Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 29, 2019

Kesi ya Zitto Kabwe Yapigwa Kalenda

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu shahidi aliyetakiwa kuanzakutoa ushahidi wake Leo amepata dharura.

Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi lakini Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine Kwani shahidi amepata dharura.

“Kwa jinsi  upande wa mashtaka tulivyokuwa tumejipanga tulitaka tuanze na ushahidi leo na shahidi tuliyekuwa tumemuandaa amepata matatizo ya kifamilia tunaomba kuahirishwa kwa muda,” amesema Katuga.

Wakili wa utetezi,  Jebra Kambole amedai mshtakiwa alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini pia ana majukumu mengine  kuomba tarehe za mwishoni.

Hakimu Shahidi baada ya kusikiliza maelezo hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, 2019  kwaajili ya kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi ya msingi,  Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo   Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za  makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Alifikishwa katika mahakama hiyo na kushtakiwa kwa mashtaka matatu ya uchochezi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )