Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Habib Mchange: Mabadiliko sheria za vyama vya siasa dawa ya viongozi ving’ang’anizi, Wanaotumia Ruzuku Vibaya

adv1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya serikali ya Alliance for Development Organisation (ADO), Habib Mchange, amesema Muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa utakuja na majibu kwa viongozi hasa wale wanaong’ang’ania madarakani na kwa wanachama wengi wa vyama hivyo tofauti na wengine wanaoupinga.

Muswada huo, ni ule wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliowasilishwa bungeni Novemba mwaka jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 6, Mchange alisema muswada huo ukipitishwa utatatua malalamiko ya wanachama wengi kwani watakuwa wamepewa nguvu za kumshtaki kiongozi wao yeyote akienda kinyume na katiba ya chama chao kwa msajili wa vyama vya siasa.

 Baadhi ya vyama vya siasa  vimekuwa vikilaumiwa juu ya matumizi mabaya ya fedha hivyo anaamini uwepo wa muswada huo ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria itadhibiti jambo hilo kwa kiwango kikubwa.

 Asasi hiyo pia imesema muswada huo kama utapitishwa na kuwa sheria rasmi, utadhibiti ukomo wa uongozi wa juu katika vyama vya siasa nchini.

Aliongeza kuwa  licha ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuulalamikia muswada huo, yeye kama mwanademokrasia nchini anaamini kuwa sheria hiyo itasaidia kukuza na kuvijenga vyama vya siasa.

“Kupitia muswada huu ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria utakwenda kusimamia vema ruzuku za kila chama cha siasa, kwani Sheria inaeleza kuwa Msajili wa vyama vya siasa atatoa ruzuku kwa vyama na kuelekeza namna ya kuzisimamia , nashangaa kwanini baadhi ya vyama vya upinzania vinapinga jambo hili,” alisema na kuongeza;

“Mimi na asasi yangu pamoja na vijana wenzangu tunamshukuru aliyependekeza muswada huu, kwani huko nyuma niliwahi kukandamizwa nikiwa katika vyama kutokana na kutokuwepo kwa sheria hii."

Alisema demokrasia ni kugombea nafasi na si watu kushikiria madaraka muda mrefu kwa kuwakandamiza wanasiasa waliopo hivyo kwa kupitia sheria hiyo itawafanya wanasiasa wote kuwa sawa.

“Kutungwa kwa muswada huu kutawasaidia  wanasiasa wanaoumia ndani ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kuondoa ukilitimba na Umungu watu,” alisema na kuongeza kuwa

“Viongozi wa chama wengi wamekuwa wakijimikisha vyama kwa kudai wanamichango mikubwa ndani ya vyama, sheria hii itaondoa migogoro na kuwa sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi,” alisema.

Aidha alisema Muswada huo utampa nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi za wananchi ipasavyo pasipo kuingiliwa na chama chochote cha siasa.

“Ndani ya vyama vya siasa kuna watu ambao awandi vyeo kila siku wana cheo kilekile, hii yote ni kutokana na uwepo wa mfumo usiokuwa bora wa chaguzi ndani ya chama,” alisema.

Hata hivyo, Mchange amewataka watanzania kutambua kuwa mabadiriko ya Katiba ni pamoja na mabadiriko ya sheria ndogo ndogo ikiwemo ya vyama vya siasa.

“Sheria itakayotungwa itawapa wanasiasa sehemu moja ya kulalamika na kuwaweka kati wanasiasa wote kwa kuongea lugha moja,”alisema

Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu muswaada huu unafaida  kubwa kwa nchi kwani itasaidia kudhibiti fedha za ruzuku na kukuza vipawa kwa wanachama .
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )