Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, January 25, 2019

Kikao Cha Mawaziri Wa Tanzania Na Uganda Wanaohusika Na Mradi Wa Bomba La Mafuta Ghafi Chafanyika Kampala Leo

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wamefanya kikao kati yao na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika  Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

Kikao hicho kinachofanyika Kampala – Uganda ni cha maandalizi kabla ya kufanyika kikao na Mawaziri wa Uganda wanaohusika na mradi huo baadaye leo.

Kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Uganda wanaohusika na mradi huo kinafanyika kufuatia majadiliano ya wataalam wa nchi hizi mbili yaliyoanza tarehe 21/1/2019 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazosimamia mradi kutoka Tanzania na Uganda kilichofanyika tarehe 24/1/2019
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )