Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

Hatima Kesi ya Kina Zitto Kabwe Kupingwa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa Kujulikana Jumatatu

adv1
Hatima ya kesi ya kupinga Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa iliyofunguliwa na wapinzani katika mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, itajulikana keshokutwa wakati mahakama itakapotoa uamuzi wa kuisikiliza au la.

Uamuzi huo ulitolewa jana katika mahakama hiyo na Jaji Benhaji Masoud, wakati wa mabishano ya kisheria kuhusu uhalali wa mahakama kusikiliza shauri hilo au la.

Upande wa serikali uliwasilisha hoja 10 za kupinga kesi hiyo iliyofunguliwa na Zitto Kabwe, ambaye ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo wa wenzake kwa niaba ya vyama 10 vya upinzani kupinga kwa muswada huo.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Mark Mulwambo, ulidai kuwa mhimili wa Mahakama hauwezi kuingilia mhimili wa Bunge katika kujadili mambo yake.

Alidai kuwa mahakama inaweza kujadili sheria iliyotungwa na Bunge na si muswada ambao haujapitishwa kuwa sheria, hivyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa ni muswada.

Katika hoja nyingine, alidai kuwa waombaji wamewasilisha maombi yao bila kuwapo kiapo chochote mahakamani hapo na kwa sababu hiyo pekee, shauri hilo linakosa nguvu ya kisheria na linapaswa kuondolewa mahakamani.

Alidai kuwa wabunge wana uwezo wa kutoa maoni ya marekebisho ya muswada huo bungeni au kuwakilisha hoja binafsi kwa ajili ya kuwakilisha wananchi na kusikilizwa.

Upande wa watoa maombi ukiongozwa na Wakili Mpoki Mpale, ulidai kuwa kifungu cha Ibara ya 5 kwenye Katiba, kinaipa mahakama mamlaka ya kutengeu sheria au hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali au mamlaka yoyote kwa kukiuka haki, uhuru na wajibu kama ilivyoanisha ibara ya 12 hadi 29 kwenye Katiba.

Alidai kuwa Katiba inatoa mamlaka kwa mahakama kusikiliza shauri hilo kwa sababu inatoa nafasi kwa mtu yeyote anapoona haki inavunjwa au Katiba kuvunjwa, hivyo kufungua kesi na si lazima mpaka iwe sheria.

Alieleza kuwa ni kweli mhimili una haki ya kutokuingiliwa lakini kinga ya Bunge si kamili kwa kuwa kuna vitu ambavyo Bunge limekosea na kupingwa mahakamani.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )