salim, tukamkuta Livna na Logate wakitusubiria katika eneo hili. Tukasalimana na wakamsalimia Jojo, tukaongozana moja kwa moja hadi katika chumba cha mapumziko na Magreti akaelekea katika chumba chake.
“Livna huyu anaitwa Jojo ni mwanangu”
Nilizungumza huku nikimtazama Livna usoni mwake, akaonekana kujawa na mshangao mkubwa sana bada ya kusikia kwamba jojo ni mwanangu.
 
“Lini Dany umekuwa na mtoto mkubwa kama Jojo sijui Jojo gani huko?”
Livna alizungumza kwa sauti iliyo jaa dharau kidogo, nikamtazama Jojo, nikamuona anavyo benua midomo yake naye akimtazama Livna.
“Mimi si mwanaume na lazima niwe na mtoto”
“Dany nimekukubalia Hawa azae hapa, nimekukubalia Yemi azalie hapa, leo hii unaniletea mtoto ambaye ni mkubwa kabisa anaye weza kujitafutia, yaani kusema kweli sipo tayari kabisa kumlea huyo mwanao, kumbuka kwamba mimi umesha nipa ujauzito na mimi”
Jojo akaachia msunyo mkali sana hadi Livna akamtolea macho ya hasira.
 
“Mwaharamu mkubwa wewe, unakazi ya kumuongopea hapa baba yangu kwamba una ujauzito, yaani huna chochote wala huna uwezo wa kubeba ujauzito. Umesahau miaka kumi nyuma kizazi chako kilifanywaje kule Urusi?”
Jojo alizungumza huku akiwa amemkazia macho Livna aliye nitazama kwa macho yaliyo jaa wasiwasi.
“Hivi unahisi hiyo roho yako mbaya unaweza kuibadilisha na kuwa nzuri, eheee?”
Jojo alizungumza kwa suati ya ukali na kumfanya Livna kutulia kwa muda kidogo huku macho yakiwa yamemtoka sana.
“Baba yangu alikuthamini sana na kukuamini ila sio hicho kitu ambacho unahitaji kukifanya kwa watu wake.”
 
“Ulipanga kumuwekea sumu, Yemi na Hawa, ili wafe na mimba zao na wewe ubaki na mimba hewa ni uongo?”
“Livna ni kweli anacho kizungumza Jojo?”
Livna akaka kimya huku macho yake akiwa ameyaelekezea chini.
“Unahisi unaweza kummiliki baba yangu, baba yangu moja ni mzuri, pili anajiweza na kujitambua. Kwa nini unataka kumrudisha nyuma ikiwa ninajua nina wadogo zangu wawili wanao kuja?”
“Livna nimekuiliza ni kweli?”
Nilizungumza kwa hasira huku nikipiga meza hii hadi Livna akastuka macho yakamtoka mwili mzima ukamtatetemeka. Waswahili wanasema kwamba ukimya nao pia ni jibu. Nikanyanyuka kwa haraka na nikamshika Livna mabega yake na kumnyanyua juu, nikamsogeza hadi ukutani huku nikiwa nimekasiria sana na macho yamenitoka.
 
“Kwa nini Livna unakuwa na roho za Kiswahili, kwa nini usingeniambia mapema kwamba nisiwalete hapa hao wasichana wa watu eheeee?”
Nilizidi kuzungumza kwa uchungu sana huku machozi ya hasira yakinimwagika usoni mwangu.
“Da……d….”
Livna alishindwa kabisa kuliita jina langu, kinywa chake kimejawa na uzito ambao hakuutarajia kuupata kwa muda huu.
 
“Unahitaji niondoke hili eneo si ndio?”
“Hapana Dany, ninakupenda, ninakuhitaji mume wangu”
“Unahitaji kwa upuuzi huo wa kuhitaji kuwaua wezako eheeee. Wamekukosea nini viumbe wa watu  ambao wapo matumboni mwa hao wasichana. Kumbuka zile ni damu zangu, ni damu zangu kama ilivyo kwa Jojo pale, bora nife mimi kuliko zife damu zangu kwa nini lakini Livna”
“Dany na mimi nina wivu, na mimi nina wasiwasi wa kuachwa na wewe ukigundua kwamba sina mimba na wezangu wana mimba”
“So umeona njia ya kuwaua wao ndio sahihi si ndio eheheeee?”
Nilizunguma kwa ukali huku mwili mzima ukinitetemeka kwa wasiwasi.
“Sasa na Magreti eti pia unamuonea wivu ukapanga ukirudi umkamate na umtese ili akujibu ni kitu gani ambacho amekifanya huko na baba yangu”
 
Mameno ya Jojo yakazidi kunipatandisha hasira laiti kama ningekuwa na wezo wa kama Joho ningeuchomoa moyo wa Livna ambao kumbe umejaa uhasama mkubwa sana juu ya watu wenye ukaribu wangu.
“Magreti naye anatatizo gani, amekufanya nini binti wa watu ambaye hata swala la mapenzi halijuia. Hivi unahisi wezako hawana hisia, hawana miooyo hawana roho za kupenda kama unavyo penda wewe eheeee?”
Livna machozi yakazidi kumwagika usoni mwake, maneno ya kujitetea yakamtoweka kabisa akilini mwake.
“Si unaogopa mimi kukuacha, basi nitakuacha kuanzia hivi sasa mimi na wewe basi. Na kama kunisiaidia, mwisho uwe leo na nitajua nitafanya nini, nikifungwa, nikikikamatwa nikiuwawa yote ni kwa ajili ya dhambi zangu nilizo zifanya na nipo tayari kuzitumikia kwa namna yoyote na muda wowote. Nitaondoja na kila nilite kuja naye hapa, pia nitaondoka na Magret kwani ndio mwanamke ambaye ameziteka hisia za moyo wangu na ndio aliye kubaliwa na mwanangu awe mke wangu. Kwaheri”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikamuachia Livna aliye toa ukunga mkali wa kulia kwani alicho kisikia ninaimani ni sawa na mkuki ulio uchoma moyo wake na kuutoboa tundu ambalo halito pona kabisa kwenye maisha yake.
 
AISIIIII……….U KILL ME 197

“Bye”   
Jojo alizungumza huku akinikimbili kwa nyuma, tukatoka katika chumba hichi. Tukaelekea katika chumba anacho ishi Hawa na Babyanka. Nikawakuta wakiwa wamekaa vitandani.
“Jiandaeni tunaondoka, Winy yupo wapi?”
“Jamani Dany hiyo ndio salamu?”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwnagu.
“Salamu ya kazi gani hembu chukueni kila kilicho chenu ninahitaji tuondoke hapa sasa hivi sawa?”
Nilizungumza kwa ukali sana.
 
“Hawa jifunze kusoma alama za nyakati”
Babyanka alizungumza huku akishuka kitandani mwake.
“Hata kama huo sio ustarabu, kukerwa akerwe na wengine hasira aje kutumalizia sisi, na unataka twende wapi?”
Hawa alizungumza kwa kujiamini huku akisimama, nikamtazama kuanzia juu hadi chini, kisha nikayarudisha macho yangu tumboni mwake na kuona ukubwa wa tumbo  umeongezeka.
“Tunaondoka katika hii meli, sihitaji nilio kuna nao humu kuendelea kuishi humu”
“Kwa sababu gani?”
“Livna alihitaji kuwau wewe na Yemi ili musiweze kuzaa watoto wenu”
Jojo aliniwahi kunijibu na kunifanya nimgeukie na kumtazama.
“Wewe ni nani unaye ingilia vitu visivyo kuhusu?”
“Nimwanangu”
“Mwanao…..!!!?”
 
“Unanitumbulia nini macho, ndio ni mwanangu”
“Hahahaaa Dany sasa unakuwa mwenda wazimu. Mtoto wa watu umemchukua humu humu ndani unajidanganya ni mwanao au ni wahiyari”
“Mwanangu wa kumzaa”
“Hhaaaa uwiiiiii, jamani hahaaa kumbe kuna siku ambazo unachangayikiwa. Sasa kama umechanganyikiwa siwezi kuondoka humu, nitmzaa mwanangu humu na atakulia humu sawa?”
Maneno ya Hawa yakazidi kunikera na kunipandisha hasira, nikatamani kumzaba kofi ila nikajikuta nikiuzuia mkono wangu kwa kukunja ngumi kwani ninafahamu kwamba nikimtandika ngumi itanigrimu sana kwenye maisha yangu na yake.
“Sijasingiziwa, huyu ni baba yangu wa damu, hata ukitupima DNA, basi tupo sawa”
 
“Heee makubwa haya”
“Babyanka hakikisheni kwamba munakusanya kila kilicho chenu tunaondoka hapa?”
“Siwezi kuondoka hapa, ninakuomba unisamehe”
“Unasemaje?”
“Nimesema kwamba siwezi kuondoka hapa ninakuomba unisamehe, sina sehemu ambayo nitakwenda na kuishi kwa amani kama ilivyo hapa kama Livna anahitaji kuwaua hawa basi ni acha na mimi nife tu”
“Mimi pia siondoki, una sehemu gani ya wewe kwenda kutuweka na kuwa salama?”
Hawa alizungumza kwa dharau sana.
“Baba tuondoke zetu”
Jojo alizungumza huku akinishika mkono.
“Baba huwezi kuwabadilisha hao, tayari wamesha kuwa wana ndoa, wanamahusiano ya jinsia moja”
Nikawaona Babyanka na Hawa wakistuka sana, wakatazamana na nikaona sura zao jinsi zinavyo poteza furaha. 
 
“Ni kweli anacho kisema Jojo?”
Hawa na Babyanka wakashindwa hata kunijibu na macho yao hayakuwa na ujasiri kabisa kunitazama usoni mwangu, nikakumbuka siku nilipo wakuta wakiwa wamekumbatiana na wamelala uchi kabisa.
“Tuondoke baba”
Jojo alizingumza huku akinishika mkono tukatoka chumbani humu na kukutana na Ester kwenye kordo akiwa ameongozana na wasichana wengine wanne wakiwa wameshika bunduki mikononi mwao.
 
“Dany samahani, ninafwata amri ya mkuu. Tumeambiwa tumkamate mwanao”
“Kwa kosa gani?”
“Sijajua kwa kweli, ila nimeambiwa nimemkamata”
“Ester natambua kwamba wewe ni mtendaji mzuri kwa Livna na hata kwangu ulifanya kila kitu kunisaidia kwa chochote ambacho nilikuomba kukifanya. Ninahitaji kukuomba hichi kitu cha mwisho tu na sinto kuomba tena”
Nikamuona Ester akishusha pumzi nyingi sana huku akiwa amejawa na huzuni kubwa sana kwani amelazimishwa kufanya kitu ambacho hajui hata sababu.
“Ninakuomba niondoke eneo hili, ninakuomba utuachie mimi na mwanangu tuweze kuondoka hapa”
Nilizungumza kwa sauti ya upole sana huku nikimtazama Ester usoni mwake.
“Muacheni apite”
Ester alizungumza huku akiwatazama vijana  wake alio ongozana nao, wasichana hawa wakatupisha taratibu na tukaanza kupita katikati yao huku nikiwa nimemshika mkokono Jojo. 
 
“Livna anajiingiaza kwenye tatizo ambalo litamshinda kulimaliza”
Jojo alizungumza huku akitazama nyuma.
“Tuachane naye”
“No lazima atawau hawa wasichana kwa kushindwa kutii amri yake.”
“Sasa tunafanyaje?”
“Hapo mbele atawatuma wasichana wengine waniangamize”
Jojo alizungumza huku tukizidi kutembea kwa mwendo wa haraka kwenye hii kordo ndefu.
“Simama”
Jojo alizungumza huku akijibaza kwenye ukuta kwa haraka na mimi nikajibanza kwenye ukuta, hazikupita hata sekunde kumi wakatokea wasichan zaidi ya sita wakiwa na silaha, kwa haraka Jojo akaanza kupambana nao, hazikupita hata dakika mbili wasichana wote wakawa wamelala chini huku wakiwa wamezimia.
 
“Siwaui kwa maana ninahitaji kumuonyesha Livna uwezo wangu”
Jojo alizungumza huku tukizidi kusonga mbele. Kadri jinsi tunavyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi tunavyo kutana na vikwazo za wasichana walio agizwa kumkamata Jojo ambaye hakuwa na haja ya kumuua zaidi ya kuhakikisha kwamba anawazimisha.
“Unaelekea wapi?”
Nilimuuliza Jojo huku tukimwafwata kwa nyuma. Jojo hakunijibu kitu chochote zaidi ya kuufungua mlango wa kuingia ndani ya chumba kimoja.
Tukamkuta Livna akiwa amekaa kwenye moja ya meza huku amezungukwa na wasichana zaidi ya kumi.
“Livna hivi unahisi kwamba una uwezo wa kupambana na mimi?”
 
Jojo alizungumza kwa sauti ya hasira kidogo huku akimtazama Livna.
“Siwezi kukuacha ukiwa hai, ni lazima nikuue”
“Hahaaa, unajiamini nini wewe, unanijua mimi ni nani?”
“Hei Livna najua una hasira ila ninakuomba mimi na mwanangu tuondoke hapa, sihitaji mafarakano mimi na wewe, au wewe na mwanangu”
“Mwanao wapi, umechukua malaya tu huko nje anaye jifanya anajua kuzungumza mambo ya watu ya nyuma ambayo hayamuhusu”
 
“Mimi ni malaya?”
Jojo alizungumza huku  akipiga hatua moja mbele kwa haraka nikamuwahi kumshika mkono wake na kumsimamisha.
“Ndio malaya”
“Livna hembu acha majibizano ya ajabu, tazama watoto wengine wa watu wamesha jeruhiwa elewa kwamba huwezi kumdhuru Jojo”
“Hembu niachie upuuzi na wewe, unaniletea malaya ndani kwangu leo hii unaniambia kwamba ni mwanao.”
Kwa kasi ya ajabu, Jojo akatoa mkono wake kwangu, kufumba na kumbua akawa amemfikia Livna aliye hisi kwamba wasichana wake wanaweza kumsaidia, nikastukia Livna akinyanyuliwa kwa mkono mmoja huku akiwa ameshikwa koo lake.
 
“Hivi unahisi kwamba ninashindwa kukua eheee”
Jojo alizungumza huku akizidi kumkaba Livna aliye anza kulitoa jicho lake akionekana kuanza kupoteza pumzi yake.
“Jojo Jojo”
Nilizungumza huku nikimftwa Jojo kwa ukaribu kabisa, nikamshika mkono alio mshika Livna, kusema kweli Jojo ana nguvu kubwa sana.
“Tafadhali  mwanangu ninakuomba umuachie”
Nilizungumza kwa upole sana huku nikumsisitizia Jojo kumuachia Livna kwa maana akiendelea kumshikilia hivi anavyo mshikilia ni lazima atakufa.
“Ukirudia na ukiendelea na mawazo ya  kuhitaji kumua yoyote kati ya wasichana wako au watu alio kuna nao baba yangu, nitahakikisha ninakurudia na nikirudi nitakigawanyisha kiuongo chako kimoja baada ya kingine.”
Jojo baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akamuachia Livna aliye anza kuvuta pumzi nyingi huku akiwa amekaa chini.
“Tuondoke”
Jojo alizungumza huku akitangulia kutoka nje, hapakuwa na msichana hata mmoja aliye jaribu kumshika wala kumsogelea Jojo. Tukapandisha juu kabisa ya meli hii.
“Ninahitaji twende nyumbani sasa baba”
Jojo baada ya kuzungumza hivyo akanikumbatia kwa nguvu kisha tukajitosa kwenye bahari na nikajikuta nikianza kupiga kelele kwani kasi tunayo kwenda nayo chini kusema kweli inatisha na kuogopesa na ukitegema ni usiku  basi ujasiri ukaniisha kabisa.
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa safatri ya kuelekea nyumbani kwa kina Jojo imeanza, je ina mafanikio yoyote kwa Dany? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )